"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, September 27, 2009

Usikate tamaa!

Usikate tamaa tumia uwezo wako!Moja ya siri kubwa ya mahusiano ya binadamu ni jinsi Mungu anavyo weza kufanya miujiza kwa mwanaume na mwanamke ambao wanaamua kufuata njia za kimungu ili ndoa yao iwe ya kuridhisha na mpya kila siku.

Ni pale tu tunapotii mpango wa Mungu na kumtegemea yeye (kitu ambacho wengi huona kigumu) huweza kupata maana halisi ya upendo wa kweli (intimacy, love and affections) kati ya mke na mume.

Mungu ameweka hamu ya kupendwa ndani yetu kwa sababu maalumu na Mungu hana mpango wa kutufanya tuishi katika ndoa ambazo zinatufanya kuwa frustrated na disappointed bali furaha na kicheko katika familia ingawa siri kubwa ya kwanza ni kumpenda Mungu kwanza.

"The love of God is direct proportional to the love of people”
Hii ina maana unampompenda Mungu kwanza ndipo utampenda mke au mume pia kwani upendo wa Mungu kwetu hufanya reflection kuwapenda wale wanaotuzunguka akiwepo partner wako.

Mpango wa Mungu ni kwamba ule upendo unaowafikisha wanandoa wapya madhabahuni kufunga ndoa huwa ni upendo kichanga kabisa (infant) siyo upendo uliokomaa kwani upendo wa kweli (real love) kati ya mke na mume huweza kuzaliwa baada ya mke na mume kuishi pamoja kwa muda mrefu kwa kupitia shida, majaribu, conflicts, storms, tofauti, furaha, amani na kila mmoja kuwa commited kwa mwenzake kwa kuzikubali tofauti na kila mmoja kuondoa uchoyo binafsi na kujenga kitu kimoja kinachofanana.

Bahati mbaya kubwa ni kwamba wanandoa wapya wengi baada ya kukutana na disappointments au frustrations huhisi ni dalili kwamba ndoa imefika mwisho kumbe huo ndiyo mwanzo wa kujenga upendo mpya.

“The fairly tale must end for the potentials of true intimacy to begin”

Ndoa huhitaji kazi na jitihada ya wawili walioamua kuishi pamoja haitokei naturally kama watu wawili wanapopendana kwa mara ya kwanza (fall in love) na kwamba inakuwa tambalale kila iitwapo leo.

Ndoa ni kuvumiliana na kujitoa ili kujenga upendo wa kweli kwa muda na si wka usiku mmoja tu. Unahitaji kuwekeza jitihada zako, uaminifu (trust), imani na matumaini.

Mke kuwa na hitaji la upendo wa ndani (intimacy) kutoka kwa mume wake tofauti na mwanaume ni hitaji ambalo hufanya kazi kama injini kwa wanandoa kuhitaji kuridhishana hata hivyo mke akiamua kuchukua njia nyingine ya kuwa mkali na mchungukwa mume anaweza kuifanya ndoa ijae uchungu na upweke na hatimaye kusambaratika.

Mungu ameweka siri kubwa sana kwa watu wawili imperfect kutengeneza kitu kimoja (mwili mmoja) hii ni kazi inayohitaji kazi ili kuwe na bond strong.

Tukumbuke kwamba wanandoa wapya wawili ambao hukubaliana kwenda mbele za Mungu kutoa viapo vya kuishi pamoja kama mke na mume ni binadamu wa kawaida ambao ni dhaifu (vulnerable & insecure) haijalishi wanajitahidi kiasi gani kuficha mapungufu yao kila mmoja kwa mwenzake hata hivyo baada ya kuoana na kuanza maisha kila mmoja hujifunza kwamba ni kitu kisichokwepeka kuficha mapungufu na kwamba upungufu ni sehemu ya binadamua na jambo la msingi ni kila mmoja kumkubali mwenzake kama alivyo.

“A woman never marries the man of her dreams, she helps the man she marries to become the man of her dreams”

Ukiwaona wachumba ambao wanategemea kuoana macho yao huwa hayaoni chochote isipokuwa uimara na ahadi kamili ya upendo uliondani ya mioyo yao.
Ikitokea ukamuuliza binti (wachumba) je, unaona kasoro yoyote kwa mchumba wako (kijana wa kiume) bila shaka atakwambia Mungu amenibariki sana kunipa mume mtarajiwa ambaye hana kasoro wala tatizo lolote.

Hata hivyo hizo ni illusions, ni maluweluwe ni fantasy ni kitu ambacho hakitadumu kwa muda mrefu kwani akishaolewa tu hatahitaji kufikiri sana kuorodhesha kasoro za mume wake na wakati mwingine atalalamika kwamba nilikuwa sijui kwamba tupo tofauti kiasi hiki.
"Wachumba huishi kwenye ikulu na wanandoa huishi kwenye nyumba halisi"

Kabla ya kuolewa mwanamke huona matumaini yanayong’aa kwa mume wake mtarajiwa, anaona ulinzi, uimara, matumaini na upendo usio mfano na mwingine huringa na kutembea kwa madaha hata hivyo baada ya kuolewa anaanza kuona udhaifu na ndoto zote zinaanza kuyeyuka na kusinyaa kama au maridadi kwenye jua kali la ikweta, hukatishwa tamaa na yote huja ghafla kama kimbunga na anaanza kuumia na kujuta kwa kuwa mahitaji yake hayajatimizwa kama alivyokuwa anaona mwanzoni.
Haamini jinsi mume asivyomjali na kumsikiliza na kumpenda.

Hadi hapo mke anaweza kuamua kuitikia kwa:-
(i) Kwa hasira kutokana na hayo mume wake amemuonesha]
(ii) Kwa Kuwekeza kwa upendo, imani katika uwezo/uimara (strength zile anaziona kwa mume wake na kuanza kuijenga ndoa upya

Ili mambo yaenda vizuri au upendo wa kweli uzaliwa mke anatakiwa kuamini uwezo wa ndani wa mume wake alionao ( streghth siyo weakness).
Anaweza kuwekeza kwa mume halisi aliyejificha kwa mume wa nje mwenye kutojali kutimiza ndoto zake za uchumba na honeymoon.

"The secret in marriage is not finding a hero to be your husband, but finding the hero in your husband”
Mungu amempa kila mwanamke uwezo wa ajabu wa kumsaidia mume wake kukua na baada ya muda mume kuwa mcha Mungu sawa na anavyotakiwa.
Bahati mbaya ni kwamba wanawake wengi wamekatishwa tamaa sana kiasi kwamba huyu mwanaume aliyenaye leo hawezi kuwekeza chochote kwa ajili ya mume huyu atakavyokuwa kesho.

No comments: