"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, November 13, 2009

Tumegundua Siri (majibu)

Hello dada Neema,
Asante sana kwa waraka ambao niliupata nami bila kuchelewa nikamshirikisha mume wangu James na tukaujadili na kwa kweli tuliufurahia sana kwani tunapenda sana ndoa yetu iwe kama yenu.
Baada ya kujadili kwa kina mimi na mume wangu James tumeamua jambo moja tu nalo ni :-
Kama maombi ni kitu halisi basi tutafanya (kuomba) kila wakati kuhakikisha ni moja ya msingi wa ndoa yetu.

Hata hivyo baada ya kuingia chumbani na kuanza kuomba jambo moja limejitokeza nalo ni namna gani tuombe kwani kuna aina fulani ya vizuizi ambavyo vimejitokeza ngoja nikueleze vizuri hapa chini naamini utaweza kutushauri pia.

Mimi ninafahamu jinsi ya kuomba (kuongea) na Mungu mwenyewe na nimezoea hivyo bila mtu mwingine kunisikiliza na huwa nakuwa wazi sana kueleza kila kitu kwa Mungu bila kumficha, nipo wazi (transparency).
Sasa tukiwa mimi na mume wangu James kwangu inakuwa ngumu sana kuomba kwa sauti kwani nahisi Mume wangu ananisikiliza na sijajua atanifikiria vipi kuna vitu ninavyoongea na Mungu nahisi mume wangu hatakiwi kuvisikia kwani kwa mume wangu ni non sense.
Na pia sijajua nikiomba kwa kumpendezesha mume wangu je Mungu atakubali maombi ya aina hiyo?
Je, niombe kwa sauti huku nikijihadhari na maneno ninayoomba ili mume wangu asijisikie vibaya, na je, Mungu atanionaje?
Naomba unielewesha kwani najikuta nipo nervous kweli, ulimi unasitasita, nipo njia panda na kama mtu anayeongea lugha mbili ili kuwafurahisha watu wawili wanaomsikiliza kila mtu na lugha yake.
Mume wangu amependekeza tuwe tunaomba kimya kimya kila mtu ndani kwa ndani, ila naona hainogi nimezoea kuongea kwa sauti mbele za Mungu wangu, unaionaje hiyo?

Tunaomba msaada wako iweje kwani tumeamua kuwa na maombi kabla ya kuwa mwili mmoja kila siku tukiwa faragha.

Usichoke kutushauri na Mungu akubariki sana na msalimie mumeo mpenzi John.
Ni mimi rafiki yako

Jane (Mrs James)

No comments: