"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, December 2, 2009

Kwa nini siku hizi..........

Ameolewa jana na anataka amiliki jumba la uhakika kama fulani! KWA NINI TALAKA NYINGI SIKU ZA LEO?
Sababu zifuatazo zinachangia sana kwa kizazi cha sasa kuwa na rekodi kubwa ya wanandoa kuachana (divorce)

Vijana wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa na matarajio ambayo si sahihi (unrealistic). Wanaingia kwenye ndoa wakiamini kwamba kila kitu kitakuwa perfect.
Wanaingia kwenye ndoa bila ufahamu wa kutosha kuhusu nini kinafanya ndoa idumu.
Jamii ya leo ni zao la jamii ya “mimi kwanza”, kila mmoja huweka mkazo katika kutimiziwa mahitaji yake.
Kila mmoja anaimba
"My needs, my needs, my needs"
Na anakuwa kipofu na kiziwi wa mahitaji ya partner wake.

Wanandoa wa sasa wanataka mambo makubwa, wanataka kuwa na kila kitu kinachopendeza macho hawakumbuki kwamba wazazi wao na mababu zao walipata kwa kujituma, kuvumilia na kufanya kazi pamoja na kuwa na ndoa nzuri zilikuwa nzuri kwa sababu waliweka efforts.
Kila anachokiona kwenye Malls au store au mwingine anacho anataka na mpenzi wake au mume au mke amnunulie.
Kazi kwelikweli!
Wengi wanaoingia kwenye ndoa leo wanaingia huku wakiwa hawakuwa waaminifu (kabla ya kuoa au kuolewa) au alikuwa na wapenzi wengi.
Baada ya kuoa au kuolewa na kuanza kumzoea aliyeoana naye huanza kupepesa macho na kwa kuwa ana mguu mmoja ndani na mwingine nje matatizo huanza na hatimaye ndoa kuelekea kwenye shimo na kapata sababu!

Wanandoa wengi wanaoana bila kujua wazo la sacrifice ambayo inahitaji kuitoa ili kuwa na ndoa imara.
Wanaamini kwamba kila siku wanandoa wanatakiwa kuwa na furaha na siku kukiwa hakuna furaha basi anaamini ameoa au kuolewa na wrong person, kitu ambacho si kweli.

Wanandoa wengi wa sasa ni product za wazazi ambao nao waliachana (divorced) hivyo wanaingia kwenye ndoa wakiwa na mtazamo kwamba siku moja mambo yakiwa mabaya naanza mbele.
Tena hawa ndo hutishia kwamba mimi nitakuacha, maana wanajua uchungu wa kuachwa na wanaogopa kuchwa wao so wanawahi wao.

Wanandoa wengi wa sasa ni wavivu na hawana subira, kukiwa na tatizo dogo tu inakuwa kesi kubwa na pia hukata tamaa haraka kwa jambo dogo tu.
Watu wa sasa wanaoana mtu kupewa talaka ni kitu positive, ni ushujaa ni haki, ni uelewa wa masuala ya haki.

Miaka ya nyuma kupewa talaka ilikuwa ni laana, ni aibu, ni kuonekana failure, dhambi na mtu aliyepewa talaka alikuwa na kibandiko cha maisha kwamba hafai, leo hakuna tena ndo maana watu hawajali wala kuogopa.

No comments: