"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, October 3, 2009

Namtafuta Mwezi, kipi nizingatie?

Kaka Mbilinyi,
Mimi ni kijana wa kiume wa miaka 25 nimeokoka nampenda Yesu na naamini nipo tayari kutafuta mchumba awe mke wangu.
Je, ni mambo gani muhimu kuzingatia wakati natafuta mwenzi wangu?
Ubarikiwe na Bwana
HB

Kaka HB,
Asante sana kwa swali zuri sana na hongera sana kwa uamuzi wako wa kutafuta mwenzi wa kuishi na wewe maisha yako yote hapa duniani.
Jambo la msingi ni kwamba uamuzi wa kwanza ambao ni muhimu sana duniani ni uamuzi wa kuukubali wokovu au kuukataa na uamuzi wa pili ni kuchagua mke au mke utakayeoana naye.

Ndoa ni moja ya vitu vizuri na vyenye Baraka kubwa sana katika maisha na pia ni moja ya vitu ambavyo husababisha majuto na masikitiko makubwa sana hasa kwa wale ambao huchagua mwenzi carelessly.

Katika maeneo yote ya maisha yetu, Mungu ndiye anayetuongoza na kutusaidia kupata mwenzi (ubavu) ambaye anatufaa pale tunamtegemea yeye na kukubali mapenzi yake kwetu (Mithali 3:5).
Hivyo kwa kuwa wewe unaamini (umeokoka) ni muhimu kuoana na Yule ambaye naye anaamini (ameokoka) si Yule tu anayesema mkristo bali Yule ambaye maisha yake yanaonesha kweli ameokoka (long term Christian behavior)

Usiongozwe na emotions zako, kuna wakati unaweza kudhani umempenda kumbe ni maluweluwe tu (infatuation) ambayo kama hupo makini unaweza kudhani ni upendio wa kweli kumbe la.
Upendo wa kweli ni kitu ambacho unakuwa na commitment na kujitoa sadaka kwa ajili hiyo. Hii ina maana kwamba katika udhaifu unaouona kwake ni wewe tu duniani unaweza kumchukulia na ni sababu ya kumuona anakufaa (sizungumzia vitu kama uchafu, uchoyo, nk) bali vitu kama ufupi wake au weusi wake au kipara chake.

Usioe kwa kuangalia mwonekano tu, au umbo lake au kwa sababu ya uwingi wa vitu alivyonayo, ni wajinga tu ndo hutumia hivyo vigezo walio na hekima na busara huangalia vile vilivyo moyoni siyo nje na ukimuomba Mungu atakupa Yule ambaye utaridhika kuanzia ndani hadi nje kwani kuna kila aina wa wanaume na wanawake wazuri yeyote anaweza kuwa nao ndani ya Yesu na maombi yanaweza kufanya chochote Mungu anaweza kufanya kwako.

Kabla hujafanya chochote piga hesabu za gharama kwanza (kumbuka habari za kutaka kujenga mnara(Luka 14:28).
Kwa kuwa ndoa ni hadi kifo (ukiingia hutoki hadi mmoja afe -1 Cor. 7:39), itakuwa maisha yako yote kutoa na kupokea, kushirikiana na kukubaliana, je upo tayari kutoa hiyo sadaka?
Kumbuka ndoa ni kudumu ile katika afya au ugonjwa, katika raha au shida, hakuna kutoka hadi kifo.

Kuoana haraka haraka (faster) si jambo la busara kabisa, wajinga huchumbia na kuoana ndani ya miezi mitatu au sita.
Mfahamu vizuri huyo mke mtarajiwa kwani ni heri kuachana wakati wachumba kuliko kuachana wakati ni mke kitu ambacho hakipo hata kama wengine wanafanya.
(Know the stuff please).
Mwaka mmoja ni wastani wa kawaida kwa watu ambao wapo wanahitaji kujuana vizuri na wale ambao wanapenda kujua mzigo amebeba kama kweli anastahili.
Usioana na yeyote ambaye unaamini ukioana naye utaweza kumbadilisha, ukweli ni kwamba kama ana tabia mbaya sasa basi ukioana naye hiyo tabia mbaya itakuwa maradufu (kwani wewe ni Yesu ndo umbadilishe?) kama hajabadilika kabla hujaoana naye hilo ni tego!
Kila mtu huwa na tabia njema kabla ya kuoana sasa kama anatabia mbaya hata kabla ya kuoana, kama hujui riadha basi………….

Uwe makini jinsi mwenzi wako mtarajiwa anavyowahudumia au anavyojihusisha na ndugu zake kama wazazi, marafiki na watu wote kwa ujumla.
Jinsi mtoto anavyofanya kwa mama yake ndivyo mara nyingi humfanyia mke wake na jinsi binti anavyomfanyia baba yake ndivyo atakavyomfanyia mume wake au mume hutamani mke wake awe kama mama yake na mke hutamani mume wake au kama baba yake so know the trick.

Usiingie kwenye ndoa bila maandalizi ya kutosha au mafundisho (premarital counseling) kutoka kwa mchungaji wako au mtu mzima ambaye ana ufahamu na mambo ya ndoa.

Zaidi unaweza kusoma articles za huko nyuma kuhusu kuchagua mwenzi.

Weekend njema

No comments: