"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 22, 2009

Mke wa Professor!

John ni professor katika chuo kikuu kimoja nchini Canada.
Huandika papers za nguvu, na kutoa lectures zenye heavy stuff na hutumia muda mwingi sana library.
Mke wake ambaye anaitwa Linda anampenda sana mume wake ingawa kimadarasa wapo tofauti sana ni kama mlima kilimanjaro na kichuguu.
Linda anapenda sana kuwa karibu na mume wake John tatizo utaongea kitu gani na Professor mwenye uelewa wa juu kiasi hicho?

Linda akafika mahali akajiuliza itakuwaje maisha kama haya ambayo mke na mume hawana kitu cha kuongea pamoja?
Baada ya kutafakari kwa umakini sana akagundua kwamba mume wake anaandaa paper inayohusu ndege (birds) na kwa kuwa hata yeye anawafanya ndege akaona ndiyo mwanya pekee wa kuunganishwa na mumewe.

Linda akaenda kununua vitabu vinavyohusu ndege, na akamuomba mumewe wahudhurie semina na kitu chochote kinachohusu ndege na ikajibu kwani hata mumewe akawa anapenda sana kuhusu ndege na wamekuwa sasa wanafanya hata vacation mahali ambapo wanaweza kwenda kuangalia ndege (bird watching)

Ni miaka 20 sasa wanafanya kitu kimoja na kufurahi pamoja. Linda hajui lectures ambazo mumme wake hutoa chuo na pia hajui kozi gani anafundisha ila anajua kitu kimoja tu kwamba yeye na mumewe linapokuja suala la ndege huongea pamoja na kuwaunganisha pamoja kama wanandoa.
Kuna usemi kwamba hobbies ni kitu kinachowaleta wanandoa pamoja na ni kitu kizuri mno.
Inawezekana mumeo ana interest na kitu fulani na kupitia hicho kitu ukiungana naye unaweza kumleta karibu zaidi katika maisha yako kuliko unavyopingana naye.
Jambo la msingi ni kuhakikisha hicho kitu si dhambi.
Kama mumeo ni mlevi wa kutupwa kuungana naye ni kujimaliza mwenyewe!

No comments: