"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 22, 2009

Nimejiunga naye.... Amebadilika!

Mume wangu hapa humtoi! James ni mwanaume anayependa sana soka si kuangalia kwenye Tv tu bali hata kuhudhuria mechi mbalimbali kuanzia uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hadi mechi ndogondogo mitaani na wakati mwingine kukiwa na mjadala wowote kuhusu soka basi hapo ni ugonjwa wake yaani anajisikia raha na anajisikia yupo nyumbani.

Mke wake Jane tangu wameoana amekuwa hapendi kabisa kusikia habari za mchezo wa soka na amekuwa analalamika (kefyakefya) kwa tabia ya mumewe James kupenda soka kiasi hicho kwani wakati mwingine huondoka nyumbani kwenda kuangalia mechi za ligi kuu ya Uingereza na kurudi usiku sana.
James ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Asernal Uingereza na timu ya Yanga jijini Dar Es Salaam.

Baada ya kusemana sana na kuzozana sana, ilifika siku Jane akaamini kwamba ni kweli mumewe hawezi kubadilika kuhusu kuacha kuwa shibiki na mwanaume mpenda soka kupindukia na zaidi kila anavyozidi kumsema na kumlalamikia ndivyo James anazidi kujiweka mbali na kupenda soka na kutumia muda zaidi kuangalia TV au kwenda kwa wenzake kuangalia na kuchelewa kurudi nyumbani.

Jane anasema kwamba
Tangu nilipogundua kwamba sasa mume wangu hawezi kubadilika nimeamua kujiunga naye (if u cant fight them join them) hivyo siku hizi namuuliza hii weekend kuna mechi ya nani na nani ili tuwe wote na kama kuna mechi kwenye Tv basi tunakaa wote tunaangalia na ikifika break time nampa snacks na tunaendelea kuangalia.
Kama kuna mechi uwanja wa taifa basi tunaenda wote na kuangalia mechi, sikutegemea kama itakuwa raha kiasi hicho kwani kitendo cha mimi kuheshimu interest zake kumekuwa na connection mpya kimapenzi ndani yetu na pia na mimi nimekuwa najisikia raha sana kuongea kitu kile na mume wangu anakipenda.
Tangu nimeanza kuwa upande wake kuhusu soka matokeo ni kwamba sasa James amekuwa mwanaume mzuri maeneo yote ya ndoa yetu na pia amekuwa sasa anapenda kuongea yale mimi napenda kwani anasema mimi napenda yale yeye anapenda na nimejifunza kwamba kulalamika kwangu hakukuwa msaada au njia nzuri ya kutufanya mimi na yeye kuwa kitu kimoja katika ndoa yetu”.


No comments: