"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, December 13, 2009

Mara ya Kwanza!

Usipokuwa makini unaweza kuligongesha siku ya kwanza tu!Sex mara ya kwanza ni uzoefu wa aina yake na hakuna kitu hufurahisha kama mnakutana wote ni bikira.
Hapa nazungumzia wale ambao amefunga ndoa tayari sizungumzii wale wanaoamua kufanya uasherati kwani ndoa ni baraka na kuwa na mume wau mke wa ujana wako ni baraka.
Je, ni mambo gani mwanaume au mwanamke ambaye ameolewa na yupo kwenye siku yake ya kwanza ya kuwa na tendo la ndoa anatakiwa kuzingatia?

MWANAUME
FAHAMU NDOTO ZAKE
Kila mwanamke ana ndoto siku moja kuwa na mume anayempenda na kumfanya kutimiza ndoto zake za kuwa mke na kuhudumiwa kama mke idara zote.
Ni jambo la msingi kwa mwanaume mpya kuwa na ufahamu wa mwanamke aliyemuoa je ni wa kisasa (contemporary) au si wa kisasa (traditional) na kwamba je response yake kwenye suala la mahaba itakuwaje.
Unavyoweza kumtimizia ndoto zake (kimahaba) ndivyo unazidi kuwa karibu na kufungua hisia zake

JE, NI BIKIRA
Suala la kuwa bikira au kutokuwa bikira halina umuhimu wowote na si tatizo lako. Pia haina haja wewe kuwa na msisitizo wa kutaka kujua kwa nini si bikira hapo si mahali pake kujadili sababu hata hivyo kama ni bikira ni vizuri pia kujua kwani kutakuwa na maumivu kidogo na ikiwezekana hata yeye mwanamke kutoa damu kidogo ingawa si kila mwanamke bikira hutoa damu.

MPE UPENDO KABLA YA KUMTAMANI
Mwanaume na mwanamke ni tofauti sana linapokuja suala la tendo la ndoa kwani mwanaume hutoa upendo ili kupewa sex na mwanamke hutoa sex ili kupewa upendo hii ina maana kwamba kwa mwanamke upendo kwanza na kwa mwanaume sex kwanza, bila kuwa makini kufahamu hii siri mnaweza kuchanganya mambo.
Mke atajiweka tayari (open) pale tu wewe mwanaume utakapoonesha upendo, caring, affections nk.
Kama akili yako na mawazo yako yapo kwenye matiti yake tu na pale chini basi hutafika popote kwani unahitaji kumpa upendo kabla ya kumtamani.

USIWE NA HARAKA:
Mwanamke huchukua muda mwingi au mrefu kuwa tayari kwa sex na akishafika anachukua muda mrefu kurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Hivyo usiwe na haraka kama afande.
Take it slow
Au hakikisha ameonesha dalili zote kwamba yupo tayari.

MUULIZE NAMNA GANI NA WAPI
Mara nyingi kwenye shughuli za mahaba wanaume wote ni ma-genius, ndio wanaoshika usukani.
Jambo la msingi ni kukumbuka kwamba kila mwanamke ni tofauti na hata mwanamke huyo mmoja anakuwa tofauti kwa siku kadhaa katika mwezi mmoja.
Kuna siku ukishika matiti husisimka na kuna siku ukishika matiti atajisikia kuumia hivyo using’ang’anie au kuanza kubabaika.
Ni vizuri kumuuliza kitu gani anapenda na ufanye namna gani anaweza kukueleza kwa maneno au kwa ishara.

AKISEMA HAPANA HAINA SHIDA
Kwa kuwa ni mara ya kwanza anaweza akasema hapana, hivyo usiumize kichwa, inawezekana anaona aibu au yupo MP, kumbuka yeye kwanza na si wewe.
Ni rahisi sana kumvua nguo mwanaume yeyote kwa ajili ya sex hata kama hamjuani au hata kama anatoka sayari nyingine ila si mwanamke.

USIJIBU JEURI
Unaweza kuulizwa swali ambalo linakufanya ushangae hata hivyo uwe na subiri na usijibu kijeuri kwani unaweza kumpiga password kwenye feelings zake na ikawa shughuli nzito na mwili mzima ukaji lock ushindwe kufanya chochote.

UZAZI WA MPANGO NI JUKUMU LAKO MWANAUME
Kutofahamu njia za kujikinga na mwanamke kupata mimba kama hamuhitaji kuzaa watoto 35 ni kuonesha mwanaume yupo caring na pia upo selfish.
Siamini kama mnaweza kufika hapa kabla ya kujadili masuala ya uzazi, watoto, mimba na lini muwe na watoto.

MKUMBATIE, BUSU NA AWE KARIBU
Kwa mwanamke tendo la ndoa si sex peke yake bali ni pamoja na hugs, kissing, cuddling na kupeana joto kwa foreplay ya kufa mtu.
Onesha jinsi unavyomuhitaji kwani kuna msema kwamba
The way man make love demonstrates his character
kama unamjali mke wako mpya basi kitandani ni mahali ambapo unaweza kuonesha mara 1,000 kwamba unamjali na kinyume na hapo wewe ni
Selfish
Pleasure seeking,
Narrow focused,
Hivyo kiss, touch and feel.

