"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, October 24, 2009

Mchumba asiye mwaminifu huwa mwenye ndoa asiyemwaminifu!

Swali:
Habari za kazi kaka naomba nisaidie naangamia kwa kuwa na mawazo yasiyo na msingi na kuumiza afya yangu, kweli nateseka mno.
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 29, nilikuwa na relation ya kwanza ambayo ilidumu kwa miaka mitatu lakini kikubwa kilichotufanya tusaparete ni dini yeye muislam mie mkristu.
But baada ya muda kupita nikapata mvulana mwingine kwa kweli nilifurahi toka siku ya kwanza kwa kuwa wote ni wakristu na nilimuona kwamba anampenda Mungu kwa matendo yake lakini kadri tulivyoendelea na relation nikagundua ana affair na wasichana wengine.
Niligundua kupitia simu yake ya mkononi, nikamwambia na nikampa masharti kama ananipenda anipeleke kwao kunitambulisha na akafanya hivyo, haijapita mwezi bado anaendelea na hao wasichana wengine tena akiwa anakuja kwangu anawambia wasitume msg wala kupiga simu, lakini pia nimegundua ana relation mpya kaanzisha tena kwa mwanamke mwingine yani kichwa kinaniumwa!

Maswali
Je, Ni kweli mwanaume wa hivi anarekebishika kweli?
Je, kwa nini anakuwa na wasichana tofauti tofauti?
Na nikajaribu kupeleleza kwao nikaambiwa ni mimi peke yangu nilipelekwa kutambulishwa.
Je, kweli anafaa kuwa mume?
Maana sihitaji kuwa nabadilisha wanaume kila siku nahitaji kupata ushauri wa kuwa kama anabadilishika bora nitulie nae kuliko kufuata mwingine na kila siku kuwa na wanaume tofautitofauti.
Kweli nampenda kwasababu familia yao ipo katika misingi ya dini imara.

Nimeelemewa na mawazo.
Ni mimi dada Yamenikuta.

MAJIBU YA SWALI LAKO

Pole sana dada Yamenikuta!

Kama mmoja ya watu ambao hupokea maswali mengi yanayohusiana na ndoa na uchumba au mahusiano kwa ujumla, ukweli kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusiana na suala la wanandoa kuoa wrong partner, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wa hawa ambao wameoana na wanaume/wanawake wasiofaa wanakiri kwamba walikuwa wanajua na kufahamu fika kwamba wachumba zao walikuwa na tatizo hata kabla ya kuoana, kwa kuwa walikuwa wamependa (fall in love) au pendana kwa muda mrefu au muda wa kuoa ulikuwa umefika waliamua kwa hiari zao kuendelea na mahusiano wakitegemea kwamba siku moja watabadilika.

Je, tunaweza kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?
Hivyo basi dada Yamenikuta, ni jambo la busara na hekima kubwa kuwa makini na maamuzi unayofanya hasa baada ya kukutana na mwanaume ambaye ameshindwa kutembea katika ahadi kamili za msingi wa mahusiano yenu na kutegemea kuwa na ndoa yenye baraka.

Usikubali kuoana naye kwa sababu eti unampenda sana na umekuwa naye kwa muda mrefu katika mahusiano kabla ya kuoana.
Urefu wa mnahusiano kabla ya kuoana (uchumba) au wewe kumpenda na kujioana huwezi kuishi bila yeye hauna uhusiano wowote na afya ya ndoa yako baadae kama huyo mchumba wako ameshindwa kuwa mwaminifu kabla ya kuoana.
Tabia alizonazo kabla ya kuoana haziwezi kubadilika ghafla baada ya kuoana.
Mwanaume asiyemwaminifu kabla ya kuoana hatakuwa mwaminifu baada ya kuoana pia.
Ndoa huwa haibadilishi mtu kiburi chake, hasira zake, umalaya wake, wizi wake, tabia zake chafu sana sana ndoa hufunua hizi tabia na kuziweka mezani uzione.

Usijidanganye mwenyewe na kujipa moyo, utaangukia pua!

Kile unachoona sasa ndicho utakachopata ukioana naye.

Si kweli kwamba huyo mwanaume anampenda Mungu kwa matendo kama ulivyosema na sijajua ulitumie vigezo gani kwani kutembea na wanawake wengine ni uthibitisho kwamba dini yake ni ovyo.

Pia yeye kukupeleka kwa wazazi wake (baada ya wewe kumlazimisha kama uthibitisho kwamba anakupenda) kukutambulisha si jambo kubwa sana ambalo linaweza kumfanya mwanaume mhuni asiwe mhuni bali ni taratibu tu za kuwaambia wazazi kwamba huyu ni mtarajiwa (siyo mke) hii ina maana hata kesho anaweza kuamka na kumtambulisha mwingine.

Pia wazazi wake kuwa wanadini wazuri haina maana mtoto wao naye atakuwa na dini nzuri na kukuhakikishia maisha safi ya ndoa, hata hivyo dini nzuri kwa maana ipi ? kwenda kanisani au kuona wagonjwa au jinsi wanavyoishi?

Ni kweli kama wewe upo makini na dini yako uamuzi wa kuchangua mume ambaye dini zinafanana ni wa busara sana unaweza kusoma hapa

Sasa tuje kujibu maswali yako.
Mwanaume wa aina hiyo huwa harekebiki na Mungu anakupenda sana kwamba amekuondoa kwenye shimo ambalo ungeingia kutoka ingekuwa kazi ya ziada, hivyo furahi na amini kwamba Mungu anaweza yote na shukuru kwa kukuonesha kwamba huyo mwanaume hafai.

Ni ngumu sana kukubali kwamba mwanaume huyo hafai kwani inaonesha ulimkabithi moyo wako wote hata bila kuchunguza vizuri ni wapi moyo wako unaweka.

Suala la kwa nini anakuwa na wasichana wengi naamini yeye ndiye anajua hata hivyo inaonesha kwamba hata kama anakupenda ana tabia mbaya ya uhuni kiasi kwamba hawezi kuwa na wewe tu bila hao wanawake wengine.

Na je anafaa kuwa mume, ukweli ni kwama hafai na kimbia na mwogope (kama njaa) kwa maelezo zaidi kuhusu kujua anafaa au hafai au ni yeye au si yeye wa kuoana naye soma hapa

Usijifariji kwamba eti afadhari ubaki naye yeye ili usionekane unabadilisha wanaume, ukweli huyo hafai na pia kama wewe umezoea kuwa na mwanaume na kumpa mwili wako ni kweli hisia zako zitakuwa zimeumia zaidi, wakati mwingine ukipata mchumba hakikisha humpi mwili wako kwanza hadi ndoa.
Kwa maelezo zaidi soma hapa Soma hapa

15 comments:

Anonymous said...

Mwanaume wa aina hiyo anakumalizia muda wako na anaweza kukusababisha kupata magonjwa ya UKIMWI bure.
Achana naye kwani huyo ni mume si utapata mwingine?
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha una kuwa busy na kazi zako ili mind iwe inafikiria mambo mengine na si yeye.
Unakap[okuwa na muda wa kutosha kufikiria jinsi alivyokufanyia utaweza kugundua kwamba ulikuwa katika hatari.
Sasa hivi umeumizwa na upo katika maumivu ila maumivu yakikomaa na kuwa hasira basi utakuwa better na utajua bahati uliyonayo ya kugundua balaa ambalo lingekupata hapo baadae.

Anonymous said...

Kwa kuwa unasema unahitaji kutulia naye kuliko kubadilisha wanaume una kazi kubwa kwani wanaume wa affair huendelea kuwa na affair tena na tena, be carefull.

Asha

Anonymous said...

