"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, October 14, 2009

Usikimbie tatizo!

Dunia tunayoishi huwezi kukwepa kukutana na tatizo au shida au mkwara au majaribu au mateso au ugumu wa maisha eneo lolote.
Hata hivyo linapokuja suala la ndoa au mahusiano kuna njia mbili tu za kukabiliana na hayo yote hata kama ndoa yako inahisi ni mbaya, hairidhishi au ambayo ndani hakuna kuelewana au unaona kabisa ni kweli inaelekea kwenye shimo.

Njia ya kwanza ni kuachana kabisa kutafuta jibu (IGNORE) na njia ya pili ni kukabiliana na tatizo lililopo hadi kuhakikisha unapata jibu (FOCUS).

Hata katika maisha ya hapa duniani njia ni mbili tu, wapo watu wakikutana na matatizo au shida huamua kukimbia au kuruka au kurudi nyuma au kukwepa na kwenda zao na wengine hukabiliana nayo uso kwa uso hadi kieleweke yaani hawa kama wameokaka basi huamua kufia kwenye maombi. (Anyway kabla hujaishiwa nguvu Mungu huwa anakuwa ameshajibu!)

Ukweli kukimbia tatizo kuna raha yake (raha ya muda) kwani kuna ahueni (relief) ambayo mtu hupata hata hivyo habari mbaya ni kwamba mwisho wa yote ni maumivu makali na kujuta.

Na wale wanaoamua kukabiliana hujikuta katika maumivu makali mwanzoni na mwisho wake ni ahaueni na kupata nafuu ya kudumu au kula kuku kwa mrija hata hivyo hapo kunahitajika imani na kuwa na imani ndipo kwenye tatizo kwani wengi imani huwaota mabawa mapema sana.

Fikiria unaumwa tumbo na unapokumbuka gharama za vipimo pamoja na shughuli nzima ya kumuona daktari unaamua kuachana nalo.
Ukweli ni kwamba maumivu ya tumbo yataendelea kwani ni dalili kwamba afya yako katika tumbo haipo sawa na dawa ni daktari kuchukua vipimo hata kama utatumia gharama na ajue tatizo la tumbo lako ni nini na zaidi akupe tiba kamili mapema.

Tumbo haliwezi kupona kwa sababu umeachana nalo kwani maumivu yataongezeka na gharama ya vipimo na kutibu itakuwa zaidi kwani unapokimbia (achana nalo) tatizo linalizidi kuwa kubwa badala ya kumalizika.

Kumbuka ndoa yako ni mfano wa tumbo pale likianza kuuma, fahamu unahitaji kufanyia uchunguzi na vipimo na hatimaye kupata dawa inayotakiwa.
Inawezekana unapita katika ndoa yeny uchungu na maumivu makali na unawaza kwamba kuachana na mume au mke ndo dawa.
Ukweli si dawa dawa ni kupiga magoti na kumuomba Mungu akupe hekima na kukabiliana na tatizo lililopo.
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana.
Ubarikiwe na Bwana!

No comments: