"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, December 31, 2009

Hupunguza Hamu....

Kunyonyesha hupunguza hamu ya sex
Kukosa hamu ya tendo la ndoa ni jambo la kawaida baada ya kujifungua mtoto na wakati mwingine huendelea hadi baada ya mwaka mzima hasa kwa mwanamke anayenyonyesha mwenyewe.
Wanandoa wengi hawajajua nini hutokea baada ya mtoto kuzaliwa na hasa mke anaponyonyesha mtoto na kujiona mke hana hamu tena ya tendo la ndoa.
Mwanamke anayenyonyesha huzalisha homoni ya Prolactin ambayo husaidia mwanamke kutengeneza maziwa ya mtoto na pia hupunguza hamu ya tendo la ndoa ingawa wanasayansi bado hawajaweza kutoa majibu kwa nini inakuwa hivyo.
Mwanamke anayenyonyesha mara nyingi hujisikia amechoka na wakati mwingine huchoka kama ng’ombe.
Hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba kwa upande wa mwanaume hamu ya tendo la ndoa hubaki palepale kama kawaida.

Na jambo kubwa zaidi ni kwamba mwanamke huelekeza nguvu zake zote kwa ajili ya mtoto ambaye amezaliwa.
Mtoto sasa ndiye anayekumbatiwa, anayepata busu na cuddling na mwanaume anakuwa kwenye reserve list na matokeo ni kwamba kuna kuwa na gap kubwa kati ya mke na mume wa kile mume anataka na mke anataka.

Wanandoa wengi iwe ni kunyonyesha kwa kawaida au kwa chupa huamini kwamba baada ya mtoto kuzaliwa itachukua kama miezi 2 tu na watarudi katika hali yao ya kwaida kusherehekea tendo la ndoa tena hata hivyo hujikuta wanakutana na roadblock ya mke kukosa hamu na matarajio makubwa ya aina hii husababisha mwanaume kuwa na big disappointment, frustrations na conflict.

Mwanamke aliyezaa kurudi kwenye hali yake ya kawaida ya kutaka tendo la ndoa kwa kwenda mbele hurudi baada ya miezi kadhaa baada ya kuacha kunyonyesha na wakati mwingine hata baada ya mwaka mmoja baada ya kuacha kunyonyesha.
Kama wanandoa watafahamu kwamba hili ni jambo la kawaida basi wanaweza kuwa na mazungumzo mazuri lini mke aweze kuacha kunyonyesha au pia kusimama pamoja kulea mtoto huku kila mmoja akifahamu kwamba sherehe za tendo la ndoa zitakuwa kwa mwendo wa kobe until further notice.

Happy New Year 2010

Thursday, December 24, 2009


Wednesday, December 23, 2009

Epuka Makosa Haya!


Hutaki kuanza.
Tatizo kubwa na sugu la wanawake wengi ni kitendo cha kutoanzisha kwamba anataka sex na mume wake (initiating) na kumwachia mwanaume kama wajibu wake katika ndoa.
Je ina maana hakuna siku unakuwa umemtamani mume wako na ukaamua wewe kuanza?

Kushindwa kuanzisha kwamba unahitaji sex ni biggest mistake wanawake wengi wanfanya kwani wanaume wengi hujiona kama si sahihi (disequillibrium) katika kuimarisha mahusiano kama kila siku ni mwanaume tu ndo anachokoza.
Kimsingi hata mwanaume anajisikia vizuri pale mke wake anapolianzisha kwamba na yeye anataka.

Je, ni kueleza kwamba wanaume tunakuwa na interest kubwa wa sex na wanawake hawana au huwa hawapendi siku zote.
Naamini kuna wanawake ambao nao wanapenda sex kama wanaume.
Ni vizuri mwanamke kuonesha interest kwa kuchukua hatua kusema kila unapenda kwa mumeo na kwamba leo unamtamani na kumuhitaji siyo kila siku yeye tu miezi 12 na siku 365 na robo naamini mumeo akiona juhudi yako ya kulianzisha atafurahi na kukupa appreciation kubwa na unaweza kupata level upya ya satisfaction.
Hivyo kama wewe ni mwanamke anza leo.
Wasiwasi kwamba mwili wako upoje:
Kufikiria jinsi mwili unavyoonekana kwa mume wako na kuwa na wasiwasi kwamba anaweza kukuona labda mnene sana (fat zimejaa vipande vipande), au matiti makubwa sana au madogo sana au makeup ulizoweka usoni na mtindo wako wa nywele kichwani au sijui sehemu zingine zina rangi ipoje husababisha ushindwe ku-enjoy tendo la ndoa na mara nyingi unaweza kuharibu kila kitu hadi ushindwe kufika kileleni.
Jambo la msingi ukishakuwa na mumeo ni kuwa na total concentration kwa tendo lenyewe kwa raha zako zote.
Wanaume hufurahia mwanamke ambaye anajiamini na mwili wake na jinsi alivyo na anahusika mia kwa mia katika furaha ya tendo la ndoa na si kuwa na hofu na kujipiga kufuli kihisia.

Tuesday, December 22, 2009

Love Vs Romance!

Love is energy flow that you experience.
You don’t have it.
Romance never lasts, the thrilling, falling in love always fades,
because romance is not the same thing as love.
If love is our home then romance is the doorway.
You go through it to get in, but it is not a dwelling, not a space where you can live.

Sunday, December 20, 2009

Uhuru wako...............

Hamu ya kumpenda mpenzi wako muda wote na wewe kupendwa kwa namna hiyo hiyo kwa muda wote ni kitu kinachofurukuta kwa kila moyo wa binadamu yeyote, vinginevyo kuna tatizo kubwa ambalo ni wewe tu unalijua au ni karama uliyopewa na Muumba.
Ingawa ni kweli tunastahili aina hiyo ya upendo (kupendwa na kupenda kunakofukuta ndani ya moyo muda wote na kufurahia na kujiona ni kweli kupendwa ni raha) si kweli kwamba hali kama hiyo inaweza kuja yenyewe au kutokea yenyewe bila kufanya chochote.

Kuwa na mapenzi ambayo yanaridhisha, yanachangamsha na kusisimua ndani ya moyo ni matokeo ya extra ordinary achievement.
Ni hata kama ni rahisi kupata mapenzi ya aina hii haina maana kwamba watu hawana uwezo (capacity) wa kupenda bali hawajui jinsi ya kuendelea kupendana tena na tena tangu kupendana kwa mara ya kwanza (fall in love).

Inawezekana unaamini kwamba kutunza upendo ule wa kwanza na kuendelea nao miaka na miaka ni kitu kisichowezekana, si kweli kwani inawezekana.
Au inawezekana umeshaumizwa kutokana na mahusiano ya kwanza na moyo wako umevunjwavunjwa na una maumivu makali na hata kama upo kwenye mahusiano mazuri bado unajikuta upo bored na umekwamba pia inawezekana kwa sasa upo kwenye penzi lenyewe unajiona upo top of the world na kwa mbali unahisi upendo unaanza kuchuja na kupotea na unawasiwasi mambo yanaweza kuwa tofauti.

Kumbuka kuishi maisha marefu, katika penzi la kweli na muunganiko mzuri wa kimapenzi na mpenzi wako (mume au mke) siyo kitu ambacho ni complicated ni kitu rahisi na kipo ndani ya uwezo wako.
Unachotakiwa kugundua na kuendelea kuunganisha ni vitu vine tu

MWILI
Amsha senses, kuona, kusikia, kuonja na feelings za upendo. Fahamu mwili wako kuwa ni hekalu takatifu la upendo, zawadi ya muumba kwako, mwili wako hubeba nafsi yako, udhihirisho wa matendo ya Mungu kwako.
Mwili ni nyumba yako na uwe na amani hata katika ngozi yako. Jiweke tayari wakati wote kujisikia raha na mwili wako.
Upe mwili wako mapenzi, mguso wa kimwili.
Wewe ni mwili na mwili wako ni uhuru.

AKILI
Hakuna kikomo katika kufikiria, kila kikomo cha kufikiria kimewekwa na wewe. Unao uwezo wa kila unafikiria na unaweza kuamua kufikiria mambo mazuri kwa ajili ya maisha yako.
Hakuna anayeweza kuondoa furaha yako isipokuwa uamue mwenyewe.
Wewe ni akili na akili zako ni uhuru wako.

MOYO
Ponya moyo wako uliovunjika.
Fungua moyo wako ulioponywa.
Toa na pokea upendo kirahisi, kiasili (naturally), ghafla, na unconditionally.
Vumbua upendo ndani yako na jipende mwenyewe kwanza.
Jikubali mwenyewe kwanza na jisamehe kwa yale unakosea.
Fahamu kwamba unastahili kupokea upendo.
Tambua na karibisha upendo kutoka kwa wengine.
Tamani kuwa mtu wa kupenda kuliko mtu yeyote (the greatest lover).
Wewe ni moyo na moyo wako ni uhuru.

NAFSI
Mwili wako, akili zako na moyo wako ni madirisha ya nafsi yako.
Unapowasiliana na Mungu ni nafsi yako inawasiliana na Mungu.
Nafsi yako ina mwili wako, akili zako, moyo wako ndani yake.
Wewe ni nafsi na nafsi yako ni uhuru.

Je, ni Skills tu?

Hata kama skills ni jambo la msingi sana katika sex, kuwa na moyo ulio wazi na hamu ya kujikabidhi kwa mume wako au mke wako husaidia kuwa na uzoefu wa sex inayokupa ridhiko zaidi.
Hata hivyo njia bora ya kujifunza au kutojifunza ni actions; kumbuka mwili wako ni uhuru wako na upo responsible ni kitu cha lazima au hiari na unaweza kuupa uhuru mwili wako kwa kufanya Yafuatayo

KWANZA
Husika na mwili wako. Usikilize unakwambia kitu gani hasa jinsi unavyojisikia na nini unataka na unachohitaji ili kufanya kazi katika kiwango chake cha juu. Upe chakula kizuri, muda wa kupumzika, mazoezi kiasi cha kutosha na milango ya fahamu iliyo imara.

PILI
Uwe mwepesi kutambua message negative kuhusu mwili wako hasa zile ambazo wengine wanakwambia na zile wewe unawapa wengine.
Hakikisha unafanya replacement na positive messages kwa mwili wako na wengine.

TATU
Ukiwa na mpenzi wako hakikisha unampa mguso wa mwili (touch) ulio mwororo na caring.

NNE
Badilisha mtazamo wako kuhusu sex kutoka kufanya na kufika kileleni (performance and orgasm) na kuwa kupeana raha na kuunganishwa (pleasure and union)
Jifunze kufanya sex kuwa sanaa yenye raha.

Kuhujumu mwili Wako

Si kweli kwamba kuguswa na sex ni vitu hatari sana, vibaya na uchafu.
Ukweli ni kwamba
Katika ndoa kupeana raha kwa kugusana (touching) na sex ni mlo kamili wa moyo, mwili, nafsi na roho.

Si kweli kwamba mume wako au mke wako ndiye anayehusika na raha yako kimapenzi.
Ukweli ni kwamba wewe mwenyewe unahusika na raha ya mwili wako hata kama umesoma kiasi gani, au una akili kiasi gani au hata kama partner wako yupo makini kiasi gani kama hujui kwamba mwenye unahusika na raha yako huwezi pata raha na kufurahia mapenzi.

Si kweli kwamba mke wako au mume wako anafahamu namna gani, lini na wapi unapenda kushikwa kimapenzi.
Ukweli ni kwamba ni jukumu lako kumfahamisha mume wako au mke wako ajue kile unapenda na unahitaji kimapenzi.
Kwani ni partners wachache sana wanaweza kusoma minds au kile unataka linapokuja suala la kufanya mapenzi.
Na kufanya mapenzi ni moja ya maeneo ambayo huwezi kufuata Golden rule kwamba “Fanya kile na wewe unapenda ufanyiwe” kwani kwenye mapenzi kila mtu anapenda kitu tofauti ili apate raha.
Kile mke au mume wako anapenda kufanyiwa katika mapenzi ni tofauti sana na wewe.

Si kweli kwamba ukiwa na mwili unaoonekana young ndipo uta-enjoy sex.
Ukweli ni kwamba jinsi mwili unavyoongeza umri ndipo huwa bora kwa sex.
Kwani Kuwa mzuri kimapenzi ni uzoefu unao patikana kwa kujifunza miaka na miaka kwa sababu sex huhitaji ufahamu na mazoezi (knowledge and practice).
Utamaduni wetu unatuambia kwamba unapoonekana young unakuwa sexy zaidi ukweli ni kwamba kuvutia kwa mwili hakuwezi kuleta kukomaa wa emotions na self-confidence katika kufanya sex kitu ambacho ni muhimu sana kuwa sexy na sex inayo inayoridhisha.

Je,naweza kukaa kivyangu?

Je, kutengana kati ya mke na mume bila kupeana talaka ni jambo linaloruhusiwa kibiblia hasa kama kuna matatizo ya ndoa kama kupigana au mmoja kutokuwa mwaminifu?

Kwa kuwa kuendelea kwa ndoa ni mapenzi ya Mungu bado kutengana kwa muda huweza kusaidia hasa pale wanandoa walio katika wakati mgumu kuendelea kupewa ushauri na usuluhishi ili warudiane bila kuumizana.
Kutengana kwa aina hii husaidia hasa kwa mwanamke ambaye ameolewa na mwanaume violent, mlevi au mwingi wa habari na hii ni kwa ajili ya safety ya mke na mke au mume haruhusiwi kuwa na partner mwingine kwani kuwa na miadi (dating, outing) na mwanaume mwingine kama ni mwanamke au mwanamke mwingine kama ni mwanaume huweza kusababisha mahusiano na ki-emotions na feeling na kusababisha kurudiana na mke au mume wake kuwa vigumu zaidi.
Na mtazamo mkubwa unatakiwa ni kulenga wanandoa kurudiana na kuendelea na ndoa yao na si vinginevyo.
(Kwa maelezo zaidi soma 1Wakorintho 7:10 - 11)

Unaridhika?

Je, maisha yako kimapenzi (sex) na mume wako au mke wako ni vile unataka iwe?
Majibu ya wengi ni HAPANA.
Hamu ya kuwa na mapenzi ya uhakika, au kuwa kama ilivyokuwa au kuwa kama ninavyotaka iwe ni kitu kipo ndani ya watu wengi kama mzigo wanaotembea nao kichwani bila sehemu ya kuutua.
Haijalishi tunawapenda namna gani wapenzi wetu bado kuna ndoto tunaota za kuwa na mapenzi yanayoridhisha zaidi.

Sasa kwa nini tunahitaji mapenzi yanaroridhisha zaidi?
Sababu kubwa ni kwamba sex is one of the supreme pleasures of life.
Hakuna kitu chenye raha kama sex.
(Thrilling, conforting and sustaining all at once).
Ni njie ya kuelezea na kuimarisha upendo na wakati huohuo inafanya cnnectiojns na senses zetu na kuumba tujisikie wazima (well being)
Kufika kileleni kumeonesha huweza kuimarisha immune sysytem ya mwili.

Sex is fun, ni njia kuelekea kwenye roho na kwa ufupi great sex hufanya watu kuwa na furaha.

Friday, December 18, 2009

Siri ya Kuvutia.....

SIRI YA KUMVUTIA MUME MUDA WOTE:
Ni kweli upo kwenye mahusiano na katika mahusiano yako mwanaume uliyenaye ni wa uhakika, safi kabisa na hongera sana.
hata hivyo linakuja wazo kwamba hivi inawezekana huyu mwanaume akaendelea kunipenda kama hivi?
Je, atakuwa yupo interested na mimi muda wote?

Haijalishi mnapendana kiasi gani ukweli ni kwamba mahusiano huhitaji kazi, huhitaji efforts, inahitaji kuwekeza jitihada kidogo ili kuvuna mambo makubwa.
Kama unapenda mume uliyenaye awe anavutiwa na wewe wakati wote kuna tips na siri nyingi unahitaji kuzifahamu vingenevyo unaweza kujikutana anakukwepa na kukuona huna lolote (huna jipya, unachosha)

Jambo la kwanza ni kweli mahusiano ni kitu cha ajabu sana huweza kupanda na kushuka kwa kiwango cha kutisha hata hivyo siri kubwa ya mahusiano unatakiwa usiwe mtu ambaye mpenzi wako anaweza kujua au kutabiri au kutarajia mara zote utasema nini au utafanya kitu gani, unahitaji kuwa na vitu vizuri ambavyo hawezi kutegemea, waingereza wanaita unakuwa spontaneous and fun na unakuwa na adventure ambazo hategemei.

Hakuna kitu mwanaume hapendi kama mwanamke aliye na usumbufu wa uhitaji (too needy). Kumtaka mume kila kitu hadi anajiona usumbufu huweza kuua mwanamke kumvutia mwanaume, ninachozungumzia hapa si ile hali ya kuonesha unamuhitaji bali ile hali inayoonesha unasumbua kwani hata kile ambacho kipo kwenye uwezo wako bado unataka mume akutimizie.
Kama anataka kutoka na rafike zake wa kiume mruhusu siyo kulalamika tu hadi anajiona mkosaji.
Kwani ukimruhusu naye akaenda kufurahi na rafiki zake na wewe ukatumia muda huo na rafiki zako kuna tatizo gani, wewe unataka kumganda all the time hadi anashindwa kupumua, kwa mwanaume hiyo ni dalili kwamba wewe mwanamke hupo huru bali upo desparate na maisha.
Pia si vizuri kumpigia simu au kumtumia sms kila dakika kutaka kujua yupo wapi anafanya nini na yupo na nani as if wewe ni auditor wa mienendo yake.
Ukiona message au simu haipokelewi ujua unamsumbua badala ya kuonesha upo caring.
Pia angalia usiwe ni mwanamke ambaye anatuma sms kwa mume au kumpigia simu mara moja kwa mwaka, this is too much!

Jambo lingine na la msingi sana mwanamke lazima ukumbuke kwamba wanaume wanasoma magazeti huwa hawasomi mawazo ya kwenye akili yako (mind) hivyo basi ni muhimu sana kumwambia mume wako kila unajisikia pale mkijadili suala lolote na siyo kukubaliana tu na kila kitu ukiamini kwamba unamfurahisha na unataka avutiwe na wewe.
Mwanaume mwenye akili timamu anafahamu fika kwamba mwanamke mwema na mwenye busara kichwani mwake ana ubongo hivyo huwezi kukubaliana na kila kitu na kusema ndiyo, ndiyo ndiyo ….
Mwanaume anahitaji mwanamke ambaye naye anaweza kupendekeza wazo jipya na kwa njia hiyo huonekana ni mwanamke strong na wanaume hupenda strong woman ambaye anaonesha uwezo hivyo kuvutia zaidi.
Hakikisha mume wako anasoma kitu kipya kuhusu wewe baada ya muda fulani na hiyo itasaidia kukuangalia kwa upya zaidi na maana yake unamvutia. Kama ulishaonesha kila kitu basi unahitaji kuwa mbunifu kwani mwanaume huhitaji kitu kipya kutoka kwa mwanamke baada ya muda fulani katika maisha.

