"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 29, 2009

Ningewapa kidonge chao hiki!

Je, ni kitu gani ambacho ungekibadilisha kuhusu wanawake wa leo au kama kungekuwa na dawa ungewapa dawa gani kutibu ugonjwa gani kwa wanawake wa leo?

Ningeaandaa matibabu kwa wanawake wote duniani bila kujali yupo Amerika, Ulaya, Asia, Australia au Africa.
Hayo matibabu ni ya kumpa kila mwanamke dose ya afya ya kujiamini (self esteem) na kujisikia anastahili vile alivyo (personal worth) ambayo wangetumia kila siku hadi dalili zote zipotee kwani hili ndilo hitaji kuu la wanawake wengi leo duniani.
Weusi wanatamani wawe weupe, wengie nyewele fupi wanatamani wawe na nywele ndefu, wafupi wanataka wawe warefu, wanene wanataka kuwa wembamba na wembamba wanataka kuwa wanene.

Mama wa nyumbani anataka kuwa mama wa ofisini na kila mwanamke ambaye ni wa nyumbani anajuta na kujiona hana maana hata kama mume wake au wote kwa pamoja na pato kubwa kuliko wanavyoweza kutumia.

Kama wanawake watakuwa respected katika roles zao katika jamii kama mke na mama wasingekuwa wanachukia kuwa mama au mke wa nyumbani au jukumu la kuwa mama na mke.
Kama wanawake wangejisikia wapo sawa na wanaume katika personal worth basi wasingetafuta usawa wa responsibilities kwa wanaume.

Kumbuka sijakataa mwanamke kuwa ofisini au mwanamke kufanya kazi ambazo wanaume wanafanya bali nazungumzia mwanamke kujiamini na kujiona kama alivyo ndivyo anafaa kuwa na si kutamani kuwa kama fulani au mwanamke mwingine.

Hofu zingine!

Mwanaume na mwanamke wanapokuwa kitandani (uchi) ni suala kubwa na linaloonesha ukaribu wa hali ya juu sana hata hivyo mwanamke (siyo wote) ndiye ambaye hujikuta yupo wazi kwa hofu kuu mbili ambazo ni:-
Kwanza ni je, mwili wangu utakataliwa au utakubaliwa na kusifiwa?
Pili ni je, mwanaume atakuwa na mtazamo gani kuhusiana na mwili wangu?
Nipo beautiful au ugly?

Turudi kwenye bible tuone mwanaume anayejua kupenda alichukua au alifanya nini kwa mpenzi wake au mke wake kuhusiana na hizi hofu kuu mbili.

Wimbo Ulio Bora 1:1-8
Inaonesha hawa wanandoa walikuwa wanapendana sana na mwanamke alikuwa na hofu kufanya kazi kwenye jua kwani jua lilimfanya aonekane mweusi mweusi.
Hata hivyo mwanaume alichokifanya ni kumwondolea hofu mke wake kwa kumsifia sura nzima (Wimbo Ulio Bora 4: 1 – 16)

Je, kama wewe ni mwanaume umewahi kumsifia mke wako kwa maneno ya kutosha naye akajisikia kweli ana mwanaume anayejali?


Atafute kipato kwanza!

Wametaka wenyewe, tumewapa!Wanaume wengi tangu watoto wamepitia malezi yanayowafanya kuwa watu muhimu kwa ajili ya kutafuta kipato cha familia.
Hilo ndilo jambo la msingi ambalo familia yoyote au jamii yoyote au tamaduni zozote huhakikisha mtoto wao wa kiume analifahamu jukumu hilo.

Jambo la pili ambalo wanafundishwa ni suala la mahusiano na jinsi ya kuishi vizuri na mke hata hivyo hivi vitu viwili ni kinyume (opposite) kwa mwanamke ambaye yeye huanza kufundishwa masuala ya mahusiano kwanza na baadae suala la kipato katika familia.

Hata hivyo dunia imebadilika sana kwani wanawake nao wanakuja juu kuhusiana na suala la kuchangia kipato katika familia na wapo ambao sasa wao (wanawake) ndio wanashika usukani kuhakikisha familia inasimama imara linapokuja suala la kipato.

Swali ni je, wanaume sasa nao wanabadilika ili kuwa wanaume wazuri linapokuja suala la mahusiano kama ambavyo wanawake wanavyokuja juu na kuwa mstari wa mbele kuhusiana na suala la kipato?

Naamini kila mmoja ana jibu lake

BBC!

Linapokuja suala la ndoa BBC ni kifupi cha maneno ya kingereza yaani Before Baby Came (Kabla mtoto kuzaliwa)
Je, BBC ina uhusiano gani kwa ndoa au mahusiano?
Wanawake hujisikia wanavutia sana kimwonekano wakati wa BBC na ikipita wanawake hujikuta wanashindwa kurudi (regain) kwenye umbo na mwonekano ule wa BBC bila kujali wanafanya mazoezi kiasi gani au kukwepa chakula (dieting)kiasi gani.

Jambo la msingi ni kujiamini mwenyewe yaani mwanamke kujikubali kwamba kama alivyo amekamilika na wakati mwingine hawezi kufanya chochote zaidi ya kuwa na mtazamo positive kuhusu yeye na mwonekano wake na kuhakikisha all the time yupo smart.

Hata wanaume nao wamekuwa na mtazamo wa kisasa (usio sahihi, uliopotofu) badala ya kusaidiana na mke wake au kumtia moyo kuhusiana na kurudi kwenye umbo lake la BBC yeye anaanza kumlaumu na kumtamkia maneno ambayo si romantic au yanayomfanya mwanamke kuwa turned off idara zote.
Kumbuka uliweka ahadi kuwa naye katika raha au shida, anenepe kama kinguruwe au awe mwembamba kama mbu ni wako na hadi kifo so jambo la msingi ni kutiana moyo na kusaidiana mke kurudi kwenye umbo lake au lile wewe unapenda na si kamwe kumsema au kumtolea maneno yasiyo ya kistaarabu.

Kazi aliyofanya mwanamke kukuzalia mtoto si utani si ndogo si mchezo si lelemama wala masihala ni kufa na kupona na kazi ya ziada na maumivu, uchungu na zoezi zima la kuzaa mtoto kwake ilikuwa muujiza na huwezi kulinganisha na mwili wake alionao sasa.
Kwa nini usiamue kumwambia nakupenda kama ulivyo na ubarikiwe kwa mtoto/watoto ambao tumezaaa pamoja kwani hilo ndilo jambo la msingi zaidi kuliko looks/appearances.

Usione vinaelea vimeundwa!

Thursday, November 26, 2009

Ni Afadhali!

Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.
(Mithali 21:9)


Wednesday, November 25, 2009

Je, ni Muhimu Kiasi gani?

Je, sex ni muhimu katika ndoa kiasi gani?
Wanandoa wengi wana struggle sana ili kuhakikisha ndoa yao inakuwa ya kuridhisha ingawa ni kweli ndoa yoyote imara huhitaji efforts kwa mke na mume ili mambo kila siku yawe mazuri na vicheko vya hapa na pale.

Swali la leo ni kwamba Je, baada ya ndoa kutokuwa na sex ni kitu gani kingine kinaweza kuwafanya wanandoa kushikana au kubaki na bond strong?
Je, ni familia yaani watoto na kule kujisikia ni mke na mume au ni urafiki wa kubaki kuishi kama dada na kaka walioamua kuishi pamoja?

Je, unaweza kuishi kwa kuridhika katika ndoa ambayo hakuna sex kwa hiari yaani si ugonjwa au tatizo ambalo daktari amethibitisha bali wanandoa wameamua tu?

Kila mmoja ana majibu yake ambayo anayo kichwani, mwingine atasema ndiyo na mwingine atasema hapana haiwezekani kuishi bila hiyo huduma.

Hata hivyo ni kweli sex ni muhimu sana katika ndoa, na ukishaingia kwenye ndoa ina maana kwamba umeingia mahali sahihi ambapo sex ni kitu cha bure na si dhambi, kwani sex ni mali ya ndoa, nje ya ndoa ni uchafu na laana kama si dhambi na kuwa na hatia.
Hii ina maana kama ni mwanandoa usipopata sex ndani ya ndoa huna sehemu nyingine ambayo unaweza kupata hiyo huduma.

Hii ina maana kwamba unayokazi ya kuhakikisha ndoa inakupa ridhiko na kuridhika huanza kwa kupata huduma muhimu kama sex.
Ni kweli siku hazifanani na hukuna ndoa ambayo kila siku na masaa yote 24 katika siku 365 na robo wanakuwa na hamu na sex, zipo siku kunakuwa na ukame na kuna siku kuna kuwa na mvua ya libido kwa wawili kuwa mwili mmoja.
Kuna njia nyingi za kuwa connected na kurudi kwenye mstari na kuruhusu mapenzi upya (intimacy), tatizo kubwa ni pale mmoja wa wanandoa anapojisahau na kukosa kuwa caring, gentle, tender na maneno mengine mengi tu ya kimapenzi kwa mwenzake.

Kitu kilicho muhimu kwetu ambao tumeoa na kuolewa ni kwamba sex ni haki yetu na tunahitaji kuwa wazi kueleza matarajio yetu, mahitaji yetu, interest zetu na vile tunajisikia au tunapenda wapenzi watu watufanyie.
Kwa wazazi wetu tulipata kila kitu ila kimoja tu ambacho ni sex na tumekubaliana kuishi pamoja kwanza ili kuondoa upweke na pili ili kuufurahia uumbaji kwa njia ya sex kwa mke na mume.
Ndoa yenye furaha na bora ni ile ambayo ina balance mizani katika vitu vitatu yaani
Kwanza ni mwili,
Pili ni nafsi na
Tatu ni roho.
Kimoja kikikosekana tu basi kasheshe huanza na tofauti huendelea kutafuna ndoa kisirisiri kama mchwa.
Ni ukweli usiopingika kwamba sex ni muhimu sana kwenye ndoa kwani ni kipimo cha wanandoa wapo karibu kiasi gani na zaidi jinsi gap la hitaji la mmoja kuhitaji huduma linavyozidi kuwa kubwa ndivyo na mambo mengine yatakavyoweza kuharibika na hatimaye migogoro mingine huzaliwa.

Inawezekana mume wako au mke wako ana hasira, ukali, majibu ya mkato, kuwa mbali na wewe, kutumia muda na rafiki zake au kufanya vitu vingine badala ya kukaa na wewe si kwa sababu ya makosa unafanya bali kutopenda kwako sex.

Sex si hitaji la mwili tu katika ndoa bali ni kuonesha (approval) kwamba mume au mke wangu ananipenda, ananihitaji, ananijali, ninamvutia na napendeza na zaidi kuwa connected.
Frustrations nyingi za wanandoa huanza kwa masuala ya kitandani kuwa baridi.

Kwa maelezo zaidi soma hapa.

Take good care!

Tuesday, November 24, 2009

Una ripoti ya ukaguzi?

Mchwa umefanya kazi yake!
Mwenye nyumba alihitaji ripoti ya ukaguzi wa mara kwa mara! "Mpenzi …………,nionyeshe uso wako, na niisikie sauti yako, kwa maana sauti yako ni tamu, na uso wako unapendeza.
Tukamatie mbweha, mbweha wadogo wale wanaoharibu mashamba ya mizabibu, mashamba yetu ya mizabibu yalichanua".
(Wimbo ulio Bora 2: 1-15)

Ukisoma kitabu cha Wimbo ulio bora katika Agano la kale sura ya 2 kuanzia mstari wa 1 hadi ule wa 14 unakutana na maneno ya wapenzi wawili (wanandoa) ambao wana wakati mzuri na wanaongea lugha ya kimahaba, wapo faragaha kimapenzi (intimacy) wapo deep in tender affection na it is romantic.

hata hivyo kufika mstari wa 15 maneno yanabadilika na wanatangaza kuwa na tahadhari na kuonya kwamba kuna mbweha wadogo wanaoharibu shamba lao la mizabibu iliyochanua na wawakamate.
pamoja na kuwa na mapenzi matamu, mapenzi yanayokua na kuongezekan kuwapa raha bado wanafahamu kwamba kuna mbweha wadogo wanaweza kuharibu ndoa yao.

Kinachofurahisha ni kwamba wapo very concerned na hao mbweha wadogo na kila mmoja anaonekana ni inspector mzuri wa mahusiano yao.

Pamoja na uzuri wote wa mapenzi bado mmoja wao amechukua hatua ya kuwa inspector na kuomba hao mbweha wadogo wakamatwe na kuondolewa.

Hili ni somo zuri kwa mwanandoa yeyote kuwa makini na mbweha wadogo ambao wanaweza kuharibu ndoa ikawa chungu kama limau.

Ni muhimu sana kukagua mahusiano yako wewe mke na mume kuangalia kama kuna mbweha wadogo na inawezekana ndoa yako isiwe na mbweha wadogo bali wadudu wadodgo kama mchwa ambao wanaweza kuvamia ndoa yako na kuodondosha ghafla bila kutegemea.

Katika sehemu ambazo kuna mchwa ni rahisi sana nyumba zilizojengwa kwa miti na mbao kutekekea kwa mchwa kuliko moto.
Mchwa ni wadogo na huwa kimya hata hivyo ni industrious zaidi kuharibu nyumba kuliko moto ambao hata media nyingi huzipa nafasi zaidi.

Kumbuka, ni vitu vidogovidogo sana ambavyo kwenye ndoa ndivyo vyenye umuhimu iwe kujenga au kubomoa na mara nyingi hasa sisi wanaume (si wote) huwa tunaamini vitu vidogovidogo (kama vile kumwambia mke nakupenda, au kumbusu, au kumkumbatia au kumsifia pale amefanya kitu kizuri au pale amependeza nk) havina nafasi sana katika kujenga ndoa au kubomoa ndoa, ukweli ni kwamba vina maana sana.

Matukio kama kupoteza kazi, Ugonjwa wa ghafla, kifo cha motto nk mara nyingi huimarisha ndoa kuliko vitu vidogo.

Hivyo kama mwanandoa hakikisha unafanya ukaguzi mara kwa mara kama kuna mchwa unakula ndoa yako au wale mbweha wadogo ambao wanapenda kuvamia shamba lenu la mizabibu iliyochanua.

Ubarikiwe na Bwana!

Monday, November 23, 2009

"Too late to catch the bus"

Afadhari hujachelewa basi la abiria!Mara nyingi hobbies husababisha wanandoa kuwa na mawasiliano mazuri, kuongea pamoja, kuwa na kicheko na kufanya vitu kwa pamoja.
Inakuwa ngumu sana kuwa na mawasiliano mazuri pale inapotokea wawili walioamua kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha kila mmoja kuwa na hobyy yake kiasi kila mmoja anachukukia kile mwenzake anapenda.

Kuna hii story kwamba kuna mwanamke mmoja katika nchi fulani isiyo na jina ambaye aliamua kuwekeza kwa watoto wake na akamsahau mume.
Hawa wanandoa wawili walioana na wakawa na wakati mzuri sana pamoja kabla ya kupata watoto.
Baada ya kupata mtoto wa kwanza mke akawa anatumia muda wote kwa ajili ya mtoto hakuwa na muda tena kwa ajili ya mume wake.
Baada ya miaka 3 mtoto wa pili akazaliwa na sasa mama akawa too much occupied na watoto hivyo mume kuwekwa pembeni kwani kila kitu sasa ni “Watoto kwanza”.

Mume kuona hivyo akaamua kuwa na maisha yake yaani kuwa na marafiki wengine ambao anaweza kuongea nao, akatafuta masikio mengine ya kike ya kumsikiliza feelings zake, si unajua mwanaume huhitaji masikio ya mwanamke wakati fulani kati maisha yake ili kuongea kile anaamini kinamfanya yeye kujiona ni mwanaume.
Lazima tukubali kwamba kila mmoja aliumbwa na uhitaji wa jinsia nyingine hata kama hakuna sex bali sharing ya siri, mafanikio na matatizo ya maisha haya au masumbufu ya maisha haya.

Mwanaume akawa na watu wapya ambao aliunganisha feelings zake iwe ni hobbies au interest ilimradi maisha yawe na ladha, jambo la msingi ni kwamba alifahamu kwamba mke wake yupo na watoto na anahitaji kuwa na maisha yake.

Maisha yakawa yanaenda kama kawaida huku mke na watoto wake na mume na kazi na maisha yake mwenyewe.
Wale watoto wakakua na wakafika wakati wa kwenda college, na wakawa sasa wanarudi wakati wa likizo tu, ndipo mke akaanza kujisikia upweke na kuanza kujitahidi kujiunganisha kwa mume wake ambaye miaka 25 iliyopita waliacha connection kama mke na mume kuongea pamoja na sharing ya mambo mbaliombali ya maisha.

Sasa mwanamke anajigonga kwa mume waanze kuongea, waanza kuwasiliana, waanze kuenjoy intimacy, waanza kufurahia maisha kama mke na mume hata hivyo mume anamwambia mke
You are too late to catch the bus
kwani alishajitengenezea maisha yake ya nani wa kuongea naye, kuwasiliana naye na zaidi yeye mke anaweza kuendelea kuongea na watoto si alijua atakuwa anaongea na watoto maisha yote?

Hata hivyo kibaya zaidi sasa watoto wameolewa na mama akitaka kwenda kwao au kuongea nao wanamwambia lazima atoe taarifa kwani wanapenda sana kutumia muda wao na wapenzi wao na si mama tena.

Sasa mke anaishi kwa upweke ingawa mume anaye.

Upweke (loneliness) ni kitu kinachohuzunisha sana bila kujali upo umri gani, hata hivyo kuwa mpweke na uzee maumivu ni makali zaidi.
Je, ingekuwaje sasa kama tangu wanaoana na kuwa na watoto huyu mwanamke na mwanaume wangekuwa walitengeneza mawasiliano mazuri?
Au Urafiki mzuri?
Au Mapenzi ya kweli?

Kumbuka kuna wanaume wengi ambao baada ya watoto kuzaliwa wamejikuta katika upweke uliokithiri.
Na baada ya kupita kwa muda wa miaka mingi barabara hii ya upweke hufika mahali ambapo hata siku mke akitaka waanze upya mawasiliano huwa too late to catch the bus.

Hivyo kama wewe ni mwanamke ni muhimu sana kuwa na busara na hekima ya kuhakikisha mume unampa nafasi katika maisha yako hata kama unajiona una wajibu mkubwa kwa mtoto au watoto ulionao na muhimu weka priorities kwa mume kwanza maana watoto hawawi watoto milele.
Unaweza kuwa mama na mke kwa wakati mmoja na mwanamke mwenye busara huanza kama mke na kumaliza kama mke.
Ubarikiwe

Sunday, November 22, 2009

Nimempa kile anapenda!

Siri kubwa
Kuna usemi wa msingi sana kuhusiana na ndoa hasa linapokuja suala la interests na hobbies kati ya mume na mke.
Jambo la msingi kwa mke ni kukumbuka kwamba kuna progress zingine katika ndoa huja polepole sana, na kama utakuwa mvumilivu na caring vya kutosha ipo siku utaona mambo yanalipa.

Ni muhimu sana kwa mke kujifunza kitu chochote hata kama ni kidogo sana kuhusiana na taaluma ya mume wake na hiyo itakuwa moja ya siri kubwa ya kuondoa upweke na kusaidia kuwa kitu kimoja kuliko kubaki kimya na kukiri kwamba that is his stuff.

The man who can do anything he feels like doing with a woman, is more likely to say everything he feels like saying.

Nina rafiki yangu ambaye ni dereva wa magari na anapenda sana masuala ya magari na mnaweza kuongea habari za magari usiku kucha na hakuna kitu anapenda kama kazi ya kuendesha magari.

Mke wake ana busara sana, anajua ugonjwa wa mume wake ni magari na kitu chochote kinahusu magari, usipopenda magari kama mke ina maana ni upweke.
Anachofanya mke wake ni kwanza siku za Birthday parties anamnunulia vitu vinavyohusu magari anayopenda mumewe kama Tshirt na kofia zenye majina ya makampuni ya magari na zaidi mke hununua movies mbalimbali zinazohusu magari na yeye na mumewe huangalia na kuwa na muda mzuri.

Ni kweli kugundua kile mume wako anakipenda kama hobbies zake au interest zake ni siri na silaha muhimu sana kwa mwanamke yeyote anayetaka mume awe anaongea lugha moja na yeye.

Inawezekana mume wako anapenda sana kuimba kwaya, au kusoma bible au kusoma vitabu au kupanda maua au kupanda miti au kucheza gitaa au vyovyote vile, siri kubwa ni kwamba ukitaka mume wako aende extra mile jiingize kwenye interest zake kama si zile za kutenda dhambi.

Nimejiunga naye.... Amebadilika!

Mume wangu hapa humtoi! James ni mwanaume anayependa sana soka si kuangalia kwenye Tv tu bali hata kuhudhuria mechi mbalimbali kuanzia uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hadi mechi ndogondogo mitaani na wakati mwingine kukiwa na mjadala wowote kuhusu soka basi hapo ni ugonjwa wake yaani anajisikia raha na anajisikia yupo nyumbani.

Mke wake Jane tangu wameoana amekuwa hapendi kabisa kusikia habari za mchezo wa soka na amekuwa analalamika (kefyakefya) kwa tabia ya mumewe James kupenda soka kiasi hicho kwani wakati mwingine huondoka nyumbani kwenda kuangalia mechi za ligi kuu ya Uingereza na kurudi usiku sana.
James ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Asernal Uingereza na timu ya Yanga jijini Dar Es Salaam.

Baada ya kusemana sana na kuzozana sana, ilifika siku Jane akaamini kwamba ni kweli mumewe hawezi kubadilika kuhusu kuacha kuwa shibiki na mwanaume mpenda soka kupindukia na zaidi kila anavyozidi kumsema na kumlalamikia ndivyo James anazidi kujiweka mbali na kupenda soka na kutumia muda zaidi kuangalia TV au kwenda kwa wenzake kuangalia na kuchelewa kurudi nyumbani.