Nami ilinipata kama wewe, niliendelea kuwa mwanamke dhaifu na dhaifu na ilifika mahali nikawa nachanganyikiwa kabisa kumkosa yeye.
Sikufahamu ila nafahamu kwamba unaweza kuwabadilika na kuwa strong, beautiful na independent woman kama mimi hadi siku nilipopata mwanaume wa uhakika ambaye nimeoana naye.
Unanishangaza unaposema hata kama anatembea na wanawake wengi kama anaweza kubadilika afadhari utulie naye, huyo hawezi kubadilika na kama yupo hivyo kabla hajakuoa na akikuooa je?
Utamlilia nani?
Kuwa na furaha lazima furaha ianze ndani yako na furaha itaanza ndani yako pale ukianza kufikiri kwamba huhitaji mtu yeyote kukupa furaha bali wewe kwanza, utakapotambua kwamba furaha yako haitokani na mwanaume kwanza.

Mama E

Anonymous said...

Huyo mwanaume hakuhitaji wewe hata kama amekutambulisha kwa wazazi.
Ningekuwa mimi ningesema bye bye mapema kabisa.

Anonymous said...

Achana naye, haina haja kuolewa na mwanaume mhuni wakati bado upo binti wa miaka 29 tu, angekuwa amefanya kosa mara moja sawa sasa ana kundi la wanawake kiasi hicho nab ado hajakuoa?
There are plenty of fish in the sea; you can find a nice man who won't cheat on you, I promise.

Jacob.

Anonymous said...

Ukweli kama utaendelea au kuamua kuoana naye matokeo yake ukishaolewa ataendelea na business yake as usual na utajikuta unaishi maisha ya ndoa yasiyo na furaha na matokeo yake ni talaka.
Kama anaendelea kutembea na hao wanawake maana yake hayupo tayari kwa ndoa hata kama amekutambulisha kwa wazazi wake na kwamba wazazi wake wana dini.

Anonymous said...

Dada anza kujifunza kuishi bila yeye.
That's a ridiculous.

Anonymous said...

Niamini ninachoongea unaweza kuishi kirahisi bila yeye kuliko kuishi kwa hofu na mashaka huku anakudanganya kila siku.
Anakupotezea muda.

Anonymous said...

Kwa kuwa unapenda kumbadilisha hakikisha unaishi naye huku anaendelea kukudanganya kwani ndicho ataendelea kufanya na mwisho oana naye ili mtenngeneza jehanamu yenu.

Anonymous said...

Huyo mwanaume amekufanyia abuse emotionally kiasi kwamba hata hukitambui vizuri, kwani uliishi vipi kabla ya huyo wa kwanza na huyu wa sasa?
Si ulikuwa na amani tele au huwezi kuishi bila mwanaume?

Baraka

Anonymous said...

Maisha yako ya furaha yanategemea sana jinsi unavyofanya maamuzi yako na njia unayochukua katika safari yako.
Kama anakupenda kiasi cha kushindwa kuwa mwaminifu sasa je una uhakika gani utaweza kuishi kwa furaha na yeye miaka 50 ijayo?

Fanya maamuzi ya busara, unaweza kumpata mwanaume mzuri ambaye atakuwa mwaminifu na akakupenda.
Yalinikuta nikafanya maamuzi ya busara na sasa nimepata mume wa kweli.

Mama Pili

Anonymous said...

Je, ingekuwa umeolewa na una watoto na mume wako anaruka na kila aina ya wanawake. Dada sasa ni wakati wa kuwekeza kwenye elimu na kazi kuliko wanaume wa aina hiyo.
Mwache atafute washamba wenzake

Anonymous said...

Hivyo unafikiria ukiolewa atakuwa better, pole sana mibaba ya aina hiyo ni migonjwa ukiolewa utajuta hata kama anakupenda namna gani kwani kupende ni matendo siyo maneno.
Huyo akikuoa atakuwa anapotea nyumbani wiki kama si mwezi na wanawake wa siku hizi wanavyojua kuwafanyizia waume za watu kazi kweli.

Anonymous said...

Dada hupo mwenyewe dunia hii, kabla ya kukutana naye ulikuwa na maisha yako hata baada ya yeye bado utakuwa na maisha yako.

Anonymous said...

Hata kama utamsamehe sasa na kuahidiana kuoana ukweli ni kwamba atakuwa na affair tena kabla hamjaoana na akioa atakuwa na affairs za kumwaga.
Dawa ni kuachana naye, tulia fanya kazi mume kutoka kwa Bwana atakuja mwenyewe.