"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, November 24, 2009

Una ripoti ya ukaguzi?

Mchwa umefanya kazi yake!
Mwenye nyumba alihitaji ripoti ya ukaguzi wa mara kwa mara! "Mpenzi …………,nionyeshe uso wako, na niisikie sauti yako, kwa maana sauti yako ni tamu, na uso wako unapendeza.
Tukamatie mbweha, mbweha wadogo wale wanaoharibu mashamba ya mizabibu, mashamba yetu ya mizabibu yalichanua".
(Wimbo ulio Bora 2: 1-15)

Ukisoma kitabu cha Wimbo ulio bora katika Agano la kale sura ya 2 kuanzia mstari wa 1 hadi ule wa 14 unakutana na maneno ya wapenzi wawili (wanandoa) ambao wana wakati mzuri na wanaongea lugha ya kimahaba, wapo faragaha kimapenzi (intimacy) wapo deep in tender affection na it is romantic.

hata hivyo kufika mstari wa 15 maneno yanabadilika na wanatangaza kuwa na tahadhari na kuonya kwamba kuna mbweha wadogo wanaoharibu shamba lao la mizabibu iliyochanua na wawakamate.
pamoja na kuwa na mapenzi matamu, mapenzi yanayokua na kuongezekan kuwapa raha bado wanafahamu kwamba kuna mbweha wadogo wanaweza kuharibu ndoa yao.

Kinachofurahisha ni kwamba wapo very concerned na hao mbweha wadogo na kila mmoja anaonekana ni inspector mzuri wa mahusiano yao.

Pamoja na uzuri wote wa mapenzi bado mmoja wao amechukua hatua ya kuwa inspector na kuomba hao mbweha wadogo wakamatwe na kuondolewa.

Hili ni somo zuri kwa mwanandoa yeyote kuwa makini na mbweha wadogo ambao wanaweza kuharibu ndoa ikawa chungu kama limau.

Ni muhimu sana kukagua mahusiano yako wewe mke na mume kuangalia kama kuna mbweha wadogo na inawezekana ndoa yako isiwe na mbweha wadogo bali wadudu wadodgo kama mchwa ambao wanaweza kuvamia ndoa yako na kuodondosha ghafla bila kutegemea.

Katika sehemu ambazo kuna mchwa ni rahisi sana nyumba zilizojengwa kwa miti na mbao kutekekea kwa mchwa kuliko moto.
Mchwa ni wadogo na huwa kimya hata hivyo ni industrious zaidi kuharibu nyumba kuliko moto ambao hata media nyingi huzipa nafasi zaidi.

Kumbuka, ni vitu vidogovidogo sana ambavyo kwenye ndoa ndivyo vyenye umuhimu iwe kujenga au kubomoa na mara nyingi hasa sisi wanaume (si wote) huwa tunaamini vitu vidogovidogo (kama vile kumwambia mke nakupenda, au kumbusu, au kumkumbatia au kumsifia pale amefanya kitu kizuri au pale amependeza nk) havina nafasi sana katika kujenga ndoa au kubomoa ndoa, ukweli ni kwamba vina maana sana.

Matukio kama kupoteza kazi, Ugonjwa wa ghafla, kifo cha motto nk mara nyingi huimarisha ndoa kuliko vitu vidogo.

Hivyo kama mwanandoa hakikisha unafanya ukaguzi mara kwa mara kama kuna mchwa unakula ndoa yako au wale mbweha wadogo ambao wanapenda kuvamia shamba lenu la mizabibu iliyochanua.

Ubarikiwe na Bwana!

No comments: