"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, October 29, 2009

Nani ana Hasira Zaidi?

Je, wanaume hukasirika zaidi kuliko wanawake?
Wengi huwaona wanawake ni viumbe ambavyo vipo emotional na very affectionate wakati wanaume ni aggressive na wakati huohuo very courageous.
Tafiti nyingi hazioneshi kwamba wanaume hukasirika haraka kuliko wanawake bali zinaonesha tofauti iliyopo hasa namna ya kuonesha (express) hizo hasira.

Ukweli ni kwamba wanaume na wanawake wote huwa na mawazo sawa ya kukasirika, ingawa wanawake huonesha intensity kubwa ya hasira na kwa muda mrefu na hupenda kutoa hasira zao kwa njia ambayo ni submissive zaidi ya wanaume.
Kwa upande mwingine mwanaume akikasirika anachukua direct approach ili kupambana na mtu amesababisha akasirike.

Hata hivyo kwa uajumla suala la kukasirika na kuonesha hasira mara nyingi lina base zaidi kwenye uwezo (power/authority) kuliko masuala ya gender kwani mara nyingi watu huonesha hasira zaidi kwa watu waliochini yao, wanyonge wao na waliowadogo .

1 comment:

Anonymous said...

Kuna wanaume wana hasira jamani hadi mke unajiona upoo jela vile na ukikosa kitu ukikumbuka atakavyo react kwa mara ya kwanza hata nguvu zinakuishia.
Ni kweli wote tuna hasira ila jinsi wanaume wanavyo express hasira zao wakati mwingine ni mbaya sana.