"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, November 5, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (5)

Ni kama kupanda ngazi usipokwama utafanikiwa!HATUA SITA AMBAZO ALIYEACHWA HUPITIA ILI KUPONYA MAUMIVU.
Kama kuugulia tunakopata kutokana na mtu kufa, hatua unazoweza kupitia baada ya kuachwa katika mahusiano zinajulikana na huwa na makali mfano wa kifo.

Hizi hatua zinaelezea hali ya kawaida na afya katika kukurejesha katika hali ya kawaida baada ya kuachwa.
Kama uponyaji (healing) umetokea kutokana na maumivu ya kuachwa bado utabakiwa na kovu (emotional scar) na si kidonda na lengo ya kuachambua hizi hatua ni ili wewe ufikie kuwa na kovu na si kubaki na kidonda miaka nenda rudi.

Watu ambao wameshindwa kumaliza hatua zote zinazotakiwa wamejikuta wakiwa katika maumivu na vidonda kutopona (hubaki vidonda ndugu) hadi zaidi ya miaka 15. Inahuzunisha sana!

Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba hizi hatua ambazo unapitia hutofautiana urefu na makali kutokana na namna ulivyodumu kwenye mahusiano na jinsi mlivyopendana.

Kuna hatua sita ambazo unaweza kupitia ukiachwa na yule ulikuwa unampenda, maumivu huwa makali sana katika hatua tatu za kwanza na unavyozidi kuendelea maumivu huendelea kupungua hadi hatua ya mwisho na wewe kurudi katika hali yako ya kawaida.
Jinsi unavyoendelea kutika hatua moja hadi nyingine hofu na mashaka huendelea kupungua.
Jambo la hatari ni pale unapokwama kwenye hatua moja bila kusonga mbele au kuendelea hatua nyingine.
Na wakati mwingine unaweza kwenda hatua moja na kwenda nyingine na kurudi tena moja na hii ni kawaida kwa kuwa ndiyo sehemu ya uponyaji wa maumivu.

HATUA YA KWANZA NI MSHITUKO
Unapoachwa na mtu unayempenda duniani utajisikia kutelekezwa, kutishwa, na kupata mshituko wa kutisha (total shock).
Hata kama kuachana kulikuwa kumetegemewa au ulikuwa unajua mapema siku ya kuachana kikwelikweli ni mshituko wa ajabu.
Ukweli hili jambo ni tofauti kwani wengi hushindwa kuendelea na kazi au shughuli zao za kila siku kama vile kushindwa kula, kulala, kwenda kazini.
Unakuwa mtu wa machozi, ni kulala na kushinda unalia kulikotawaliwa na upweke na hofu ya watu watakuonaje, watasemaje na zaidi your future.

Badala ya kuishi kama kawaida unaanza kuishi kwa feelings, na feelings huwa na nguvu kuliko wewe (nafsi)
Unajawa na hofu na mashaka ya kuwa mwenyewe na kwamba upo abandoned milele.
Hata hivyo unahitaji kuwa na feelings za aina hii ili uweze kupokea healing na hili tukio.
Katika hatua kama hii unahitaji kuwa na watu wa karibu kukutia moyo kwani uwepo wao hukusaidia kuondoa upweke.

HATUA YA PILI NI MAJONZI/HUZUNI AU MASIKITIKO
Hii hatua huweza kuwa ndefu kutokana na kuugulia au kusononeka au kuomboleza mambo mazuri ulikuwa unafanya naye, umepanga naye na kuahidiana naye na zaidi yale ambazo mlipanga na hamjatimiza bado.
Katika hatua hii hasira huzaliwa na kuwa kubwa, unaweza kumkasirikia aliyekuacha, unaweza kumkasirikia Mungu kwa kuruhusu haya yatokee na unaweza kumchukia mtu yeyote ambaye unahisi amehusika wewe kuachwa.
Bahati mbaya ni kwamba wote umelekeza hasira zako wanaweza wasiwe na taarifa kwamba umewakasirikia.
Unakuwa depressed na kuvunjika kwa mahusiano na mstakabali ya baadae kuhusu mahusiano.
Katika hatua hii unakuwa na mawazo ambayo ni potofu wewe na kuachwa kwa mfano unaweza kuwaza na kujisemea kwamba:-
“Hakuna anayefahamu uchungu na maumivu niliyonayo”
“Afadhari nife kuliko aibu kama hii”
“Kila mtu ananiongelea mimi na kuachwa kwangu”
“Kila ninakopita wananinyoshea vidole kunisema na kunicheka”
“Hata rafiki zangu wananikwepa”
Jambo la msingi ni kufahamu kwamba si wewe mtu wa kwanza duniani kuachwa na kukutana na maumivu na mateso kama si aibu kama hiyo hivyo wapo wanaojua na kufahamu yale unapitia na maumivu unapata.
Wanajua na kufahamu feelings za kuachwa, wanafahamu jinsi kisu cha maumivu kinavyokata hadi kukosa usingizi, kula na kwenda kazini.

Unaweza kujawa na mawazo kwamba kila mtu anakuchukia na pia unaweza kuwaza kwamba Mungu amekuchukia hata hivyo inawezekana wengine wanakwepa kuongea na wewe kwa kuhofia kushindwa nini waongea (kama umepata talaka) pia kumbuka Mungu anachukia kupeana talaka hata hivyo Mungu anampenda mtu yeyote aliyepewa talaka.
Hatua za msingi za kuchukua katka hatua hii ni kwanza omba kwa sauti kumshirikisha Mungu yale uliyonayo (share your concern).
Mwambie Mungu kile unapenda afanye kutokana na yale yaliyoujaza moyo wako na mawazo yako.
Pili soma haya maandiko kwa sauti
Isaya 26:3
Efeso: 4:23
Wakolosai 3:1,2
2Wakorintho 10:5
Wafilipi 4:6-9
Tutaendelea na hatua zilizobaki...........

No comments: