"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, October 31, 2009

Umri ni namba tu!

Mamia ya watu walihudhuria sherehe za harusi ya mzee Ahmed Muhamed Dore mwenye miaka 112 akiaoana na binti aitwaye Safia Adulleh mwenye miaka 17.
“Leo Mungu ameniwezesha kufikia ndoto yangu” alisema mzee Ahmed Muhamed Dore baada ya kuoana na binti mbichi kabisa kutoka maeneo ya Galguud huko katikati ya Somalia.

Mambo yanayovutia kuhusu hii ndoa
Wanafamilia wa binti wanasema binti yao amefurahi kupata mume.
Bwana harusi alikuwa anasubiri kwa karibu zaidi binti aendelea kukua hadi amshauri waoane bila kumlazimisha bali kumvutia kwa upendo ili waoane.
Ni ndoa ya aina yake kwenye eneo ya Horn of Africa kwa babu miaka 112 kuoana na binti wa miaka 17.
Wapo watu ambao hawaridhiki na tofauti ya umri ingawa katika sheria za kiislamu inaruhusiwa.
Wapo waliofurahi na kukiri kwamba umri si kizuizi linapokuja suala la ndoa na kupendana.
Bwana harusi tayari ana watoto na wajukuu 114 huku motto wake wa kwanza akiwa na miaka 80.
Bado anaamini huyu mke mpya ataendelea kumzalia watoto.
Zaidi anakiri kwamba ni Baraka sana kuwa na mtu unayempenda na akaendelea kukutunza.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Friday, October 30, 2009

Utaumia!

Tafadhari chukua glass ya maji mkononi, usisome tu naomba kama unaweza chukua glass jaza maji na ishike mkononi.
Swali ambalo naweza kukuuliza ukisha ichukua mkononi ni je, glass ya maji ni nzito kiasi gani?
Naamini jibu ni kwamba haina uzito wowote.
Upo sahihi na umebarikiwa kwa jibu zuri.
Hata hivyo ukweli ni kwamba hata kama uzito wa glass yenye maji si lolote, kama ukiishika kwa zaidi ya saa moja utaanza kusikia uzito wake, unavyozidi kuishika kwa muda mrefu ndivyo utajisikia uzito unaongezeka zaidi ingawa uzito wa glass ya maji ni ule ule.
Utajisikia mkono kuanza kuuma na kulemewa na uzito kama vile umeshika bonge zito la tofali la sementi.

Ndivyo mahusiano ya ndoa yanavyofanya kazi wakati mwingine.

Kuishi wawili ni sharing ya mambo mbalimbali na kuna wakati mwenzako anaweza kukwaza, kukuumiza, kukusema vibaya, kufanya vibaya, kukutukana, kukudanganya nk na kila kitu unafanya kwake au wewe unafanyiwa kina uzito mkubwa au mdogo sana moyoni kwa partner wako.
Hata hivyo unavyozidi kutunza vitu vidogovidogo vinavyokuumiza moyo bila kuviweka wazi kwa mwenzako ili muongee na kuyamaliza. Siku zinavyoongezeka na kwenda itafika siku mkusanyiko ya hayo mambo moyoni mwako utaanza kuwa mzito na kujisikia vibaya kwa mwenzako.


Inawezekana chanzo cha hasira zako au uchungu ulionao au maumivu uliyonayo nk ni matokeo ya vitu ambavyo uliweka moyoni mwako miaka 5 au 10 au 25 iliyopita katika ndoa yako.
Kubwa zaidi hukufanya juhudi yoyote kuhakikisha unaongea bayana na wazi kwa mke wako au mume wako na kutokana na hiyo tabia leo umefika hapa baada ya hayo mambo kujijenga kwenye moyo wako kwa miaka zaidi ya 5 nk.

Huku mwenzi wako akiwa amesahau hayo mambo, wewe umeendelea kuyashika ndani ya moyo wako na ni wewe unayeumia kwani mwenzio hajui kama bado yapo moyoni mwako.

Hata ukimwambia leo anaweza kuwa shocked kusikia kwamba bado ulikuwa umeweka jambo au mambo kama hayo moyoni.
Kwa kuwa umeshindwa kuachilia imefika mahali umeona ndoa haina maana kwako, haikupi furaha na unaanza kufikiria mlango wa kutokea (anyway ndoa haina exit, ni deaend).
Unajisikia humpendi tena mume wako au mke wako.
Badala ya kidonda kupona sasa inazidi kuwa fresh.
Na kidonda kinazidi kuliwa na wadudu na damu kutoka bila wewe kujua.

Jifunze kuwa wazi na kuongea kwa mpenzi wako kama amekukosea mwambie na msahemeane na kusahau yaliyopita.

Thursday, October 29, 2009

Nani ana Hasira Zaidi?

Je, wanaume hukasirika zaidi kuliko wanawake?
Wengi huwaona wanawake ni viumbe ambavyo vipo emotional na very affectionate wakati wanaume ni aggressive na wakati huohuo very courageous.
Tafiti nyingi hazioneshi kwamba wanaume hukasirika haraka kuliko wanawake bali zinaonesha tofauti iliyopo hasa namna ya kuonesha (express) hizo hasira.

Ukweli ni kwamba wanaume na wanawake wote huwa na mawazo sawa ya kukasirika, ingawa wanawake huonesha intensity kubwa ya hasira na kwa muda mrefu na hupenda kutoa hasira zao kwa njia ambayo ni submissive zaidi ya wanaume.
Kwa upande mwingine mwanaume akikasirika anachukua direct approach ili kupambana na mtu amesababisha akasirike.

Hata hivyo kwa uajumla suala la kukasirika na kuonesha hasira mara nyingi lina base zaidi kwenye uwezo (power/authority) kuliko masuala ya gender kwani mara nyingi watu huonesha hasira zaidi kwa watu waliochini yao, wanyonge wao na waliowadogo .

Wednesday, October 28, 2009

Hataki kuongea!

Tunaendesha Km 8 huku hatuongei, acha tu!
Swali:
Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa sasa mwaka wa 8 nimekuwa nikitatizika sana na tabi ya mume wangu kushindwa kuongea na mimi, kila nikitaka kuongea chochote anaonesha hali ya ku-ignore kile nataka kumwambia.
Kinachoshanga zaidi ni kwamba tunapoenda kazini wote tunatumia gari moja hata hivyo zaidi ya Km 8 zote tunakuwa mabubu hadi kila mmoja anaenda kazini kwake na ni kama vile tumekuwa watu wawili tofauti.
Nifanyeje ili mume wangu awe anaongea na mimi tena kama wakati wa uchumba na miaka ya kwanza ya ndoa yetu.
Ni mimi mwenye mume bubu!

Jibu
Dada mwenye mume bubu!
Asante sana kwa swali zuri ambalo naamini si wewe tu ambaye unakutana na hali kama hiyo wapo wanawake wengi tu hawasemi au wanaume wengi tu ambao wamejikuta kila mmoja hana hamu ya kuongea na mwenzake tena, kinachoshangaza ni kwamba wameapa kwamba wataishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.

Kabla hatujaanza kujibu swali vizuri jambo la msingi unatakiwa kutambua kwamba ndoa hupitia hatua mbalimbali na kwamba unapokutana na hali kama hiyo unatakiwa kuwa makini zaidi ili kuhakikisha unairudisha kwenye mstari au badala ya kuweka maji kwenye moto wewe unaongeza petrol.

Inawezekana unapokumbuka mume wako alivyokuwa anaongea na wewe kwa simu au text messages au email au kukutana tu na kuwa na hamu na wewe kabla ya kuoana na leo hii, hisia zako zinaumia sana kwani inawezekana alikuwa anakesha na si kuongea na wewe tu bali kuhakikisha anaongea vitu ambavyo vinakufanya uwe au ujisikia happy na kwamba una mume anayejua kupenda na ni yeye tu duniani, leo umeoana mambo ni kinyume.

Wanandoa wengi hujisahau (wanaume na wanawake) kwamba wanahitaji kuendeleza romance na surprises hata baada ya kuoana.

Kama wanandoa wawili wamefika mahali hawawezi kuongea tena hii ina maana kwamba mmoja wao hajisikii kuvutiwa (hisia) kuweza kuongea na mwenzake, anajisikia unam-bore, humvutii tena.

Inaweza kuwa ni wewe mwenyewe umesababisha mume wako awe disconnected na wewe au ni yeye amepata mwingine ambaye anamvutia zaidi na kumfanya anapoongea ajisikia vizuri.
Kabla ya kuamini kwamba ni yeye labda ni vizuri kuanza kuisafisha nyumba yako moyoni mwako kwanza yawezekana ndo itakuwa dawa kamili.

Je, bado upo attractive kama ulivyo kuwa enzi zako zile za uchumba, honeymoon na miaka ya kwanza ya ndoa yenu?
Je, unamheshimu mume wako kama wakati wa uchumba au mwanzo wa ndoa yenu?
Je, unaongea tu, na
kumkefyakefya (nagging) kwa kila kitu hata kitu kisicho na maana hadi yeye kujikuta hana majibu na jibu sahihi ni kujibakia kimya?
Je, umakuwa unalalamika kwa kila kitu hata yeye kutoongea na wewe?
Je, mahusiano yako kimapenzi ni mazuri na yeye (yaani kuna enjoyment ya kuridhisha linapokuja suala la sex)?

Kuna msemo kwamba “People take things for granted when married” kwa sababu wanaamini wanaishi kwenye mapenzi tayari hivyo wanakuwa jeuri kwa wapenzi wao.

Dawa ya kuweza kuongea na yeye ni wewe kuwa na bonding mpya na mume wako yaani ajisikie yupo connected na attracted na wewe na hii haiwezi kutokea overnight kuna kazi unahitaji kufanya.
Unaweza kuanza kufanya vitu vile yeye anapenda kufanya, kama vile michezo, project, business hata mambo anayopenda kuongea, hapo atajisikia vizuri kwani unagusa maeneo yake.
Wanaume hufanya bond haraka kwa kufanya activities pamoja na si kwa kukaa na kupiga soga kama wanawake, hivyo ukitaka mumeo aongee mfuate kwenye shughuliza zake binafsi anazopenda kufanya.

Kama kuna kazi amefanya au kitu amefanya jitahidi kuhakikisha unampa credit au praise, kumsifu kwa vitu anavyofanya kunampa feelings kwamba unatambua mchango wake na kwamba yupo respected na wewe pia atafahamu unatambua juhudi zake katika familia hivyo ataanza kuongea na wewe.

Pia inawezekana kutokana na yeye kushindwa kuongea na wewe umeamua kuwa rough yaani humpi respect nah ii imeathiri ego yake na anakuona hakuna lolote, hivyo geuza kibao kwa kumpa respect kwanza.

Pia unaweza kujipa kalikizo kadogo kwenda mbali kidogo ili ujenge hamu ya kukutaka au wewe kutokuwepo kuna kujisikia Fulani ambalo kwa wawili wanaoishi pamoja lazima itajenga hamu ya kukuhitaji tena.

Pia kumbuka approach ya maisha na mapenzi kwa ujumla kwa mwanamke na mwanaume ni tofauti hivyo unatakiwa kuwa makini na namna unavyoongea na mume wako kwani sasa mnaishi kwenye ndoa ni maisha halisi ni kitu halisi.

Pia inawezekana sasa hakuna fun zozote, hakuna kucheza wala kutaniana wala kufurahishana, wote mmejikita kwenye kazi na responsibilities na matokeo yake hakuna kicheko na mnakuwa disconnected, jiulize wewe na mume wako mmecheza mchezo wowote lini?

Kama unaweza basi kuanzia leo jifanye ni mchumba na act kama mchumba uone kama hataongea.

Usipende kuongeea naye eti kwa kuwa kuna issue muhimu ya kuongea, ongea naye hata wakati hakuna issue sensitive, just for fun.

Haina haja kuongea (kuchonga) ili kutaka mume wako aongee na kujibu kila swali unalomuuliza au kuzunguka kutoa maelezo mengi badala ya kuongea point ndipo wanaume wengi hujisikia wanawake hawaeleweki na too much na wakati mwingine mume amechoka wewe unataka kuongea na maswali kibao.

Uwe na hekima, wakati mwingine wanaume anahitaji kwenda pangoni.
Hata kama hatulipii kuongea haina maana tuongee ovyo na kuuliza maswali yote, ni vizuri kuwa makini na jinsi tunavyoongea na si kila wakati ni wakati wa kuongea.

Tuesday, October 27, 2009

Kutojiamini - 2

Kuwa na staha ya chini au kutojiamini ni ugonjwa ambao unawakumba wanawake siku za leo kuliko nyakati zote katika historia ya dunia.
Traditionally, kazi ya wanawake ilikuwa nin kulea watoto au familia na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa hapo nyumbani wakati mwanaume yupo kuwinda na kuhakikisha anarudi na chochote kwa ajili ya familia.
Siku za leo mwanamke ambaye anaamua kukaa nyumbani hana respect yoyote, hakuna status yoyote. Mama wa nyumbani (house wife) sasa anataniwa na kupewa jina kwamba yeye ni supermom.
Matokeo yake hawa ma-supermoms wanajikuta katika frustration kiasi kwamba wengi hutamani wangekuwa wengine kama wale ambao wanaenda maofisini na kufanya kazi zao.
Hapa hatukatai kwamba mwanamke hatakiwi kufanya kazi zingine au kusaidia kuingia kipato bali tunazungumzia mwanamke kutojiamini au kuwa na staha ya chini (low self esteem)
Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba wanawake ambao si supermoms au ambao hawashindi nyumbani wanawacheka wenzao ambao wanashinda nyumbanin na kuwaona hawa supermoms ni creatures wa ajabu sana ambayo lazima something is wrong in their mind kwa nini wanapenda domestic duties.
Pia jambo lingine linalosumbua wanawake na kujikuta wana low self esteem ni suala la urembo. Leo physical attractiveness ni factor muhimu kwa mwanamke wakati mwingine kuliko mwanamke kuwa na brain ya uhakika.
Mwanamke ambaye hapendezi hujiona inferior kuliko wale wanaopendeza katika rika yake.
Ushahidi wa kisayansi unathibitisha kwamba hakuna tofauti yoyote kati ya mwanamke na mwanaume linapokuja suala la akili au intelligence, ingawa kuna maeneo ambayo kila gender huwa imara zaidi kama vile wanaume ni wazuri kwenye mahesabu (abstract reasoning) na wakawake ni wazuri kwenye Lugha (verbal skills).
Pia hakuna aliye na faida zaidi ya mwenzake ingawa wanawake ni rahisi kuwa na hofu na uwezo wao (mental) kuliko wanaume na hakuna sababu maalumu.
Matokeo yake wanaume hujiona ni muhimu kuwa na akili au kuonekana ana akili kuliko mwonekano mzuri, hata wanawake huangalia mwanaume mwenye akili kuliko urembo wakati mwingine (yaani mwanaume hata akiwa anafanana na sokwe mtu kama ana akili na mipesa bado huwa ni sumaku ya uhakika kuvuta wanawake.
Kwa wanawake hilo ni tofauti kwao urembo ni jambo la msingi kuliko kuwa na akili (brain) wanadai kwamba wanaume huona mwanamke mrembo zaidi kuliko mwenye akili.
Hata hivyo suala la kujiamini ni muhimu sana kwa mwanamke wakati mwingine afadhari uwe na mke ambaye hajasoma ila anajiamini kuliko kuwa na mke aliyesoma na hajiamini.

Monday, October 26, 2009

Eti Kulala Pamoja si Afya!

Tafiti za karibuni zinaonesha kwamba wanandoa kulala kitanda kimoja si afya kama kila mwanandoa yaani mke na mume kulala kila mmoja kitandani chake mwenyewe.

Kitendo cha wanandoa kulala kitanda kimoja kilianza wakati wa mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) kitu kilichosababisha watu kuhamia katika miji na kujikuta wanakosa accommodation na kulazimika mke na mume kulala kitanda kimoja.

hali hiyo imeendelea hadi leo na kuwa kama mfumo ambao watu wakioana tu huamua kulala kitanda kimoja.


Pia bado baadhi ya jamii zinazoishi vijijini mke na mume huendelea kulala kila mmoja kitanda chake hadi leo.

Kwa wastani wanandoa wanaolala pamoja huweza kusumbua mwenzake (disturb) nusu ya usingizi anaotakiwa kulala kama kila mmoja angelala kitanda chake.

Wanandoa kulala pamoja huweza kusababisha kusumbuana na hatimaye kusababisha magonjwa kama vile kuchoka, magonjwa ya moyo. Depression, stroke. Matatizo ya kupumua nk.

Pia historia inaonesha kwamba kitandani hakukuwa mahali pa kulala wanandoa bali ilikuwa sehemu muhimu (maalumu) ya wanandoa kukutana pamoja kwa ajili ya kuwa mwili mmoja (tendo la ndoa) na si wanandoa kulala pamoja.

Daktari wa sociology kutoka chuo kikuu cha Surrrey Dr. Robert Meadows anasema kwamba watu hujisikia vizuri wakilala kitanda kimoja na wapenzi wao hata hivyo ushahidi ni kwamba kulala kitandani kimoja si afya.

Je, unaonaje suala Hili la kulala kila mwanandoa kitanda chake mwenyewe?

Saturday, October 24, 2009

Mchumba asiye mwaminifu huwa mwenye ndoa asiyemwaminifu!

Swali:
Habari za kazi kaka naomba nisaidie naangamia kwa kuwa na mawazo yasiyo na msingi na kuumiza afya yangu, kweli nateseka mno.
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 29, nilikuwa na relation ya kwanza ambayo ilidumu kwa miaka mitatu lakini kikubwa kilichotufanya tusaparete ni dini yeye muislam mie mkristu.
But baada ya muda kupita nikapata mvulana mwingine kwa kweli nilifurahi toka siku ya kwanza kwa kuwa wote ni wakristu na nilimuona kwamba anampenda Mungu kwa matendo yake lakini kadri tulivyoendelea na relation nikagundua ana affair na wasichana wengine.
Niligundua kupitia simu yake ya mkononi, nikamwambia na nikampa masharti kama ananipenda anipeleke kwao kunitambulisha na akafanya hivyo, haijapita mwezi bado anaendelea na hao wasichana wengine tena akiwa anakuja kwangu anawambia wasitume msg wala kupiga simu, lakini pia nimegundua ana relation mpya kaanzisha tena kwa mwanamke mwingine yani kichwa kinaniumwa!

Maswali
Je, Ni kweli mwanaume wa hivi anarekebishika kweli?
Je, kwa nini anakuwa na wasichana tofauti tofauti?
Na nikajaribu kupeleleza kwao nikaambiwa ni mimi peke yangu nilipelekwa kutambulishwa.
Je, kweli anafaa kuwa mume?
Maana sihitaji kuwa nabadilisha wanaume kila siku nahitaji kupata ushauri wa kuwa kama anabadilishika bora nitulie nae kuliko kufuata mwingine na kila siku kuwa na wanaume tofautitofauti.
Kweli nampenda kwasababu familia yao ipo katika misingi ya dini imara.

Nimeelemewa na mawazo.
Ni mimi dada Yamenikuta.

MAJIBU YA SWALI LAKO

Pole sana dada Yamenikuta!

Kama mmoja ya watu ambao hupokea maswali mengi yanayohusiana na ndoa na uchumba au mahusiano kwa ujumla, ukweli kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusiana na suala la wanandoa kuoa wrong partner, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wa hawa ambao wameoana na wanaume/wanawake wasiofaa wanakiri kwamba walikuwa wanajua na kufahamu fika kwamba wachumba zao walikuwa na tatizo hata kabla ya kuoana, kwa kuwa walikuwa wamependa (fall in love) au pendana kwa muda mrefu au muda wa kuoa ulikuwa umefika waliamua kwa hiari zao kuendelea na mahusiano wakitegemea kwamba siku moja watabadilika.

Je, tunaweza kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?
Hivyo basi dada Yamenikuta, ni jambo la busara na hekima kubwa kuwa makini na maamuzi unayofanya hasa baada ya kukutana na mwanaume ambaye ameshindwa kutembea katika ahadi kamili za msingi wa mahusiano yenu na kutegemea kuwa na ndoa yenye baraka.

Usikubali kuoana naye kwa sababu eti unampenda sana na umekuwa naye kwa muda mrefu katika mahusiano kabla ya kuoana.
Urefu wa mnahusiano kabla ya kuoana (uchumba) au wewe kumpenda na kujioana huwezi kuishi bila yeye hauna uhusiano wowote na afya ya ndoa yako baadae kama huyo mchumba wako ameshindwa kuwa mwaminifu kabla ya kuoana.
Tabia alizonazo kabla ya kuoana haziwezi kubadilika ghafla baada ya kuoana.
Mwanaume asiyemwaminifu kabla ya kuoana hatakuwa mwaminifu baada ya kuoana pia.
Ndoa huwa haibadilishi mtu kiburi chake, hasira zake, umalaya wake, wizi wake, tabia zake chafu sana sana ndoa hufunua hizi tabia na kuziweka mezani uzione.

Usijidanganye mwenyewe na kujipa moyo, utaangukia pua!

Kile unachoona sasa ndicho utakachopata ukioana naye.

Si kweli kwamba huyo mwanaume anampenda Mungu kwa matendo kama ulivyosema na sijajua ulitumie vigezo gani kwani kutembea na wanawake wengine ni uthibitisho kwamba dini yake ni ovyo.

Pia yeye kukupeleka kwa wazazi wake (baada ya wewe kumlazimisha kama uthibitisho kwamba anakupenda) kukutambulisha si jambo kubwa sana ambalo linaweza kumfanya mwanaume mhuni asiwe mhuni bali ni taratibu tu za kuwaambia wazazi kwamba huyu ni mtarajiwa (siyo mke) hii ina maana hata kesho anaweza kuamka na kumtambulisha mwingine.

Pia wazazi wake kuwa wanadini wazuri haina maana mtoto wao naye atakuwa na dini nzuri na kukuhakikishia maisha safi ya ndoa, hata hivyo dini nzuri kwa maana ipi ? kwenda kanisani au kuona wagonjwa au jinsi wanavyoishi?

Ni kweli kama wewe upo makini na dini yako uamuzi wa kuchangua mume ambaye dini zinafanana ni wa busara sana unaweza kusoma hapa

Sasa tuje kujibu maswali yako.
Mwanaume wa aina hiyo huwa harekebiki na Mungu anakupenda sana kwamba amekuondoa kwenye shimo ambalo ungeingia kutoka ingekuwa kazi ya ziada, hivyo furahi na amini kwamba Mungu anaweza yote na shukuru kwa kukuonesha kwamba huyo mwanaume hafai.

Ni ngumu sana kukubali kwamba mwanaume huyo hafai kwani inaonesha ulimkabithi moyo wako wote hata bila kuchunguza vizuri ni wapi moyo wako unaweka.

Suala la kwa nini anakuwa na wasichana wengi naamini yeye ndiye anajua hata hivyo inaonesha kwamba hata kama anakupenda ana tabia mbaya ya uhuni kiasi kwamba hawezi kuwa na wewe tu bila hao wanawake wengine.

Na je anafaa kuwa mume, ukweli ni kwama hafai na kimbia na mwogope (kama njaa) kwa maelezo zaidi kuhusu kujua anafaa au hafai au ni yeye au si yeye wa kuoana naye soma hapa

Usijifariji kwamba eti afadhari ubaki naye yeye ili usionekane unabadilisha wanaume, ukweli huyo hafai na pia kama wewe umezoea kuwa na mwanaume na kumpa mwili wako ni kweli hisia zako zitakuwa zimeumia zaidi, wakati mwingine ukipata mchumba hakikisha humpi mwili wako kwanza hadi ndoa.
Kwa maelezo zaidi soma hapa Soma hapa

Ladies, you don't need a man that drives an X6, M3, Land Rover, Mercedes or Hummer to feel special!!

The happiest people don't necessarily have the best of everything;
They just make the best of everything they have.

Source: MtandaoThursday, October 22, 2009

Kujiamini!

Nini maana ya kujiamini au staha?
Kujiamini au Staha (self esteem) ni jinsi unavyojiona mwenyewe, ni image yako mwenyewe, kama una staha ya juu (high self esteem) maana yake unajiona mzuri kila eneo na kama una staha ya chini maana yake unajiona mbaya katika maeneo yote ya maisha yako.
Kuwa na staha ya chini (low self esteem, low self image) ni ugonjwa unaowasumbua wanawake wengi sana katika jamii yetu ya sasa kuliko wakati wowote katika historia ya dunia.

Tunaposema mwanamke fulani ana low self esteem au low self image tuna maana gani?
Hii ina maana kwamba mwanamke anakaa mwenyewe na kuanza kujishangaa kwa nini hana marafiki wa kweli.
Anakuwa na hamu ya kuongea na mtu ana kwa ana na anajua huyo mtu hayupo.
Ni mwanamke anayejisikia kwamba wengine hawawezi kumpenda wakigundua kwamba ni yeye halisi so anajitahidi kujifanya fulani ili watu wampende.
Ni mwanamke anayeogopa kuongeea na wanawake wenzake wa rika moja kwa maana kwamba yeye hayupo smart kama wao.
Ni mwanamke anayeamini wafanyakazi wa kike wa ofisini kwa mume wake ni wazuri zaidi kuliko yeye hivyo kila siku mume akirudi anaonywa na kwamba ajihadhari na hao wanawake.


Ni mwanamke anayejisikia mjinga fulani au maskini fulani au failure fulani hasa akiwa nyumbani kwake peke yake akifikiria maisha.
Ni kujishangaa kwa nini watu wengine wana uwezo na talents nyingi kuliko yeye.
Ni mwanamke anayejisikia hapendezi na havutii tena kimapenzi (sexually unattractive).
Ni mwanamke kujisikia ameshindwa kuwa mke na mama.
Ni mwanamke ambaye hapendi kitu chochote kuhusu yeye na kutamani ingekuwa vile na vile kama wengine.
Ni mwanamke kutamani muda wote angekuwa Fulani au angekuwa mtu mwingine.
Ni mwanamke anayejisikia hapendwi na hapendi mtu na matokeo yake anafunikwa na huzuni na upweke.

Ni mwanamke anayejisikia moyoni yupo empty hasa kwa kukosa upendo wa kweli.
Ni mwanamke ambaye anahisi wanawake ambao mume wake anaongea nao ni wazuri kuliko yeye hivyo wanaweza kumchukua au kutembea naye.
Ni mwanamke anayesubiri kuwe kweusi aanze kutoa machozi mazito kwa kujihurumia kwa hali aliyonayo na amefunikwa na msongo wa mawazo.
Ni mwanamke anayejiangalia kwenye kioo na kujiona hafai na kutamani sura yake ingekuwa kama ya fulani au angekuwa kijana zaidi.
Ni mwanamke anayejiangalia mwili wake na kujiona amenenepa na kwamba hakuna mtu atampenda tena na kwamba maisha yake ya kimapenzi na mumewe mwisho kwa kuwa amenenepa mno.
Na mengine mengi yanayofanana na hayo!

Je, low self esteem huwapata wanawake tu?
Kuwa na staha ya chini au ndogo si kwa wanawake tu bali huwapata zaidi wanawake.
Low self esteem ni tishio la dunia nzima hakuna cha motto, kijana mzee, rangi, tamaduni au jamii au kabila wote hukumbana na kuwa na staha ya chini.
Hili dubwana huweza kummeza mtu yeyote pale tu akianza kujisikia hayupo respected na mwingine.

Asilimia 90 ya wazo la low self esteem au low self image hyujengwa kwa kuwaza kuhusu wengine wanavyowaza kuhusu wewe.
Kawaida huwa inakuwa ngumu sana kujiamini mwenyewe kama the rest of the world wanaamini wewe ni dumb, ugly, mvivu, boring, uncreative, undesirable nk.

“No one can stand the awful knowledge that he/she is not needed”

Tutaendelea

Wednesday, October 21, 2009

Marriage is not a noun; it's a verb.
It isn't something you get.
It's something you do.
It's the way you love your partner every day.

Tuesday, October 20, 2009

Usisahau kutaja jina lake!

Mke si barabara asiwe na jina!Tendo la ndoa ni sanaa kama sanaa zingine na hakuna mtu anaweza kukufundisha kwamba unapotaka kuwa mwili mmoja na mke wako au mume wako kitu cha kufanya ni hivi na hivi kwani kila mwanamke ni tofauti na hata huyo mwanamke mmoja anatofautiana kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja kutokana na mzunguko wake.
Hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuwa na skills za kutosha kuhakikisha unamsoma vizuri mke wake na kujua mambo ya msingi kuzingatia wakati wa tendo hili takatifu na lililobarikiwa.
Kwa mfano:
Kwanza kabla ya mambo yote ni jambo la msingi sana wewe mwanaume kuwa clean na umeoga vizuri na unanukia version nzuri inayovutia, hii inatasaidia yeye kuwa na focus zaidi kwa sex kuliko harufu ya ajabu ambayo inatoka kwako, hapa haijalishi una sexual skills au sexual techniques za juu kiasi gani kwani kuwa mchafu na harufu chafu ya mwili ni total turn off.
Pia ni muhimu sana kuwa na mouthwash ambayo inaweza kuua wadudu ambao wanaweza kusababisha ukawa na harufu mbaya sana mdomoni kwani kuwa na clean and fresh breath ni muhimu sana hasa suala la kubusiana.

jambo lingine muhimu ambalo kila mmoja hufahamu na kulipenda ingawa wakati wa foreplay au sexual act husahauliwa ni kukumbuka kumnong’oneza jina lake ukirudiarudia ikiendana sambamba na unavyopumua na huku ukimbusu shingo yake na sehemu zingine ambazozinamsisimua.
Utafiti unaonesha kwamba kila mtu (binadamu) hupenda kusikia jina lake na wanawake hawana exception kwenye hili.
Unapomnong’oneza (taka) jina lake huonesha kwamba upo focused kwake na unamfikiria kuhusu yeye na kile mnafanya na inaweza kuwapa connection (emotionally) na matokeo yeye atajifungua zaidi sexually kiasi ambacho wewe mwenyewe utashangazwa.
Onyo:
Ole wako utaje jina ambalo si lake!
Jambo lingine la msingi ni kwamba foreplay ambayo haihusishi kuchezea matiti (fondling) na kuchezea sehemu ya siri (vaginal area) hujenga njaa na kutamani kuchezewa hayo maeneo kitu ambacho kitamfanya baadae ukigusa huko apate raha zaidi.
Hivyo focus sehemu zingine kwanza na matiti na south pole ni sehemu ya mwisho kwa foreplay.