MWANAMKE:

MTAZAMO:
Mwonekano wa nje (appearance) mara nyingi huwezesha wanaume kujipiga switch ya sex haraka iwezekanavyo, pia chemistry ya mwili nni jambo la msingi sana ni kama asset kwa ajili nya sex hata hivyo kwa kuwa na tendo la ndoa zuri siku ya kwanza jambo la msingi kwa mwanamke ni mtazamo wako kuhusu sex.
Ni muhimu sana kujiamini kwamba unaweza na pia mume wako atakufurahia na kwamba anakuhitaji na upo tayari kusaidiana kuhakikisha wote mnakuwa na wakati mzuri pamoja na ni jukumu lenu wote na si kulala kama gogo lisilo na feelings ukiamini mambo yataenda sawa.

USAFI
Ni vizuri sana kuzingatia suala la usafi kwani ni jambo linalopendeza kunukia vizuri katika harufu ya asili ya mwili wako.
Kwani ukiwa unavutia na mwenye kunukia vizuri basi mwanaume atakuwa crazy tu na atafanya kila analoweza kuhakikisha anakupa kile unastahili.

MAANDALIZI
Jambo la msingi ni kwa wewe mwanamke kuwa wazi kuonge na kuongea na kuongea na kuongea, yaani jiweke huru kuwa wazi kuongea kila kitu.
Kumbuka kubusiana huja baada ya kuongea kwani maneno matamu huleta hamu ya kuwa karibu zaidi kimwili.

KAMA UPO MP
Wanaume wengi huwa hawajali kama mwanamke yupo MP au la hata hivyo suala hili hufanya mwanamke mwenyewe asijisikie vizuri ( embarrassed).
Ni vizuri sana kuwa na discussion na wote mfanye kile mmekubaliana kama hapana iwe hapana kwa wote na kama ndiyo iwe ndiyo kwa wote na si vinginevyo.

USIMUHUKUMU
Wanawake wengi wanaamini mwanaume lazima awe kiongozi linapokuja suala la sex hata hviyo wapo wanaume ambao huhitaji ujasiri wa mwanamke ili kila kitu kiende sawa.
Hivyo ukiona mume wako haoneshi dalili ya kwamba anaweza kuanzisha chochote ni vizuri ukachukua jukumu na katika kuchukua jukumu isifanye kwa dhihaka hadi kuumiza utu wake.
Anyway huyo ni mume wako, mwili ni mali yako na tendo la ndoa ni haki yako na mali yenu na kila kitu unafanya ni Baraka.

KILELENI
Kufika kileleni au kutokufika yote hutegemea wewe na mwenzi wako.
Ufike kileleni usifike jambo la msingi ni wewe ku-enjoy siku yako ya kwanza kuwa na mume wako na zaidi bado ni grade one so bado safari ni ndefu hadi kuwa na PhD ya mahaba kama mke na mume na ndipo utafurahia kufika kilele.

KIASI GANI
Ukweli hakuna kanuni ni kiasi gani inatosha kwani hakuna formula ya how much is too much or too little.

MWAMBIA “NAKUPENDA”
Wakati mwingine mzuri wa kumwambie mume wako nakupenda ni wakati wa sex na hapo itasaidia kuweka memories kwenye ubongo wake na hatimaye unaweza kuwa na better sex and fulfilling.
Kwa maelezo zaidi soma hapa

2 comments:

Anonymous said...

Habari kaka!

Samahani natoka nje ya mada naomba kuelewa nimesoma blogs mbalimbali kuhusu wedding gaun hv kuvaa nyeupe ni kweli ina maana bibi harusi ni bikira? kama kweli mbona watu wanaolewa na matumbo ambayo hata watoto wanayaona halafu wanavaa gauni jeupe hapo sijaelwa vizuri naomba ufafanuzi wa hili,
Halafu jamani kwa wachungaji wetu wanafungisha ndoa mtu akiwa na tumbo kubwa tuu hapo mtoto asizaliwe nje ya ndoa kwa mimi naona tayari ni nje ya ndoa maana walizini mtoto tayari aliumbwa na Mungu kimwili tu haonekani ila kiroho yu pamoja nasi na ndio maana mtoto akiwa tumboni ana mawasiliano na sisi tunaamini hilo.

Ni hayo tuuu.Nikutakie siku njema!

Mama P !

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Asante sana kwa maswali mazuri, kwanza samahani sikuwepo kwa siku kadhaa na nimerudi na tutarudi na nitajitahidi kujibu vizuri maswali yako muhimu sana ya vazi la harusi na kufunga ndoa huku bibi harusi tumbo limeshajibu.
Kazi kwelikweli!

Upendo daima