"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, October 18, 2009

Mwanaume anahitaji zaidi!

Kila mmoja anamuhitaji mwenzake!Je, wanaume wanawahitaji wanawake zaidi kuliko wanawake wanavyowahitaji wanaume?

Hili ni swali ambalo si gumu wala si rahisi ila inatokana na mtazamo wa jinsi kila mmoja anavyozifahamu hizi gender mbili.

Wanawake mara nyingi huonekana wanawategemea sana wanaume kuliko wanaume wanavyowategemea sana wanawake.
Na pia mwanamke huonesha kwa uwazi zaidi kwamba anamilikiwa na mwanaume kuliko mwanaume kuonesha mwanamke ndiye anayemmiliki.

Wanawake hupanda kuelekea mafanikio hasa kutokana na kusifiwa (praise) na kutiwa moyo wanakopewa na wale wanaowazunguka.
Wanawake huwa na interest na watu na hupenda kutegemea watu (mwanaume) wakati wanaume huwa na interest na vitu na pia hupenda kujitegemea au kutegemewa.

Mke mara nyingi huhitaji approval kutoka kwa mume, upendo kutoka kwa mume, kutiwa moyo kutoka kwa mume na kupewa attention kutoka kwa mume wakati mwanaume hupenda competition na kwamba kufanikiwa katika kazi au business ndicho kitu kinachompa approval na kujisikia kweli naye ni mwanaume wa uhakika.
Kwa haraka haraka unaweza kufikia conclusion kwamba ni kweli mwanamke anamuhitaji mwanaume zaidi kuliko mwanaume anavyomuhitaji mwanamke?

Je, mwanaume ambaye yupo umri ambao alitakiwa kuwa na mke na familia na anaishi mwenyewe anafaa (fit) katika jamii kuliko mwanamke ambaye alitakiwa kuwa na mume au familia na ainaishi mwenyewe?

Mwanaume na mwanamke waliumbwa kila mmoja kumuhitaji mwenzake na kwamba kila mmoja akiwa mwenyewe hujisikia hajakamilika.

Hata hivyo wanawake hufanya vizuri zaidi bila kuwa na mume kuliko mwanaume kuwa mwenyewe bila mke.
Ingawa hii huonekana ni kinyume kidogo na mtazamo wa jamii nyingi kwani mtazamo wa wengi ni kwamba mwanamke ambaye hajaolewa au anayeishi mwenyewe (single) huonekana ni mtu miserable katika jamii na hafai kitu ambacho si kweli kwani mwanamke single ana mambo mazuri mengi ukilinganisha na mwanaume single.

Ni mara nyingi sana kukuta mwanaume ambaye yupo mwenyewe bila mke wala familia anakuwa mlevi wa kupindukia, anaweza kutumia drugs, anaweza kujihusisha na uhalifu, hata Landlord’s wengi huwa hawapendi kupangisha nyumba kwa mwanaume asiye na mke, hata baadhi ya insurance hugoma.

Wanaume wasio na mke wala familia wengi huendesha magari kwa speed au fujo, wana hasira, pia wanakuwa na risk kubwa ya antisocial behavior na wakati mwingine kipato chao huwa kidogo kwa sababu wanajiona hawana responsibilities na wanaweza kuruka kutoka kazi moja hadi nyingine, who cares? hahahaha!

Pia mwanamke asiye na mume huwa tofauti kutokana na nguvu ya uzazi aliyonayo (uwezo wa kuumba mtoto ambao wanao ndani yao) huwawezesha kuwa tofauti na wanaume linapokuja suala la watoto bila kujali awe mtoto wake wa kuzaa au hapana na hii huwapa uwezo wa kuwa mtu tofauti katika jamii tofauti na mwanaume ambaye anachojua sana ni kusubiri siku bunduki yake itoe askari wake a marine na mtoto azaliwe.

Mwanamke akiolewa na mwanaume kile anafanya ni kuitumia nguvu ya mwanaume (sexual energy) ambayo alikuwa nayo na anaitumia kuunda kupata mtoto na mwanaume hujikuta anakuwa na responsibilities na pia anawajibika katika kulinda na kuipa familia kila inachohitaji na mabadiliko ya aina hii ni muhimu sana kwa jamii na tamaduni zozote ambazo kuna mwanaume na mwanamke.

Ni kweli wanawake wanawahitaji wanaume lakini si kama wanaume wanavyowahitaji wanawake ili dunia iwe mahali bora kuishi.

“One of the saddest creatures on earth is a man without a woman”

Wewe unasemaje?

No comments: