"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, December 3, 2009

Je, ni Sababu ya Msingi?

Swali:
Mimi ni mwanaume mwenye miaka 29 nilioa ndoa takatifu kanisani miaka miwili iliyopita na tumekuwa na wakati mgumu sana (migogoro) na mke wangu.
Ni miezi sita sasa hatujakutana kimwili (tendo la ndoa).
Naamini tendo la ndoa ni moja ya haki ambayo mume na mke ni muhimu haki kwani ni moja ya sababu zinazofanya tuoe.
Sioni dalili ya kupata suluhisho kwa migogoro yetu je, naweza kuachana naye (talaka) kwani naamini ninayo sababu ya msingi.

MAJIBU
Asante sana kwa swali lako ambalo naamini si wewe peke yako ambaye umejikuta unanyimwa tendo la ndoa kutoka na migogoro kati ya wanandoa.

Ukweli kujibu swali linalohusu talaka au kuachana ni sawa na kukata kitunguu ganda kwa ganda huku unaugulia kwa machozi hata hivyo nitajitahidi kujibu kama ifuatavyo.

Jambo la msingi ni kwamba sababu uliyonayo haina msingi na haiwezi kukufanya kutoa talaka kama ndoa yako ni takatifu kama unavyosema.
Sababu ya msingi ambayo inaweza kukufanya uoe mwanamke mwingine ni pale tu kifo kikitokea na sivinginevyo.

Pia kukosa tendo la ndoa haina maana ndoa haipo au ndoa inaweza kuvunjika kwani ndoa ni muungano (union) na agano (covenant) wa watu wawili mbele za Mungu waliokubaliana kuishi pamoja hadi kifo kitakapowatenganisha.

Msingi mkubwa wa ndoa ni kuondoa upweke (loneliness).
Mungu mwenyewe anatoa jibu kwamba
‘‘Si vema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa”.
(Mwanzo 2:18)

Ndoa ilianzishwa kwa sababu Adam alikuwa mpweke siyo kwa sababu alikosa tendo la ndoa na hivyo Mungu akaona kwamba “Haikuwa vema”.

Hivyo companionship ndio msingi wa ndoa na ndoa ni agano la companionship kwa wawili wanaooana.
Na huu ushirika wa ndoa ni kuwa pamoja katika mawazo, malengo, mipango, jitihada na miili.
Na msingi wa ndoa ni upendo wa kila mmoja kumpenda mwenzake ili kuondoa upweke.

(Soma Malaki 2:14, Mithali 2:17)

Tendo la ndoa halifanyi ndoa bali katika ndoa kuna tendo la ndoa na kutokuwepo kwa tendo la ndoa hakuwezi kusababisha ndoa isiitwe ndoa.

Ndoa huwepo kabla ya tendo la ndoa.
Je, wakati unafungua ndoa baada ya kula kiapo mchungaji aliwaruhusu mwende kwanza honeymoon na baada ya kurudi honeymoon ndipo atangaze kwamba ninyi sasa ni mke na mume?
HAPANA!

Ninachofahamu ni kwamba baada ya kula kiapo tu, mchungaji alitangaza mbele za mashahidi (KANISA) ninyi ni mume na mke.

Naungeenda honeymoon kabla ya kwenda kanisani na kutoa kiapo (vow) mbele za Mungu na kanisa (mashahidi) wewe na mchumba wako mngeitwa waasherati maana mmefanya mapenzi (sex) kabla ya kuoana kwa desturi za kiyayudi ungetoa talaka hata hivyo wewe unalalamika kukosa tendo la ndoa ndani ya ndoa kitu ambacho talaka ni impossible.

Hivyo kukosa tendo la ndoa hakukupi sababu ya msingi ya kuachana au talaka.
Tendo la ndoa halifanyi ndoa na haliwezi kutenganisha walioana kwani tendo la ndoa ni matokeo ya wanandoa kuishi pamoja na wana wajibu wa kufanya tendo la ndoa ili kuzaa na kuongezekana na hata wasipozaa haina maana ndoa inaweza kutenganishwa.

Ukiwa honeymoon una enjoy tendo la ndoa kwa kuwa unakuwa umeoa tayari, ni tendo takatifu.
Hii ina maana hata ukizini baada ya kuoa au kuolewa haiwezi kusababisha ndoa kuwa dissolved isipokuwa kifo.
Jambo la msingi ni kwamba kwa Mungu hakuna lisilowezekana na ukimwamini Mungu ametoa ahadi kwamba hakuna tatizo katika ndoa lisilo na solution kwani kwake hakuna lisilowezekana au kwa Mungu yote yanawezekana.
Mathayo 19:26

2 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli sijawahi kuchangia hapa kaka mbilinyi..ila leo umemjibu huyo kaka VIZURI SANA,kwani kwanza umempa maelezo kutokana na vifungu vya bible,hata kama si mkristo.Ila kuna kitu kimoja kuwa amekuwa feedup..kwani kusema kuwa haoni kama kuna suluhisho la migogoro ni uongo,nadhani kuna makosa katika ndoa ambayo watu wanaweza kudai wana sababu ya talaka,kama kumshika uchawi,kumfumania ugoni mwezi na sio eti kukosa tendo la ndoa kwamiezi sita ni sababu ya kuachana.Kwanza wangeongea na wazee au watu wakubwa kwao kwa umri wasuluhishe kwani hakuna jambo geni chini ya dunia ,ili wajipe second chance again...

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana kwa comments zako ni kweli hakuna tatizo la ndoa lisilo na solution kwani tatizo kubwa ni jinsi mtazamo wetu unakuwa pale kukiwa na mgogoro kuna wengine tatizo kidogo anataka kwenda zake kwa kuwa ameona dhahabu (feki) sehemu nyingine hata hivyo ndoa si chama cha siasa kwamba siku ukiona vipi unahama. Ndoa ni agano si mkataba tu. Kabla ya kuoa tunatakiwa kufahamu mambo haya vizuri siyo unaingia then ukiona mambo tofauti unaanza kushangaa. Hakuna kitu kizuri kama ndoa hata hivyo ili ndoa iwe nzuri ni muhimu kuwa makini na yule unachagua kuingia naye kwenye ndoa.

Upendo daima.