Mwisho haijalishi anafurahia kiasi gani utaalamu wako na ufundi wako jambo lingine muhimu ni kuhakikisha kunakuwa hakuna routine na inabidi ubadilishe mambo mara kwa mara, chumba kilekile, kitanda kilekile, mwelekeo uleule, saa ile ile, mwanga au giza lilelile, muziki uleule, mlalo uleule huwa inasumbua baada ya muda na inaweza kuzima kabisa moto wako kitandani.
Siku njema!

Sunday, October 18, 2009

Mwanaume anahitaji zaidi!

Kila mmoja anamuhitaji mwenzake!Je, wanaume wanawahitaji wanawake zaidi kuliko wanawake wanavyowahitaji wanaume?

Hili ni swali ambalo si gumu wala si rahisi ila inatokana na mtazamo wa jinsi kila mmoja anavyozifahamu hizi gender mbili.

Wanawake mara nyingi huonekana wanawategemea sana wanaume kuliko wanaume wanavyowategemea sana wanawake.
Na pia mwanamke huonesha kwa uwazi zaidi kwamba anamilikiwa na mwanaume kuliko mwanaume kuonesha mwanamke ndiye anayemmiliki.

Wanawake hupanda kuelekea mafanikio hasa kutokana na kusifiwa (praise) na kutiwa moyo wanakopewa na wale wanaowazunguka.
Wanawake huwa na interest na watu na hupenda kutegemea watu (mwanaume) wakati wanaume huwa na interest na vitu na pia hupenda kujitegemea au kutegemewa.

Mke mara nyingi huhitaji approval kutoka kwa mume, upendo kutoka kwa mume, kutiwa moyo kutoka kwa mume na kupewa attention kutoka kwa mume wakati mwanaume hupenda competition na kwamba kufanikiwa katika kazi au business ndicho kitu kinachompa approval na kujisikia kweli naye ni mwanaume wa uhakika.
Kwa haraka haraka unaweza kufikia conclusion kwamba ni kweli mwanamke anamuhitaji mwanaume zaidi kuliko mwanaume anavyomuhitaji mwanamke?

Je, mwanaume ambaye yupo umri ambao alitakiwa kuwa na mke na familia na anaishi mwenyewe anafaa (fit) katika jamii kuliko mwanamke ambaye alitakiwa kuwa na mume au familia na ainaishi mwenyewe?

Mwanaume na mwanamke waliumbwa kila mmoja kumuhitaji mwenzake na kwamba kila mmoja akiwa mwenyewe hujisikia hajakamilika.

Hata hivyo wanawake hufanya vizuri zaidi bila kuwa na mume kuliko mwanaume kuwa mwenyewe bila mke.
Ingawa hii huonekana ni kinyume kidogo na mtazamo wa jamii nyingi kwani mtazamo wa wengi ni kwamba mwanamke ambaye hajaolewa au anayeishi mwenyewe (single) huonekana ni mtu miserable katika jamii na hafai kitu ambacho si kweli kwani mwanamke single ana mambo mazuri mengi ukilinganisha na mwanaume single.

Ni mara nyingi sana kukuta mwanaume ambaye yupo mwenyewe bila mke wala familia anakuwa mlevi wa kupindukia, anaweza kutumia drugs, anaweza kujihusisha na uhalifu, hata Landlord’s wengi huwa hawapendi kupangisha nyumba kwa mwanaume asiye na mke, hata baadhi ya insurance hugoma.

Wanaume wasio na mke wala familia wengi huendesha magari kwa speed au fujo, wana hasira, pia wanakuwa na risk kubwa ya antisocial behavior na wakati mwingine kipato chao huwa kidogo kwa sababu wanajiona hawana responsibilities na wanaweza kuruka kutoka kazi moja hadi nyingine, who cares? hahahaha!

Pia mwanamke asiye na mume huwa tofauti kutokana na nguvu ya uzazi aliyonayo (uwezo wa kuumba mtoto ambao wanao ndani yao) huwawezesha kuwa tofauti na wanaume linapokuja suala la watoto bila kujali awe mtoto wake wa kuzaa au hapana na hii huwapa uwezo wa kuwa mtu tofauti katika jamii tofauti na mwanaume ambaye anachojua sana ni kusubiri siku bunduki yake itoe askari wake a marine na mtoto azaliwe.

Mwanamke akiolewa na mwanaume kile anafanya ni kuitumia nguvu ya mwanaume (sexual energy) ambayo alikuwa nayo na anaitumia kuunda kupata mtoto na mwanaume hujikuta anakuwa na responsibilities na pia anawajibika katika kulinda na kuipa familia kila inachohitaji na mabadiliko ya aina hii ni muhimu sana kwa jamii na tamaduni zozote ambazo kuna mwanaume na mwanamke.

Ni kweli wanawake wanawahitaji wanaume lakini si kama wanaume wanavyowahitaji wanawake ili dunia iwe mahali bora kuishi.

“One of the saddest creatures on earth is a man without a woman”

Wewe unasemaje?

Saturday, October 17, 2009

Upendeleo kwa mtoto mmoja

Swali:
Nataka kujua zaidi katika malezi ya watoto kuna kitu inaitwa parental favouratism.
Iwapo mtoto mmoja anajisikia kutopendwa sana kama mwenzake au wenzake na wazazi ,inaweza ikamletea athari gani baadae?
Na kwanini wazazi wengine wanakuwa na upendo zaidi kwa mtoto fulani.
Utakuta mwingine mtoto wa baba, mwingine yupo tu.

Jibu
Mzazi mwenzangu asante sana kwa swali zuri.
Ni kweli tabia ya kumpendelea mtoto mmoja au kila mzazi kuwa na mtoto wake ambaye anagusa zaidi moyo wake ipo sana katika familia zetu.
Kuna msemo wa waingereza unaosema “The elephant is in the living room” kwa maana kwamba wengi huwa kulitaja au kuliongelea kwa undani ingawa ni kweli familia nyingi zitakiri kwamba hili ni tatizo sugu na pia inawezekana wewe ni mmoja ya watoto waliopendwa au ambao hawakupendwa na moja ya wazazi wenu.

Kwa nini upendeleo hutokea kwa mtoto mmoja?
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni njema zaidi kuliko wengine, wakipewa kazi mmoja anafanya na mwingine hafanyi mara zote, anayetii hujikuta anapendwa zaidi.
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni rahisi na mwenzake au wenzake ni ngumu.
Inawezekana mtoto anafanana na mzazi zaidi kuliko wengine (tabia na mwonekano).
Inawezekana huyo mtoto anafanikisha matarajio ya wazazi wake au mzazi mmoja.

Inawezekana kwa sababu ni mvulana peke yake au msichana peke yake mzazi hujikuta anampenda zaidi.
Pia inawezekana talents zake au vipaji vyake vinafanana na vile mzazi anataka mtoto awe au inawezekana ndiyo values za familia.
Pia inawezekana mtoto asiyependwa ni mtoto ambaye ni mbishi au ni mtoa hamasa (challenge authority) kuliko mwenzake au wenzake. Mtoto ana njia zake au mitazamo yake kuhusu maisha na vitu hivyo wazazi au mzazi hujikutana wanabishana kila kitu.

Pia kuna mazingira ya kuzaliwa ambayo hufanya mtoto kupendelewa zaidi ya wenzake kama vile mtoto kuzaliwa siku au wakati (huohuo) ambao mzazi wa baba au mama (babu au bibi) yake anafariki, ingawa haina ushahidi wa kisayansi ila matukio mengi huonesha kwamba mtoto wa aina hii huonekana wa thamani kuliko wengine na ni kama vile roho ya babu au bibi huenda kwa mtoto anayezaliwa na wazazi kujikuta wanampenda kuliko kawaida.
Au inaweza kuwa ngumu sana mzazi kuweka bond na huyo mtoto kutokana na huzuni, stress na depression mzazi alipata wakati anazaa na wakati huohuo mzazi wake mwenyewe (baba au mama) naye anafariki.

Mtoto kuzaliwa bila kutegemea hasa baada ya wazazi kudhani wamemaliza kuzaa.
Mtoto kuwa na matatizo ya afya hivyo wazazi kutumia muda mwingi kwake na wengine kujiona mwenzao anapendelewa.
Wakati mwingine inatokea tu mzazi hujikuta anampenda mtoto fulani katika familia kuliko wengine.

Nini mojawapo ya Dalili za mtoto kupendelewa?
Kununuliwa zawadi zaidi ya wenzake.
Kutoa adhabu rahisi kuliko wenzake kwa kosa moja, wenzake wanakula fimbo yeye anaonywa tu.
Sherehe au sikukuu zake kuwa tofauti na wenzake kwa jinsi zinavyoandaliwa nk.
Wenzake wakiomba kitu hichohicho wanakataliwa lakini yeye anapewa au kuruhusiwa.
Mzazi kutumia jina lake kumaanisha watoto wake wote kama vile baba anarudi kazini na watoto hawapo na mtoto anayempenda anaitwa James na badala ya kuuliza watoto wapo wapi yeye anauliza “akina James wako wapi?”
Tumia muda mwingi na mtoto mmoja.
Kuonesha upendo wa dhahiri kwa mtoto mmoja nk nk nk.
Je, mtoto ambaye anajisikia hapendelewi na mzazi au wazazi hujisikiaje?
Mtoto anakuwa na wakati mgumu sana kujikubali na kujipenda mwenyewe kwa kuwa anaamini mzazi/wazazi hawampendi na anaweza kuwa na tatizo sugu la kutojiamini (chronic low self-esteem)
Mtoto hujiona duniani hakuna haki na kwa kuwa hatendewi haki nay eye anaweza kuanza kutowatendea haki wengine kwani “unfairness begets unfairness”

Je, mtoto anayependwa anaweza kupata madhara yoyote?
Ukweli ni kwamba hata mtoto ambaye anajiona anapendwa pia anaweza kupata tatizo la kukosa kujiamini kwani anakuwa too much spoiled.
Kwa kuwa anapendwa basi atajitahidi kufanya zaidi kwani anaamini asipofanya kila kitu juu anaweza kupoteza kuendelea kupata upendeleo hivyo kama ni shule atajitahidi kupata grades za juu, kama ni tabia atajitahidi asikasirike nk na matokeo yake atakuwa hajiamini na anaweza kupota msongo mawazo.

Mtoto anayependelewa anaweza kuwa si mzuri sana linapokuja suala la wenzake wa rika moja au walimu au watu wengine kwenye maisha kwani kile kitendo cha kujiona anapendelewa na wazazi au mzazi humpa kakiburi Fulani.

Mtoto anayependwa hujiona yeye ndo mzuri na huwa hakosei hata hivyo maisha hayako hivyo na matokeo yake atakuwa na wakati mgumu mbele ya maisha hasa llikija suala la kupambana na matatizo.

Hasara ya kumpendelea mtoto mmoja huendelea hadi kwa wajukuu na inaweza kuleta matatizo na migogoro kwa kuwa wajukuu wa watoto wote huanza kuzozana kwa kuwa mmoja wa wazazi wao alikuwa anapendwa zaidi na babu au bibi.


Je, kwa mume na mke ni tatizo?
Ndiyo kunaweza kutokea mgogoro kati ya mke na mume hasa kwa mtoto mmoja kupendelewa na mzazi mmoja, kwa mfano baba anampa fedha nyingi zaidi mtoto mmoja anayempenda bila kujali ni mdogo kuliko wenzake, mama akiona au kusikia naye huja juuu kitendo ambacho kitafanya ndoa iwe katika mzozo.

Je, unaweza kuepuka vipi kumpendelea mtoto mmoja?
Kwanza wewe mzazi jikubali kwamba wewe ni binadamu na kwamba katika watoto wako mmoja anakubalika kwako zaidi kuliko wengine.
Wasikilize watoto wengine ambao wanakwambia unampendelea mwenzao na usijilinde, wasikilize na anza kufanyia kazi yale wanasema (kuacha kumpendelea mmoja)

Gundua utofauti wa kila mtoto na kile anapenda kufanya (characteristics, skills, interest) na mhudumie kutokana na vile anavipenda.

Usiwalinganishe au kumsema mmoja kwa sababu ya mwingine kwani kila mtoto yupo tofauti, sentensi kama “mwenzako James akirudi shule anafanya homework yake vizuri na animalize wewe hadi ulazimishwe!”
Ni kweli amekosea hata hivyo kila mtoto yupo tofauti na kila mtoto anatakiwa kuambiwa kama yeye na si mwingine.
Kama unanunua zawadi ni vizuri kununua zawadi zinazolingana siyo mmoja unanunua zawadi ya Tsh. 100,000 na mwingine Tsh. 20,000
Tumia muda vizuri na sawa kwa watoto wote.

Kumbuka jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo utakuwa na kibarua kigumu zaidi, kwani unahitaji kutafuta muda maalumu kwa kila mtoto na kugundua kipaji chake na kuhakikisha unakiendeleza sawa na watoto wengine.

Jambo la msingi ni kila mzazi kumpa (treat) kila mtoto sawa katika hali zote na juhudi za ziada zinahitaji katika mazingira ya nyumbani kuhakikisha watoto wote wanalelewa sawa na kila mmoja kujiona ana thamani sawa kwa wazazi mmoja mmoja na kwa pamoja.

Thursday, October 15, 2009

Tunatofautiana muda!

Wanaume wengi huamini kwamba jinsi wao walivyo tayari kwa tendo la ndoa na jinsi wanavyohitaji tendo la ndoa basi na mwanamke naye yupo hivyo.

Kama tulivyoangalia huko nyuma, mwanamke na mwanaume wana system tofauti linapokuja suala la sex na mapenzi kwa ujumla.
Haina maana kwamba mwanaume akiwa tayari maana yake mwanamke naye yupo tayari na hili ni tatizo moja kubwa sana ambalo wanaume wengi huwa hawalioni.

Hata kama kuna direct route ambayo mwanamke akiandaliwa vizuri anaweza kuwa tayari hadi kufika kileleni bado anahitaji dakika 20 wakati mwanaume huhitaji dakika 2 tu.
Maandalizi kwa ajili ya tendo la ndoa kwa mwanamke si luxury bali ni hitaji muhimu (need/necessity)

Kama ni mwanaume unayejali basi kuanzia leo ni muhimu kuongeza dakika 15 kumuandaa mke wako.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

Wednesday, October 14, 2009

Inashangaza mno!

Training: How to cuddle
http://www.oc-cuddle.com Wanaume wengi huwa hawaoni umuhimu wa kuwabembeleza wake zao kwa kuwakumbatia, pakata (cuddle, hold, touch), busu, shikashika nk) baada ya ya sex.
Kibaolojia mwanaume akimaliza sex anarudi kwenye hatua yake ya kawaida (pre- aroused state) na mwanamke akimaliza sex (baada ya kufika kileleni) huwa anarudi katika yali ya kuwa nusu yaani semi- aroused state) yaani kwake bado moto upo na anaweza kupika tena chakula hahahaha!

Hii ina maana kwamba mwanaume akimaliza tendo la ndoa anakuwa ameishiwa nguvu (total system shut down/crashing) au anaenda ICU kwa matibabu ya karibu, hajiwezi wengine ndo huishia kukoroma kiasi kwamba hata vibaka hawawezi kuingia hiyo nyumba, wakati huohuo wanawake wao wakimaliza bado huhitaji kuendelea na tendo la ndoa zaidi na zaidi na kwao cuddling ni kuwapa connection na wakati mwingine kuwa na sex tena na tena.

Hivyo ili mwanamke asiamini kwamba mwanaume huna feelings kama jiwe (stone), inakupasa wewe mwanaume baada ya kumaliza sex fanya hitimisho (conclusion) kwa kuendelea kumkumbatia, busu na kumpa maneno matamu ya sifa na kimapenzi, kumbuka ni mkeo hivyo mpe kila anastahili na utaona mabadiliko.

Pia wanawake wengi wanashangaa kwa nini mwanaume anaweza kutenganisha sex na love (tafsiri kwa Kiswahili mwennyewe)
Wakati wa sex wanawake huzalisha kiwango kikubwa sana cha homoni ya oxytocin ambayo husaidia kuwasisimua katika emotions zao na wanakuwa connected na mume wake wakati wa sex na hii husababisha mwanamke kujihusanisha (integrate) sex na emotions (love).
Wanaume hawazalishi na kama yupo anayezalisha hiyo momoni basi ni kiwango kidogo sana kiasi kwamba kwake sex na love ni vitu viwili tofauti.
Ndiyo maana ni rahisi kwa mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke ambaye hampendi na kwa mwanamke ni ngumu kwani mwanamke upendo kwanza ndipo huwa tayari kwa sex.
Mume ambaye hamjali mke, hampendi, hampi sifa kwa yale mke anafanya na kumkosesha upendo atajikuta kila siku anaomba sex na amke akijitetea kichwa kinauma.

Usikimbie tatizo!

Dunia tunayoishi huwezi kukwepa kukutana na tatizo au shida au mkwara au majaribu au mateso au ugumu wa maisha eneo lolote.
Hata hivyo linapokuja suala la ndoa au mahusiano kuna njia mbili tu za kukabiliana na hayo yote hata kama ndoa yako inahisi ni mbaya, hairidhishi au ambayo ndani hakuna kuelewana au unaona kabisa ni kweli inaelekea kwenye shimo.

Njia ya kwanza ni kuachana kabisa kutafuta jibu (IGNORE) na njia ya pili ni kukabiliana na tatizo lililopo hadi kuhakikisha unapata jibu (FOCUS).

Hata katika maisha ya hapa duniani njia ni mbili tu, wapo watu wakikutana na matatizo au shida huamua kukimbia au kuruka au kurudi nyuma au kukwepa na kwenda zao na wengine hukabiliana nayo uso kwa uso hadi kieleweke yaani hawa kama wameokaka basi huamua kufia kwenye maombi. (Anyway kabla hujaishiwa nguvu Mungu huwa anakuwa ameshajibu!)

Ukweli kukimbia tatizo kuna raha yake (raha ya muda) kwani kuna ahueni (relief) ambayo mtu hupata hata hivyo habari mbaya ni kwamba mwisho wa yote ni maumivu makali na kujuta.

Na wale wanaoamua kukabiliana hujikuta katika maumivu makali mwanzoni na mwisho wake ni ahaueni na kupata nafuu ya kudumu au kula kuku kwa mrija hata hivyo hapo kunahitajika imani na kuwa na imani ndipo kwenye tatizo kwani wengi imani huwaota mabawa mapema sana.

Fikiria unaumwa tumbo na unapokumbuka gharama za vipimo pamoja na shughuli nzima ya kumuona daktari unaamua kuachana nalo.
Ukweli ni kwamba maumivu ya tumbo yataendelea kwani ni dalili kwamba afya yako katika tumbo haipo sawa na dawa ni daktari kuchukua vipimo hata kama utatumia gharama na ajue tatizo la tumbo lako ni nini na zaidi akupe tiba kamili mapema.