Jane anasema kwamba
Tangu nilipogundua kwamba sasa mume wangu hawezi kubadilika nimeamua kujiunga naye (if u cant fight them join them) hivyo siku hizi namuuliza hii weekend kuna mechi ya nani na nani ili tuwe wote na kama kuna mechi kwenye Tv basi tunakaa wote tunaangalia na ikifika break time nampa snacks na tunaendelea kuangalia.
Kama kuna mechi uwanja wa taifa basi tunaenda wote na kuangalia mechi, sikutegemea kama itakuwa raha kiasi hicho kwani kitendo cha mimi kuheshimu interest zake kumekuwa na connection mpya kimapenzi ndani yetu na pia na mimi nimekuwa najisikia raha sana kuongea kitu kile na mume wangu anakipenda.
Tangu nimeanza kuwa upande wake kuhusu soka matokeo ni kwamba sasa James amekuwa mwanaume mzuri maeneo yote ya ndoa yetu na pia amekuwa sasa anapenda kuongea yale mimi napenda kwani anasema mimi napenda yale yeye anapenda na nimejifunza kwamba kulalamika kwangu hakukuwa msaada au njia nzuri ya kutufanya mimi na yeye kuwa kitu kimoja katika ndoa yetu”.


Unaweza kustaafu mpweke!

Kustaafu kazi huwa maisha ya upweke sana kwa wanandoa kama waliishi maisha yakukuwa bila mawasiliano kwa miaka mingi.

Wanandoa wawili ambao mume alikuwa anapenda sana kucheza Golf walikuwa na kwaida ya kwenda vacation katika kisiwa Fulani huko Amerika ya kusini.
Mume alipenda sana kwenda huko katika hicho kisiwa kwani alikuwa na wakati mzuri sana kucheza golf ingawa mke wake na golf vilikuwa vitu viwili tofauti kama vile kibaka na polisi.

Huyu mwanaume alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa na hawakubahatika kuwa na watoto hivyo alipanga kwamba akistaafu kazi atahamia kwenye hicho kisiwa ili amalizie maisha yake kwa kucheza golf kwani kwa kucheza golf kutamsaidia kuweka mwili wake fit ukiacha kwamba golf ilikuwa interest yake na moja ya hobby muhimu sana kwake.

Swali lilikuwa na mke wake mpenzi ambaye kwake Golf ilikuwa ni kitu kigeni na kitu ambacho hapendi si kusikia tu bali kuona mume wake mwenyewe anapenda.
Hata hivyo siku moja alikaa chini na kujiuliza hivi maisha yatakuwaje kama tukistaafu mume wangu ameamua tuhamia kwenye kisiwa maarufu cha golf na kununua nyumba na kumalizia maisha yetu huko.
Je, nitaishi maisha gani kama mwenzangu kila siku itakuwa ni golf tu na mimi na upweke wangu?
Si nitakuwa mjane wakati mume bado ninaye?
Itakuwaje kama na mimi nikijifunza golf na kuhakikisha atakapokuwa anaenda kwa golf tunakuwa wote sambamba?
Je, ni raha ilioje kama wote kwa pamoja tutakuwa na wakati mzuri pamoja kucheza golf kila siku?
Je, nitaanzeje wakati hata golf sijui?

Kwa kuwa walikuwa wamebakiza miaka miwili tu na kuhamia moja kwa moja kwenye kisiwa maarufu cha golf huyu mwanamke alifanya uamuzi wa kuanza kujifunza kucheza golf kwa nguvu zote na uwezo wote.
mara nyingi tunakubali hatuwezi au hatutaki kwa sababu tumeamua kwamba hatuwezi na hatatuki na huo ndio mtazamo wetu hata hivyo mwenzetu aliamini kwamba bado anaweza kujifunza na kuwa mcheza golf mzuri.
Kwa kuwa shughuli za mumewe zilikuwa ni za kusafiri mara kwa mara ilimfanya mke wake kuwa na muda wa kutumia vifaa vyake na kwenda kujifunza (si unajua kuna wanaume wala huwa hawajali wake wanafanya nini baada ya wao kusafiri).
Alijifunza kwa miaka miwili na kuficha hiyo siri kwa mumewe hata hivyo baada ya kuhamia kwenye hicho kisiwa ikawa golf na wao na wao na golf na ikawa furaha ilioje kwa mume kuona mke wake nae kwenye golf wamo.
Hii ni moja ya success story ya kumfanya mume awe anaongea na wewe mwanamke.

Kumbuka unachokifanya sasa ni muhimu sana kwa ajili ya maisha yako ya uzeeni kama wanandoa.
Kama hamuwezi kuwasiliana leo, usitegemee kesho mtaweza kuwasiliana ghafla.

Mke wa Professor!

John ni professor katika chuo kikuu kimoja nchini Canada.
Huandika papers za nguvu, na kutoa lectures zenye heavy stuff na hutumia muda mwingi sana library.
Mke wake ambaye anaitwa Linda anampenda sana mume wake ingawa kimadarasa wapo tofauti sana ni kama mlima kilimanjaro na kichuguu.
Linda anapenda sana kuwa karibu na mume wake John tatizo utaongea kitu gani na Professor mwenye uelewa wa juu kiasi hicho?

Linda akafika mahali akajiuliza itakuwaje maisha kama haya ambayo mke na mume hawana kitu cha kuongea pamoja?
Baada ya kutafakari kwa umakini sana akagundua kwamba mume wake anaandaa paper inayohusu ndege (birds) na kwa kuwa hata yeye anawafanya ndege akaona ndiyo mwanya pekee wa kuunganishwa na mumewe.

Linda akaenda kununua vitabu vinavyohusu ndege, na akamuomba mumewe wahudhurie semina na kitu chochote kinachohusu ndege na ikajibu kwani hata mumewe akawa anapenda sana kuhusu ndege na wamekuwa sasa wanafanya hata vacation mahali ambapo wanaweza kwenda kuangalia ndege (bird watching)

Ni miaka 20 sasa wanafanya kitu kimoja na kufurahi pamoja. Linda hajui lectures ambazo mumme wake hutoa chuo na pia hajui kozi gani anafundisha ila anajua kitu kimoja tu kwamba yeye na mumewe linapokuja suala la ndege huongea pamoja na kuwaunganisha pamoja kama wanandoa.
Kuna usemi kwamba hobbies ni kitu kinachowaleta wanandoa pamoja na ni kitu kizuri mno.
Inawezekana mumeo ana interest na kitu fulani na kupitia hicho kitu ukiungana naye unaweza kumleta karibu zaidi katika maisha yako kuliko unavyopingana naye.
Jambo la msingi ni kuhakikisha hicho kitu si dhambi.
Kama mumeo ni mlevi wa kutupwa kuungana naye ni kujimaliza mwenyewe!

Wednesday, November 18, 2009

Usiumie!

Hello rafiki Jane,

Asante kwa barua yako ambayo niliipata jana usiku.

Pia pole sana kwa wasiwasi na hofu hata mashaka kutokana na yale unakutana nayo kuhusu mumeo kupata secretary mpya ambaye unahisi anaweza kumteka mumeo.

Kwanza mdogo wangu naomba usipaniki, wala kuwa na hofu na mashaka, usioni ndoa yetu na John imefika umri wa miaka 30 kwani kuna milima na mabonde tumevuka pamoja na moja ya milima ni kama huo wa kwako kujipa wasiwasi kwamba mumeo atachukuliwa na mwanamke anayeshinda naye kazini.

Ni Adamu na Hawa ambao hawakuwa na maisha ya wasiwasi wa mume au mke kuchukuliwa na mwingine kwani wao ndo walikuwa wanandoa wa kwanza duniani hata hivyo kabla ya kuanza kuwa na hofu na mashaka naomba jiangalie kwanza kwenye kioo (sina maana uchukue kioo) nina maana jiangalie mwenyewe kwanza je unampenda mumeo kiasi ambacho unaamini mtu mwingine haweza kuchukua nafasi, maana kuna wakati sisi wenyewe wanawake tunajisahau mno kwenye ndoa zetu.

Nakumbuka nilipokutana na tatizo kama hilo la kwako ilinipasa niende kwa dada wa jirani hapa ambaye ni nyumba ndogo ya kigogo mmoja hapa mjini nikamuuliza inakuwaje au anafanya vipi kuhakikisha mume wa mtu anabaki kwake muda wote hadi anasahau familia yake.

Yule dada alinijibu kwamba anachofanya ni kumpa uhuru huyo mwanaume kusema na kufanya kile ambacho kwa mke wake hapati nafasi, hii ina maana kwamba mwanaume akifika kwake anakuwa huru kusema chochote anataka na kufanya chochote anataka kuanzia jikoni hadi chumbani.

Ile mume wa mtu akifika tu mlango anampokea kwa mabusu na hugs.
Swali je wewe unafanya hayo?

Unampa James nafasi na uhuru kiasi hicho au kila unachofanya unafanya just for granted?

Ukifanya kila kitu kwa kadri ya upendo wako wote kwake basi haina haja kuwa na hofu na huyo secretary labda awe ni mwanaume ovyo.

Tutawasiliana zaidi na pia nitakupigia simu baadae saa mbili usiku tuongee zaidi na nitakushauri zaidi mdogo wangu.

Ni mimi Neema

Tuesday, November 17, 2009

Inaniuma sana!

Hello Neema,

Naamini wewe na mumeo John mnaendelea vema.

Mimi na mume wangu James tunaendelea vizuri ingawa kuna tatizo kidogo.
Ni mwezi sasa mume wangu amepata secretary mpya ofisini kwake na nimesikia huyo secretary bado ni msichana mbichi kabisa na mume wangu amekuwa akimtajataja na kilichonistua zaidi ni kwamba sasa mume wangu amekuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani tofauti na ilivyokuwa kabla ya huyo secretary wake mpya, kibaya zaidi jana amerudi saa sita usiku eti walikuwa na Board meeting.

Ninajaribu kujisahaulisha nisiwaze kuhusu mume wangu na secretary wake kitucha ajabu ni kwamba ndiyo nawaza zaidi na ninavyowaza zaidi natamani kuchukua hatua kubwa zaidi kuhusiana na hili jambo.
Nahisi mume wangu anaweza kutekwa na huyu secretary mpya maana mabinti wa siku hizi hawaaminiki kabisa na mume wangu anavyojua kutoa pesa hapa nina homa ya jiji.

Kilichonistua zaidi ni kwamba jirani ameniambia kwamba eti secretary ni mke wa boss ofisini yaani hapa inaniumia sana, sijui ni wivu au hasira au sijiamini acha tu!

Nishauri nifanyeje?

Ni mimi Jane

Monday, November 16, 2009

Wanaume wengine Ovyo!

Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Bakari akimsaidia mke wake hawa kuosha vyombo baada ya mlo huko Senegal.
Huyu mwanaume si ovyo!Umemfanyia vitu vyote ambavyo mwanaume anastahili kupata wa mke wake hapa duniani.
Umejitahidi kufanya vyote unaweza ili ajue wewe unawajibika kama mke ni yeye tu kusherehekea, hata hivyo matokeo yamekuwa zero!
Sasa swali linakuja
Je, ni kweli kuna wanaume wengine ni ovyo kabisa?
Naamini jibu ni ndiyo, wapo wengi tu iwe mjini au vijijini hali ni sawa.
Je, mwanaume ovyo yupoje?
Mwanaume ovyo ni yule ambaye hataki mabadiliko, na mojawapo ya mifano ya wanaume ovyo ni kama ifuatavyo:-

1. MWANAUME MLEVI (alcoholic)
Ni mwanaume mzuri sana (wonderful) akiwa hajalewa, tatizo ni kwamba si rahisi kumkuta hajalewa.
Anautwika siku nzima, tangu akitokea kazini kwenda nyumbani anakuwa tayari amelewa, anaporudi nyumbani huanza kufungua mlango wa nyumba kwa kelele tangu mita mia kabla ya kuufikia, akifika nyumbani anaanza kuangalia TV na anaenda kulala hapohapo kwenye kiti chake na siku zingine na haja ndogo hapohapo.
Kila siku au muda mwingine ananukia breweries na hii mke hujikuta yupo turned off completely idara zote.

2. MWANAUME ASIYEMWAMINIFU
ndani yake kuna kitu kinamuambia bila mwanamke mwingine yeye si mwanaume tena, hata mke wake ampe zawadi ya mwili kila siku bado akimuona mwanamke mwingine akili zake zinamruka na anachanganyikiwa bila kujali kinachoelea ni dhahabu au maluweluwe.

3. MWANAUME WA PESA, MALI NA MAFANIKIO
Ahadi yake ni kwamba siku tukipata milioni tutaanza kufurahia maisha, baada ya kupata hiyo milioni sasa anasema tukipata milioni 2 ndo tutaanza maisha, baada ya kupata milioni 2 sasa anasema tukipata milioni tatu ndipo tutaanza kufurahia maisha, inaendelea na kuendelea hadi uzeeni.
Ukweli huu ni ugonjwa ila hataki kukubali kwamba ni ugonjwa na kwamba anaumwa.
Eti atacheza na watoto akipata milioni 5, kumbuka watoto hawabaki watoto bali ipi siku wanakuwa watu wazima na kuondoka zao.
Hataki tufurahie tendo la ndoa eti yupo busy kutafuta hizo milioni, hajui miili ikizeeka inaishi kwa medication na hakuna nguvu tena za ku-enjoy sex kama wanandoa.

4. MWANAUME KATARI , JAMII YA AKINA HITLLER
unajua ilivyongumu kuishi na mwanaume mwenye mtazamo kwamba kila kitu unafanya fanya kama ninavyokuelekeza au in my way na anaamini huo ndio ushirikiana wa wanandoa.
Ni kama anajitahidi kufidia yale mama yake alikuwa anamfanyia na ni kweli kwake mwanamke ni kifaa fulani si mtu, si kiumbe sibinadamu.

5. MWANAUME BARIDI
Pole sana, huyu Ukitaka suala la sex amekufa, hana hamu, havutiwi na anaweza kukaa na mke miezi sita bila kufanya mapenzi na akaona ni kawaida.

Anaogopa kuongea na Daktari au mtu yeyote ili kupata msaada wa ushauri.
Anamuonya mke wake hakuna kutaka au kuongelea hili suala mahali popote na mtu yeyote.
Ni kama anamlazimisha mke kuwa na maamuzi ambayo mke hapendi na hakutegemea kama yangempata kwenye ndoa yao.

6. MWANAUME MWENYE WIVU WA KUPINDUKIA
Humuamsha mke wake usiku wa manane ajibu maswali yake ya nani aliongea naye mchana, ilikuwaje akawa ana smile alipokutana na James, nani alikuwa anaongea naye kwenye siku nk.
Mke huchoka kwa visa vya kutiliwa mashaka na kujiona mtumwa au yupo jela ndani ya ndoa yake.
Hii orodha ya wanaume hopeless huendelea hadi 7, 8, 9 hadi 116

Hizi ni ndoa ambazo kama ni daraja basi upande mmoja limevunjika na mmoja amegoma kufanya repair kwa ule upande umeharibika.
Katika ndoa za aina hii kuna mambo mawili yanaweza kutokea nayo ni
(a) Mwanamke huweza kuchukua kile tu anaona anakipata na kuamua kuishi katika uhusiano huu na zaidi mke hujijengea aina ya maisha yake anayayajua ndani ya ndoa aina hii na kuendelea kama vile hakuna matatizo yoyote
(b) Mwanamke huamua kuanza mbele (check out)

Na kama mwanamke ameamua kuchukua uamuzi (b) basi kuna maswali magumu na mazito yanahitaji majibu.
Utafanya nini kuhusiano na kipato,
Je utaondoka kwenda wapi?
Je watoto itakuwaje?
Je, Utakuwa mpweke bila yeye au siku moja hali itabadilika?
Kuna usemi wa kingereza kwamba:-
“Divorce doesn’t help a person prone to excessive anxiety and emotional upset”.

Wapo watu huendelea na safari kutoka kushindwa ndoa moja hadi nyingine au kutoka ya kwanza kwenda ya pili na kushindwa na kuendelea na tatu na kushindwa hadi nne, tano na nk, hadi pale wakibadili tabia na mitazamo yao.

Wanasaikolojia wanaita hii tabia ni symbiotics kwa maana kwamba kawaida tatizo hutafuta tatizo lingine (problems looking for matching problem) na hutokea ndiyo maana mara nyingi mwanamke anayemuacha mwanaume hopeless huenda kumpata mwanaume hopeless mwingine mwenye matatizo mapya kabisa.
Kuna data zinaonesha kwamba kati ya wanandoa 4 ambao hupeana talaka na kuoa tena 4 huishia kuachwa au kuachana tena.

NB:
Kumbuka kuna matumaini kwa mwanaume yeyote ambaye yupo ovyo au hopeless katika ndoa yako.
Hivyo basi ukimwamini Mungu ndoa yako inaweza kurudia katika matumaini mapya bila kujalisha ipo katika hali tete kiasi gani.
Kwani kwa Mungu yote yanawezekana.
(Mathayo 19:26)

Sunday, November 15, 2009

Uangavu

Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi????Kama kuna neno moja la msingi ambalo ni msingi wa ndoa yoyote neon hili ni Uangavu (transparency).
Kamusiinafafanua kwamba neno uangavu maana yake ni kuona kitu moja kwa moja hadi ndani, ni kuwa wazi, kuwa huru kimawasiliano na zaidi ni kuwajibika.
Uangavu katika ndoa maana yake kumuona mpenzi wako hadi ndani na kumfahamu vizuri bila shaka maeneo yote ya maisha yenu.

uangavu katika ndoa ni mwanaume au mwanamke kuweza kusoma sms na kupokea simu za mwenzake bila mashaka wala wasiwasi, kusoma emails zilizomo kwenye inbox yake bila wasiwasi wala hofu, Kufahamu akaunti yake benki ina kiasi gani, kuongea siri zako kwake bila mashaka na zaidi kuwa huru kuhakikisha mwenzako anajisikia vizuri kihisia.
Uangavu ni kuwa wewe bila kuwa na aina yoyote ya unafiki.
wanadamu tuliumbwa na uwezo au hamu ya kutaka kumfahamu mwenzako kwa undani hadi usiwe na shaka wala wasiwasi.
Transparency ni process na haiwezi kutokea usiku mmoja tangu umefahamiana na mpenzi wako ingawa wapo watu ambao hata akiwa kwenye mahusiano hataki mwenzake afahamu mambo yake kitu ambacho si lengo la mahusiano.
Uangavu ni kugundua au kupata uvumbuzi wa mambo mbalimbali mapya kwa mume wako au mke wako kwa sababu ya kuwekana wazi.
Bila kuwa na mawasiliano ambayo ni wazi mahusiano yanaweza kukwama.
Jambo la msingi ni wewe kuwa wazi kueleza kilichondani yako au siri zako kwa mwenzi wako (sincerely & straightfowawrd) na zaidi kushirikiana kupeana habari za kila kitu kinachohusu maisha yenu ili kuondoa wasiwasi, hofu na mashaka kwa mwenzako.
Kuficha vitu si jambo la busara na unapokuwa wazi na mwenzako naye anakuwa wazi kwako kwani kuwa wazi ni kufahamiana na kufahamiana ni mahusiano na binadamu tuliumbwa kuwa na mahusiano.
Je, upo wazi kwa mke wako au mume, au mchumba wako kiasi kwamba chake ni chako na chako ni chake?

Unachonga sana!

Ndoa nzuri huanza na watu wawili lonely, wakati mwingine huanza na wawili wasiojua kuongea (communicate) na baadae wakawa wazuri zaidi.

Je kuna njia yoyote ambayo mwanamke anaweza kufanya mume wake aongee kama hataki kuongea naye?

Ukweli siku zote ukitaka kuleta mabadiliko ni wewe mwenyewe kuanza kujiangalia kwenye kioo (yaani kwa kujiangalia mwenyewe).

Na jambo la msingi ni mwanamke mwenyewe kujiuliza je unaongea sana, je unachonga sana.
Wakati mwingine tunaweza kumasaidia mtu mwingine kuongea hasa kwa sisi wenyewe kupiga zip kwenye midomo yetu.

Wapo wanawake huongea kama kasuku muda wote na hii ni mbaya sana kwa mwanaume yeyote.
Kama hujajua kama wewe ni mwongeaji kuliko kawaida ukitaka kujichunguza basi angalia ukiwa na rafiki zako au ukiwa na mumeo unaongea asilimia ngapi ya maongezi kama ni asilimia 51 basi ina maana you talk too much.

Jambo la pili ni kuangalia unaongelea topic gani au ni topic zipi huwa zinatawala maongezi yako? Na je maongezi yako ni kuhusu wewe mwenyewe tu, au maongezi yako ni nyimbo ambazo mumeo hazipendi.

Jambo la tatu je unaongea topic za wanawake tu?
Hakuna mwanaume ambaye atavumilia kusikiliza women stuff muda wote au feminine stuff all the time.
Hivyo ni muhimu kuangalia subject na muda unaotumia kuongea.
Jambo lingine la msingi ni wewe mwanamke kujifunza vitu ambavyo huweza ku turn off mwanaume na asiongee na wewe.
Kwa maelezo zaidi soma hapa

Mmmmm.................

Mara nyingi tunaamini kile mtu anaongea sisi tunafahamu zaidi hata kabla hajamaliza na zaidi tunawakatisha kuendelea kuongea na kuwasaidia kumalizia kile walikuwa wanaongea.
Hatusubiri hadi wamalize kile wanaongea huku tukiwasilikiza ili waongee chote walitaka kuongea.

Sasa jawabu ni nini?
Wanasaikolojia wanasema kwamba jibu la hili tatizo ni pale tu watu tutakapoamua kusikiliza kwa kutumia sikio la tatu.
Hili sikio la tatu ni lile ambalo hutufanya kusikia maana ya yale maneno ambayo tunasikia, baada ya kuambiwa kila mtu mwingine anasema tunatakiwa kusikiliza na kusikiliza na kusikiliza na kusikiliza………..
Tunatakiwa kusikiliza hadi tunaelewa na kufahamu maana ya kile kinaongelewa.

Hii ni sanaa, hivyo unaweza kuwa na aina fulani ya signal kuonesha unaelewa kile anaongea.
Na signal nzuri kwenye ndoa ni uwezo wa kuitikia “Mmmmmmmm…. Na maana yake ni kwamba unavutiwa na kile anaongea na kwamba anatakiwa kukueleza zaidi au kuongea zaidi kwani upo tayari kusikiliza.

Wanaume nao........

Wanaume hufa mapema zaidi kuliko wanawake:
Kuna wazo ambalo kampuni nyingi za Bima zinalitamka wazi kwamba wanawake wengi wazee watakuwa wajane miaka 7 hadi 11 baada ya mume kufa.
Hii ina maana kwamba wanaume hufa miaka 7 hadi 11 kabla ya wake zao.
Sasa swali ni kwa nini wanaume hufa mapema zaidi ya wake zao.

Wanaume wengi hawako honest kwa wake zao kuhusu kitu chochote katika maisha.
Wanakuwa na maisha yaliyofungwa (boxed) zaidi kuliko wake zao.
Hii ina maana kwamba wanaume wengi huficha true feelings walizonazo, na kila wanapoficha hisia zao hupunguza life span yao.
Ni ngumu kuona mwanaume anatoa machozi, kulia kwa sauati, kukubali amechukia, kukubali ameshindwa, kukubali hawezi nk.
Ni kama anapozidi kuficha feelings zake anazidi kukaza kamba kujiua mwenyewe.
Je, hii ina maana wanaume ni green, hufa mapema hivyo kuwa na kiwango kidogo cha carbon print?
So wanaume ni environmentally friendly!

Ni mmoja tu au wawili duniani!

Matatizo ya kimapenzi katika ndoa
Kila mwanandoa isipokuwa mmoja au wawili tu duniani hatakuwa na matatizo yanayohusu tendo la ndoa na wengi wanaokwambia hawana matatizo yoyote watakuwa wanakudanganya na unatakiwa kuwa makini kuwasilikiliza kwa sikio lako la tatu.

Kila mwanaume tangu siku akioa lazima atakutana na tatizo lolote iwe kukojoa mapema (pre ejaculation), kutosimamisha (kudindisha), kukosa uzazi nk. Vyote ni sehemu za changamoto ya kuendelea kujifunza.

Habari njema ni kwamba kuna njia ya kuondoa haya matatizo ukianza na moja hadi jingine na njia sahihi ni kukubali kwamba kuna tatizo na kuanza kupambana nayo hadi unapata jibu na si kutumia muda mwingi kufikiria tu bali fanyia kazi.

Friday, November 13, 2009

Kucheza kimapenzi

Katika moja ya misingi ya kujenga mahusiano kati ya mke na mume ni pamoja na mke na mume kuwa na muda wa kucheza pamoja.
Kabla hatujafika mbali hivi ni lini wewe na mume wako au mke wako mmekuwa na muda wa kucheza pamoja?
Kama ni ndiyo basi ubarikiwe na kama hukumbuki ni lini bado hujachelewa ndiyo maana umekuja kusoma hapa ili nikukumbushe.
Kucheza pamoja kwa mume na mke husaidia kujenga urafiki na ndoa kwani ndani ya kucheza kuna interest na vicheko na pia kucheza pamoja maana yake unajali (caring).
Kujenga mahusiano ni pamoja na mke na mume kuwa marafiki na kuwa marafiki ni pamoja na kuwa na muda wa ku-enjoy pamoja kwa kucheza na matokeo yake ni kila mmoja kumuhitaji mwenzake mara kwa mara kwa kuwa kuna kitu mnacho in common.

Tuache kucheza michezo mingine tuangalie kucheza kimapenzi.
Je, ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kucheza mchezo wowote wa kimapenzi (sexual play)
Kwanza, lazima muwe ninyi wawili tu.
Pili, mnahakikisha kuna kuheshimiana katika kuchagua mchezo mnaotaka kucheza.
Tatu, mchezo wenu hauwezi kusababisha maumivu kimwili, hisia na kukwazana kiroho.
Nne, mnahakikisha mchezo wenu una msingi katika mahusiano yenu.
Na tano hakuna kuingiliana kimapenzi (no genital union)
(A Husband Shares Common Interests with the Woman of His Dreams by Playing Together)

Tumegundua Siri (majibu)

Hello dada Neema,
Asante sana kwa waraka ambao niliupata nami bila kuchelewa nikamshirikisha mume wangu James na tukaujadili na kwa kweli tuliufurahia sana kwani tunapenda sana ndoa yetu iwe kama yenu.
Baada ya kujadili kwa kina mimi na mume wangu James tumeamua jambo moja tu nalo ni :-
Kama maombi ni kitu halisi basi tutafanya (kuomba) kila wakati kuhakikisha ni moja ya msingi wa ndoa yetu.

Hata hivyo baada ya kuingia chumbani na kuanza kuomba jambo moja limejitokeza nalo ni namna gani tuombe kwani kuna aina fulani ya vizuizi ambavyo vimejitokeza ngoja nikueleze vizuri hapa chini naamini utaweza kutushauri pia.

Mimi ninafahamu jinsi ya kuomba (kuongea) na Mungu mwenyewe na nimezoea hivyo bila mtu mwingine kunisikiliza na huwa nakuwa wazi sana kueleza kila kitu kwa Mungu bila kumficha, nipo wazi (transparency).
Sasa tukiwa mimi na mume wangu James kwangu inakuwa ngumu sana kuomba kwa sauti kwani nahisi Mume wangu ananisikiliza na sijajua atanifikiria vipi kuna vitu ninavyoongea na Mungu nahisi mume wangu hatakiwi kuvisikia kwani kwa mume wangu ni non sense.
Na pia sijajua nikiomba kwa kumpendezesha mume wangu je Mungu atakubali maombi ya aina hiyo?
Je, niombe kwa sauti huku nikijihadhari na maneno ninayoomba ili mume wangu asijisikie vibaya, na je, Mungu atanionaje?
Naomba unielewesha kwani najikuta nipo nervous kweli, ulimi unasitasita, nipo njia panda na kama mtu anayeongea lugha mbili ili kuwafurahisha watu wawili wanaomsikiliza kila mtu na lugha yake.
Mume wangu amependekeza tuwe tunaomba kimya kimya kila mtu ndani kwa ndani, ila naona hainogi nimezoea kuongea kwa sauti mbele za Mungu wangu, unaionaje hiyo?

Tunaomba msaada wako iweje kwani tumeamua kuwa na maombi kabla ya kuwa mwili mmoja kila siku tukiwa faragha.

Usichoke kutushauri na Mungu akubariki sana na msalimie mumeo mpenzi John.
Ni mimi rafiki yako

Jane (Mrs James)

Wednesday, November 11, 2009

Tumegundua Siri!

Hello dada Jane,
Naamini unaendelea vizuri na mumeo James,
Leo nimeona nikuandikie waraka kukujibu lile swali lako uliloniuliza kwamba nini hata baada ya kutimiza miaka 30 katika ndoa yetu na mume wangu John, bado tunaendelea ku-enjoy sex at maximum kuliko wakati wote katika maisha yetu, mwenzangu lazima tukueleze wazi kwani ndoa yako bado changa sana miaka 4 na sex kwa mwezi mara moja au mbili tena kwa dakika 5 tu, Pole sana!

Kuna siri moja ambayo tumeigundua na mimi na mume wangu ni watu wa vitendo na si maneno, tuliamua kwamba kama kweli kufanya hili jambo kabla ya kuwa mwili mmoja lina maana na huleta matokeo tuliamua kufanyia kazi kwa nguvu zote.
Tumeamini usemi kwamba:-
“Great prayers are the way to great sex”
Si nilikwambia tulisoma kila aina ya vitabu na kupata kila aina ya mafundisho hata hivyo tukajikuta hakuna kitu hata hivyo kwa kuomba ya pamoja kabla ya sex tumeona mabadiliko zaidi na kwa kweli tunapokuwa faragha ni kama tunapaa hewani huwa tunahisi kama tumechukuliwa na International Space shuttle kwenda anga za mbali, ni raha na inabariki sana.

Pia tumegundua kwamba:-
“Sex at its best is spiritual”

Ni kweli tumegundua kwamba miili huunganika vizuri pale roho zinapounganika zaidi na njia nzuri ni maombi ya pamoja hivyo kabla ya tendo la ndoa tunaanza kwa maombi, kuombeana na pia kuomba Mungu atusaidie ili tunapopeana zawadi ya mwili kila mmoja apate raha nk.

Sasa hivi nikimsikia mume wangu John ananiambia twende chumbani kuomba mwili mzima unanisisimka na najua sasa raha inakuja na kuridhika kumewadia acha tu…….

Pia tumegundua kwamba kila kitendo cha kuomba pamoja (mara nyingi tukiwa tumekumbatiana) na kuwa karibu kiroho na kimwili hutusaidia kufanya discovery ya qualities za ndani na nje ambazo bila maombi tusingeweza kuziona na hivyo kupendana zaidi, ni kama kila siku namuona mume wangu ni mpya na anang'aa zaidi katika tabaia na u-handsome wake, eti naye anasema siku hizi nimekuwa mrembo ya uhakika na pia tabia yangu ni nzuri sana, naamini ni kwa sababu ya maombi.
Hii ina maana kwamba kumbe maombi hunua hata sifa njema ambazo zimejificha na zaidi kila tunavyoendelea kuombeana ndivyo tunavyozidi kufanya discovery ya vitu vingi zaidi, quality nyingi zaidi, positive nyingi zaidi na mambo mazuri mengi zaidi na matokeo yake mume wangu ananiambia siku hizi mimi ni mzuri zaidi na mtamu zaidi wakati huohuo na mimi namuona yeye ni mzuri na mtamu zaidi.

“Ninamuona special na yeye ananiona mimi ni special”
Kawaida ndoa inavyozidi kuendelea uzuri wa mume na mke huanza kuchakaa na wanandoa huweza kufikia kiwango cha kuchokana, tumegundua ni maombi peke yake huweza kuendelea kuwaboresha na kuwafanya wanandoa wasichakae wala kuchuja, si unaona sisi tuna miaka 30 katika ndoa na ndoa inazidi kuwa tamu, kweli maombi ni jibu.

Waingereza wanasema
“Prayers at its best are great Unifiers”
Tumeamini kwamba huu usemi ni kweli tupu.

Hivyo dada Jane kama unataka wewe na mumeo james mambo yawe sawa usisahau hii siri ya kuomba pamoja kabla ya kuwa mwili mmoja.

Kumbuka:-
“Jinsi Mume na Mke wanavyoweka urafiki pamoja na Mungu kwa njia ya maombi, ndivyo Mungu anavyoidi kuimarisha urafiki kati ya mke na mume”

Ni mimi rafiki yako
Neema (Mrs John)
(Ndugu msomaji James & Jane, John na Neema ni majina ambayo si ya watu ninaowafahamu ni majina yamewekwa tu kufanya ujumbe ukamilike)

Tuesday, November 10, 2009

Kuna aina tofauti!

Aina za tendo la ndoaKuna wakati wanandoa hujikuta wanahitaji kuwa na tendo la ndoa ambalo ni perfect, kama tetemeko la ardhi, kama fireworks na kufika kileleni kwa mpigo na raha ya ajabu.
Hata hivyo hii haina maana kwamba kila mtakapoamua kupeana mwili kati ya mume na mke wako mara zote mtajisikia hivyo na wala haina shida kwani jambo la msingi ninyi wawili ni kuhakikisha mpo connected kupitia sex.
Kuna wakati itakuwa just functional sex, huna mood ila mume wako au mke wako anataka, unampa.
Kuna wakati maisha yanaweza kuwapa wakati mgumu, mkawa na wakati mrefu wa kuomboleza na mnaweza kupeana faraja (comfort sex) na mkapeana faraja kwa zawadi ya tendo la ndoa na kila mmoja kujisikiaraha ajabu na zaidi kuwa na mtu muhimu kama wewe.

Utakuwa umepiga hatua kubwa sana au umefanikiwa sana katika ndoa kama utafahamu kuwa kuna aina mbalimbali za sex na wakati mwingine haitajalisha kama utafika kileleni au la kwani lengo ni kuhakikisha mke wako au mume wako yupo connected katika feelings zake na wewe.
Ubarikiwe na Bwana!

Saturday, November 7, 2009

Usitanie ni mali yenu!

Je, wanandoa wote tungekuwa tupo makini (maombi) mara zote kiasi hiki ingekuwaje?Mzuri kitandani?
Tunapooana kama wanandoa tunakubaliana kwamba tutakuwa tunafanya tendo la ndoa sisi wawili tu maisha yetu yote (monopoly) haijalishi tunafanya kwa kufikiria, au kwa kutofikiria, au tunafanya bora liende au kwa ufanisi, tunfanya kwa kupenda au kulazimishwa, tunafanya kwa ubunifu au kwa uchoyo au kwa kubania au kwa hiari au vyovyote vile kitabu kimefungwa na lazima kila mmoja apate kile mwenzake anampa iwe nusu au kitu kizima au kunyimwa kabisa au kupewa kila ukihitaji.
Hakuna kuangalia kushoto wala kulia ngoma ni ninyi wawili tu kuicheza hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ukweli wengi wetu huwa tunachukua kila kitu for granted, hakuna efforts zozote tunaweza kuziwekeza kuhakikisha mwenzako anapata the best kutoka kwako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa kwani ni wewe tu ndiye mwanamke au mwanaume duniani ambaye amekubali kuishi na wewe na kushirikiana kupeana hiyo zawadi ya mwili ambayo ni mali ya ndoa yenu na sivinginevyo.
Naomba ujiulize ndani ya moyo wako tena ukiwa na akili nzuri kabisa kama Mungu alivyokujalia kuoana na mwanaume au mwanamke special kama huyo uliyenaye.
Je, ni kweli unataka leo kumbariki mke wako au mume wako kwa mwili wako kwa kuwa hakuna kwingine anaweza kupata hii huduma?
Je, una hamu ya kumpa kitu cha uhakika (mapenzi, mahaba) kwa sababu ya jinsi anavyokupenda, anavyokujali na jinsi alivyoshirikiana na wewe hadi hapa mmefika?

Au umefika mahali umechoka, huna hamu tena ya kuhakikisha mume wako anapata kila mlikubaliana wakati mnaoana?
Au unasubiri hadi umpoteze ndipo ujue thamani yake?
Je unajua huko nje ya ndoa yako kuna wanawake au wanaume wengi kiasi gani wanamtamani sana huyo mume wako au mke wako?

Je, kwa nini huweki juhudi yoyote kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa mahali bora kukimbilia kama mke na mume?

Sex ni mali ya ndoa na ndivyo Mungu alivyo design, hivyo kama upo kwenye ndoa ina maana suala la tendo la ndo lisichukuliwa just for granted, panga, andaa na wekeza kwa uwezo wako wote kuhakikisha mke wako au mume wako anaridhika na wewe na utendaji wako.

Kumbuka Bibilia inasema:
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
Waebrania 13:4

Ndoa haibadilishi jiko.....................

Jiko la mkaa na Microwave
Mwanaume huweza kusisimka ndani ya dakika 2 au 2 na wakati mwingine sekunde 30, Lakini mwanaume huchukua zaidi ya mara 10 ya mwanaume kusisimka hii ina maana ni dakika 20 kwenda 30 kwa mwanaume kuwa amesisimka kiwango cha kutosha.
Kumbuka ndoa haiweze kubadilisha jiko la mkaa kuwa microwave.
Jambo la msingi ni kila mwanandoa kumtanguliza mwenzake hasa mwanaume kuhakikisha anakuwa mvumilivu kumtanguliza mke linapokuja suala la kupeana zawadi ya tendo la ndoa na si mume kuwa mbinafsi na akishamaliza raha zake anamwacha mwenzake anaugulia na jiko lake la mkaa.

Biblia inasema:-
Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno.
Upendo hauna kiburi.
Haukosi kuwa na adabu.
Upendo hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.
Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli.
Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.
(1Wakorintho 13)

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Kulala vizuri ni kuwa sexy!

Pumzika
Wanawake ambao hujimyima usingizi hawapo sexy, hivyo kabla ya kufikiria kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi na mke wako au mume wako zingatia kwanza kuwa na muda mzuri wa kupumzika.
Mwanamke asiyelala huwa mchovu hivyo kushindwa kujishughulisha vizuri na suala la tendo la ndoa kwani mwili wake huwa mchovu na zaidi ya yote kukosa usingizi husababisha kutokuwa na furaha.
Hakikisha mke wako au mume wako anapata usingizi wa kutosha ili kupumzisha mwili vizuri kwa faida ya ndoa yenu.
Kumbuka usiporidhika kimapenzi (tendo la ndoa) utajisikia ndoa hairidhishi na usiporidhika na ndoa yako ni mwanzo wa kuanza matatizo ya ndoa yako.
Usichimbe shimo ambalo ukiingia kutoka huwezi!

Eti Sivutiwi!

Wakati mwingine Inashangaza sana jinsi wanawake wanavyowawekea kiwango cha chini wanaume kuhusiana na hamu yao ya tendo la ndoa.
Hawajafahamu mwanaume kupewa zawadi ya tendo la ndoa inavyoweza kuathiri kukubalika kwake kwa mkewe na hatimaye kuweza kuendelea kujiona ni mwanaume mwenye mke anayejali.
Kumbuka wanaume na wanawake ni tofauti ndiyo maana wanawake hawana ndevu na nywele kifuani kama wanaume yote ni kwa sababu ya homoni za testosterone.

Ni kubusu tu!

Usiweke kiwango cha chini kumbusu mume wako au mke wako.
Hakikisha unambusu kila siku kabla ya kuagana asubuhi, muda wowote mchana na kabla ya kulala usiku hata usiku wa maneno ukikumbuka kwani kubusu ni kipimo cha hali ya mapenzi katika ndoa.
Kwa maelezo zaidi soma hapa

Kileleni kwa mpigo!

Kuna imani potofu kwamba mke na mume huweza kusisimka kwa wakati mmoja na kufika kilele kwa wakati mmoja na hii kufanya tendo la ndoa kuwa la kuridhisha zaidi.
Ukweli ni kwamba hii ni aina ya sex ambayo inakuwa ya mwelekeo wa kufikia lengo (goal-oriented sex) kuliko kupeana raha (pleasure-oriented sex) ambayo kila mmoja anahitaji.
Tendo la ndoa ambalo huwa ni kufikia lengo kwa pamoja hujawa na:-
Mahangaiko, keherehere, kukuru, macheleo.
Mitafaruku, masumbuko, tafrani.
Ubabaifu, mateso na wasiwasi na
Mara nyingi mkishindwa kufikia mnajiona ni failures,
kitu kinachozuia mwili kufurahia tendo lake la kiasili la kupeana raha.

Usiwe bubu wa ishara

Kutoa Ishara
Kuonesha ishara (positive) wakati mke na mume wapo kitandani huweza kusaidia ufanisi na kila mmoja kujisikia vizuri hata hivyo lawama au kukosoana au upekuzi au kumlalamikia au kusutana na mwenzako kwa kile anakufanyia (criticism) kamwe havichangamani na kusisimuana kimapenzi.
Tunapokuwa tumesisimka tunakuwa wazi rahisi kukabiliwa (vulnerable) hivyo ni jambo la busara kuepuka na kutoa comments negative kuhusu mke wako au mume wako mnapokuwa kitandani.
Kama unahisi unahitaji kumrekebisha kile anafanya ni vizuri kutoa comments zako zikiwa positive kuliko zikiwa negative.
Badala ya kusema kwa sauti ya juu na hasira
“Wewe vipi mbona unanikandamiza kwa nguvu niache”
kwa nini usiseme kwa kumnong’oneza
“Mpenzi polepole nitajisikia vizuri zaidi na asante

Pia ni vizuri kufahamu kwamba mkiwa kitandani kuna lugha ya alama (Non verbal cues) ambapo mnaweza kuwasiliana vizuri bila kuongea kwa maneno.
Baada ya kila mmoja kufahamu hii lugha ya alama mnaweza kuwa na enjoyment zaidi katika faragha yenu.

Kama vile kila mmoja kuupeleka mkono wa mwenzake pale anaona kuna njaa ya kuguswa.
Pia unaweza kupeleka au elekeza mwili wako au kiungo chako sawa sawa na stimulation unayotaka.
Pia mnaweza kutoa signal ambayo inaonesha kile anafanya kinazaa matunda au hakuna kitu.
Pia ni muhimu kuwa wabunifu.


Husisimka sawa

Mwanaume na kuongezeka Umri.
Mwanaume anavyozidi kuongezeka umri huhitaji direct stimulation ya stick yake kuwa tayari kwa ajili ya sex kuliko kuitikia kwa kuona kama kawaida ya wanaume.

Hata hivyo kitendo hiki kuimarisha tendo zima la ndoa kati ya wanandoa kwani mke na mume wanavyozidi kuongezeka umri sasa wote huhitaji kuchezeana viungo vyao ili kuwa aroused na tayari kwa kupeana zawadi yao ya tendo la ndoa.

Zaidi soma hapa

Kupanga

Kila kitu ni kupangaInashangaza sana mke huwa na mipango kamili na kuwekeza jitihada kubwa kwa ajili ya maandalizi ya mlo wa kawaida iwe chakula cha mchana au usiku au kifungua kinywa.
Lakini tunaamini kwamba tendo la ndoa linatakiwa kuwa ghafla kama vile kwenda jikoni na kuanza kupanga sahani za chakula na kusema leo tutakuwa na mlo wa ghalfa, naamini mlo wa aina hiyo haupo kwani inabidi kupanga kwanza.

Hata tendo la ndoa ni the same, ingawa hatufanyi hivyo hatuna planning, bila kupanga, maandalizi, makusudi, maazimio au kuwa na jitihada tunaweza kujikuta tumechoka na hakuna kuridhishana.
Kama tunahitaji tendo la ndoa linaloridhisha kupanga ni muhimu na kuwasiliana kati ya mke na mume kuhusiana na tendo hili takatifu ndani ya ndoa ni muhimu sana.

Pia tunahitaji kuweka kipaumbele kwa ajili ya tendo la ndoa kama tunavyoweka kipaumbele vitu vingine kama vile kulipa bills, kuhakikisha watoto wanapata chakula, ni rahisi sana kufikiria kwamba mbona hata kesho ipo hata hivyo wakati mwingine tunahitahitaji kuzipa hisia zetu kile zinataka.

Zaidi soma hapa

Kuponya Maumivi ya Kuachana (7)

HATUA YA NNE NI KUSEMA KWA HERI
Hii ni hatua ngumu sana kukutana nayo kwani ni hatua ambayo unakubali na kumwambia kwa heri Yule amekuacha.
Hapa ni hatua ambayo unakubali kwamba ni kweli mahusiano yamefika mwisho.
Hapa una admit kwamba huyu mtu hayupo tena katika maisha yangu na sasa natakiwa kuendelea mwenyewe.
Hata hivyo wapo ambao hujikuta wanakwamba wakifika hapa kwani wakati mwingine huamini sasa kwa heri na baada ya wiki mbili anarudi tena kuwaza kama inawezekana wakarudiana kitu ambacho hata aliyemuacha hana mpango kabisa.

Kumbuka ukitaka kuwa mtu huru na uweze kuendelea mbele jambo la msingi katika hatu hii ni wewe KUMSAMEHE.
Andika kwenye karatasi yale unaamini mpenzi wako amekukosea na yasome na kuomba Mugu akusamehe na yeye pia umsamehe.
Bila kusaheme inakuwa ni sababu muhimu sana ya kuzuia Baraka zako kwwa mahusiano yajayo na mahusiano yako wewe na Mungu.
Tunaweza kusaheme kwa sababu Mungu anatusamehe.

Inawezekana wakati upon a mpenzi wako kulikuwa na maeneo muhimu ambayo mlikuwa mnaenda pamoja inaweza kuwa ni kanisa, hotel, viwanja na sehemu za vacation na tangu mmeachana ukizikumbuka hizo sehemu unajisikia uchungu sana.
Kama unapotembelea hizo sehemu unajisikia hofu na uchungu kitu cha msingi kufanya ni wewe kwenda na rafiki zako/yako na ziombee kwa Jina la Yesu.
Mungu atakupa amani na utajisikia raha kuwepo hizo sehemu tena.

HATUA YA TANO NA SITA KUJIJENGA NA MATUMAINI MAPYA
Kwenye hatua hizi mbili sasa unaweza kuiongelea future huku ukiwa na matumaini mapya.
Hata hivyo tunatakiwa kukumbuka kwamba kukiwa na tukio la kuachana huwa kunakuwa na matokeo ya aina tatu kwa aliyeathirika.
Kwanza unaweza kubadilika na kuwa maisha mazuri zaidi, pia unaweza kubadilika na kuwa na maisha ya ovyo kabisa au tatu unaweza kubadilika na kurudi katika maisha yako kama kawaida.
Mara nyingi huwa ngumu sana kuwa na mabadiliko ya kuwa na maisha mazuri kama umekataliwa, umeachwa, upo dumped au rejected hata hivyo ukisimama vizuri na kumwangalia Mungu na kuitopoteza focus ya kuwa positive katika mtazamo wako unaweza kuwa na maisha bora tena na yenye Baraka.

Kuponya Maumivu ya Kuachana (6)

HATUA YA TATU NI KULALAMIKA
Hisia za lawama huweza kukupata na ukazielekeza kwa yule amekuacha au hata wewe mwenyewe.
Tabia yako na matendo yako huweza kubadilika na wewe mwenyewe ukajishangaa, unaweza kujiingiza katika Ulevi wa pombe kupindukia, kutembea (sex) na wanaume/wanawake tofauti na huko nyuma.
Hofu ya kukataliwa, upweke (isolation) na kujiona hujakamilika huweza kusababisha uwe na tabia ambazo ni tofauti na values zako mwenyewe.

Ukiwa kwenye hatua hii unaweza kujiingiza kwenye makosa ambayo yanaweza kusababisha kushindwa kupona maumivu ya kuachwa kwani unaweza kujikuta unakuwa na mawazo ya jumla kuhusiana na maisha na jinsi unavyowaona wengine (wanawake na wanaume) unaweza kuamini kwamba:-
“Wanawake wote hufuata wanaume kwa sababu ya pesa”
Wanaume ni viumbe wa sex kama wanyama hakuna mapenzi”
“Wanawake wote wamejaa emotions na hawawezi kufikiria mambo”
Hayo ni mawazo yako tu yote si kweli na ukiamini hivyo unaweza kujikuta huna matumaini tena kwa future.

Pia katika hatua kama hii unaweza kujikuta unajipa utabiri wako mwenyewe na utabiri ambao siku zote si kweli kama vile:-
Sitaolewa tena au sitaoa tena kwani sioni kama kuna mtu atanipenda tena”
“Nitabaki single maisha yangu yote kwani najiona nimeshajizeekea nani atanioa”
Utabiri potofu wa aina hii huweza kukufanya kuwa kipofu kuona uwezekana na Baraka zilizo mbele yako.
Mtazamo kama huu hukufanya uwe defeated mapema kabisa.
Utabiri wako potofu unakwambia mahali ulikotoka badala ya mahali unapotakiwa kwenda.
Utabiri kama huu badala ya kujenga husaidia kuwa kilema wa relation inayofuata.

Kosa lingine kubwa ambalo linaweza kukupata katika hatua hii ni kuwa na matarajio yasiyowezekana.
Unaweka matarajio kwa ajili yako na wengine kama vile:-
“Lazima niwe perfect ili nipendwe”
“Kama sijatimiza mahitaji yake anaweza asinipende”
“Kama akiniuliza kuhusu mahusiano yangu ya zamani basi atakuwa hanipendi”
Kuwaza hivyo na kuwa na matarajio ya aina hiyo ni kujiweka katika mtego ambao ukinasa unaweza kujiharibia mahusiano yanayofuata.

Kosa lingine la kawaida ambalo unaweza kulifanya katika hatua hii ni kulipa kisasi (revenge loving).
Unaamua kujitoa kuanza mahusiano mapya na mtu mwingine haraka huku bado una hasira za kuachwa na hili hujidhihirisha katika njia tatu.
Kwanza unajiangiza kwenye mahusiano mapya ili aliyekuacha au uliyemuacha apate wivu.
Unafanya kila njia na juhudi kuhakikisha aliyekuacha au ulimuacha anafahamu na kukuona na mpenzi mpya.

Pili ukiwa na mpenzi mpya unakuwa na tabia ya kumpa suluba kama ulizokuwa unapewa, kama ulikuwa unateswa au kutukanwa unatumia the same weapon kwa mpenzi wako mpya.
Tatu unaamua kum-control mpenzi mpya idara zote kuogopa na yeye asijeakakuacha na kukuumuza tena.
Hata hivyo maisha ya kisasi aina zote tatu haziwezi kukusaidia matokeo yake utaishia kuumizwa, kutokuwa na furaha katika hayo mahusiano na zaidi hataridhika.

Tatizo lingine kubwa ambalo unaweza kukutana nalo kwenye hii hatua ni kuwaza kuwa na mpenzi mpya ambaye kwa viwango vya duniani hayupo kwa maana kwamba unaweka qualification za juu kuliko binadamu yeyote.
Ingawa lengo lako ni zuri kwamba unataka upate mpenzi mpya ambaye hatakuumiza wala kukurudisha ulikotoka hata hivyo idealization ya aina hiyo inaweza kukufanya ushindwe kumpata mtu halisi kwani hayupo.

Kosa lingine ni kwamba unaweza kujikuta unaangukia kwa mwanaume wa aina ile ile tena au mwanamke wa aina ile ile tena kitu kinachodhihirisha kwamba matatizo yaliyokuwepo mara ya kwanza badala ya kuyatatua mliamua kulaluana wenyewe.

Thursday, November 5, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (5)

Ni kama kupanda ngazi usipokwama utafanikiwa!HATUA SITA AMBAZO ALIYEACHWA HUPITIA ILI KUPONYA MAUMIVU.
Kama kuugulia tunakopata kutokana na mtu kufa, hatua unazoweza kupitia baada ya kuachwa katika mahusiano zinajulikana na huwa na makali mfano wa kifo.

Hizi hatua zinaelezea hali ya kawaida na afya katika kukurejesha katika hali ya kawaida baada ya kuachwa.
Kama uponyaji (healing) umetokea kutokana na maumivu ya kuachwa bado utabakiwa na kovu (emotional scar) na si kidonda na lengo ya kuachambua hizi hatua ni ili wewe ufikie kuwa na kovu na si kubaki na kidonda miaka nenda rudi.

Watu ambao wameshindwa kumaliza hatua zote zinazotakiwa wamejikuta wakiwa katika maumivu na vidonda kutopona (hubaki vidonda ndugu) hadi zaidi ya miaka 15. Inahuzunisha sana!

Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba hizi hatua ambazo unapitia hutofautiana urefu na makali kutokana na namna ulivyodumu kwenye mahusiano na jinsi mlivyopendana.

Kuna hatua sita ambazo unaweza kupitia ukiachwa na yule ulikuwa unampenda, maumivu huwa makali sana katika hatua tatu za kwanza na unavyozidi kuendelea maumivu huendelea kupungua hadi hatua ya mwisho na wewe kurudi katika hali yako ya kawaida.
Jinsi unavyoendelea kutika hatua moja hadi nyingine hofu na mashaka huendelea kupungua.
Jambo la hatari ni pale unapokwama kwenye hatua moja bila kusonga mbele au kuendelea hatua nyingine.
Na wakati mwingine unaweza kwenda hatua moja na kwenda nyingine na kurudi tena moja na hii ni kawaida kwa kuwa ndiyo sehemu ya uponyaji wa maumivu.

HATUA YA KWANZA NI MSHITUKO
Unapoachwa na mtu unayempenda duniani utajisikia kutelekezwa, kutishwa, na kupata mshituko wa kutisha (total shock).
Hata kama kuachana kulikuwa kumetegemewa au ulikuwa unajua mapema siku ya kuachana kikwelikweli ni mshituko wa ajabu.
Ukweli hili jambo ni tofauti kwani wengi hushindwa kuendelea na kazi au shughuli zao za kila siku kama vile kushindwa kula, kulala, kwenda kazini.
Unakuwa mtu wa machozi, ni kulala na kushinda unalia kulikotawaliwa na upweke na hofu ya watu watakuonaje, watasemaje na zaidi your future.

Badala ya kuishi kama kawaida unaanza kuishi kwa feelings, na feelings huwa na nguvu kuliko wewe (nafsi)
Unajawa na hofu na mashaka ya kuwa mwenyewe na kwamba upo abandoned milele.
Hata hivyo unahitaji kuwa na feelings za aina hii ili uweze kupokea healing na hili tukio.
Katika hatua kama hii unahitaji kuwa na watu wa karibu kukutia moyo kwani uwepo wao hukusaidia kuondoa upweke.

HATUA YA PILI NI MAJONZI/HUZUNI AU MASIKITIKO
Hii hatua huweza kuwa ndefu kutokana na kuugulia au kusononeka au kuomboleza mambo mazuri ulikuwa unafanya naye, umepanga naye na kuahidiana naye na zaidi yale ambazo mlipanga na hamjatimiza bado.
Katika hatua hii hasira huzaliwa na kuwa kubwa, unaweza kumkasirikia aliyekuacha, unaweza kumkasirikia Mungu kwa kuruhusu haya yatokee na unaweza kumchukia mtu yeyote ambaye unahisi amehusika wewe kuachwa.
Bahati mbaya ni kwamba wote umelekeza hasira zako wanaweza wasiwe na taarifa kwamba umewakasirikia.
Unakuwa depressed na kuvunjika kwa mahusiano na mstakabali ya baadae kuhusu mahusiano.
Katika hatua hii unakuwa na mawazo ambayo ni potofu wewe na kuachwa kwa mfano unaweza kuwaza na kujisemea kwamba:-
“Hakuna anayefahamu uchungu na maumivu niliyonayo”
“Afadhari nife kuliko aibu kama hii”
“Kila mtu ananiongelea mimi na kuachwa kwangu”
“Kila ninakopita wananinyoshea vidole kunisema na kunicheka”
“Hata rafiki zangu wananikwepa”
Jambo la msingi ni kufahamu kwamba si wewe mtu wa kwanza duniani kuachwa na kukutana na maumivu na mateso kama si aibu kama hiyo hivyo wapo wanaojua na kufahamu yale unapitia na maumivu unapata.
Wanajua na kufahamu feelings za kuachwa, wanafahamu jinsi kisu cha maumivu kinavyokata hadi kukosa usingizi, kula na kwenda kazini.

Unaweza kujawa na mawazo kwamba kila mtu anakuchukia na pia unaweza kuwaza kwamba Mungu amekuchukia hata hivyo inawezekana wengine wanakwepa kuongea na wewe kwa kuhofia kushindwa nini waongea (kama umepata talaka) pia kumbuka Mungu anachukia kupeana talaka hata hivyo Mungu anampenda mtu yeyote aliyepewa talaka.
Hatua za msingi za kuchukua katka hatua hii ni kwanza omba kwa sauti kumshirikisha Mungu yale uliyonayo (share your concern).
Mwambie Mungu kile unapenda afanye kutokana na yale yaliyoujaza moyo wako na mawazo yako.
Pili soma haya maandiko kwa sauti
Isaya 26:3
Efeso: 4:23
Wakolosai 3:1,2
2Wakorintho 10:5
Wafilipi 4:6-9
Tutaendelea na hatua zilizobaki...........

Wednesday, November 4, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (4)

Nimeachwa, nimechanganyikiwa, sina mwelekeo!Kuvunjika moyo, kukatishwa tamaa, upweke, nk ni maneno yanayoelezea feelings za uzoefu ambao binadamu hupitia pale mahusiano yanapovunjika iwe urafiki wa kawaida, uchumba au ndoa.
Wakati mwingine aliyeachwa huamua hata kutishia kwamba atajinyonga wasiporudiana au tishia kufanya kitu chochote au kujitoa hata kuhonga chochote anachoweza na bado juhudi zote huzaa nothing na hali kuwa mbaya zaidi.
Kuachwa hasa uchumba huumiza sana wakati mwingine kwa sababu aliyekuacha (dump, abandon) anaweza kumuoa/olewa rafiki yako au ndugu yako au mtu kwa karibu na wewe unayemfahamu na zaidi unakutana nao mitaani na inaawezekana wewe ni mzuri zaidi yake.

Kila survivor wa kuvunjika kwa mahusiano huendelea kuwindwa na mabaki ya hofu na mashaka ya mahusiano yatakayofuata.

Wapo ambao baada ya mahusiano kuvunjika huanza mahusiano mapya ambayo huvunja moyo tena kama mara ya kwanza na hawakati tamaa na hujifunza kwa kuondoa hofu na mashaka na kujenga trust upya na kuendelea kufurahia mahusiano mapya tena.

Wengine huruhusu vidonda (emotional) kuendelea kuwatawala na wanakuja wamejifungia (locked) kutoruhusu kupenda na kupendwa upya.

Jambo la msingi ni kwamba maumivu ya kupotelewa au kuachwa na mtu unayempenda ni moja ya maumivu makali sana na baada ya kuachwa kupenda tena huwa ni moja na hofu kubwa sana mtu anapitia katika maisha yake kwani wengi hujikutana wanakutana na walewale.

Unapompenda mtu kwa moyo wako wote na hisia zako zote na kwa mapenzi yako yote, mahusiano yanapovunjika maisha hubadilika na kuathiriwa kiasi cha kusimama ghafla.
Kuna usemi kwamba
“Usually the first love lost is the most painful”
Jambo linalostua zaidi ni kwamba wale wanauumia zaidi ni mwanaume au mwanamke ambaye hata baada ya mahusiano kuvunjika (mfano uchumba) bado hung’ang’ania au kuendelea kutaka warudiane kwa kuwa walikuwa deep na attached kwenye hilo penzi, hujisikia bila huyo mtu hupo desperate na hana control.

Na wakati mwingine hufikiria mbali zaidi kwa kuamua kufanya kitu chochote kuhakikisha wanarudiana kibaya zaidi partners wao huwa walishafanya maamuzi na hawawezi kurudi tena.

Pia unapoachwa na mpenzi feelings zako hujigawa pande mbili, upande wa kwanza unakwambia unaweza kuanza mahusiano mapya sasa na upande mwingine unakwambia usifanye na ukifanya au jiingiza kwenye kupenda tena utaishia kuumizwa kama mwanzo.

Pia kuacha au kuachwa hujenga kujisia hatia (guilt) bila kujalisha wewe ni uliyeachwa au uliyeacha, rejected au rejecting, dumped au dumper wote huwa na hisia za kujiona ni failure.
Kujisikia hatia hujenga hali ya kujisikia kutojiamini na kutojiamini huzaa hofu ambayo huendelea kukuwinda kila mara unapokumbuka mahusiano yalivyovunjika.
Hiyo hofu huingia akilini na kugonga kama nyundo kukumbushia machungu na makali ya kuachwa hadi unafikia hali unajikuta kuchanganyikiwa kama si kupaniki.
Vilevile hofu hii huweza kupooza hatua yoyote unayotaka kuchukua ili kuanza mahusiano mapya na unajikuta huwezi kuwekeza tena kwenye kupenda na kupendwa upya, unakuwa mwoga kupenda upya na unaogopa pia kukaa mwenyewe bila mtu wa kukupenda, ni kizunguzungu tu.

Jambo la kujiuliza kwa nini unajisikia hatia je, ni kweli ni wewe uliyesababisha mahusiano kuvunjika au ni illusions tu?
Je, ni kweli ulivunja kiapo (vow/covenant) ulichoahidiana na mpenzi wako?
Je, ni kweli hukuwa responsible kwenye mahusiano hadi hajavunjika?
Kama si kweli basi unajichukulia lawama ambazo hustahili.

Je, ni hatua ngapi mtu aliyeachwa anaweza kutumia ili kuponya maumivu yake na kurudi kwenye maisha ya kawaida?
Tutaendelea................

Kuponya Maumivu ya Kuachana (3)

Wangekalea vizuri kasingekuwa kavuta bangi!Kuachwa (na mpenzi) ni tukio gumu na zito na huja na mabadiliko tofauti na kumpa mtu uzoefu wa aina yake, ni ngumu na inaumiza sana, lakini watu hujifunza kukua, hupata mitazamo mipya kimaisha, uelewa mpya, na uchujaji wa mambo upya na matumaini mapya ingawa huwa ngumu sana kuona mbali au mbele baada ya kukutana na hii patashika.

Hakuna anayependa kuachwa, kwani ukiachwa unajiona umefeli na tumefundishwa katika maisha jambo la msingi ni kuwa washindi si kufeli au kuwa failrues. (winners not losers).
Kushindwa ni kubaya na huumiza, huandamana na ncha kali kama za kiwembe ambazo huweza kuchana nerves hadi kutoa maumivu makali sana yasiyovumilika.
Haijalishi umeshindwa kidogo au kiasi kikubwa vyote huumiza.

Inaumiza sana kwa sababu hatujafundishwa kutegemea kushindwa na pia hatujafundishwa tukishindwa tufanye namna gani (how to handle).
Mtu yeyote anapokutana na kushindwa wengine huanza kumlaumu na kumtamkia maneno kama vile:-
“Angekuwa mke mwema wala asingeachwa na mume wake”
“Wazazi wake wangekuwa makini mtoto wao asingejiunga na wavuta bangi”
“Asingekuwa anajifanya mjuaji asingefukuzwa kazi”
“Wangekuwa wanaishi Kikristo haya yote (mabaya) yasingetokea”
Je, umewahi kuwa na mawazo ya namna hiyo kwa wanaoshindwa?
Naamini umewahi na ndivyo binadamu tulivyo.
Biblia imeeleza wazi pia kwani siku moja wanafunzi wa Yesu walikutana na mtu kipofu na kwa kuwa kipofu waliamini yule kipofu au wazazi wake au ndugu zake walifanya dhambi hata hivyo majibu ya Yesu yalikuwa tofauti.

Yohana 9:1-3
Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza,
“Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’
Yesu akawajibu,
“Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake.

Mungu anachukia wanandoa kuachana, anachukia talaka na talaka si mpango wa Mungu bali mwanadamu, hata hivyo Mungu anawapenda walioachwa na waliacha, Mungu anawapenda walipewa talaka na bado ana mpango na maisha yao ingawa sisi binadamu huweza kuwakwepa walioachwa na kutalikiwa na kuwaona ni watu wenye hitilafu katika maisha.
Kumbuka ni Yesu Peke yake ndiye anajua machungu uliyopitia au unayopitia hata kama umeachwa leo au karibuni au zamani na bado Mungu anampango na maisha yako.
Yesu ndiye rafiki wa kweli anajua kuachwa na kukanwa kama vile Petro alivyomkataa kwamba hamjui.
Tumaini bado lipo na maisha bado yapo hata baada ya kuachwa.
Usikate tamaa.
Tutaendelea..................