"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 1, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (1)

Kawaida mahusiano yoyote ya mapenzi yanapofika kwenye mzozo mkali (battlefields) huwa na matukio matatu tu.
Kwanza mmoja huamua kuondoka zake na kuanza mbele au pili wote au mmoja huamua kuendelea kuishi katika mahusiano ambayo hata hayaridhishi/bora liende au tatu wote au mmoja huamua kuanza kupenda upya katika hali zote kuhakikisha mahusiano yanarudi kwenye mstari.

Hata hivyo inakuwaje pale mmoja anaamua kuanza mbele na kumuacha mwenzake kwenye mataa?
Mara nyingi mahusiano yanapokatika iwe uchumba au iwe ndoa au iwe urafiki a kawaida unaweza kujikuta umechanganyikiwa bila kujali ni wewe uliyeamua kumuacha mwenzako au wewe uliyeachwa (The Dumper and The Dumped).
Kujiamini hurudi ground zero, maumivu ni makali, unajiona ni failure na kikubwa zaidi maisha yanatakiwa kwenda hata baada ya kumpoteza Yule ulikuwa unampenda.
Bahati mbaya ni kwamba si wote wenye uwezo na nguvu za kujikusanya na kuendelea na maisha kama kawaida kwani wengine hudhoofishwa na kufikia mahali wanaona maisha hayana maana tena.

Kila mahusiano lazima yatakufikisha mahali ambapo utajifunza na kukua haijalishi yanaendelea au yamefeli. Hata hivyo mahusiano yanayoshindwa hufundisha zaidi na hutoa uzoefu mkubwa kwani mafanikio huja si kwa kurudia makosa yale tumefanya au kuchukulia vitu for granted bali kuepuka yale tulifeli mara ya kwanza.

Nimewahi sikia mtu mmoja muhimu sana akiongea maneno haya:
“Nisingeweza kufikia mafanikio yote haya kama si kuwa na mtazamo mpya na kuongeza juhudi kujenga taaluma yangu baada ya kuachwa na mchumba wangu wa mwanzo na hatimaye kumpata mume bora niliyenaye sasa”
Inaonesha ilikuwa muhimu kwake uchumba kuvunjika ili akaze kamba kuendeleza taaluma yake na hatimaye akapata liubavu lake; huko si kukaa na kuhuzunika na kujiambia kwamba “I am finished”.

Tutaendelea kesho............................

No comments: