"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, September 30, 2009

Usijisahau!

Wengine kupiga mswaki tu huwa vita! kazi kweli kweli!Ili ufurahi kuwa mwili mmoja maandalizi hayaanzii chumbani bali huanza tangu asubuhi unavyoamka na yote unafanya siku nzima (communication) na mume wako au mke wako huweza kuongeza hamu na pia kujikuta mpo connected na hatimaye kuwa na usiku wenye raha.
Mbusu (romantically) wakati unaondoka asubuhi au mnaagana kila mmoja kwenda na kupambana na shughuli za maisha na familia.
Mpigie simu au text au email mchana kwamba una mkumbuka na mwambie kitu chochote kizuri kuhusu yeye.

Hata hivyo kuna mambo madogo lakini muhimu sana ambayo kila mwanandoa ni muhimu kukumbuka ili kuhakikisha akitaka kuwa mwili mmoja na mwenzake mambo yanakuwa motomoto,

Kwanza, kama mke wako (kama wewe ni mwanaume) umeona analalamika kwamba huwa unamshika/mpapasa/gusa/chezea (touch), busu pale tu ukitaka kuwa mwili mmoja na sivinginevyo basi wewe unafanya makosa makubwa sana na unamnyima haki yake ya kuzaliwa ya kupewa non sexual touch.

Pili, kumbuka kukiwa na non sexual touch nyingi zinafumfanya mwili wako kujisikia vizuri na hupeleka feelings hadi moyoni mwake kwamba kuna mtu anamjali na kumbuka pia kuna wanawake touching ndiyo ugonjwa wao so ukimpatia kwako itakuwa paradise kila siku.
Jitahidi angalau gusa bega lake, mshike mikono, mkumbatie nk.

Tatu, watu 100 waliambiwa waandike vitu ambavyo husababisha kuwa turned off na wake zai au waume zao, asilimia 99 waliandika kwamba mwonekano mbaya ni sababu mojawapo.
Usijidanganye eti hata nikivaa ovyo kama ananipenda atanipenda tu, Pole sana anaweza kukupenda lakini asitamani kuwa mwili mmoja na wewe kwani upo rough, mchafu, unanuka, huvutii na mzembe na hufai kabisa.

Nne, kunukia vizuri ni moja ya sifa za kwamba upo sexy.
Ukinukia vizuri mume wako au mke wako anatamani kuwa karibu na wewe na kunuka ni kinyume chake, hata ulalamike na ukajitahidi kumpeleka kisimani kunywa maji hanywi.
Ukiwa na majasho na hujaoga unafunika homoni za pheromones ambazo huvutia na kuwafanya wanaopendana kuwa na bond imara.
Hivyo smell good!

Tano, uwe mzuri na maridadi kwenye mawasiliano hasa kama wewe ni mwanaume, mke wako anaporudi kazini au jioni anapoongea kuhusu yale amekutana nayo siku nzima msikilize na uwe pamoja naye kuhakikisha anaongea maneno yako yote huku ukimsikiliza na ajue unamsikiliza na upo makini na unapenda kumsikiliza kwa njia hiyo unafungua hisia zake na anakuwa open kukuruhusu baada ya mda ufurahia mwili wake.

Tutaendelea…………………….

1 comment:

Anonymous said...

Hapa umenena, japo hujamaliza, I wish ningekuwa na muda nichangie mada.
BAD COMMUNICATION HUUA KABISA HISIA ZA MWANAMKE.
Mwanaume anaweza kuwa turned on hata kama mmegombana muda si mrefu akukuona au akikumbukia kile kitu. Mwanamke akiwa na neno nawe kila akikuona anakumbuka na hasira inakuja.
Sio ati mchana wote hamuongei kisha unangoja usiku ufike ndo unamsogelea kama kibaka anayetaka kupiga roba wakati hakuna communication zozote, as if yeye ni sex machine.

Wanawake tunahitaji love and affection kabla ya yote.