"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 29, 2009

BBC!

Linapokuja suala la ndoa BBC ni kifupi cha maneno ya kingereza yaani Before Baby Came (Kabla mtoto kuzaliwa)
Je, BBC ina uhusiano gani kwa ndoa au mahusiano?
Wanawake hujisikia wanavutia sana kimwonekano wakati wa BBC na ikipita wanawake hujikuta wanashindwa kurudi (regain) kwenye umbo na mwonekano ule wa BBC bila kujali wanafanya mazoezi kiasi gani au kukwepa chakula (dieting)kiasi gani.

Jambo la msingi ni kujiamini mwenyewe yaani mwanamke kujikubali kwamba kama alivyo amekamilika na wakati mwingine hawezi kufanya chochote zaidi ya kuwa na mtazamo positive kuhusu yeye na mwonekano wake na kuhakikisha all the time yupo smart.

Hata wanaume nao wamekuwa na mtazamo wa kisasa (usio sahihi, uliopotofu) badala ya kusaidiana na mke wake au kumtia moyo kuhusiana na kurudi kwenye umbo lake la BBC yeye anaanza kumlaumu na kumtamkia maneno ambayo si romantic au yanayomfanya mwanamke kuwa turned off idara zote.
Kumbuka uliweka ahadi kuwa naye katika raha au shida, anenepe kama kinguruwe au awe mwembamba kama mbu ni wako na hadi kifo so jambo la msingi ni kutiana moyo na kusaidiana mke kurudi kwenye umbo lake au lile wewe unapenda na si kamwe kumsema au kumtolea maneno yasiyo ya kistaarabu.

Kazi aliyofanya mwanamke kukuzalia mtoto si utani si ndogo si mchezo si lelemama wala masihala ni kufa na kupona na kazi ya ziada na maumivu, uchungu na zoezi zima la kuzaa mtoto kwake ilikuwa muujiza na huwezi kulinganisha na mwili wake alionao sasa.
Kwa nini usiamue kumwambia nakupenda kama ulivyo na ubarikiwe kwa mtoto/watoto ambao tumezaaa pamoja kwani hilo ndilo jambo la msingi zaidi kuliko looks/appearances.

Usione vinaelea vimeundwa!

No comments: