"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, November 4, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (3)

Wangekalea vizuri kasingekuwa kavuta bangi!Kuachwa (na mpenzi) ni tukio gumu na zito na huja na mabadiliko tofauti na kumpa mtu uzoefu wa aina yake, ni ngumu na inaumiza sana, lakini watu hujifunza kukua, hupata mitazamo mipya kimaisha, uelewa mpya, na uchujaji wa mambo upya na matumaini mapya ingawa huwa ngumu sana kuona mbali au mbele baada ya kukutana na hii patashika.

Hakuna anayependa kuachwa, kwani ukiachwa unajiona umefeli na tumefundishwa katika maisha jambo la msingi ni kuwa washindi si kufeli au kuwa failrues. (winners not losers).
Kushindwa ni kubaya na huumiza, huandamana na ncha kali kama za kiwembe ambazo huweza kuchana nerves hadi kutoa maumivu makali sana yasiyovumilika.
Haijalishi umeshindwa kidogo au kiasi kikubwa vyote huumiza.

Inaumiza sana kwa sababu hatujafundishwa kutegemea kushindwa na pia hatujafundishwa tukishindwa tufanye namna gani (how to handle).
Mtu yeyote anapokutana na kushindwa wengine huanza kumlaumu na kumtamkia maneno kama vile:-
“Angekuwa mke mwema wala asingeachwa na mume wake”
“Wazazi wake wangekuwa makini mtoto wao asingejiunga na wavuta bangi”
“Asingekuwa anajifanya mjuaji asingefukuzwa kazi”
“Wangekuwa wanaishi Kikristo haya yote (mabaya) yasingetokea”
Je, umewahi kuwa na mawazo ya namna hiyo kwa wanaoshindwa?
Naamini umewahi na ndivyo binadamu tulivyo.
Biblia imeeleza wazi pia kwani siku moja wanafunzi wa Yesu walikutana na mtu kipofu na kwa kuwa kipofu waliamini yule kipofu au wazazi wake au ndugu zake walifanya dhambi hata hivyo majibu ya Yesu yalikuwa tofauti.

Yohana 9:1-3
Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza,
“Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’
Yesu akawajibu,
“Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake.

Mungu anachukia wanandoa kuachana, anachukia talaka na talaka si mpango wa Mungu bali mwanadamu, hata hivyo Mungu anawapenda walioachwa na waliacha, Mungu anawapenda walipewa talaka na bado ana mpango na maisha yao ingawa sisi binadamu huweza kuwakwepa walioachwa na kutalikiwa na kuwaona ni watu wenye hitilafu katika maisha.
Kumbuka ni Yesu Peke yake ndiye anajua machungu uliyopitia au unayopitia hata kama umeachwa leo au karibuni au zamani na bado Mungu anampango na maisha yako.
Yesu ndiye rafiki wa kweli anajua kuachwa na kukanwa kama vile Petro alivyomkataa kwamba hamjui.
Tumaini bado lipo na maisha bado yapo hata baada ya kuachwa.
Usikate tamaa.
Tutaendelea..................

No comments: