"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, December 23, 2009

Epuka Makosa Haya!


Hutaki kuanza.
Tatizo kubwa na sugu la wanawake wengi ni kitendo cha kutoanzisha kwamba anataka sex na mume wake (initiating) na kumwachia mwanaume kama wajibu wake katika ndoa.
Je ina maana hakuna siku unakuwa umemtamani mume wako na ukaamua wewe kuanza?

Kushindwa kuanzisha kwamba unahitaji sex ni biggest mistake wanawake wengi wanfanya kwani wanaume wengi hujiona kama si sahihi (disequillibrium) katika kuimarisha mahusiano kama kila siku ni mwanaume tu ndo anachokoza.
Kimsingi hata mwanaume anajisikia vizuri pale mke wake anapolianzisha kwamba na yeye anataka.

Je, ni kueleza kwamba wanaume tunakuwa na interest kubwa wa sex na wanawake hawana au huwa hawapendi siku zote.
Naamini kuna wanawake ambao nao wanapenda sex kama wanaume.
Ni vizuri mwanamke kuonesha interest kwa kuchukua hatua kusema kila unapenda kwa mumeo na kwamba leo unamtamani na kumuhitaji siyo kila siku yeye tu miezi 12 na siku 365 na robo naamini mumeo akiona juhudi yako ya kulianzisha atafurahi na kukupa appreciation kubwa na unaweza kupata level upya ya satisfaction.
Hivyo kama wewe ni mwanamke anza leo.
Wasiwasi kwamba mwili wako upoje:
Kufikiria jinsi mwili unavyoonekana kwa mume wako na kuwa na wasiwasi kwamba anaweza kukuona labda mnene sana (fat zimejaa vipande vipande), au matiti makubwa sana au madogo sana au makeup ulizoweka usoni na mtindo wako wa nywele kichwani au sijui sehemu zingine zina rangi ipoje husababisha ushindwe ku-enjoy tendo la ndoa na mara nyingi unaweza kuharibu kila kitu hadi ushindwe kufika kileleni.
Jambo la msingi ukishakuwa na mumeo ni kuwa na total concentration kwa tendo lenyewe kwa raha zako zote.
Wanaume hufurahia mwanamke ambaye anajiamini na mwili wake na jinsi alivyo na anahusika mia kwa mia katika furaha ya tendo la ndoa na si kuwa na hofu na kujipiga kufuli kihisia.

4 comments:

Anonymous said...

bwana asifiwe kaka yangu jina langu ek naomba ushauri wako mimi ni msichana bado sijaolewa ila kuna kaka ambae ameokoka natumekuwa na ukaribu sana hatakuweza kushauliana na kusaidiana mambo mbalimbali katka maisha yeye pia hajaoa sasa imefika mahali mimi nampenda ila yeye bado hajasema kitu lakini anaonekana kama anamwelekeo ila mbaya zaidi mimi niko uk yeye yuko tz sasa nifanyeje uwende lipwela yunemunyalukolo

Lazarus Mbilinyi said...

Dada,
Asante kwa swali zuri naomb nitumie email lazarusmbilinyi@gmail.com

Ubarikiwe na Bwana

Lazarus

Anonymous said...

Bwana asifiwe kaka naamini imekuwa j.pili njema kwako ni mimi Ek nashukuru kwa majibu yako mazuri.Lakini nilikuwa naomba unijibu tu kupitia blog yako ili ipate kuwafundisha na wengine maana najua tupo wengi wenye matatizo kama hayo naipenda blog yako kwa maana nalikuwa kipofu kwa mambo haya lakini sasa naona .Naomba utukumbuke na sisi ambao bado hatujaingia kwenye ndoa.Mfano masomo kama ya uchumba nk maana mwaka uliopita ulielekeza sana kule kwa wanandoa.Ubarikiwe.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada EK,

Asante sana kwa swali lako zuri pia nashukuru kwa busara zako kuhusiana na hii issue kwa maana kwamba unapenda na wengine wajifunze kutokana na swali lako ni vizuri sana na muhimu sana na hongera sana.

Pia si mara ya kwanza kuulizwa swali la namna hii (dada una fall in love na kaka ambaye siku zinakwenda hataki kutamka wazi kwamba anakupenda kiasi cha kukuoa ili muanze maandalizi ya harusi) Ni kweli hii ni issue ngumu sana kwa akina dada hasa katika tamaduni zetu za kiafrika ambazo bado mwanaume hutakiwa kuoongoza issue nzima ya kutamka kwamba tuoane.
Pia issue huwa ngumu zaidi kwa kuwa wanaume wengi theses days (hata mabinti) huwa wanajikuta njia panda wakiwa na zaidi ya mtu mmoja kuchagua yupi tuoane na matokeo yake ni kuchanganya mambo.

Kuhusu issue yako swali ambalo ningependa kufahamu kwanza je, ulishawahi kukutana naye physically na mkaongea kuhusu mahusiano yenu? Pia je katika kuongea kwenu katika mawasiliano yenu msingi hasa wa urafiki wenu huwa ni nini (kuoana au basi kuwa rafiki kama kaka na dada) maana wewe tayari moyo wako umejibu (fall in love)?
Je, katika kuwasiliana kwenu hujawahi kuongelea suala la urafiki wa kudumu au ndoa? na je yeye huwa anasemaje?

Ukiona moyo unazidi kumpenda zaidi unaweza kufanya mambo mawili kwani kuchelewa sana ukiachwa utaumia zaidi hivyo
(a) Muombe Mungu hadi ufahamu kama ni kweli anakupenda ili akuoe au
(b) Muulize wazi kabisa kama anakupenda atakwambia jibu kamili kwani kuna aina tofauti za vijana wa kiume wengine hadi umfunge kamba shingoni ndipo ataongea kuhusu kuaona kwani anaweza kuwa anakupenda zaidi ya wewe ila anashindwa kuongea inatokana na malezi na jinsi alivyo. Siyo wanaume wote ni initiator wa mambo yote.

Jambo la msingi jiamini uwe na subira na muombe Mungu kila kitu kitaenda vizuri.

Upendo daima