Pia ni muhimu sana kuachana na imani potofu kama vile
"The key to a man's heart is through his stomach"
Ni kweli wanaume huwasifia sana wanawake wanaokaangiza vizuri hata hivyo si misosi mizuri tu ndiyo ticket ya mume kuvutiwa na wewe.
Pia wapo wanaoamini kwamba ili mume avutiwe na mke ni pale mke anapotoa sex kwa kwenda mbele, ni kweli mwanaume akipewa hiyo offer hawezi kulazia damu hata hivyo mwanaume anaweza kufanya sex na asiwe amevutiwa na wewe kwani kwa mwanaume sex na love ni vitu viwili tofauti.
Je, kama si chakula kitamu au sex kila siku ni kitu gani muhimu ili kumvutia mwanaume?
Jibu ni rahisi mno mwanaume anahitaji heshima, kumjali, kutukuzwa, kuenziwa, kusifiwa, thaminiwa na kunyenyekewa, kuhusudiwa (respect, admire).
Hakuna hitaji kubwa kwa mwanaume kama lile la kwamba anahitajiwa (needed) na mke wake.
Weekend njema!
God Bless you!
Dieu vous bénisse!
Mungu akubariki!

Thursday, December 17, 2009

Ni ngumu sana!

Kwa wayahudi ni mwanaume tu aliruhusiwa kutoa talaka na si vinginevyo!Suala la talaka ni issue ngumu sana katika nyakati mbali mbali ambazo binadamu amekuwa chini ya uso wa dunia.
Suala la talaka lilikuwa gumu sana wakati wa Musa.
Likawa gumu sana kwa mafarisayo hata wakaamua kumuuliza Yesu ingawa wao swali lao lilijikita katika kumtega Yesu na si kuelewa issue nzima ya talaka.

Suala la talaka ni gumu zaidi leo hadi limepelekea hata watu waliopo kanisani (Christians) kujikuta wamejigawa katika makundi mawili wale wanaokubali na (liberal Christian) wale wanaokataa (conservative Christian) na kila kundi (school) lina maandiko ambayo linasimamia kutoka katika Biblia.

Issue inakuwa ngumu zaidi kwa kuwa hata tafsiri (translation nyingi mpya za Biblia sasa nimebadilisha baadhi ya maneno ya msingi hata yale yanayohusiana talaka.
Kwa mfano Mathayo 19:9

Kiswahili Biblia inasema:
Mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini.” Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.”

Matthew 19:9 (King James Version)
And I say unto you, Whosoever shall put away his wife, except it be for fornication, and shall marry another, committeth adultery: and whoso marrieth her which is put away doth commit adultery.

Matthew 19:9 (New International Version)
I tell you that anyone who divorces his wife, except for marital unfaithfulness, and marries another woman commits adultery."

Matthew 19:9 (Contemporary English Version)
I say that if your wife has not committed some terrible sexual sin, [a] you must not divorce her to marry someone else. If you do, you are unfaithful

Matthew 19:9 (Worldwide English (New Testament))
But I tell you this. No man may send his wife away unless she has committed adultery. If he does, and if he marries another woman, he commits adultery. And if a man marries a woman who has been sent away by her husband, he commits adultery.'

Kutokana na translations za hapo ikitokea kila mmoja akawa na Biblia yake likija suala la talaka (divorce) hawa watu 5 hawatakubaliana kwani Kiswahili tunajua Uasherati(fornication) ni tofauti na uzinzi (adultery) na hata siku moja huwezi kuita zinaa (sexual immorarity au marital unfaithful) au uzinzi (adultery) ni uasherati bali uasherati ni aina ya zinaa.
Uasherati ni kwa wale ambao hawajaoana na uzinzi ni kwa wale ambao wameoana.


Kutofahamu maana au tofauti na uasherati na uzinzi husababisha kutoelewa nini Yesu aliongea katika Mathayo 19: 1-10.

Hata hivyo suala la talaka linaweza kupewa majibu kibiblia na Biblia ipo wazi na inaeleweka kabisa na Yesu mwenyewe alieleweka kabisa kwamba ukishaolewa hakuna kitu kinaitwa talaka isipokuwa kifo.

Swali walilouliza!

Wakajikuta swali lao limekosewa! Ni kweli zogo (controversy) au hekaheka kubwa inayowagawa watu katika makundi mawili kuhusu talaka inapatikana katika injili ya Mathayo 5:32 na 19:9
Kumbuka Injili ya Luka na Marko pia imeripoti tukio la Mathayo 19:9 Yesu alipotegwa swali na Mafarisayo isipokuwa ni Mathayo peke yake ameandika kuhusu exception ya kutoa talaka ambayo ni kosa la uasherati (tutaangalia baadae kwa nini ni mathayo peke yake ameripoti hivyo).

Kabla ya kufika huko ni Muhimu sana kufahamu mazingira (geography) iliyopelekea Yesu kuulizwa swali na Mafarisayo.
Tukumbuke kwamba Yesu alikuwa Galilaya na alikuwa amemaliza huduma yake na sasa alikuwa anasafiri kupitia eneo la Perea ili kurudi Yerusalemu kwa ajili ya pasaka (yaani kifo chake).

Mafarisayo waligundua kiwamba Yesu atapita hilo eneo ambalo kwa wakati huo lilikuwa chini ya himaya ya Herodi.
Hivyo mafarisayo walijua ni wakati muafaka wa kumuuliza swali (trick question) ili ajichanganye na wapate sababu ya kumuua.
(kumbuka mafarisayo walikuwa wanamfafuta sana Yesu wamuue ila walikosa sababu au shitaka Mathayo 12:14, Marko 3:6)
Kwa hiyo mafarisayo walimuuliza Yesu swali ambalo lengo ni kumtega yeye (test) na si kutaka kujua.

Kumbuka miaka 2 iliyopita Yohana mbatizaji ambaye alimtangulia Yesu alikuwa amefungwa Jela kwa sababu aliongelea suala la talaka ya Herode Antipas ambaye alioa mke wa mdogo wake Filipo ambaye mke wake alitoa talaka kwa mume wake Filipo na kwenda kuolewa na Herodi Antipas (kaka mtu) Soma Mathayo 14:1-12.

Yohana mbatizaji hakubabaika au kujisikia vibaya kumkemea Herodi na dhambi yake hata kama ni ikulu (Math 14:4) matokeo yake akawa arrested na kutupwa jela na baadae kukatwa kichwa.

Kwa kuwa Yesu alikuwa anapita maeneo ambayo ni himaya ya herodi Antipas, mafarisayo walijua fika kwamba Yesu atajichanganya tu na jibu la swali watakaloulizwa na atajimaliza kwa kumtaja Herode na dhambi yake ya kuoa mke wa mdogo wake na kama Yohana mbatizaji kwa kutamka tu aliuawa Yesu Je ambaye anapita kwenye himaya yake?
Swali aliloulizwa Yesu lilikuwa:
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
Kumbuka wakati Yesu yupo duniani talaka ilikuwa inakubalika kutokana na Musa alivyoamuru hata hivyo kulikuwa na gumzo na utata wa sababu ipi hasa mume anaweza kutoa talaka kwa mke au sababu ipi hasa inaweza kupelekea mume kutoa talaka kwa mke wake na kumbuka pia wayahudi walikuwa hawaruhusu mwanamke kutoa talaka bali mwanaume tu.

Ndipo kukawa na makundi matatu yanayopingana

KUNDI LA KWANZA – SHAMMAI
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ilikuwa ni uzinzi (adultery)
KUNDI LA PILI – HILLEL
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ni pale mke akipika chakula kisichoiiva au kibaya au ovyo.
KUNDI LA TATU – RABBI
Wao walikubalkiana kwamba hata mume akikutana na mwanamke mzuri zaidi ya Yule anaye nyumbani basi anaweza kutoa talaka

Sasa swali kwa Yesu lilikuwa wewe upo upande gani?
SHAMMAI, HILLEL AU RABBI?

Yesu alifahamu fika mioyo ya mafarisayo inawaza kitu gani na akawajibu kwa swali (counter attack) kwa kuwauliza tangu mwanzo Mungu alifanya kitu gani kwa ajili ya mke na mume.

Mafarisayo wakajikuta swali lao limekosewa na kwamba wamekosa point kwani wao walitaka ajibu Kumbukumbu la Torati 24:1-4) na Yeye akajibu Mwanzo 2:24.

Ikabidi wamrukie kwa swali kuhusu Musa kuruhusu talaka ndipo wakajibiwa kwamba Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kukataa kwao design ya ndoa tangu mwanzo na ndipo Yesu akazusha mambo 4 muhimu kabisa

JAMBO LA KWANZA
Hapo mwanzo Mungu aliumuumba mwanaume mmoja kwa ajili ya mwanamke mmoja, kama angetaka Adamu awe na wanawake wengi basi angewaumba akina Sandra, Joan, Jane, Linda wakutosha na si Eva peke yake.
(mwanzo 1:27, 5:2, Marko 10:16)

JAMBO LA PILI
Yesu anatia mkazo kwamba ndoa ndicho kifungo (strongest bond) duniani hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa ni muhimu sana anayehusika kufahamu kwamba anaingia kwenye kitu ambacho huwezi kutoka labda kifo kitokee kati ya wawili.
(Mwanzo 2:24, Marko 10:7)

JAMBO LA TATU
Katika ndoa wawili huwa mtu mmoja, mwili mmoja (one flesh)
(Mwanzo 2:24, Marko 10:8)

JAMBO LA NNE
Yesu alithibitisha kwamba Mungu ndiye huwaunganisha wawili wanaooana na kwamba kile Mungu amekitenganisha binadamu asikitenganishe.

