"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, October 1, 2009

Chunguza kwa makini kwanza!

Tunaishi kwenye ulimwengu wa kisasa ambao vitu feki au artificial vimetapakaa kila mahali.
Pia tumekuwa wazoefu wa kupenda vitu rahisi na bandia, unaweza kwenda kununua kiatu ukadhani cha ngozi halisi kumbe siyo nk.

Hivyo basi kama unataka kitu halisi kwa sasa unahitaji kuwa makini kukichunguza vinginevyo unaweza kudanganywa.
Hata hivyo kuchunguza kwa makini ndiyo jambo la msingi kwani ukiangalia kwa undani bila haraka ndipo utajua kitu ni halisi (authentic) na pia ni bora zaidi na kwamba kina thamani kubwa.

Kuna hadithi (labda umewahi sikia) kijana mmoja (mtanashati) alimpenda msichana ambaye ni mwimbaji bora nchini kwao na hakumfahamu vizuri yule mwanamke kwani ilichukua muda mfupi sana na kwa kuwa alikuwa muimbaji maarufu, yule kijana aliona ni bahati kubwa sana na hivyo kwa kuwa amekubali kuolewa na yeye ni busara ndoa ifungwe haraka iwezekanavyo.

Na aliamini kwa kumuona mwimbaji maarufu basi ataishi maisha ya furaha maisha yake yote yaliyobaki duniani, ingawa kwa mbali yule kijana alihisi kwamba yule mwanamke amemzidi umri kidogo ingawa haikuwa tatizo kwake kwani age is just a number!

Siku ya kufunga ndoa ikafika, kanisani wakafika na mbele ya madhabahu wakafika, viapo vikaapwa!
(Ninakuchukua kuwa mke/mume wangu katika raha na shida, katika afya na ugonjwa hadi kifo kitakapotutenganisha, na watu wakadakia kwa vigelegele).

Baada ya sherehe za harusi wakaondoka zao honeymoon.
Usiku umefika na maisha ya wawili inabidi yaanze sasa unakutana na kitu halisi kwani ndoto zote sasa zinaanza kutimia.
Dada ambaye sasa ni mke akaanza kujiandaa kwa ajili ya usiku wao kwa mara ya kwanza duniani kwani walikuwa hawajawahi kuwa pamoja.

Huku kijana (mume) akimuangalia mke wake mrembo anayevutia kama malaika akijiandaa kwenda kuoga; akamuona mke wake anaondoa kidevu (bandia) na kukiweka pembeni kwenye meza, akaendelea akatoa wigi ambalo lilifunika kichwa, hakuishia hapo akaondoa meno (bandia)/ (dentures) na kuyaweka pembeni, akainama chini kuondoa mguu wake wa bandia na kuuweka pembeni.
Akaendelea kutoa kucha zake artificial zilizomo kwenye mikono yake akaziweka pembeni, akaondoa miwani ambayo imewekwa kimtindo kusaidia kuona na pia kufunika kifaa cha kusaidia kusikia (hearing aid). Kijana akawa (mume mpya kabisa duniani) akawa ameduwaa, Guess what!

Yule kijana alizimia kwa yale anayoyaona!

Lengo si kutaka kuwasema wanawake wale wanavaa hivyo vimetajwa hapo juu bali ni kutaka kuelezea kwamba ni vizuri kufahamu kwamba hiki ni kitu artificial au siyo ili ukiwa nacho usije zimia kwa mshangao.
Suala muhimu kama la kuoa ni commitment ya maisha hivyo ni muhimu sana kuwa makini na kuhakikisha unapata kile kitu halisi unachokipenda au hata kama unataka artificial uwe unajua kabla siyo kuja kushtuka mbele ya safari.
Chunguza kabla hujabeba!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Yaani nimecheka mpaka mbavu zikaniuma kazi kwelikweli. Kweli ni muhimu kuchunguzana.

Lazarus Mbilinyi said...

Hongera sana kwani kicheko ni afya dadangu,

Hata hivyo huwa inapendeza na wala huwezi kuzimia pale ukiwa umeshaelezwa kabla kwamba hapa kila kitu ni artificial si real wala natural. Kudhani kitu ni natural halafu siku ya siku ukute ni artificial hapo utajuta!

Kalaghe baho!

Upendo daima!

Anonymous said...

Hello kaka Mbilinyi
Huwezi amini Blogu yako imekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi na hata watu wazima, huo ni ukweli na kuna idadi kubwa ya watu wanasoma materials zako though hawana muda wa kuweka comment zao lakini fahamu hivyo, umekuwa msaada sana!
Haupotezi muda na one day utakuja kufahamu kwa nini ulikuwa ukispend muda wako kwa ajili ya kuwapa watu 'mawe ya thamani' kama haya materials.

Mungu akubariki wewe na familia yako
I really mean It.
Ubarikiwe mpaka ushangae....
Umejiatahidi kuondoa ujinga kwa Watu ambao tupo makanisani na watanzania kwa ujumla!

Keep it up!
MS

Anonymous said...

Hello MS,

Asante sana kwa ujumbe wako na Mungu akubariki sana.

Asante sana kama unajifunza kitu kwa kupita hapa "The Hill of Wealthy" kwani hapa tunaamini ndoa ni msingi jamii yoyote zaidi nashukuru sana kwamba wapo nwanaotoa maoni na wapo ambao hawatoi maoni pia inatokana na aina ya material unayosoma kwani unaweza ukasoma ukashindwa hata utoe maoni gani kwani ni issue zinazotuhusu mno pia jambo la msingi ni wewe kujifunza na napenda sana maswali kwani ndiyo yanayofanya tujifunza zaidi.

Pia nachukua nafasi hii kuwashukuru wote wamekuwa wananitumia emails iwe maoni au swali au ufafanuzi au dukuduku au kutoridhika na kitu chochote kwani kwa sababu ya wewe mimi nakamilishwa na bila wewe hakuna mimi.

Tuombeane tu kwani nina mambo mengi sana ya kuongea na kuandika ila muda unanimaliza.

Ubarikiwe sana na Bwana

UPENDO DAIMA!