"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, October 17, 2009

Upendeleo kwa mtoto mmoja

Swali:
Nataka kujua zaidi katika malezi ya watoto kuna kitu inaitwa parental favouratism.
Iwapo mtoto mmoja anajisikia kutopendwa sana kama mwenzake au wenzake na wazazi ,inaweza ikamletea athari gani baadae?
Na kwanini wazazi wengine wanakuwa na upendo zaidi kwa mtoto fulani.
Utakuta mwingine mtoto wa baba, mwingine yupo tu.

Jibu
Mzazi mwenzangu asante sana kwa swali zuri.
Ni kweli tabia ya kumpendelea mtoto mmoja au kila mzazi kuwa na mtoto wake ambaye anagusa zaidi moyo wake ipo sana katika familia zetu.
Kuna msemo wa waingereza unaosema “The elephant is in the living room” kwa maana kwamba wengi huwa kulitaja au kuliongelea kwa undani ingawa ni kweli familia nyingi zitakiri kwamba hili ni tatizo sugu na pia inawezekana wewe ni mmoja ya watoto waliopendwa au ambao hawakupendwa na moja ya wazazi wenu.

Kwa nini upendeleo hutokea kwa mtoto mmoja?
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni njema zaidi kuliko wengine, wakipewa kazi mmoja anafanya na mwingine hafanyi mara zote, anayetii hujikuta anapendwa zaidi.
Inawezekana tabia ya huyo mtoto ni rahisi na mwenzake au wenzake ni ngumu.
Inawezekana mtoto anafanana na mzazi zaidi kuliko wengine (tabia na mwonekano).
Inawezekana huyo mtoto anafanikisha matarajio ya wazazi wake au mzazi mmoja.

Inawezekana kwa sababu ni mvulana peke yake au msichana peke yake mzazi hujikuta anampenda zaidi.
Pia inawezekana talents zake au vipaji vyake vinafanana na vile mzazi anataka mtoto awe au inawezekana ndiyo values za familia.
Pia inawezekana mtoto asiyependwa ni mtoto ambaye ni mbishi au ni mtoa hamasa (challenge authority) kuliko mwenzake au wenzake. Mtoto ana njia zake au mitazamo yake kuhusu maisha na vitu hivyo wazazi au mzazi hujikutana wanabishana kila kitu.

Pia kuna mazingira ya kuzaliwa ambayo hufanya mtoto kupendelewa zaidi ya wenzake kama vile mtoto kuzaliwa siku au wakati (huohuo) ambao mzazi wa baba au mama (babu au bibi) yake anafariki, ingawa haina ushahidi wa kisayansi ila matukio mengi huonesha kwamba mtoto wa aina hii huonekana wa thamani kuliko wengine na ni kama vile roho ya babu au bibi huenda kwa mtoto anayezaliwa na wazazi kujikuta wanampenda kuliko kawaida.
Au inaweza kuwa ngumu sana mzazi kuweka bond na huyo mtoto kutokana na huzuni, stress na depression mzazi alipata wakati anazaa na wakati huohuo mzazi wake mwenyewe (baba au mama) naye anafariki.

Mtoto kuzaliwa bila kutegemea hasa baada ya wazazi kudhani wamemaliza kuzaa.
Mtoto kuwa na matatizo ya afya hivyo wazazi kutumia muda mwingi kwake na wengine kujiona mwenzao anapendelewa.
Wakati mwingine inatokea tu mzazi hujikuta anampenda mtoto fulani katika familia kuliko wengine.

Nini mojawapo ya Dalili za mtoto kupendelewa?
Kununuliwa zawadi zaidi ya wenzake.
Kutoa adhabu rahisi kuliko wenzake kwa kosa moja, wenzake wanakula fimbo yeye anaonywa tu.
Sherehe au sikukuu zake kuwa tofauti na wenzake kwa jinsi zinavyoandaliwa nk.
Wenzake wakiomba kitu hichohicho wanakataliwa lakini yeye anapewa au kuruhusiwa.
Mzazi kutumia jina lake kumaanisha watoto wake wote kama vile baba anarudi kazini na watoto hawapo na mtoto anayempenda anaitwa James na badala ya kuuliza watoto wapo wapi yeye anauliza “akina James wako wapi?”
Tumia muda mwingi na mtoto mmoja.
Kuonesha upendo wa dhahiri kwa mtoto mmoja nk nk nk.
Je, mtoto ambaye anajisikia hapendelewi na mzazi au wazazi hujisikiaje?
Mtoto anakuwa na wakati mgumu sana kujikubali na kujipenda mwenyewe kwa kuwa anaamini mzazi/wazazi hawampendi na anaweza kuwa na tatizo sugu la kutojiamini (chronic low self-esteem)
Mtoto hujiona duniani hakuna haki na kwa kuwa hatendewi haki nay eye anaweza kuanza kutowatendea haki wengine kwani “unfairness begets unfairness”

Je, mtoto anayependwa anaweza kupata madhara yoyote?
Ukweli ni kwamba hata mtoto ambaye anajiona anapendwa pia anaweza kupata tatizo la kukosa kujiamini kwani anakuwa too much spoiled.
Kwa kuwa anapendwa basi atajitahidi kufanya zaidi kwani anaamini asipofanya kila kitu juu anaweza kupoteza kuendelea kupata upendeleo hivyo kama ni shule atajitahidi kupata grades za juu, kama ni tabia atajitahidi asikasirike nk na matokeo yake atakuwa hajiamini na anaweza kupota msongo mawazo.

Mtoto anayependelewa anaweza kuwa si mzuri sana linapokuja suala la wenzake wa rika moja au walimu au watu wengine kwenye maisha kwani kile kitendo cha kujiona anapendelewa na wazazi au mzazi humpa kakiburi Fulani.

Mtoto anayependwa hujiona yeye ndo mzuri na huwa hakosei hata hivyo maisha hayako hivyo na matokeo yake atakuwa na wakati mgumu mbele ya maisha hasa llikija suala la kupambana na matatizo.

Hasara ya kumpendelea mtoto mmoja huendelea hadi kwa wajukuu na inaweza kuleta matatizo na migogoro kwa kuwa wajukuu wa watoto wote huanza kuzozana kwa kuwa mmoja wa wazazi wao alikuwa anapendwa zaidi na babu au bibi.


Je, kwa mume na mke ni tatizo?
Ndiyo kunaweza kutokea mgogoro kati ya mke na mume hasa kwa mtoto mmoja kupendelewa na mzazi mmoja, kwa mfano baba anampa fedha nyingi zaidi mtoto mmoja anayempenda bila kujali ni mdogo kuliko wenzake, mama akiona au kusikia naye huja juuu kitendo ambacho kitafanya ndoa iwe katika mzozo.

Je, unaweza kuepuka vipi kumpendelea mtoto mmoja?
Kwanza wewe mzazi jikubali kwamba wewe ni binadamu na kwamba katika watoto wako mmoja anakubalika kwako zaidi kuliko wengine.
Wasikilize watoto wengine ambao wanakwambia unampendelea mwenzao na usijilinde, wasikilize na anza kufanyia kazi yale wanasema (kuacha kumpendelea mmoja)

Gundua utofauti wa kila mtoto na kile anapenda kufanya (characteristics, skills, interest) na mhudumie kutokana na vile anavipenda.

Usiwalinganishe au kumsema mmoja kwa sababu ya mwingine kwani kila mtoto yupo tofauti, sentensi kama “mwenzako James akirudi shule anafanya homework yake vizuri na animalize wewe hadi ulazimishwe!”
Ni kweli amekosea hata hivyo kila mtoto yupo tofauti na kila mtoto anatakiwa kuambiwa kama yeye na si mwingine.
Kama unanunua zawadi ni vizuri kununua zawadi zinazolingana siyo mmoja unanunua zawadi ya Tsh. 100,000 na mwingine Tsh. 20,000
Tumia muda vizuri na sawa kwa watoto wote.

Kumbuka jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo utakuwa na kibarua kigumu zaidi, kwani unahitaji kutafuta muda maalumu kwa kila mtoto na kugundua kipaji chake na kuhakikisha unakiendeleza sawa na watoto wengine.

Jambo la msingi ni kila mzazi kumpa (treat) kila mtoto sawa katika hali zote na juhudi za ziada zinahitaji katika mazingira ya nyumbani kuhakikisha watoto wote wanalelewa sawa na kila mmoja kujiona ana thamani sawa kwa wazazi mmoja mmoja na kwa pamoja.

7 comments:

Anonymous said...

Najisikia kama mama yangu anawapendelea watoto wengine kwa sababu nafanana sana na yeye katika tabia kwani yupo controlling mno, the boss na anataka kila anachosema kila mtu afanye na kwamba yupo sahihi kila siku, mimi nina njia zangu, nina tabia zangu kwa nini nikubali kila kitu?
Bahati mbaya baba na mama waliachana mimi nikiwa na miaka 2 na mama akaolewa na mwanaume mwingine ambaye mimi hatuendani.
Mama hanipendi, baba hapoatikani, bibi alishakufa na shangazi alishahama na sijajua yupo wapi, maisha naishi kivyangu.
Wazazi ni muhimu kuwa makini kutopendelea mtoto mmoja.

Anonymous said...

Mimi ndo mkubwa kwa wazazi na kitu kinachoshangaza ni kwamba pamoja na tabia zake mbaya bado wazazi wangu humsikiliza yeye kuliko mimi, inaumiza san asana!
Kuna siku mdogo wangu aliharibu kitu muhimu sana ndani ya nyumba nikamwambia mama na hakusema chochote na hakunijali, baadae yeye akamwambia mama kwamba ameharibu kitu ndani ya nyumba na kibao nikageuziwa mimi eti sikuwa makini kumzuia asiharibu.

Bado najiuliza hivi nilifanya kosa gani kwa wazazi wangu hata hawanipendi?
Inaumiza sana

Anonymous said...

Wazazi wanaweza kumpendelea mtoto anayefanya vizuri zaidi ya mwenzake ambaye kila siku ni kuleta matatizo. Kama unataka kupendelewa fanya vizuri, uwe na tabia njema.
Hata hivyo kama una tabia nzuri nab ado wazazi hawakupendi basi kweli hapo kuna tatizo na hakuna unachoweza kufanya.
Haya mambo sijui yanakuwaje.

Anonymous said...

haya mambo magumu ,mimi ni victim wa parental favoritism .kwa case yangu tangu ,nimekuwa mtoto mzuri tangu mdogo ,kinidhamu ,kitaaluma n.k kiasi ambacho hata majirani/jamii inayotuzunguka wengi ,hata leo wanakiri kwamba nilikuwa tofauti na wenzangu wengine .wazazi wenyewe hilo pia wanalijua .lakini kwakweli sijui ,na kwa kweli imeniathiri mpaka leo .
unasoma shule mmoja ya boarding ya boarding na ndugu zake , wenzako wanauliza we mbona huka kile kama ndugu yako ,we mbona hiki chako kiko tofauti ,nilikuwa nakosa majibu maana kwa kweli sijui .nilikuwa na nalia sana ,hiki kitu mpaka leo huwa nikikumbuka nalia.afadhali ningekuwa mjeuri au mjinga ningepata amani nikijua labda hiyo ndio sababu.sina watoto bado ,lakini nikipata nimejifunza hakuna kibaya kama hicho ,japo ukibahatika kupendelea unaweza usielewe jinsi gani inaumiza .Rai kwa wazazi ,hata kama unadhani kwasababu unampenda mwingine zaidi ,huwezi kuwapenda sana ,jitahidi usionyeshe.
kaka mbilinyi amezungumzia sherehe kuwa tofauti imenigusa sana ,hilo pia lilinipata pia nafikiria hata sielewi .kwa hilo swala kwa ujumla nina kidonda ambacho sijui kitapona lini

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana kwa wote ambao wameumizwa na wazazi hasa kutokana na tabia hii ya kupendelea mtoto mmoja.
Kwa sisi wazazi tukumbuke kuwa fair kwa watoto wote haijalishi ni mtoto mkorofi au mtiifu kiasi gani kwani kila mtoto yupo tofauti sana na ana haki ya kupendwa sawa na wengine.

Wazazi tukumbuke ukimpendelea mtoto mmoja unamuumiza yeye na unawaumiza wengine pia na hii ni maisha yao yote.

Upendo daima

angel said...

hy
katika familia yenye watoto zaidi ya wanne lazima kupendeleana kuwepo,maana hata israel(yakobo)alikua na watoto 12 lakini yule wa mwisho Joseph alipendwa zaidi ata wenzake wakapatwa na wivu ndio maana walimuuza(from bibble)
but al in al hakuna mzazi aliye normal amchukiaye mwanae wa kumzaa
god bless you guys

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Angel,

Upo sahihi kwamba upendeleo upo na wakati mwingine hata watoto wawili tu bado kila mzazi au wazazi wote hupendelea mmoja wapo na wakati mwingine ni kama something natural.

Kitu cha msingi kama wazazi tunatakiwa kuhakikisha tunajitahidi kutoonesha upendeleo wazi ambao hata watoto wenyewe wakilalamika mama au baba anakuwa kama kiziwi kwani kuna matokeo mabaya sana kwa mtoto anayependelewa na yule asiyependelewa katika maisha yao baadae na katika jamii pia.

Treatment tunazowapa watoto wetu ziwe sawa bila kupendelea.

Upendo daima