Hivyo swali la mafarisayo
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
Jibu la Yesu ni HAPANA KUBWA
Na kwamba Yesu hakuwa kwenye kundi lolote iwe SHAMMAI AU HILLEL AU RABBI.

Yesu alielezea kudumu (permanency) na kutovunjika (inviolability) ya ndoa hadi wanafunzi wakaendelea kumuuliza jioni yake huku wakipendeleza kwamba kama masuala ya ndoa ni hivyo basi ni busara sana mwanaume asioe kabisa.

Wednesday, December 16, 2009

Kwa nini Yeye tu?

Inawezekana unahusika na matatizo yaliyopo au matatizo yaliyopita katika ndoa yako.
Ni ngumu sana kukubali kwamba unahusika hata hivyo kumbuka kwamba ndoa ni mkusanyika wa watu wawili, mume na mke ambao huja na issues tofauti kwenye mahusiano. Kabla hujaanza kumlalamikia (complain) kwa mke wako au mume wako kwamba hafanyi vile unataka kwanza jicheki mwenyewe kwanza.
Lazima ukubali kwamba hata wewe ni perfect asilimia mia kwa mia, ndiyo maana haiwezekani mke wako au mume wako awe ndiye anayekosea kila siku, mara zote na kila mahali.
Jaribu kujiuliza maswali yafuatayo:

Je, ni majaraha yoyote kutokana na maisha yangu ya huko nyuma iwe kwa wazazi au mahusiano ya kwanza au vyovyote vile?

Je, kila ninalofanya nafanya kwa hofu na mashaka na wasiwasi kutokana na hisia zangu?

Je, ninamlaumu mke wangu au mume wangu kwa vitu vile ambavyo nimefanya mwenyewe?

Je, ninajidanganya mwenyewe kwa kwenda kinyume na ukweli kutoka watu wengine wanavyosema kuhusu wanawake au wanaume walivyo?

Je, ninakubali kwamba naweza kubadilika kwanza mimi mwenyewe?

Je, nina mahusiano mazuri na Mungu au nimerudi nyuma na kumkimbia Mungu? Kumbuka unaweza kumkimbia Mungu ingawa huwezi kujificha!

Badala ya kulalamika kila wakati kuhusu mke wako au mume wako karibu kuangalia je wewe unachangia kiasi gani kwa tatizo lililopo.
Anza kwa kumuuliza Mungu akuoneshe vitu vile unakosea ambavyo vinahitaji mabadiliko.

Sunday, December 13, 2009

Mara ya Kwanza!

Usipokuwa makini unaweza kuligongesha siku ya kwanza tu!Sex mara ya kwanza ni uzoefu wa aina yake na hakuna kitu hufurahisha kama mnakutana wote ni bikira.
Hapa nazungumzia wale ambao amefunga ndoa tayari sizungumzii wale wanaoamua kufanya uasherati kwani ndoa ni baraka na kuwa na mume wau mke wa ujana wako ni baraka.
Je, ni mambo gani mwanaume au mwanamke ambaye ameolewa na yupo kwenye siku yake ya kwanza ya kuwa na tendo la ndoa anatakiwa kuzingatia?

MWANAUME
FAHAMU NDOTO ZAKE
Kila mwanamke ana ndoto siku moja kuwa na mume anayempenda na kumfanya kutimiza ndoto zake za kuwa mke na kuhudumiwa kama mke idara zote.
Ni jambo la msingi kwa mwanaume mpya kuwa na ufahamu wa mwanamke aliyemuoa je ni wa kisasa (contemporary) au si wa kisasa (traditional) na kwamba je response yake kwenye suala la mahaba itakuwaje.
Unavyoweza kumtimizia ndoto zake (kimahaba) ndivyo unazidi kuwa karibu na kufungua hisia zake

JE, NI BIKIRA
Suala la kuwa bikira au kutokuwa bikira halina umuhimu wowote na si tatizo lako. Pia haina haja wewe kuwa na msisitizo wa kutaka kujua kwa nini si bikira hapo si mahali pake kujadili sababu hata hivyo kama ni bikira ni vizuri pia kujua kwani kutakuwa na maumivu kidogo na ikiwezekana hata yeye mwanamke kutoa damu kidogo ingawa si kila mwanamke bikira hutoa damu.

MPE UPENDO KABLA YA KUMTAMANI
Mwanaume na mwanamke ni tofauti sana linapokuja suala la tendo la ndoa kwani mwanaume hutoa upendo ili kupewa sex na mwanamke hutoa sex ili kupewa upendo hii ina maana kwamba kwa mwanamke upendo kwanza na kwa mwanaume sex kwanza, bila kuwa makini kufahamu hii siri mnaweza kuchanganya mambo.
Mke atajiweka tayari (open) pale tu wewe mwanaume utakapoonesha upendo, caring, affections nk.
Kama akili yako na mawazo yako yapo kwenye matiti yake tu na pale chini basi hutafika popote kwani unahitaji kumpa upendo kabla ya kumtamani.

USIWE NA HARAKA:
Mwanamke huchukua muda mwingi au mrefu kuwa tayari kwa sex na akishafika anachukua muda mrefu kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Hivyo usiwe na haraka kama afande.
Take it slow
Au hakikisha ameonesha dalili zote kwamba yupo tayari.

MUULIZE NAMNA GANI NA WAPI
Mara nyingi kwenye shughuli za mahaba wanaume wote ni ma-genius, ndio wanaoshika usukani.
Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba kila mwanamke ni tofauti na hata mwanamke huyo mmoja anakuwa tofauti kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja.
Kuna siku ukishika matiti husisimka na kuna siku ukishika matiti atajisikia kuumia hivyo using’ang’anie au kuanza kubabaika.
Ni vizuri kumuuliza kitu gani anapenda na ufanye namna gani anaweza kukueleza kwa maneno au kwa ishara.

AKISEMA HAPANA HAINA SHIDA
Kwa kuwa ni mara ya kwanza anaweza akasema hapana, hivyo usiumize kichwa, inawezekana anaona aibu au yupo MP, kumbuka yeye kwanza na si wewe.
Ni rahisi sana kumvua nguo mwanaume yeyote kwa ajili ya sex hata kama hamjuani au hata kama anatoka sayari nyingine ila si mwanamke.

USIJIBU JEURI
Unaweza kuulizwa swali ambalo linakufanya ushangae hata hivyo uwe na subiri na usijibu kijeuri kwani unaweza kumpiga password kwenye feelings zake na ikawa shughuli nzito na mwili mzima ukaji lock ushindwe kufanya chochote.

UZAZI WA MPANGO NI JUKUMU LAKO MWANAUME
Kutofahamu njia za kujikinga na mwanamke kupata mimba kama hamuhitaji kuzaa watoto 35 ni kuonesha mwanaume yupo caring na pia upo selfish.
Siamini kama mnaweza kufika hapa kabla ya kujadili masuala ya uzazi, watoto, mimba na lini muwe na watoto.

MKUMBATIE, BUSU NA AWE KARIBU
Kwa mwanamke tendo la ndoa si sex peke yake bali ni pamoja na hugs, kissing, cuddling na kupeana joto kwa foreplay ya kufa mtu.
Onesha jinsi unavyomuhitaji kwani kuna msema kwamba
The way man make love demonstrates his character
kama unamjali mke wako mpya basi kitandani ni mahali ambapo unaweza kuonesha mara 1,000 kwamba unamjali na kinyume na hapo wewe ni
Selfish
Pleasure seeking,
Narrow focused,
Hivyo kiss, touch and feel.

MWANAMKE:

MTAZAMO:
Mwonekano wa nje (appearance) mara nyingi huwezesha wanaume kujipiga switch ya sex haraka iwezekanavyo, pia chemistry ya mwili nni jambo la msingi sana ni kama asset kwa ajili nya sex hata hivyo kwa kuwa na tendo la ndoa zuri siku ya kwanza jambo la msingi kwa mwanamke ni mtazamo wako kuhusu sex.
Ni muhimu sana kujiamini kwamba unaweza na pia mume wako atakufurahia na kwamba anakuhitaji na upo tayari kusaidiana kuhakikisha wote mnakuwa na wakati mzuri pamoja na ni jukumu lenu wote na si kulala kama gogo lisilo na feelings ukiamini mambo yataenda sawa.

USAFI
Ni vizuri sana kuzingatia suala la usafi kwani ni jambo linalopendeza kunukia vizuri katika harufu ya asili ya mwili wako.
Kwani ukiwa unavutia na mwenye kunukia vizuri basi mwanaume atakuwa crazy tu na atafanya kila analoweza kuhakikisha anakupa kile unastahili.

MAANDALIZI
Jambo la msingi ni kwa wewe mwanamke kuwa wazi kuonge na kuongea na kuongea na kuongea, yaani jiweke huru kuwa wazi kuongea kila kitu.
Kumbuka kubusiana huja baada ya kuongea kwani maneno matamu huleta hamu ya kuwa karibu zaidi kimwili.

KAMA UPO MP
Wanaume wengi huwa hawajali kama mwanamke yupo MP au la hata hivyo suala hili hufanya mwanamke mwenyewe asijisikie vizuri ( embarrassed).
Ni vizuri sana kuwa na discussion na wote mfanye kile mmekubaliana kama hapana iwe hapana kwa wote na kama ndiyo iwe ndiyo kwa wote na si vinginevyo.

USIMUHUKUMU
Wanawake wengi wanaamini mwanaume lazima awe kiongozi linapokuja suala la sex hata hviyo wapo wanaume ambao huhitaji ujasiri wa mwanamke ili kila kitu kiende sawa.
Hivyo ukiona mume wako haoneshi dalili ya kwamba anaweza kuanzisha chochote ni vizuri ukachukua jukumu na katika kuchukua jukumu isifanye kwa dhihaka hadi kuumiza utu wake.
Anyway huyo ni mume wako, mwili ni mali yako na tendo la ndoa ni haki yako na mali yenu na kila kitu unafanya ni Baraka.

KILELENI
Kufika kileleni au kutokufika yote hutegemea wewe na mwenzi wako.
Ufike kileleni usifike jambo la msingi ni wewe ku-enjoy siku yako ya kwanza kuwa na mume wako na zaidi bado ni grade one so bado safari ni ndefu hadi kuwa na PhD ya mahaba kama mke na mume na ndipo utafurahia kufika kilele.

KIASI GANI
Ukweli hakuna kanuni ni kiasi gani inatosha kwani hakuna formula ya how much is too much or too little.

MWAMBIA “NAKUPENDA”
Wakati mwingine mzuri wa kumwambie mume wako nakupenda ni wakati wa sex na hapo itasaidia kuweka memories kwenye ubongo wake na hatimaye unaweza kuwa na better sex and fulfilling.
Kwa maelezo zaidi soma hapa

Saturday, December 12, 2009

Mengi yanarekebika!

Huhitaji nyundo kubwa kiasi hiki!Mahusiano ni kazi kwani zaidi ya kupendana wakati mwingine migogoro hujitokeza, msongo wa mawazo huja, furaha huota mabawa.
Jambo kubwa zaidi ni kwamba watu hutofautiana jinsi ya kutatua matatizo yanapotokea, desturi hutofautiana hata matarajio hutofautiana hata hivyo ukweli ni kwamba wengi bado tunahangaika kujua na kufahamu ni namna gani tunaweza kuishi vizuri na wengine hasa wale tunaowapenda kwani wakati mwingine yale tulitarajia imekuwa tofauti.
Unapokuwa umempata Yule unayempenda, Yule ambaye umeamua maisha yako yote duniani utaishi naye iwe katika shida au raha, iwe katika umaskini au utajiri au katika hali yoyote kazi kubwa ni kujenga mahusiano endelevu mwaka hadi mwaka.
Wengi kujenga huu uhusiano ni kukutana na milima na mabonde kwani inawezewekana upendo wa kweli kuzaliwa au kinyume chake .

Wanandoa wengu huachana kwa matatizo ambayo yanaweza kurekebishwa (fixable problems). Matatizo ambayo yanaweza kurekebika ni matatizo ambayo huhusisha watu wawili (mke na mume) ambao walianza kwa kupendana na upendo kuanza kuchuja na wao kutofanya chochote ili kurejesha upya penzi lao kwenye mstari kama kawaida.
Kila jambo huwa na msingi wake na msingi ukitikiswa na kufanya nyufa ambazo huendelea kuongezeka ni kweli jingo la mahusiano haliwezi kufika popote.

Wengi wanaoachana hukiri kwamba “Sikutegemea kama ingetokea kwangu” ni kweli hakuna ambaye huingia kwenye mahusiano akiwa amejiandaa au akijua kwamba ipo siku wataachana kama wapo basi ni wachache sana na lazima akili zao zina matatizo.
Hata hivyo mambo ya ndoa au mahusiano yana mambo mengi sana ambayo ni udanganyifu na watu wengi wanaamini udanganyifu badala ya ukweli na matokeo yake wameangamia.
Je ni udanganyifu gani ambao wengi wanaamini ni ukweli?
Tutaendelea

Wednesday, December 9, 2009

Love is a flower which turns into fruit at marriage.
~Finnish Proverb

Tuesday, December 8, 2009

Kujenga Uhusiano na Mtoto

Nikirudi nyumbani namkuta keshajiweka sawa kwenda kiwanjani!Mahusiano yako na mtoto wako atakapokuwa mtu mzima huelezea ubora wa mahusiano uliyokuwa nayo wakati yeye angali mtoto mdogo.

Aina mbalimbali za wazazi ambao watoto huwa nao.

Kundi A
Wakali, wasumbufu, wasio na utaratibu, wasio samehe, wakorofu, wanaoweka donge moyoni, wanaopenda sifa, wasioaminika, wasio na subira, wanaowaka wakikasirika, wanakasirika haraka na wanaoshindwa kuwa na kiasi nk.

Kundi B
Wakarimu, wanaojali, wapole, wanaosamehe, wanaoheshimika, ukifanya makosa wanasamehe na kusahau, wanyenyekevu, wakweli, wenye subira, wanahasira lakini wanazihimili, wana kiasi, wacheshi, wanaofurahisha nk.
Je, ungekuwa mtoto ungechagua mzazi wa kundi gani?
Ni yupi kama una matatizo shule ungemwambia?
Ni yupo anaporudi nyumbani ungemkimbilia na kujisikia upo mahali salama?
Ni yupi ukifanya makosa unaweza kukiri wazi kabisa kwamba umefanya makosa?

Kumbuka mtoto hawezi kubaki mtoto miaka yote hivyo wakati akiwa mtoto hakikisha unampa kile anastahili kwa wakati wake.
Kwa mfano usipocheza na mtoto leo usidhani miaka 10 ijayo unaweza cheza mchezo uleule ulitaka kucheza naye miaka 10 iliyopita.

Je, ili kujenga uhusiano na mtoto wako ni mambo gani ya msingi kufanya?

CHEZA PAMOJA NYUMBANI:
Cheza mchezo wowote kama vile kadi, colouring, puzzle nk.
Unatakiwa kubuni mchezo ambao unaweza kucheza na mtoto/watoto wako.

CHEZA NJE YA NYUMBANI:
Unaweza kutembea au kukimbia kwa ajili ya maendelea ya afya ya mtoto. Unaweza kwenda naye kwenye Pak, kutafuta maua au wadudu au kurusha mawe kwenye mto nk.
Kumbuka issue si kwenda naye tu bali na wewe uhusike kucheza nay eye.

PENDA VITU AMBAVYO MTOTO WAKO ANAVIPENDA (INTEREST)
Ni muhimu sana uwe una admire vile vitu mtoto wako anapenda au kuonesha interest na wewe husika na endelea kumsaidia yeye kuwa mbunifu zaidi kwa vitu anavipenda kufanya.
Kama anapenda kutengeneza magari msaidie na kumtia moyo kwani anaweza kuwa designer wa magari baaadae, au kama anapenda kufuga wadudu anaweza kuwa ni conservation officer (wildlife) baadae.

MSAIDIE HOMEWORK NA PROJECT ZA SHULE:
Utakuwa unamtia moyo sana mwanao kwa kuwa kile muhimu kwake na kwako ni muhimu.
Unapofanya hivyo unamsaidia mtoto kuwa organized, pia unaweza kumwingizia (instill) ethics zako kuhusu maisha ya shule kama vile juhudi na kutokata tama.

TAFUTA MUDA WA KUJIBU MASWALI YAKE:
Ni muhimu sana kujibu maswali ya mtoto aina zote hata kama atakuuliza swali ambalo ni la mambo ya kikubwa kwani ni mtoto anataka jibu na si kumkemea, kwani hata akiwa na swali mahali popote atajua mzazi wangu ni mtu muhimu nitamuuliza hivyo utamlinda pia.

MTOTO AKIKASIRIKA RESPOND VIZURI:
Hakuna kitu muhimu kama kuwa makini na mtoto akikasirika na jinsi wewe unavyo respond kwani ukiwa na hekima na busara utakuwa unamtengeneza vizuri mtoto wako jinsi yak u-behave akiwa amekasirika hata katika maisha yake baadae akiwa mkubwa kwenye ndoa yake.

MWAMBIE NAKUPENDA:
Hivi ni lini umemwambia mtoto wako nakupenda? Hakuna kitu kizuri kama mtoto kuambiwa anapendwa na wazazi wake na pia ni vizuri mtoto afahamu baba na mama wanapendana.

SHUGHULIKIA TABIA MBAYA MAPEMA
Mtoto wako akionesha tabia mbaya mshughulikie kwa upendo.
Pia kusema HAPANA maana yake bado unampenda, si busara kumwambia ndiyo mtoto hata kitu ambacho unaona hakina faida kwake eti atalia.

UKIKOSEA OMBA MSAMAHA
Wakati mwingine wazazi hukasirika na kuwaadhibu watoto wakati mwingine wakiwa hawana makosa.
Hivyo kama ni kweli umekosea, omba msamaha.

UWE NAO KWENYE SHUGHULI ZAKO:
Ni muhimu sana kuhakikisha unakuwa na mtoto kwenye shughuli zako kama ni ofisini siku zingine nenda naye ili na yeye akakae kwenye kitu chako na kujiona ni boss fulani.
Pia inampa picha nini mzazi anafanya na itampa picha ya maisha na future yake.
Kama ni dereva nenda naye kwenye gari siku moja.
Kama ni forester nenda naye kwenye forest nay eye ajifunze kupanda miti.
Kupika je? Kufua nguo je? Kulima Je?

WAFUNDISHE KUHUSU MUNGU:
Ni muhimu sana watoto wanavyoongezeka na imani yao ya kumjua Mungu iongezeke, imani ya wazazi ina impact kubwa sana kwa mtoto kuliko mahali popote.
Linapokuja suala ma Mungu mtotot huambulia 80% kwa wazazi, asilimia 15 Sunday school (kanisa) na 5% mtaani.
Hivyo mzazi una impact kubwa sana kuhusu Mungu kwa mtoto wako.

TUMIA MUDA PAMOJA KAMA FAMILIA
Kila mtoto ana picha ya wazazi (baba na mama) na kwamba anajisikia raha pale anapokuwa pamoja na wazazi wote.
Pia kama mzazi jifunze kumfurahia mtoto, jitahidi mtoto ajisikia raha kuwa na wewe na si kukukimbia.

Ubarikiwe

Monday, December 7, 2009

Nimechoka, Najisikia Uchungu sana!

Hadi kupika napika!Hello Jane,

Sijajua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu, tulizoea kuwa na tendo la ndoa mara 3 kwa wiki na sasa ni mara moja kwa miezi minne na hata tunapokuwa kwenye tendo la ndoa unajilaza kama gogo tu na unanipa sura ambayo inanipa nitafsiri kwamba unaniambia “Hujamaliza bado, ondoka mwilini mwangu unachofanya sijisikii chochote”
Je, ni kitu gani kimetokea kwani ulikuwa sexy, exciting na ulikuwa ni mwanamke niliyekuoa unayependa kufanya mapenzi na mimi.

Ndoa yetu ina miaka 10 sasa na ni miaka 3 tu ulifanya nijisikie nimeoa mke ambaye anatimiza ndoto zangu hata hivyo hii miaka 7 ambayo umekuwa huna hamu ya tendo la ndoa imesababisha nijikie nimechoka na nipo hatua ya mwisho hasa baada ya kuweka juhudi kubwa kukurejesha kwenye mstari na nimeendelea kuambulia kuendelea kukataliwa tendo la ndoa.

Nafahamu fika mke wangu unapenda vitu gani, ninafahamu unapenda affections, unajisikia raha kupendwa, unajisikia raha kupelekwa outing angalau mara mbili kwa wiki, unajisikia raha kupewa zawadi, unajisikia raha mimi kuwa na watoto na wewe ukapata muda wa ziada (free time), unapenda kupewa extra money kwa ajili ya shopping, pia unajisikia raha nikupe pesa kwa ajili ya kwenda vacation na dada yako, unajisikia raha ninapokusaidia kazi za nyumbani ili usiende kulala umechoka na nimekuwa najinyima, najipinda mgongo wangu kuhakikisha haya yote unayapata hii miaka 7 ambayo hata hivyo wewe umekuwa unaninyima tendo la ndoa na nikikuomba unaniamba “Nimepotoka na mpenda sex”

Nimekuwa najiuliza kwa nini nijinyime na kupinda mgongo wangu kujitoa kwa mambo yote haya kama wewe unashindwa kunitimizia hitaji moja tu la sex angalau mara mbili kwa wiki?
Kwa kweli nimechoka na nimeanza kujisikia hasira na nimepoteza interest kwani najisikia wewe huoni umuhimu wa kunitimizia mahitaji yangu.

Ninafahamu fika kwamba hamu ya kufanya mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke ni tofauti na nimejitahidi mara zote kuhakikisha wewe unapata kile unahitaji ili ujisikie vizuri na uwe tayari kwa sex hata hivyo juhudi zangu zimekuwa hazina maana.

Sikukuoa ili unipe sex tu, na pia sikukuoa ili usinipe sex, sex ni moja ya sababu maelfu zilizonifanya nikuoe. Nilikuoa ili kuondoa upweke, ili uwe life partner, nishirikiane na wewe katika ndoto na malengo ya maisha pamoja, kulea watoto ambao Mungu ametupa na kupeana sex na mwanamke ambaye ninampenda na ambaye nimemchagua kufanya mambo haya yote.

Kumbuka naweza kupata vitu vyote kwa mtu yeyote ambaye naweza kuamua kuishi naye isipokuwa sex tu kwani ni wewe tu unaweza kunipa na ndiyo maana niliacha wazazi wangu ambao walinipa kila kitu nahitaji isipokuwa sex kwani hata kama ningetaka mtoto ningeweza kufanya adoption.
Sex inanifanya nijisikia nipo connected na wewe, sex inanifanya nijione na kukuona wewe ni mwanamke special.

Swali linakuja kwa nini mwanaume aweke commitment ya maisha kwa mwanamke ambaye hawezi kumpa sex?

Kama mke wangu ungeniambia tangu mapema kwamba hamu yako ya kufanya mapenzi itakuwa ni miaka 3 tu nina uhakika nisingepoteza muda wangu kukubaliana kuoana na wewe, nisingekubali kuingia katika shida kubwa namna hii ya kunyimwa sex na mke wako mwenyewe na unajua fika siwezi kupata hii huduma mahali popote isipokuwa kwako na kama nilivyokwambia siwezi kukuacha wala kushawishika kutembea na mwanamke mwingine kwani ninakupenda.

Kinachoniuma zaidi ni kitendo chako cha kuninyima na huku unafurahia na nikitaka tuongee unanijia juu eti mimi ni mpenda sex nisiyejali na ninayejua ndoa ni sex tu.
Nafahamu nimefanya the biggest mistake in my entire life, nimekwama kwa mtu ambaye nampenda na hawezi kutimiza hitaji langu, najiona nimenasa kwenye chambo ya kizamani na Inaumiza sana.
Najuta, najuta najuta mno!

Nimeamini inachukua efforts kidogo sana kumfanya mwanaume afurahi na ni ngumu sana kumfanya mwanamke afurahi.
Nipe sex mara 2 kwa wiki nitakuwa mwanaume mwenye furaha na nitakufanya uwe na furaha ziku zote.
Nini kigumu hapo mke wangu?

Ukinipa sex najisikia nipo connected na wewe kimwili, kinafsi na kiroho!

Najisikia uchungu sana!

James!

Sunday, December 6, 2009

Wanampinga!

Kuna mwanaume ambaye kanisa limempendekeza awe moja ya viongizi wa kanisa, mke wake pamoja na wale waliompendekeza kuwa kiongozi wamekasirika sana kwani wengi (washirika wa kanisa) wanapingana na huyo mwanaume kuwa kiongozi wa kanisa kwa kuwa huyu mwanaume alishatoa talaka kwa mke wake wa kwanza na kanisa limeweka sheria kwamba kila anayekuwa kiongozi wa kanisa anatakiwa asiwe ni Yule amewahi kutoa talaka au kupewa talaka (divorced).
Kwa ufahamu wangu naamini Mungu anachukia talaka lakini anawapenda waliotalikiana na amewasaheme kwani divorce ni dhambi inayosameheka.
Je, maandiko yanasemaje kuhusu hili?

Kwanza swali lako siyo jipya sana hasa kwa makanisa ya magharibu (ulaya na Amerika) ambako hata viongozi wa kanisa au ministries walishakumbana na talaka iwe kwa washirika wao au wao wenyewe.
Mojawapo ni John Hagee, Juanita Bynum, Paula White, Joyce Meyer nk.
Na hili suala la divorce limewagawa watu katika makundi mawili wale wanaokubali (liberal) na wale wanaokataa (conservative).
Pia suala la divorce na remarriage lilikuwa gumu sana wakati wa Musa na likawa gumu sana kwa mafarisayo hadi wakati wa yesu ilibidi wamtege (test) kwa swali la talaka (soma Mathayo 19:1-10) pia limekuwa suala gumu sana kwa kanisa leo na bado ni gumu hata hivyo Biblia ipo wazi kuelezea kila ugumu uliopo.

Kwa kifupi ili kujibu swali lako hapa kuna mambo mawili muhimu
Kwanza ni kweli Mungu anasamehe dhambi zote katika Kristo.
Na upo sahihi kwamba Mungu anasamehe dhambi zote.

Kuna dhambi moja tu ambayo huwezi kusamehewa nayo ni kumkufuru Roho mtakatifu
Biblia inaelezea kwamba ni kweli binadamu huweza kusamehewa dhambi za uzinzi
(1 Wakoritho 6:9-11)

Jambo la pili ni kwamba kusamehewa dhambi hakuwezi kuondoa matokeo (consequences) ya dhambi umefanya.
Kusamehewa maana yake Mungu hakuhesabii dhambi tena na anayesamehewa hahukumiwi tena hata hivyo matokeo ya zile dhambi katika jamii bado zitakukuta na utapambana nazo mbele ya safari.
Kama kabla ya kuokoka au kuamini ulifumaniwa na wakakukata mkono kwenye hekaheka za kufumaniwa, siku unatubu dhambi ya uzinzi na kuokoka haina maana mkono wako uliokatwa utarudi au kuota, kilema cha kukatwa mkono utapambana nacho kama matokeo ya dhambi ya uzinzi (kufumaniwa) katika maisha yako hata kama umeokoka.

Kama kabla ya kuokoka ulikuwa na wake wengi, ukiokoka ndiyo unasamehewa lakini Biblia ipo wazi kwamba huwezi kuwa kiongozi wa kanisa na si kwa sababu hujasamehewa na Mungu bali kwa sababu kanisa halitakiwa kuongozwa na watu wasio na sifa njema, kanisa linahitaji kuongozwa na watu wenye ushuhuda mwema mbele ya watu na wasio na lawama
(1 Timotheo 3:2, Tito 1:6)

Unapotoa talaka au kupewa talaka maana yake miaka ijayo mbele huwezi kupewa uongozi katika kanisa kwa kuwa una sifa mbaya ambayo ni lawama kwa wengine wanaoliangalia kanisa la Mungu kuwa mfano kwao.
Hivyo wanaompinga wapo sahihi kama kweli sheria ya kanisa imesema ukiwa divorced huweza kushika uongozi wa kanisa.

Kumbuka Unapoachana na mke au mume na kupewa talaka ni label ya maisha ambayo utatembea nayo na inasema wewe ni failure.

Thursday, December 3, 2009

Je, ni Sababu ya Msingi?

Swali:
Mimi ni mwanaume mwenye miaka 29 nilioa ndoa takatifu kanisani miaka miwili iliyopita na tumekuwa na wakati mgumu sana (migogoro) na mke wangu.
Ni miezi sita sasa hatujakutana kimwili (tendo la ndoa).
Naamini tendo la ndoa ni moja ya haki ambayo mume na mke ni muhimu haki kwani ni moja ya sababu zinazofanya tuoe.
Sioni dalili ya kupata suluhisho kwa migogoro yetu je, naweza kuachana naye (talaka) kwani naamini ninayo sababu ya msingi.

MAJIBU
Asante sana kwa swali lako ambalo naamini si wewe peke yako ambaye umejikuta unanyimwa tendo la ndoa kutoka na migogoro kati ya wanandoa.

Ukweli kujibu swali linalohusu talaka au kuachana ni sawa na kukata kitunguu ganda kwa ganda huku unaugulia kwa machozi hata hivyo nitajitahidi kujibu kama ifuatavyo.

Jambo la msingi ni kwamba sababu uliyonayo haina msingi na haiwezi kukufanya kutoa talaka kama ndoa yako ni takatifu kama unavyosema.
Sababu ya msingi ambayo inaweza kukufanya uoe mwanamke mwingine ni pale tu kifo kikitokea na sivinginevyo.

Pia kukosa tendo la ndoa haina maana ndoa haipo au ndoa inaweza kuvunjika kwani ndoa ni muungano (union) na agano (covenant) wa watu wawili mbele za Mungu waliokubaliana kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.

Msingi mkubwa wa ndoa ni kuondoa upweke (loneliness).
Mungu mwenyewe anatoa jibu kwamba
‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa”.
(Mwanzo 2:18)

Ndoa ilianzishwa kwa sababu Adam alikuwa mpweke siyo kwa sababu alikosa tendo la ndoa na hivyo Mungu akaona kwamba “Haikuwa vema”.

Hivyo companionship ndio msingi wa ndoa na ndoa ni agano la companionship kwa wawili wanaooana.
Na huu ushirika wa ndoa ni kuwa pamoja katika mawazo, malengo, mipango, jitihada na miili.
Na msingi wa ndoa ni upendo wa kila mmoja kumpenda mwenzake ili kuondoa upweke.

(Soma Malaki 2:14, Mithali 2:17)

Tendo la ndoa halifanyi ndoa bali katika ndoa kuna tendo la ndoa na kutokuwepo kwa tendo la ndoa hakuwezi kusababisha ndoa isiitwe ndoa.

Ndoa huwepo kabla ya tendo la ndoa.
Je, wakati unafungua ndoa baada ya kula kiapo mchungaji aliwaruhusu mwende kwanza honeymoon na baada ya kurudi honeymoon ndipo atangaze kwamba ninyi sasa ni mke na mume?
HAPANA!

Ninachofahamu ni kwamba baada ya kula kiapo tu, mchungaji alitangaza mbele za mashahidi (KANISA) ninyi ni mume na mke.

Naungeenda honeymoon kabla ya kwenda kanisani na kutoa kiapo (vow) mbele za Mungu na kanisa (mashahidi) wewe na mchumba wako mngeitwa waasherati maana mmefanya mapenzi (sex) kabla ya kuoana kwa desturi za kiyayudi ungetoa talaka hata hivyo wewe unalalamika kukosa tendo la ndoa ndani ya ndoa kitu ambacho talaka ni impossible.

Hivyo kukosa tendo la ndoa hakukupi sababu ya msingi ya kuachana au talaka.
Tendo la ndoa halifanyi ndoa na haliwezi kutenganisha walioana kwani tendo la ndoa ni matokeo ya wanandoa kuishi pamoja na wana wajibu wa kufanya tendo la ndoa ili kuzaa na kuongezekana na hata wasipozaa haina maana ndoa inaweza kutenganishwa.

Ukiwa honeymoon una enjoy tendo la ndoa kwa kuwa unakuwa umeoa tayari, ni tendo takatifu.
Hii ina maana hata ukizini baada ya kuoa au kuolewa haiwezi kusababisha ndoa kuwa dissolved isipokuwa kifo.
Jambo la msingi ni kwamba kwa Mungu hakuna lisilowezekana na ukimwamini Mungu ametoa ahadi kwamba hakuna tatizo katika ndoa lisilo na solution kwani kwake hakuna lisilowezekana au kwa Mungu yote yanawezekana.
Mathayo 19:26

Serikali Nayo!

Serikali zingine hazina dini! SERIKALI NA TALAKA
Mtazamo wa serikali kuhusiana na talaka umewekwa kutokana na kile raia wake wanataka (desires).
Kama raia wake watataka kuwa na sheria zinawapa au kuruhusu talaka kirahisi, serikali huwapa.
Tatizo kubwa ni kwamba binadamu mahali popote walipo kawaida huwa wanapenda uhuru wa kufanya wanavyotaka na hawataki kuishi katika standards za kibiblia au katika uadilifu ambao Mungu ameuweka
.

Mungu ameweka institution mbili duniani ambazo ni serikali na ndoa na hizi zinawafunga wanaoamini (waliokoka) na wasioamini).
Wote wanahitaji kutii serikali kama vile kulipa kodi haijalishi umeokoka au la kwani bila kulipa kodi kuna adhabu yake tena ya uhakika.
Hata kwenye ndoa uwe umeokoka au hujaokoka lazima utii standards za ndoa na kinyume chake ni penalty.

Serikali nyingi (English speaking) zinaweza kutoa talaka hata kwa kuwepo kwa tofauti katika ya mke na mume (differences and disagreements) .
Hata kama serikali inatoa talaka hii haina maana kwamba talaka zinaruhusiwa. Serikali haina common sense linapokuja suala la uadilifu (God’s morality standards). Hata kama serikali inauza pombe (liquor) hii haina maana pombe ni kitu sahihi.

Serikali haiwezi kutatua tatizo lolote la uadilifu wa binadamu kufuata standards ambazo Mungu ameweka.
Suala la talaka haliwezi kutatuliwa na binadamu yeyote aliye na hekima wala mahakama.

Mke na mume wanapoenda mahakamani ili kupeana mahakama jaji huwaeleza ukweli kwamba wao kama mahakama hawahusiki na suala la kiroho, sheria za Mungu, au sakramenti au kiapo chochote cha dini kuhusiana na kuachana kwani hilo ninyi wahusika mtatatua wenyewe na kwamba sheria za serikali au mahakama hazina uwezo wa kuamua kile mliahidiana mbele za Mungu.

Hii ina maana ninyi mnaopeana talaka mtahusika na Kipengele cha “Hadi kifo kitakapo tutenganisha” na kwamba mahakama haiwezi kutengenisha kile kilichounganishwa na Mungu.

Jaji William J. Gainer wa New York Marekani ameeleza wazi kwamba pamoja na kwamba mahakama ina uwezo wa kutoa talaka bado suala la kiroho linabaki mikono mwa wahusika (Plaintiff na Defendant) kwani mahakama haiingilii sheria za Mungu.
Maana yake unaenda mahakamani na kupeana talaka hata hivyo conditions zote za kuwa mke na mume bado zinabaki palepale untouched.
Bado ninyi ni mke na mume na kila anayeoa au kuolewa anazini.

Wednesday, December 2, 2009

Maafa ya talaka!

Talaka ikitolewa huathiri wote hata wale tusiowaona!Mahusiano ni kazi (hardwork), migogoro hujitokeza, msongo wa mawazo haukosekani, matarajio huyeyuka hata hivyo kila mmoja ana ufahamu na uwezo tofauti wa kukabiliana na hizi challenges.
Jambo moja la msingi ni kwamba matatizo yote ya ndoa huweza kuwa fixed na talaka huweza kuzuilika kama wawili wakiamua.

Hata hivyo ni muhimu kujua maafa ya uamuzi wa kupeana talaka ili kama unawaza talaka ni muhimu kufahamu ili uweze kubadilisha mtazamo wako ambao unaudanganyifu uliokithiri.
Moja:
TALAKA HUVUNJA NYUMBA
Familia iliyoanzishwa na wawili walioana huharibiwa muda wote ambao wahusika wataishi chini ya jua.
Kunakuwa na kovu (scar) ambalo huambatana na wahusika na kamwe haliwezi kufutika.
Talaka huvunja nyumba familia ambayo ingekuwa Baraka kwa mama, baba na watoto/mtoto.
Mbili:
TALAKA HUSABABISHA MIOYO KUTOA DAMU (ngeu)
Talaka haiathiri wahusika tu (yaani mke na mume) bali huathiri familia, ndugu, jamii na taifa kwa ujumla.
Talaka husababisha marafiki na ndugu kuomboleza kwa machozi ya damu bila kusema lolote.
Tatu:
TALAKA HUATHIRI WATOTO
Watoto huchanganyikiwa na kitendo cha wazazi kuachana na hakuna mtu duniani anayeweza kufahamu ugumu na uchungu ambao huwakuta watoto katika mioyo na akili zao.
Kila mtoto anaufahamu wa kwamba anahitaji kupata upendo wa baba na mama pamoja na anaona hata kwa watoto wenzake.
Mtoto huchanganyikiwa mno pale wazazi wakitalikiana.
Nne:
TALAKA HUHARIBU USHUHUDA

Kila anayepewa talaka au kutoa talaka hujiwekea alama (mark/label) katika maisha yake na watu huisoma hiyo alama kwamba “Huyu ni failure” na huweza kusababisha kukosa acceptance kwa watu wengine bila sababu ya msingi, kisa talaka!
Tano:
TALAKA NI KUKANA KIAPO
Wakati wa kufunga ndoa wahusika walitoa ahadi zao (vows) kukubali na kuahidi kwamba wataishi pamoja katika afya na uzima, raha na shida hadi kifo kitakapowatenganisha.
Walitoa ahadi mbele za Mungu na mashahidi.
Je, walikuwa hawamaanishi?
Je, kichwani akili zilihama?
Je, walikuwa wanatania?
Je, ilikuwa kweli au uwongo?
Talaka ni kukana kiapo na pia kuikana Biblia.

Ni kanuni tu!

Wangefuata kanuni, yasingewakuta haya! Talaka ni issue ambayo imejikita katika suala la maadili na uadilifu.
Maisha ya binadamu yametawaliwa na kanuni (standards/discipline) na bila kufuata hizi kanuni basi kila mmoja hufanya anavyotaka na matokeo yake ni maafa.
Kuna standards za ujenzi,
biashara,
uhasibu,
elimu nk na zikiwe implemented vizuri kila kitu huenda vizuri.
Nyumba iliyojengwa kwa kufata standards za ujenzi haiwezi kuporomoka kwani imejengwa kwa kuzingatia standards zinazotakiwa.

Katika serikali ya Mungu kuna standards zilizowekwa ambazo binadamu anatakiwa kuzifuata, hata hivyo wengi hawataki kuishi katika standards za kimungu.
Tumekuwa na man-made standards ambazo tunadhani ni msaada zaidi kitu ambacho si kweli.
Standards ambazo zimewekwa na Mungu ni Baraka kwa jamii ya binadamu na hazibadiliki na hazijawahi kubadilika na Mungu hajatoa tangazo lolote kwamba sasa standards za kuishi duniani ambazo aliziweka kama msingi zimebadilika.

Katika ndoa Mungu ameweka standards wazi na halisi ambazo binadamu anatakiwa kuzifuata ili aishi maisha ya Baraka leo na hata milele.

MFANO WA KANUNI ZA MUNGU KWA NDOA
Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikjitenganishe.
(Mathayo 19:6)
Hilo ni wazo la Mungu tangu mwanzo.

Ndoa ni zaidi ya mkataba, ndoa ni agano (covenant) ambalo Mungu aliweka hata kabla ya sheria ambazo tunatumia wakati wa kupeana talaka zilikuwa hazipo.
Ndoa ni union ya watu wawili kuwa mmoja, ni muujiza ambao ni Mungu tu anaweza yaani mtu mmoja kuwa wawili (Adam katika usingizi na Eva akaumbwa) na wawili kuwa mmoja (Adam na Eva kuwa mwili mmoja).
Je, kuna binadamu duniani anaweza kufanya hivyo?
HAKUNA KUBWA!

Hivyo ni kifo tu huweza kutenganisha na talaka haiwezi kutenganisha wawili walioana na kupeana ahadi ya kuishi pamoja hadi kifo mbele za Mungu.

Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka katika sheria ya ndoa.
Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi.
Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa, naye akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.
(Warumi 7:2-3)

Kwa nini siku hizi..........

Ameolewa jana na anataka amiliki jumba la uhakika kama fulani! KWA NINI TALAKA NYINGI SIKU ZA LEO?
Sababu zifuatazo zinachangia sana kwa kizazi cha sasa kuwa na rekodi kubwa ya wanandoa kuachana (divorce)

Vijana wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa na matarajio ambayo si sahihi (unrealistic). Wanaingia kwenye ndoa wakiamini kwamba kila kitu kitakuwa perfect.
Wanaingia kwenye ndoa bila ufahamu wa kutosha kuhusu nini kinafanya ndoa idumu.
Jamii ya leo ni zao la jamii ya “mimi kwanza”, kila mmoja huweka mkazo katika kutimiziwa mahitaji yake.
Kila mmoja anaimba
"My needs, my needs, my needs"
Na anakuwa kipofu na kiziwi wa mahitaji ya partner wake.

Wanandoa wa sasa wanataka mambo makubwa, wanataka kuwa na kila kitu kinachopendeza macho hawakumbuki kwamba wazazi wao na mababu zao walipata kwa kujituma, kuvumilia na kufanya kazi pamoja na kuwa na ndoa nzuri zilikuwa nzuri kwa sababu waliweka efforts.
Kila anachokiona kwenye Malls au store au mwingine anacho anataka na mpenzi wake au mume au mke amnunulie.
Kazi kwelikweli!
Wengi wanaoingia kwenye ndoa leo wanaingia huku wakiwa hawakuwa waaminifu (kabla ya kuoa au kuolewa) au alikuwa na wapenzi wengi.
Baada ya kuoa au kuolewa na kuanza kumzoea aliyeoana naye huanza kupepesa macho na kwa kuwa ana mguu mmoja ndani na mwingine nje matatizo huanza na hatimaye ndoa kuelekea kwenye shimo na kapata sababu!

Wanandoa wengi wanaoana bila kujua wazo la sacrifice ambayo inahitaji kuitoa ili kuwa na ndoa imara.
Wanaamini kwamba kila siku wanandoa wanatakiwa kuwa na furaha na siku kukiwa hakuna furaha basi anaamini ameoa au kuolewa na wrong person, kitu ambacho si kweli.

Wanandoa wengi wa sasa ni product za wazazi ambao nao waliachana (divorced) hivyo wanaingia kwenye ndoa wakiwa na mtazamo kwamba siku moja mambo yakiwa mabaya naanza mbele.
Tena hawa ndo hutishia kwamba mimi nitakuacha, maana wanajua uchungu wa kuachwa na wanaogopa kuchwa wao so wanawahi wao.

Wanandoa wengi wa sasa ni wavivu na hawana subira, kukiwa na tatizo dogo tu inakuwa kesi kubwa na pia hukata tamaa haraka kwa jambo dogo tu.
Watu wa sasa wanaoana mtu kupewa talaka ni kitu positive, ni ushujaa ni haki, ni uelewa wa masuala ya haki.

Miaka ya nyuma kupewa talaka ilikuwa ni laana, ni aibu, ni kuonekana failure, dhambi na mtu aliyepewa talaka alikuwa na kibandiko cha maisha kwamba hafai, leo hakuna tena ndo maana watu hawajali wala kuogopa.

Tuesday, December 1, 2009

Ndoa ni ......

Hawa nao ni Adamu na Eva! NDOA, TALAKA NA KUOLEWA TENA
UTANGULIZI
Ndoa ilianzishwa (instituted) na Mungu. Mungu aliumba mke kwa ajili ya Adamu kwa kuwa Mungu aliona “Haikuwa vema” kwa Adamu kuwa peke yake.
Mungu alimuumba mke (Eva) kuwa msaidizi (suitable helper) wa Adamu kutawala dunia, kulea familia na kumuabudu Mungu.
(Mwanzo 2:18, 42)

Ndoa ni mke mmoja na mume mmoja (monogamous).
Mungu alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu na si Eva na Jane, Ingawa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba wanawake wengi kadri anavyoweza ila alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu.
Agano la kale kulikuwa na polygamist na matokeo yake hakukuwa na amani.
(Mwanzo 2:22)

Ndoa ni mke na mume. Biblia haizungumzii kuumbwa kwa Adamu na James au Eva na Linda na kufanya ndoa bali Adamu na Eva.
(Mwanzo 2:22, 1:28)

ndoa inahusisha Mume kuondoka kwa wazazi ili kuanza familia yake kama mke na mume na pia kuna kuwa na taarifa kwa jamii (public recognition) kwamba fulani na fulani ni mke na mume hata kama formalities au tamaduni hutofautiana.

Ndoa inawafunga mke na mume hadi kifo.
Marko 10:9
1Wakorintho 7:39
Warumi 7:2-3

Ndoa inahusisha wajibu wa kila mmoja katika mahusiano kwa mke kutii (submissive) na Mume kumpenda mke wa kujitoa sadaka (sacrificial love)
Efeso 5:22-24, 25-28)


Ndoa huhusisha mume kuwa kichwa cha nyumba au mke kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa
Efeso 5:23
1Wakorintho 11:3

Ndoa ni suala zito ni uamuzi wa pili kwa uzito duniani (kwanza ni wokovu na pili ni ndoa) hivyo si kuingia tu kwa kadri unavyijisikia kwani barabara unayoingia ni dead end hakuna kutoka hadi kifo.

Dunia imejaa udanganyifu wa kila aina kuhusiana na suala la ndoa jambo la msingi ni kujua kweli na kweli itakuweka huru.

Unapoingia kwenye ndoa unahitaji kuwa makini, mbele ya safari kujitetea eti nilikuwa bado nina akili ya kitoto, au nilidhani atabadilika au sikuwa na akili timamu au sikujua kama itakuwa hivi haitakusaidia kwani ukiingia ni hadi kifo kitakapowatenganisha hivyo kama hujaoa au kuolewa please be extra carefull siyo unabeba bora liende then kesho unasema “I made a terrible mistake” naweza kuachana naye! hakuna kitu kama hicho.

Ubarikiwe!