"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, September 15, 2009

Unadanganya hadi kisimani kunywa maji!

SWALI:
Mimi ni mwanamke na nipo kwenye ndoa kwa miaka 4 sasa na nimekuwa bingwa wa kudanganya kwamba nimefika kileleni (fake orgasm).
Tadhari napenda kujua hivi ni kitu gani huweza kusababisha mwanamke kufika kileleni, Ukiacha oral sex?
Je, uume unatakiwa kugusa spot au angle gani kwenye uke ili mwanamke kufika kileleni?
Au niseme nini kitaweza kunisisimua ili nifike kileleni?

JIBU:
Kwanza asante kwa kuulizwa swali la msingi ambalo wanawake wengi hupitia kwa maana kwamba huwa wanawafunga kamba waume zao kwamba wamefika kileleni kumbe ni hakuna lolote.

Tukirudi kwenye swali lako, ukweli ni kwamba kinachomfanya mwanamke mmoja afike kileleni kinaweza kuwa tofauti na mwanamke mwingine kwani kila mwanamke yupo tofauti katika mwitikio wa mapenzi (sex) na hata mwanamke mmoja huwa na tofauti ya mwitikio wa mapenzi kwa siku tofauti katika mwezi mmoja.

Wanawake wote ni tofauti kimwitikio linapokuja suala la kusisimka hadi kufika kileleni, kuna mwingine ukigusa chuchu tu anasisimka, mwingine atakwambia anaumia na kuna mwingine akichezewa vizuri kisimi husisimka mwingine hapana nk.

Ku-fake kufika kileleni huonekana kama wazo zuri katika kumfanya mume wako ajione amefanya kazi ya uhakika, hata hivyo haina maana yoyote katika kuwahakikishia mnakuwa na great sex maana mwisho wa siku wewe ndo unapunjwa.

Ni kama huwa unajenga matarajio hewa ndo maana hujajua nini kinaweza kukufanya ufike kileleni kiukweli.

Jambo la kwanza ambalo unaweza kufanya ni kwanza kuutambua mwili wako au kujua nini kinakusisimua au ni wapi unasisimuka na kunakupa raha ambayo inaweza kukupelekea kufika kileleni ukiwa na mume wako.
Hii ni pamoja na kumsaidia mume wako ajue kitu gani akikufanyia wewe kinakufikisha na kukupa raha ya kukufikisha kileleni au ndege kupaa hewani.

Ukiwa na mume wako akufanyie experiments nyingi sana kwa kuanza na milalo tofauti (sexual position), kukugusa sehemu zote unazosisimka kama clitoris, vulva, nje ya uke, ndani ya uke na mwili mzima tena kwa ujuzi wa kila aina huku ukiwa wazi kwa upendo na kutiana moyo.

pia inaonekana unaamini kwamba oral sex ndiyo ticket pekee ya mwanamke kufika kileleni, hii si kweli kwani kuna wanawake wanapenda sana na kuna wengine huona ni kitu kigumu kama kulipa kodi, kama kwako is fine, it is ok.

Jambo la msingi ni wewe kupenda kufanya kile unapenda na si kile unasikia wengine wanafanya kwani kila mtu ana ladha yake linapokuja suala la mapenzi hasa kutokana na background na tamaduni na malezi.
Tutaendelea.......................

1 comment:

Anonymous said...

Asante kwa aliyeuliza swali maana hata wengine tumejifunza.
Kazi njema
AM