Tumbo haliwezi kupona kwa sababu umeachana nalo kwani maumivu yataongezeka na gharama ya vipimo na kutibu itakuwa zaidi kwani unapokimbia (achana nalo) tatizo linalizidi kuwa kubwa badala ya kumalizika.

Kumbuka ndoa yako ni mfano wa tumbo pale likianza kuuma, fahamu unahitaji kufanyia uchunguzi na vipimo na hatimaye kupata dawa inayotakiwa.
Inawezekana unapita katika ndoa yeny uchungu na maumivu makali na unawaza kwamba kuachana na mume au mke ndo dawa.
Ukweli si dawa dawa ni kupiga magoti na kumuomba Mungu akupe hekima na kukabiliana na tatizo lililopo.
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
Ubarikiwe na Bwana!

Friday, October 9, 2009

Ni bubu!

Swali.
Mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa na nina miaka 5 kwenye ndoa yetu, Mume wangu huwa kimya (bubu) wakati wote tunapofanya tendo la ndoa.
Hata mimi sasa nimejikuta nakuwa mkimywa kwani kumnong’oneza maneno matamu mtu ambaye hata hana response inaumiza sana.
Napenda kujua tatizo lake ni nini?

Jibu
Dada muuliza swali,
Binafsi nafikiri hakuna tatizo kwa mume wako kuwa bubu wakati wa kuwa mwili mmoja.
Wapo watu wengi wana hiyo style ya kuwa silent wakati wa sex (silent style).

Ukweli huwa wanakuwa wamesisimuliwa na wanajisikia kushukuru au kusifia na wanathamini sana kile partners wao wanawafanyia (appreciate) ila wanashindwa kuongea kwa maneno.

Labda huwa wanajisikia kuongea maneno kunawasumbua au kunawapunguzia au kunawafanya kupoteza ladha au utamu wa tendo lenye (sensation/pleasure) sina maana wale wanaopiga yowe au kuguna kimahaba au kelele hadi majirani hawalali huwa hawapati raha, kila mtu ameumbwa tofauti.

Angekuwa huwa analala kama gogo tu na hajishughulishi kwa lolote kweli hapo kungekuwa kuna tatizo ila kama unaona mwendo (movement/thrusting) wake si kawaida (mzuri), kuhema kwake si kawaida, mapigo ya moyo si kawaida na stick yake imesimama kwa muda ambao unakufanya uridhike, ukweli mshukuru sana badala ya kumlaumu na kuona ni tatizo.

Au niseme kama kuna tatizo basi tatizo lenyewe ni kwamba wewe style yako ni ile ya kuongea (non silent style) na yeye ni ile ya mabubu (silent style) na hii ndo inafanya wewe ujisikie vibaya.
Na kwamba anapokuwa bubu anakufanya wewe ujisikie huthaminiwi kwa kile unafanya kwani kwako sex ni nzuri pale kukiwa na ukelele, kukiwa na kuongea maneno au kunong’onezana vimaneno vya kimahaba au sweet nothings.

Ili kuondokana na hili tatizo ni muhimu kwako kuangalia signs za asili ambazo mume wako anazitoa kwako (silent style) kuliko kuangalia signs zako za asilia ili kufahamu kwamba anakuthamani (non silent style).

Pia kama inawezekana kaa naye kwa upendo na ongea naye, mweleze jinsi unavyomfurahia na kwamba utafurahi zaidi kama atakuwa anaongea wakati wa kuwa mwili mmoja hasa kutokana na maswali unayomuuliza ingawa kutokana na raha anayopata anaweza akawa bubu, hivyo vumilia kwani kwake ni kitu kipya anachojifunza haitatokea over one night.
Pia inatakiwa uwe na mazoezi ya kuongea naye issue za chumbani pamoja wote mkiwa huru kwani inaonesha kwamba kwenu kuongea masuala ya sex ni kazi kwelikweli.

Siku njema na weekend njema!

Thursday, October 8, 2009

Wanafaa sana!

Je, umechoka kusikia kuhusiana na tofauti kati ya mwanamke na mwanaume?
Ni kweli mwanaume na mwanamke wapo tofauti sana na hakuna mjadala kuhusu hili.
Wote mwanaume na mwanaume wanatabia ambazo ni negative na positive, hebu tuangalie sifa positive za mwanamke na mwanaume.

Kwanza wanawake!
Wanawake ni wanajali (caring) na wanajua kupenda (loving),
Wanawake hutoa machozi hata wakiwa na furaha,
Wanawake hufanya hata vitu vidogo vidogo kuonesha wanajali,
Wanawake huweza kusimama mahali popote kwa ajili ya kitu kile wanaamini ni the best kwa watoto wao.
Wanawake wanauwezo wa kutabasamu hata kama wamechoka, hawawezi kujizuia.


Wanajua jinsi ya kubadilisha mlo wa wa kwaida na kuwa special kwa occasion yoyote.
Wanajua jinsi ya kumfariji rafiki au mtu ambaye anaumwa.
Wanawake huleta kicheko na furaha duniani.
Wanajua jinsi wa kumliwaza mtoto kwa msaaa mengi mengi mengi mengi.
Wanawake wengi ni wakweli na watiifu.
Wanawake wengi hujikuta wanatoa machozi wakikutana na kukosa haki yao.
Wanawake wanajua jinsi ya kufanya mwanaume ajisikia ni king.
Wanaweza kwenda extra mile kumsaidia rafiki yao.
Wanawake wanawezesha dunia kuwa mahali bora kuishi.

Je, wanaume sifa muhimu ni ipi?
Wanaume wanajua kunyanyua vitu vizito na kuua spiders.

Today's Quote!
The saddest organism on earth is the unmarried man!

Wednesday, October 7, 2009

Chunga sana........ Fedha!

Linapokuaja sula la fedha, kwa ndoa mpya wakati mwingine fedha ni kama mtungi wa gas ambao unasubiri kushika moto na kuwaka siku mambo yakiwa ovyo.
Kwenye ndoa linapokuwa suala la pesa mara nyingi mambo makubwa yanayotokea na kusababisha matatizo ni kufanya makosa yanayohusu pesa (maamuzi), bills kubwa (hasa nchi za magharibi) na madeni hasa banks.
Kwa mfano!
James na Jane (as usual) baada ya kuoana wakaamua kununua nyumba mpya kwa (mortgage), nunua fanicha mpya na vifaa vingine vya ndani kwa mkopo, wakaamua kuweka madirisha na milango mipya yote kwa kukopa pesa bank pia wakaamua kujenga garage mpya kwa ajili ya kuhifadhi gari lao na kuweka fence kuzunguka nyumba vyote kwa mkopo.

James anafanya kazi na mkewe Jane naye anafanya kazi na kutokana na plan zao kila kitu kilikuwa shwari ingawa ili kulipa kila kitu ilimpasa James kuongeza kazi siku za weekend na muda wa ziada kila jioni (parttime) pia ili kuhakikisha baada ya mapato yote angalau wanabakiwa na kiasi kidogo cha fedha bada ya kulipa bills zote na madeni ya bank.

James huondoka kazini saa kumi na mbili asubuhi na kurudi saa tano na nusu usiku siku saba kwa wiki miezi 12 kwa mwaka.
Jane naye anapata mimba na kuzaa mtoto na inampasa Jane kuacha kazi pia mtoto naye akaja na pressure zake za matumizi ya pesa.
Sasa kipato kimepungua na loans zipo palepale.

Mama yupo busy na mtoto na anachoka, pia kazi za pale nyumbani list haiishi na ukifika usiku analala bila hoi na baba ndo yupo busy na kazi kwani sasa inabidi ahangaike kuhakikisha bills zote zinalipwa, nyumba, fanicha, fence, garage nk.
Ukweli ni kwamba James anarudi nyumbani kwa ajili ya kuoga, kulala na kuvaa na kuondoka asubuhi kumi na mbili na kurudi usiku saa tano na nusu amechoka na anaishia kwenda pangoni.
Jane anajikuta mpweke na disconnected na mume wake James na hakuna mapenzi tena. Nyumba nzuri lakini haina raha na hawaifaidi kwa chochote kwani bila kufanya kazi hawezi kulipa madeni yote.
Kazi kubwa ambayo James anafanya ni kumtumikia pesa kwa nguvu zote, akili zote na mawazo yote ili kila kitu kiende, hatakiwi kuugua wala kuwa na likizo maana akikosa pesa vitu vyako vyote anapoteza kwani alinunua kwa mikopo.
Mapenzi hakuna, furaha hakuna, kupumzika hakuna na muda wa pamoja kama mke na mume hakuna kisa ni kuwa na pesa ili kulipa madeni yote na hatimaye mwisho wa mwezi ufike.
Tatizo si kutokuwa waaminifu kwa pesa zao bali ni mismanagement na maamuzi mabaya bila kufikiria mbali.
Kumbuka maisha tunaishi sasa na si baadae, mawazo kwamba tujifunge mkanda tutafaidi baadae kwanza tuwekeze inabidi kubalance kwani utafaidi kitu gani baada ya kuwa mzee, uzee ni wakati wa kutoa wosia kwa wajukuu.
Ua utafaidi kitu gani kama utapoteza mke au mume au familia ambayo kwako ni kitu cha thamani.
Issue hapa ni kuwa makini si kukopa bank ili uwe na vitu vya msingi katika maisha yako.
Issue ni kuwa na muda wa kazi, mume, mke au familia na kufurahia maisha.

Hivyo kabla ya kufanya jambo lolote fikiria kwa makini.

Tuesday, October 6, 2009

Fikiri kwanza!

Wengine hulia usiku kucha! Inakuwaje watu wawili waliopendana deep idara zote inafika siku wanakuwa baridi na wanajiona ni watu wawili tofauti kabisa kwenye ndoa yao?


Kuna mambo mengi sana husababisha kuanzia na yale yaliyo ndani ya ndoa yao na yale yaliyo nje ya ndoa yao hata hivyo ukweli love is so terrible and is so important, kuna wakati mwingine mpenzi (mke au mume) anaweza kukupa au kukunulia gari au kukujengea nyumba ya uhakika lakini bado ikawa haina maana kama hatatimiza mambo ya msingi kuhusiana na upendo wake kwako.


Ndiyo unakuja ule usemi
“Buying very expensive gifts doesn’t make woman happy but real love and affections”


Kuna aina tofauti za migogoro na jinsi ya kukabiliana nayo, wengine mgogoro ukizuka hata majirani wanajua leo kuna vita kati ya Mr James na Mrs wake (Jane) [siyo majina halisi] na baada ya muda wanarudi kwenye mstari. Wengine vita vyao huwa slow, kimya kimya, hakuna kelele ni cold war na kila mmoja huanza mbali na mwenzake kihisia, kiroho na kimwili polepole ila matokeo yake ni hatari tupu.


Kama ni mwanandoa mpya ni vizuri kuwa makini katika maamuzi mbalimbali mnayofanya na kufikiria kwa makini huku ukiangalia zaidi ya miaka 5 ijayo, kwa mfano;


James na Jane wameamua baada ya kuoana tu wanazaa mtoto haraka iwezekanavyo kwa kuwa kila mmoja ana kazi hivyo shida ipo wapi kama pesa zipo. (Ingawa ukweli pesa huwa hazitatui matatizo yote)

Hata hivyo uamuzi wa kuwa na mtoto haraka kabla hawajajuana vizuri na kufikia mahali wakawa wanafahamiana tofauti na uchumba ni jambo la msingi. (siyo lazima ukubali huu ushauri kwani inatokana mmejuana kiasi gani na mchumba wako)

Kuna watoto wakizaliwa huja na package ambayo mzazi hulali kama vile kulia (cry) muda wote na mke kumtumikia huyo mtoto all the time (cha ile ya kumaliza madaktari wote kujua kwa nini mtoto analia usiku mzima na wanakwambia hakuna tatizo) na kufikia mahali mume akawekwa pembeni kwani mtoto kwanza na wakati huohuo ndoa bado changa.

Mke hujikuta mtoto anamuhitaji na mume anamuhitaji na hawawezi kubalance kwani bado ni mgeni na hii institution.


Watoto wengine huwa na matatizo ya kula, kiasi kwamba mama hujikuta hawezi hata kumwachia mtu yeyote amtunzie mtoto na matokeo yake mama hujikuta muda wote anatumikia mtoto na wakati mwingine kuacha kazi (ajira) na pia mume kuwekwa pembeni.


Matokeo yake wanandoa hujikuta wanakuwa mbali na feelings kufa na kila mmoja anaanza kuona ndoa hairidhishi wakati hata miaka 2 haijamaliza.


Jambo la msingi ni mwanamke kufahamu vizuri aina ya mume uliyenaye kwani kuna wanaume ambao wanaweza kuwa baba na kuna wengine ni kazi, wanaendana na usemi kwamba:


“Men don’t become fathers overnight, where as women have strong maternal instinct in them”
Suala la kule mtoto linahitaji mke na mume wote kushirikiana kuhakikisha si mmoja ndiye anakuwa na mzigo zaidi.


Sunday, October 4, 2009

Wanagombana baada ya kuoana!

Kwa nini kugombana?
Mahusiano ni kitu special na maalumu na wakati mwingine hushangaza sana.
Hivi inakuwakeje wapenzi wengi hugombana baada ya kuoana tu?
Ni mara chache sana kuwaona wachuma wakigombana.

Issue hapa ni kwa nini watu hugombana (arguments/ fighting) baada ya kuoana na wakati kabla ya kuoana kila mtu alikuwa anamuelewa mwenzake hadi wakafikia hatua kukubaliana kuoana na wakioana tu mambo huanza, yaliyojificha huanza kuwekwa juu ya meza?
Ukiangalia kwa undani sana utakuta kwamba kabla ya kuoana mambo mengi unafanya ni hiari (voluntary) na baada ya kuoana ni wajibu (compulsory).

Kabla ya kuoana una options (upo open) kwa maana kwamba unaweza kujitoa au kuendelea naye na baada ya kuoana hakuna options, mwisho wa reli, closed end, no exit, hakuna njia, dead end, unafungwa kwenye box hakuna kutoka. Upo hapo?

Pia kabla ya kuoa wengi huwa hawawi 100% honest, kila anachofanya kwa mchumba ni kizuri kwani uchumba huhusicha social activities na rtomantic interest, so wengi hufungana kamba kwamba everything is ok, hata kama hapendi au anaona kina bore bado atajifanya anakipenda ana hakuna shida. Mkioana hakuna kufungana kamba wala kufurahishana ni task oriented institution na deep sharing ya kila kitu na ni real life na kazi.
Mfano:
James amependana na Jane (siyo ya majina halisi) na ni wachumba ambao si muda mrefu watafunga ndoa kuwa mke na mume.
James anapenda sana kwenda kutazama Soka National Stadium, imefika siku Yanga na Simba wana mechi na James hawezi kukosa anamwambia mchumba wake leo naenda kutazama mechi Yanga na Simba wanacheza je tunaweza kwenda?
Jane hapendi ila kumfurahisha mchumba wake anakuali waende na tiketi zinakwatwa wanaenda, wanafurahi na Jane anashangilia mchezo bega kwa bega na mpenzi wake James.

Wiki inayofuata Jane anajiunga na kwaya kanisani na anamuomba awe anamsindikiza kwaya na ikiwezekana wakimaliza anamtudisha nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa James anataka kuonesha anajali (caring) hana shida yupo tayari kukoda hata Tax mpenzi awahi kwanya church au akimaliza kwaya aende nyumbani salama (moyoni James hapendi kwaya anampenda jane tu na anafanya ili Jane afurahi).

Baada ya kuoana, kuna mechi ya Yanga na Simba na James anamuomba Jane waende kutazama mechi (unajua wanaume tuna nerves nyingi kuhusu Sports, ni ugonjwa wetu), Jane anakataa kata na kutoa sababu kwamba hapendi kwenda kupoteza muda kwa kuangalia Yanga na Simba wakati ana mambo ya msingi ya kufanya.
James anashangaa kwani kabla ya kuoana alisema anapenda. Anaoana amedanganywa.

Wiki inayofuata James anaombwa na mke wake Jane amsindikize kanisani kuimba kwaya, James anakataa kwa madai kwamba ana kazi za msingi sana kulikon kwenda kumsindikiza mkewe kwaya na hata hivyo si anaweza kwenda mwenyewe na kurudi kwani kwaya si huduma yake (James anajitetea). Mke wake naye anashangaa inakuwaje kabla ya kuoana alikuwa ananisindikiza hata kunitafutia tax ili niende na kurudi salama leo inakuwaje?
Je, wewe hujawahi kuwa James au Jane katika mahusiano yako?
Orodha ya mambo huendelea na inafika mahali kila mmoja anajiona kama amedanganywa kwani Yule alitegemea amebadilika hapo frustration na disappointments huanza na migogoro huanza na kama wajinga wote kunaanza disconnection ya emotions kimwili na kiroho.
Hapa mmoja anajisikia hasikilizwi not understood, valued, loved au appreciated, kila mmoja anapenda mwenzi wake amsikilize, amwelewe na ampe thamani ya kila anafanya.
Kila mmoja anajiona mwenzake hawezi msukumo wa kutosha kuhusu Mahusiano yao na kwamba yeye si kipaumbele tena ndipo closeness huanza kupotea.

Ukweli ni kwamba disagreement ni part of marriage, huwezi kukwepa muhimu ni kuzingatia kwamba unahitaji kuwa
Positive,
Fanya kila kitu katika wakati wake,
Uwe unachunga mdomo wako,
Usibishane au kugombana na spouse wako mbele ya public,
Ukikosa kubali na omba msamaha na wote kusameheana na kusahau
Zaidi mawasiliano ni muhimu sana.
Usimlaumu mwenzako badala yake fahamu kwamba sasa unaishi kwenye realm life hivyo changamka na mpende Zaidi ikiwezekana Fanya yale ulikuwa unafanya hata kabla hamjaoana, simple!

Soma Epheso 4:25 32

Saturday, October 3, 2009

... Yanawachanganya sana wanaume!

Wengine wanayaita "Watermelon"Ingawa matiti ni kwa ajili ya chakula cha mtoto mchanga, baba ndiye hujikuta mara zote anaishia kuchezea kama mali zake na pia wapo wanawake wengi sasa ambao hawataki kunyonyesha kabisa watoto ili kulinda matiti yao yabaki umbo lilelile ambalo wanaume wanatawafurahia virtually.
Titi ni jug la asili la maziwa ya motto ingawa huja katika size na shape tofauti na huvalishwa bra kwa design tofauti kwa gharama toauti kutokana na hadhi ya mwanamke wakati sehemu zingine duniani mwanamke hutembea kufua wazi bila tatizo.
Matiti yamekuwa yakipewa heshima (kuabudiwa na kushabikiwa) tangu enzi za zamani hata hivyo attention ambayo matiti yanapewa leo hii (information society) inashangaza na imefika mahali wanawake (hasa mabinti) wanatumia pesa nyingi ili kufanyia upasuaji kuwa na umbo ambalo wanaume wengi husherehekea wakiyaona.
Matiti yamepewa majina mbalimbali na jamii tofauti kama vile Nido, Mtindi, Jugs, Apples, Balloons, Bean bags, Boobies, Boobs, Bullets, Glands, grapefruits, quaver, hand-warmer, Hills, Headers, Lulus, Mams, Mangoes, Meatballs, Meat loaves, Melons, Milk cans, Milk shop, Mountains, Nature’s fonts, Ninnies, Nuts, Oranges, pair. Papaya, pears, Pillows, Pumpkins, Rib cushions, Sandbags, Sphere, shakers, Upper deck, Warheads, Watermelons, Yams na mengine mengi unayojua wewe.
Swali bado ni kwa nini wanaume huchanganywa sana na matiti?
Kwanza matiti huwafanya wanaume kujisikia utulivu, kuburudika, kuliwazwa, kulegezwa, kustarehe, kupoa, kupozwa, kupumzishwa na kujisikia shwari (calmness) kutokana na ulimwengu chepe, korofi, unaokwaruza na rafu, hivyo kwa matiti kuwa soft; yanayokarirbisha na hayatishi, mwanaume hujisikia yupo salama (Naongelea mke na mume hahahaha!)
Kwani tangu mwanaume akiwa mtoto, ikitokea kuna hatari au kitu chochote ambacho kinamtisha na hata kuanza kulia, alikimbia kifuani kwa mama yake kunyonya titi na kunyamaza hivyo kulindwa na kile kinachomuumiza au kukutana na ubaya wowote.

Pili matiti ni alama (symbol) ya uzazi kwa mwanamke hivyo matiti hutoa dalili kwamba huyu mwanamke anauwezo wa kuzaa na kuendeleza kizazi, kwani huwezi kukutana na msichana ambaye hajabalehe na ana NIDO za uhakika bali akishabalehe huwa na matiti ya uhakikika kuonesha yupo tayari kuzaa au kuwa na uzazi (not all the time).

Kutokana na maelezo ya Charles Darwin (Natural Selection) mwanaume hujikuta anatumia kigezo cha matiti kuchagua partner ambaye ana matiti umbo fulani bila yeye kujua, kumbe ni kuchagua partner mwenye afya na mwenye uwezo wa kuzaa.
Kutokana na maelezo ya bwana Darwn, wanaume hutiwa na kuchanganyikiwa kabisa na matiti sharp kwani ni dalili kwamba huyo mwanamke anauwezo wa kuendeleza species yao.
Tatu matiti ni ufunguo (key) kwa mwanamke kusisimka kimapenzi.
Muulize mwanaume yeyote ambaye ni mzuri kimapenzi (good lover) atakwambia kwamba matiti yana direct connection na msingi wa mwanamke kusisimka kimapenzi (libidinal zones), hivyo mwanaume anapenda matiti na anachanganyikiwa nayo kwa sababu yanaweza kumsisimua mke wake vizuri na kuwa tayari kuwa mwili mmoja.
Kwa hiyo moja ya Home Entertainment Center ya mwanaume ni matiti ya mkewe so mwanamke anayejua siri huhakikisha mume anaitumia hiyo hardware.
Nne matiti husisimua wanaume visually kwani wanaume husisimka kwa kile wanaona, matiti yaliyosimama (shape, A class) husisimua zaidi na kutoa attention kubwa kwa mwanaume, ukiacha genitals, pia matiti ni moja ya physical feature ambayo inamtambulisha mwanamke na kumvutia mwanaume (attraction).

Tano, mwanaume huchanganyikiwa na matiti kwa sababu ya msukumo wa jamii.
Kwani ni binadamu peke yao (katika wanyama wote) ambaye hutumia matiti (fondling) ili kusisimuana kimapenzi.
Magazeti, Televisions, mamodel, Catalogs, matangazo ya biashara, fashions, movies, films yote ni source ya kutangaza uzuri wa mwanamke na matiti 24/7 katika siku 365 za mwaka, mwanaume anayekutana macho kwa macho ya vyote hivi kwa nini asichanganyiwe akiona kifua cha mwanamke ndiyo maana mara nyingi wanaume wanapoongea na mwanamke huangalia kifuani badala ya usoni kwa mwanamke!
Swali la kujiuliza hivi ingekuwaje kama matiti yangekuwa hayafunikwi?
Kama masikio au pua au shingo au lips yangepata attention kama yanavyofichwa?

Binadamu ana sifa moja kubwa ya kutaka kupata kile kimefichwa;
je hii inaweza kuwa proved?
Na je, ni kweli wanaume wanastahili kulaumiwa kwa kuwa attracted na matiti ya mwanamke yeyote?
Je, matiti ni sifa muhimu kwa mwanaume kuzingatia wakati wa kuoa hasa kutokana na msukumo wa jamii, saikolojia na mvuto kimwili ili aoe mke ambaye matiti yake yatamfanya mwanaume ayasherehekee na kuyafurahia?

Namtafuta Mwezi, kipi nizingatie?

Kaka Mbilinyi,
Mimi ni kijana wa kiume wa miaka 25 nimeokoka nampenda Yesu na naamini nipo tayari kutafuta mchumba awe mke wangu.
Je, ni mambo gani muhimu kuzingatia wakati natafuta mwenzi wangu?
Ubarikiwe na Bwana
HB

Kaka HB,
Asante sana kwa swali zuri sana na hongera sana kwa uamuzi wako wa kutafuta mwenzi wa kuishi na wewe maisha yako yote hapa duniani.
Jambo la msingi ni kwamba uamuzi wa kwanza ambao ni muhimu sana duniani ni uamuzi wa kuukubali wokovu au kuukataa na uamuzi wa pili ni kuchagua mke au mke utakayeoana naye.

Ndoa ni moja ya vitu vizuri na vyenye Baraka kubwa sana katika maisha na pia ni moja ya vitu ambavyo husababisha majuto na masikitiko makubwa sana hasa kwa wale ambao huchagua mwenzi carelessly.

Katika maeneo yote ya maisha yetu, Mungu ndiye anayetuongoza na kutusaidia kupata mwenzi (ubavu) ambaye anatufaa pale tunamtegemea yeye na kukubali mapenzi yake kwetu (Mithali 3:5).
Hivyo kwa kuwa wewe unaamini (umeokoka) ni muhimu kuoana na Yule ambaye naye anaamini (ameokoka) si Yule tu anayesema mkristo bali Yule ambaye maisha yake yanaonesha kweli ameokoka (long term Christian behavior)

Usiongozwe na emotions zako, kuna wakati unaweza kudhani umempenda kumbe ni maluweluwe tu (infatuation) ambayo kama hupo makini unaweza kudhani ni upendio wa kweli kumbe la.
Upendo wa kweli ni kitu ambacho unakuwa na commitment na kujitoa sadaka kwa ajili hiyo. Hii ina maana kwamba katika udhaifu unaouona kwake ni wewe tu duniani unaweza kumchukulia na ni sababu ya kumuona anakufaa (sizungumzia vitu kama uchafu, uchoyo, nk) bali vitu kama ufupi wake au weusi wake au kipara chake.

Usioe kwa kuangalia mwonekano tu, au umbo lake au kwa sababu ya uwingi wa vitu alivyonayo, ni wajinga tu ndo hutumia hivyo vigezo walio na hekima na busara huangalia vile vilivyo moyoni siyo nje na ukimuomba Mungu atakupa Yule ambaye utaridhika kuanzia ndani hadi nje kwani kuna kila aina wa wanaume na wanawake wazuri yeyote anaweza kuwa nao ndani ya Yesu na maombi yanaweza kufanya chochote Mungu anaweza kufanya kwako.

Kabla hujafanya chochote piga hesabu za gharama kwanza (kumbuka habari za kutaka kujenga mnara(Luka 14:28).
Kwa kuwa ndoa ni hadi kifo (ukiingia hutoki hadi mmoja afe -1 Cor. 7:39), itakuwa maisha yako yote kutoa na kupokea, kushirikiana na kukubaliana, je upo tayari kutoa hiyo sadaka?
Kumbuka ndoa ni kudumu ile katika afya au ugonjwa, katika raha au shida, hakuna kutoka hadi kifo.

Kuoana haraka haraka (faster) si jambo la busara kabisa, wajinga huchumbia na kuoana ndani ya miezi mitatu au sita.
Mfahamu vizuri huyo mke mtarajiwa kwani ni heri kuachana wakati wachumba kuliko kuachana wakati ni mke kitu ambacho hakipo hata kama wengine wanafanya.
(Know the stuff please).
Mwaka mmoja ni wastani wa kawaida kwa watu ambao wapo wanahitaji kujuana vizuri na wale ambao wanapenda kujua mzigo amebeba kama kweli anastahili.
Usioana na yeyote ambaye unaamini ukioana naye utaweza kumbadilisha, ukweli ni kwamba kama ana tabia mbaya sasa basi ukioana naye hiyo tabia mbaya itakuwa maradufu (kwani wewe ni Yesu ndo umbadilishe?) kama hajabadilika kabla hujaoana naye hilo ni tego!
Kila mtu huwa na tabia njema kabla ya kuoana sasa kama anatabia mbaya hata kabla ya kuoana, kama hujui riadha basi………….

Uwe makini jinsi mwenzi wako mtarajiwa anavyowahudumia au anavyojihusisha na ndugu zake kama wazazi, marafiki na watu wote kwa ujumla.
Jinsi mtoto anavyofanya kwa mama yake ndivyo mara nyingi humfanyia mke wake na jinsi binti anavyomfanyia baba yake ndivyo atakavyomfanyia mume wake au mume hutamani mke wake awe kama mama yake na mke hutamani mume wake au kama baba yake so know the trick.

Usiingie kwenye ndoa bila maandalizi ya kutosha au mafundisho (premarital counseling) kutoka kwa mchungaji wako au mtu mzima ambaye ana ufahamu na mambo ya ndoa.

Zaidi unaweza kusoma articles za huko nyuma kuhusu kuchagua mwenzi.

Weekend njema

Friday, October 2, 2009

........ Is Love!

There's nothing you can do that can't be done.
Nothing you can sing that can't be sung.
Nothing you can say but you can learn how to play the game.
It's easy.
There's nothing you can make that can't be made.
No one you can save that can't be saved.
Nothing you can do but you can learn how to be in time.
It's easy.

All you need is love
There’s nothing you can know that isn't known.
Nothing you can see that isn't shown.
Nowhere you can be that isn't where you're meant to be.
It's easy.
All you need is love
The Beatles (John Lennon/Paul McCartney)

Thursday, October 1, 2009

Chunguza kwa makini kwanza!

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.
Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.

Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi (authentic) na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.

Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja (mtanashati) alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.

Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!

Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).

Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja.

Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia (hearing aid). Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa, Guess what!

Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!

Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!