"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, November 23, 2009

"Too late to catch the bus"

Afadhari hujachelewa basi la abiria!Mara nyingi hobbies husababisha wanandoa kuwa na mawasiliano mazuri, kuongea pamoja, kuwa na kicheko na kufanya vitu kwa pamoja.
Inakuwa ngumu sana kuwa na mawasiliano mazuri pale inapotokea wawili walioamua kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha kila mmoja kuwa na hobyy yake kiasi kila mmoja anachukukia kile mwenzake anapenda.

Kuna hii story kwamba kuna mwanamke mmoja katika nchi fulani isiyo na jina ambaye aliamua kuwekeza kwa watoto wake na akamsahau mume.
Hawa wanandoa wawili walioana na wakawa na wakati mzuri sana pamoja kabla ya kupata watoto.
Baada ya kupata mtoto wa kwanza mke akawa anatumia muda wote kwa ajili ya mtoto hakuwa na muda tena kwa ajili ya mume wake.
Baada ya miaka 3 mtoto wa pili akazaliwa na sasa mama akawa too much occupied na watoto hivyo mume kuwekwa pembeni kwani kila kitu sasa ni “Watoto kwanza”.

Mume kuona hivyo akaamua kuwa na maisha yake yaani kuwa na marafiki wengine ambao anaweza kuongea nao, akatafuta masikio mengine ya kike ya kumsikiliza feelings zake, si unajua mwanaume huhitaji masikio ya mwanamke wakati fulani kati maisha yake ili kuongea kile anaamini kinamfanya yeye kujiona ni mwanaume.
Lazima tukubali kwamba kila mmoja aliumbwa na uhitaji wa jinsia nyingine hata kama hakuna sex bali sharing ya siri, mafanikio na matatizo ya maisha haya au masumbufu ya maisha haya.

Mwanaume akawa na watu wapya ambao aliunganisha feelings zake iwe ni hobbies au interest ilimradi maisha yawe na ladha, jambo la msingi ni kwamba alifahamu kwamba mke wake yupo na watoto na anahitaji kuwa na maisha yake.

Maisha yakawa yanaenda kama kawaida huku mke na watoto wake na mume na kazi na maisha yake mwenyewe.
Wale watoto wakakua na wakafika wakati wa kwenda college, na wakawa sasa wanarudi wakati wa likizo tu, ndipo mke akaanza kujisikia upweke na kuanza kujitahidi kujiunganisha kwa mume wake ambaye miaka 25 iliyopita waliacha connection kama mke na mume kuongea pamoja na sharing ya mambo mbaliombali ya maisha.

Sasa mwanamke anajigonga kwa mume waanze kuongea, waanza kuwasiliana, waanze kuenjoy intimacy, waanza kufurahia maisha kama mke na mume hata hivyo mume anamwambia mke
You are too late to catch the bus
kwani alishajitengenezea maisha yake ya nani wa kuongea naye, kuwasiliana naye na zaidi yeye mke anaweza kuendelea kuongea na watoto si alijua atakuwa anaongea na watoto maisha yote?

Hata hivyo kibaya zaidi sasa watoto wameolewa na mama akitaka kwenda kwao au kuongea nao wanamwambia lazima atoe taarifa kwani wanapenda sana kutumia muda wao na wapenzi wao na si mama tena.

Sasa mke anaishi kwa upweke ingawa mume anaye.

Upweke (loneliness) ni kitu kinachohuzunisha sana bila kujali upo umri gani, hata hivyo kuwa mpweke na uzee maumivu ni makali zaidi.
Je, ingekuwaje sasa kama tangu wanaoana na kuwa na watoto huyu mwanamke na mwanaume wangekuwa walitengeneza mawasiliano mazuri?
Au Urafiki mzuri?
Au Mapenzi ya kweli?

Kumbuka kuna wanaume wengi ambao baada ya watoto kuzaliwa wamejikuta katika upweke uliokithiri.
Na baada ya kupita kwa muda wa miaka mingi barabara hii ya upweke hufika mahali ambapo hata siku mke akitaka waanze upya mawasiliano huwa too late to catch the bus.

Hivyo kama wewe ni mwanamke ni muhimu sana kuwa na busara na hekima ya kuhakikisha mume unampa nafasi katika maisha yako hata kama unajiona una wajibu mkubwa kwa mtoto au watoto ulionao na muhimu weka priorities kwa mume kwanza maana watoto hawawi watoto milele.
Unaweza kuwa mama na mke kwa wakati mmoja na mwanamke mwenye busara huanza kama mke na kumaliza kama mke.
Ubarikiwe

No comments: