"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, October 26, 2009

Eti Kulala Pamoja si Afya!

Tafiti za karibuni zinaonesha kwamba wanandoa kulala kitanda kimoja si afya kama kila mwanandoa yaani mke na mume kulala kila mmoja kitandani chake mwenyewe.

Kitendo cha wanandoa kulala kitanda kimoja kilianza wakati wa mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) kitu kilichosababisha watu kuhamia katika miji na kujikuta wanakosa accommodation na kulazimika mke na mume kulala kitanda kimoja.

hali hiyo imeendelea hadi leo na kuwa kama mfumo ambao watu wakioana tu huamua kulala kitanda kimoja.


Pia bado baadhi ya jamii zinazoishi vijijini mke na mume huendelea kulala kila mmoja kitanda chake hadi leo.

Kwa wastani wanandoa wanaolala pamoja huweza kusumbua mwenzake (disturb) nusu ya usingizi anaotakiwa kulala kama kila mmoja angelala kitanda chake.

Wanandoa kulala pamoja huweza kusababisha kusumbuana na hatimaye kusababisha magonjwa kama vile kuchoka, magonjwa ya moyo. Depression, stroke. Matatizo ya kupumua nk.

Pia historia inaonesha kwamba kitandani hakukuwa mahali pa kulala wanandoa bali ilikuwa sehemu muhimu (maalumu) ya wanandoa kukutana pamoja kwa ajili ya kuwa mwili mmoja (tendo la ndoa) na si wanandoa kulala pamoja.

Daktari wa sociology kutoka chuo kikuu cha Surrrey Dr. Robert Meadows anasema kwamba watu hujisikia vizuri wakilala kitanda kimoja na wapenzi wao hata hivyo ushahidi ni kwamba kulala kitandani kimoja si afya.

Je, unaonaje suala Hili la kulala kila mwanandoa kitanda chake mwenyewe?

1 comment:

Anonymous said...

Kila mwanandoa kulala kitanda chake ni idea nzuri kwani inaweza kusaidia kujua nani ana libido kubwa kuliko mwenzake kwani lazima ukitaka kuwa mwili mmoja uende kwa mwenzake kitu ambacho kitasaidia kujua nani ni nani katika.................

Nitanunua kitanda kingine ili mimi na wife kila mmoja awe na chake, ingawa wakati wa kibaridi mmmm raha kulala wawili ili kupata joto natural.

AM