"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 15, 2009

Uangavu

Je, unaweza kumruhusu partner wako asome sms zako hivi????Kama kuna neno moja la msingi ambalo ni msingi wa ndoa yoyote neon hili ni Uangavu (transparency).
Kamusiinafafanua kwamba neno uangavu maana yake ni kuona kitu moja kwa moja hadi ndani, ni kuwa wazi, kuwa huru kimawasiliano na zaidi ni kuwajibika.
Uangavu katika ndoa maana yake kumuona mpenzi wako hadi ndani na kumfahamu vizuri bila shaka maeneo yote ya maisha yenu.

uangavu katika ndoa ni mwanaume au mwanamke kuweza kusoma sms na kupokea simu za mwenzake bila mashaka wala wasiwasi, kusoma emails zilizomo kwenye inbox yake bila wasiwasi wala hofu, Kufahamu akaunti yake benki ina kiasi gani, kuongea siri zako kwake bila mashaka na zaidi kuwa huru kuhakikisha mwenzako anajisikia vizuri kihisia.
Uangavu ni kuwa wewe bila kuwa na aina yoyote ya unafiki.
wanadamu tuliumbwa na uwezo au hamu ya kutaka kumfahamu mwenzako kwa undani hadi usiwe na shaka wala wasiwasi.
Transparency ni process na haiwezi kutokea usiku mmoja tangu umefahamiana na mpenzi wako ingawa wapo watu ambao hata akiwa kwenye mahusiano hataki mwenzake afahamu mambo yake kitu ambacho si lengo la mahusiano.
Uangavu ni kugundua au kupata uvumbuzi wa mambo mbalimbali mapya kwa mume wako au mke wako kwa sababu ya kuwekana wazi.
Bila kuwa na mawasiliano ambayo ni wazi mahusiano yanaweza kukwama.
Jambo la msingi ni wewe kuwa wazi kueleza kilichondani yako au siri zako kwa mwenzi wako (sincerely & straightfowawrd) na zaidi kushirikiana kupeana habari za kila kitu kinachohusu maisha yenu ili kuondoa wasiwasi, hofu na mashaka kwa mwenzako.
Kuficha vitu si jambo la busara na unapokuwa wazi na mwenzako naye anakuwa wazi kwako kwani kuwa wazi ni kufahamiana na kufahamiana ni mahusiano na binadamu tuliumbwa kuwa na mahusiano.
Je, upo wazi kwa mke wako au mume, au mchumba wako kiasi kwamba chake ni chako na chako ni chake?

No comments: