"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 29, 2009

Atafute kipato kwanza!

Wametaka wenyewe, tumewapa!Wanaume wengi tangu watoto wamepitia malezi yanayowafanya kuwa watu muhimu kwa ajili ya kutafuta kipato cha familia.
Hilo ndilo jambo la msingi ambalo familia yoyote au jamii yoyote au tamaduni zozote huhakikisha mtoto wao wa kiume analifahamu jukumu hilo.

Jambo la pili ambalo wanafundishwa ni suala la mahusiano na jinsi ya kuishi vizuri na mke hata hivyo hivi vitu viwili ni kinyume (opposite) kwa mwanamke ambaye yeye huanza kufundishwa masuala ya mahusiano kwanza na baadae suala la kipato katika familia.

Hata hivyo dunia imebadilika sana kwani wanawake nao wanakuja juu kuhusiana na suala la kuchangia kipato katika familia na wapo ambao sasa wao (wanawake) ndio wanashika usukani kuhakikisha familia inasimama imara linapokuja suala la kipato.

Swali ni je, wanaume sasa nao wanabadilika ili kuwa wanaume wazuri linapokuja suala la mahusiano kama ambavyo wanawake wanavyokuja juu na kuwa mstari wa mbele kuhusiana na suala la kipato?

Naamini kila mmoja ana jibu lake

No comments: