"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, November 7, 2009

Kuponya Maumivu ya Kuachana (6)

HATUA YA TATU NI KULALAMIKA
Hisia za lawama huweza kukupata na ukazielekeza kwa yule amekuacha au hata wewe mwenyewe.
Tabia yako na matendo yako huweza kubadilika na wewe mwenyewe ukajishangaa, unaweza kujiingiza katika Ulevi wa pombe kupindukia, kutembea (sex) na wanaume/wanawake tofauti na huko nyuma.
Hofu ya kukataliwa, upweke (isolation) na kujiona hujakamilika huweza kusababisha uwe na tabia ambazo ni tofauti na values zako mwenyewe.

Ukiwa kwenye hatua hii unaweza kujiingiza kwenye makosa ambayo yanaweza kusababisha kushindwa kupona maumivu ya kuachwa kwani unaweza kujikuta unakuwa na mawazo ya jumla kuhusiana na maisha na jinsi unavyowaona wengine (wanawake na wanaume) unaweza kuamini kwamba:-
“Wanawake wote hufuata wanaume kwa sababu ya pesa”
Wanaume ni viumbe wa sex kama wanyama hakuna mapenzi”
“Wanawake wote wamejaa emotions na hawawezi kufikiria mambo”
Hayo ni mawazo yako tu yote si kweli na ukiamini hivyo unaweza kujikuta huna matumaini tena kwa future.

Pia katika hatua kama hii unaweza kujikuta unajipa utabiri wako mwenyewe na utabiri ambao siku zote si kweli kama vile:-
Sitaolewa tena au sitaoa tena kwani sioni kama kuna mtu atanipenda tena”
“Nitabaki single maisha yangu yote kwani najiona nimeshajizeekea nani atanioa”
Utabiri potofu wa aina hii huweza kukufanya kuwa kipofu kuona uwezekana na Baraka zilizo mbele yako.
Mtazamo kama huu hukufanya uwe defeated mapema kabisa.
Utabiri wako potofu unakwambia mahali ulikotoka badala ya mahali unapotakiwa kwenda.
Utabiri kama huu badala ya kujenga husaidia kuwa kilema wa relation inayofuata.

Kosa lingine kubwa ambalo linaweza kukupata katika hatua hii ni kuwa na matarajio yasiyowezekana.
Unaweka matarajio kwa ajili yako na wengine kama vile:-
“Lazima niwe perfect ili nipendwe”
“Kama sijatimiza mahitaji yake anaweza asinipende”
“Kama akiniuliza kuhusu mahusiano yangu ya zamani basi atakuwa hanipendi”
Kuwaza hivyo na kuwa na matarajio ya aina hiyo ni kujiweka katika mtego ambao ukinasa unaweza kujiharibia mahusiano yanayofuata.

Kosa lingine la kawaida ambalo unaweza kulifanya katika hatua hii ni kulipa kisasi (revenge loving).
Unaamua kujitoa kuanza mahusiano mapya na mtu mwingine haraka huku bado una hasira za kuachwa na hili hujidhihirisha katika njia tatu.
Kwanza unajiangiza kwenye mahusiano mapya ili aliyekuacha au uliyemuacha apate wivu.
Unafanya kila njia na juhudi kuhakikisha aliyekuacha au ulimuacha anafahamu na kukuona na mpenzi mpya.

Pili ukiwa na mpenzi mpya unakuwa na tabia ya kumpa suluba kama ulizokuwa unapewa, kama ulikuwa unateswa au kutukanwa unatumia the same weapon kwa mpenzi wako mpya.
Tatu unaamua kum-control mpenzi mpya idara zote kuogopa na yeye asijeakakuacha na kukuumuza tena.
Hata hivyo maisha ya kisasi aina zote tatu haziwezi kukusaidia matokeo yake utaishia kuumizwa, kutokuwa na furaha katika hayo mahusiano na zaidi hataridhika.

Tatizo lingine kubwa ambalo unaweza kukutana nalo kwenye hii hatua ni kuwaza kuwa na mpenzi mpya ambaye kwa viwango vya duniani hayupo kwa maana kwamba unaweka qualification za juu kuliko binadamu yeyote.
Ingawa lengo lako ni zuri kwamba unataka upate mpenzi mpya ambaye hatakuumiza wala kukurudisha ulikotoka hata hivyo idealization ya aina hiyo inaweza kukufanya ushindwe kumpata mtu halisi kwani hayupo.

Kosa lingine ni kwamba unaweza kujikuta unaangukia kwa mwanaume wa aina ile ile tena au mwanamke wa aina ile ile tena kitu kinachodhihirisha kwamba matatizo yaliyokuwepo mara ya kwanza badala ya kuyatatua mliamua kulaluana wenyewe.

No comments: