"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, October 28, 2009

Hataki kuongea!

Tunaendesha Km 8 huku hatuongei, acha tu!
Swali:
Mimi ni mwanamke ambaye nipo kwenye ndoa sasa mwaka wa 8 nimekuwa nikitatizika sana na tabi ya mume wangu kushindwa kuongea na mimi, kila nikitaka kuongea chochote anaonesha hali ya ku-ignore kile nataka kumwambia.
Kinachoshanga zaidi ni kwamba tunapoenda kazini wote tunatumia gari moja hata hivyo zaidi ya Km 8 zote tunakuwa mabubu hadi kila mmoja anaenda kazini kwake na ni kama vile tumekuwa watu wawili tofauti.
Nifanyeje ili mume wangu awe anaongea na mimi tena kama wakati wa uchumba na miaka ya kwanza ya ndoa yetu.
Ni mimi mwenye mume bubu!

Jibu
Dada mwenye mume bubu!
Asante sana kwa swali zuri ambalo naamini si wewe tu ambaye unakutana na hali kama hiyo wapo wanawake wengi tu hawasemi au wanaume wengi tu ambao wamejikuta kila mmoja hana hamu ya kuongea na mwenzake tena, kinachoshangaza ni kwamba wameapa kwamba wataishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.

Kabla hatujaanza kujibu swali vizuri jambo la msingi unatakiwa kutambua kwamba ndoa hupitia hatua mbalimbali na kwamba unapokutana na hali kama hiyo unatakiwa kuwa makini zaidi ili kuhakikisha unairudisha kwenye mstari au badala ya kuweka maji kwenye moto wewe unaongeza petrol.

Inawezekana unapokumbuka mume wako alivyokuwa anaongea na wewe kwa simu au text messages au email au kukutana tu na kuwa na hamu na wewe kabla ya kuoana na leo hii, hisia zako zinaumia sana kwani inawezekana alikuwa anakesha na si kuongea na wewe tu bali kuhakikisha anaongea vitu ambavyo vinakufanya uwe au ujisikia happy na kwamba una mume anayejua kupenda na ni yeye tu duniani, leo umeoana mambo ni kinyume.

Wanandoa wengi hujisahau (wanaume na wanawake) kwamba wanahitaji kuendeleza romance na surprises hata baada ya kuoana.

Kama wanandoa wawili wamefika mahali hawawezi kuongea tena hii ina maana kwamba mmoja wao hajisikii kuvutiwa (hisia) kuweza kuongea na mwenzake, anajisikia unam-bore, humvutii tena.

Inaweza kuwa ni wewe mwenyewe umesababisha mume wako awe disconnected na wewe au ni yeye amepata mwingine ambaye anamvutia zaidi na kumfanya anapoongea ajisikia vizuri.
Kabla ya kuamini kwamba ni yeye labda ni vizuri kuanza kuisafisha nyumba yako moyoni mwako kwanza yawezekana ndo itakuwa dawa kamili.

Je, bado upo attractive kama ulivyo kuwa enzi zako zile za uchumba, honeymoon na miaka ya kwanza ya ndoa yenu?
Je, unamheshimu mume wako kama wakati wa uchumba au mwanzo wa ndoa yenu?
Je, unaongea tu, na
kumkefyakefya (nagging) kwa kila kitu hata kitu kisicho na maana hadi yeye kujikuta hana majibu na jibu sahihi ni kujibakia kimya?
Je, umakuwa unalalamika kwa kila kitu hata yeye kutoongea na wewe?
Je, mahusiano yako kimapenzi ni mazuri na yeye (yaani kuna enjoyment ya kuridhisha linapokuja suala la sex)?

Kuna msemo kwamba “People take things for granted when married” kwa sababu wanaamini wanaishi kwenye mapenzi tayari hivyo wanakuwa jeuri kwa wapenzi wao.

Dawa ya kuweza kuongea na yeye ni wewe kuwa na bonding mpya na mume wako yaani ajisikie yupo connected na attracted na wewe na hii haiwezi kutokea overnight kuna kazi unahitaji kufanya.
Unaweza kuanza kufanya vitu vile yeye anapenda kufanya, kama vile michezo, project, business hata mambo anayopenda kuongea, hapo atajisikia vizuri kwani unagusa maeneo yake.
Wanaume hufanya bond haraka kwa kufanya activities pamoja na si kwa kukaa na kupiga soga kama wanawake, hivyo ukitaka mumeo aongee mfuate kwenye shughuliza zake binafsi anazopenda kufanya.

Kama kuna kazi amefanya au kitu amefanya jitahidi kuhakikisha unampa credit au praise, kumsifu kwa vitu anavyofanya kunampa feelings kwamba unatambua mchango wake na kwamba yupo respected na wewe pia atafahamu unatambua juhudi zake katika familia hivyo ataanza kuongea na wewe.

Pia inawezekana kutokana na yeye kushindwa kuongea na wewe umeamua kuwa rough yaani humpi respect nah ii imeathiri ego yake na anakuona hakuna lolote, hivyo geuza kibao kwa kumpa respect kwanza.

Pia unaweza kujipa kalikizo kadogo kwenda mbali kidogo ili ujenge hamu ya kukutaka au wewe kutokuwepo kuna kujisikia Fulani ambalo kwa wawili wanaoishi pamoja lazima itajenga hamu ya kukuhitaji tena.

Pia kumbuka approach ya maisha na mapenzi kwa ujumla kwa mwanamke na mwanaume ni tofauti hivyo unatakiwa kuwa makini na namna unavyoongea na mume wako kwani sasa mnaishi kwenye ndoa ni maisha halisi ni kitu halisi.

Pia inawezekana sasa hakuna fun zozote, hakuna kucheza wala kutaniana wala kufurahishana, wote mmejikita kwenye kazi na responsibilities na matokeo yake hakuna kicheko na mnakuwa disconnected, jiulize wewe na mume wako mmecheza mchezo wowote lini?

Kama unaweza basi kuanzia leo jifanye ni mchumba na act kama mchumba uone kama hataongea.

Usipende kuongeea naye eti kwa kuwa kuna issue muhimu ya kuongea, ongea naye hata wakati hakuna issue sensitive, just for fun.

Haina haja kuongea (kuchonga) ili kutaka mume wako aongee na kujibu kila swali unalomuuliza au kuzunguka kutoa maelezo mengi badala ya kuongea point ndipo wanaume wengi hujisikia wanawake hawaeleweki na too much na wakati mwingine mume amechoka wewe unataka kuongea na maswali kibao.

Uwe na hekima, wakati mwingine wanaume anahitaji kwenda pangoni.
Hata kama hatulipii kuongea haina maana tuongee ovyo na kuuliza maswali yote, ni vizuri kuwa makini na jinsi tunavyoongea na si kila wakati ni wakati wa kuongea.

No comments: