"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, November 22, 2009

Unaweza kustaafu mpweke!

Kustaafu kazi huwa maisha ya upweke sana kwa wanandoa kama waliishi maisha yakukuwa bila mawasiliano kwa miaka mingi.

Wanandoa wawili ambao mume alikuwa anapenda sana kucheza Golf walikuwa na kwaida ya kwenda vacation katika kisiwa Fulani huko Amerika ya kusini.
Mume alipenda sana kwenda huko katika hicho kisiwa kwani alikuwa na wakati mzuri sana kucheza golf ingawa mke wake na golf vilikuwa vitu viwili tofauti kama vile kibaka na polisi.

Huyu mwanaume alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa na hawakubahatika kuwa na watoto hivyo alipanga kwamba akistaafu kazi atahamia kwenye hicho kisiwa ili amalizie maisha yake kwa kucheza golf kwani kwa kucheza golf kutamsaidia kuweka mwili wake fit ukiacha kwamba golf ilikuwa interest yake na moja ya hobby muhimu sana kwake.

Swali lilikuwa na mke wake mpenzi ambaye kwake Golf ilikuwa ni kitu kigeni na kitu ambacho hapendi si kusikia tu bali kuona mume wake mwenyewe anapenda.
Hata hivyo siku moja alikaa chini na kujiuliza hivi maisha yatakuwaje kama tukistaafu mume wangu ameamua tuhamia kwenye kisiwa maarufu cha golf na kununua nyumba na kumalizia maisha yetu huko.
Je, nitaishi maisha gani kama mwenzangu kila siku itakuwa ni golf tu na mimi na upweke wangu?
Si nitakuwa mjane wakati mume bado ninaye?
Itakuwaje kama na mimi nikijifunza golf na kuhakikisha atakapokuwa anaenda kwa golf tunakuwa wote sambamba?
Je, ni raha ilioje kama wote kwa pamoja tutakuwa na wakati mzuri pamoja kucheza golf kila siku?
Je, nitaanzeje wakati hata golf sijui?

Kwa kuwa walikuwa wamebakiza miaka miwili tu na kuhamia moja kwa moja kwenye kisiwa maarufu cha golf huyu mwanamke alifanya uamuzi wa kuanza kujifunza kucheza golf kwa nguvu zote na uwezo wote.
mara nyingi tunakubali hatuwezi au hatutaki kwa sababu tumeamua kwamba hatuwezi na hatatuki na huo ndio mtazamo wetu hata hivyo mwenzetu aliamini kwamba bado anaweza kujifunza na kuwa mcheza golf mzuri.
Kwa kuwa shughuli za mumewe zilikuwa ni za kusafiri mara kwa mara ilimfanya mke wake kuwa na muda wa kutumia vifaa vyake na kwenda kujifunza (si unajua kuna wanaume wala huwa hawajali wake wanafanya nini baada ya wao kusafiri).
Alijifunza kwa miaka miwili na kuficha hiyo siri kwa mumewe hata hivyo baada ya kuhamia kwenye hicho kisiwa ikawa golf na wao na wao na golf na ikawa furaha ilioje kwa mume kuona mke wake nae kwenye golf wamo.
Hii ni moja ya success story ya kumfanya mume awe anaongea na wewe mwanamke.

Kumbuka unachokifanya sasa ni muhimu sana kwa ajili ya maisha yako ya uzeeni kama wanandoa.
Kama hamuwezi kuwasiliana leo, usitegemee kesho mtaweza kuwasiliana ghafla.

No comments: