"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, November 18, 2009

Usiumie!

Hello rafiki Jane,

Asante kwa barua yako ambayo niliipata jana usiku.

Pia pole sana kwa wasiwasi na hofu hata mashaka kutokana na yale unakutana nayo kuhusu mumeo kupata secretary mpya ambaye unahisi anaweza kumteka mumeo.

Kwanza mdogo wangu naomba usipaniki, wala kuwa na hofu na mashaka, usioni ndoa yetu na John imefika umri wa miaka 30 kwani kuna milima na mabonde tumevuka pamoja na moja ya milima ni kama huo wa kwako kujipa wasiwasi kwamba mumeo atachukuliwa na mwanamke anayeshinda naye kazini.

Ni Adamu na Hawa ambao hawakuwa na maisha ya wasiwasi wa mume au mke kuchukuliwa na mwingine kwani wao ndo walikuwa wanandoa wa kwanza duniani hata hivyo kabla ya kuanza kuwa na hofu na mashaka naomba jiangalie kwanza kwenye kioo (sina maana uchukue kioo) nina maana jiangalie mwenyewe kwanza je unampenda mumeo kiasi ambacho unaamini mtu mwingine haweza kuchukua nafasi, maana kuna wakati sisi wenyewe wanawake tunajisahau mno kwenye ndoa zetu.

Nakumbuka nilipokutana na tatizo kama hilo la kwako ilinipasa niende kwa dada wa jirani hapa ambaye ni nyumba ndogo ya kigogo mmoja hapa mjini nikamuuliza inakuwaje au anafanya vipi kuhakikisha mume wa mtu anabaki kwake muda wote hadi anasahau familia yake.

Yule dada alinijibu kwamba anachofanya ni kumpa uhuru huyo mwanaume kusema na kufanya kile ambacho kwa mke wake hapati nafasi, hii ina maana kwamba mwanaume akifika kwake anakuwa huru kusema chochote anataka na kufanya chochote anataka kuanzia jikoni hadi chumbani.

Ile mume wa mtu akifika tu mlango anampokea kwa mabusu na hugs.
Swali je wewe unafanya hayo?

Unampa James nafasi na uhuru kiasi hicho au kila unachofanya unafanya just for granted?

Ukifanya kila kitu kwa kadri ya upendo wako wote kwake basi haina haja kuwa na hofu na huyo secretary labda awe ni mwanaume ovyo.

Tutawasiliana zaidi na pia nitakupigia simu baadae saa mbili usiku tuongee zaidi na nitakushauri zaidi mdogo wangu.

Ni mimi Neema

2 comments:

Anonymous said...

Habari za leo kaka Mbilinyi? Hongera kwa kazi nzuri ya kutuelimisha juu ya maisha yetu ya ndoa.

Mimi ni kijana wa kiume na niliye kwenye ndoa kwa mwaka mmoja sasa. Nimekuwa na tatizo la kuchelewa kusimama mara baada ya kukoja (ejaculate). Huwa inanichukua dakika 30 mpaka 45 mpaka kuweza kusimama tena. Hii hali inamdisappoint pia mke wangu maana bado anakuwa hot.

Sasa nauliza je hii delay ya muda huo ni kawaida? Kama sio kawaida ni muda gani ndio kawaida na nifanyaje kurekebisha hii hali?

Nashukuru sana kaka kwa kazi yako nzuri.

Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,

Hongera kwa kuuliza swali na pole sana kwa yale unakutana nayo hata hivyo kumbuka hakuna lisilowezekana kwa Mungu, Naomba nitumie email kwa lazarusmbilinyi@gmail.com ili nikupe maeleza muhimu.

Salimia sana mkeo mpenzi!

Upendo daima