"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, December 7, 2009

Nimechoka, Najisikia Uchungu sana!

Hadi kupika napika!Hello Jane,

Sijajua kitu gani kimetokea katika ndoa yetu, tulizoea kuwa na tendo la ndoa mara 3 kwa wiki na sasa ni mara moja kwa miezi minne na hata tunapokuwa kwenye tendo la ndoa unajilaza kama gogo tu na unanipa sura ambayo inanipa nitafsiri kwamba unaniambia “Hujamaliza bado, ondoka mwilini mwangu unachofanya sijisikii chochote”
Je, ni kitu gani kimetokea kwani ulikuwa sexy, exciting na ulikuwa ni mwanamke niliyekuoa unayependa kufanya mapenzi na mimi.

Ndoa yetu ina miaka 10 sasa na ni miaka 3 tu ulifanya nijisikie nimeoa mke ambaye anatimiza ndoto zangu hata hivyo hii miaka 7 ambayo umekuwa huna hamu ya tendo la ndoa imesababisha nijikie nimechoka na nipo hatua ya mwisho hasa baada ya kuweka juhudi kubwa kukurejesha kwenye mstari na nimeendelea kuambulia kuendelea kukataliwa tendo la ndoa.

Nafahamu fika mke wangu unapenda vitu gani, ninafahamu unapenda affections, unajisikia raha kupendwa, unajisikia raha kupelekwa outing angalau mara mbili kwa wiki, unajisikia raha kupewa zawadi, unajisikia raha mimi kuwa na watoto na wewe ukapata muda wa ziada (free time), unapenda kupewa extra money kwa ajili ya shopping, pia unajisikia raha nikupe pesa kwa ajili ya kwenda vacation na dada yako, unajisikia raha ninapokusaidia kazi za nyumbani ili usiende kulala umechoka na nimekuwa najinyima, najipinda mgongo wangu kuhakikisha haya yote unayapata hii miaka 7 ambayo hata hivyo wewe umekuwa unaninyima tendo la ndoa na nikikuomba unaniamba “Nimepotoka na mpenda sex”

Nimekuwa najiuliza kwa nini nijinyime na kupinda mgongo wangu kujitoa kwa mambo yote haya kama wewe unashindwa kunitimizia hitaji moja tu la sex angalau mara mbili kwa wiki?
Kwa kweli nimechoka na nimeanza kujisikia hasira na nimepoteza interest kwani najisikia wewe huoni umuhimu wa kunitimizia mahitaji yangu.

Ninafahamu fika kwamba hamu ya kufanya mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke ni tofauti na nimejitahidi mara zote kuhakikisha wewe unapata kile unahitaji ili ujisikie vizuri na uwe tayari kwa sex hata hivyo juhudi zangu zimekuwa hazina maana.

Sikukuoa ili unipe sex tu, na pia sikukuoa ili usinipe sex, sex ni moja ya sababu maelfu zilizonifanya nikuoe. Nilikuoa ili kuondoa upweke, ili uwe life partner, nishirikiane na wewe katika ndoto na malengo ya maisha pamoja, kulea watoto ambao Mungu ametupa na kupeana sex na mwanamke ambaye ninampenda na ambaye nimemchagua kufanya mambo haya yote.

Kumbuka naweza kupata vitu vyote kwa mtu yeyote ambaye naweza kuamua kuishi naye isipokuwa sex tu kwani ni wewe tu unaweza kunipa na ndiyo maana niliacha wazazi wangu ambao walinipa kila kitu nahitaji isipokuwa sex kwani hata kama ningetaka mtoto ningeweza kufanya adoption.
Sex inanifanya nijisikia nipo connected na wewe, sex inanifanya nijione na kukuona wewe ni mwanamke special.

Swali linakuja kwa nini mwanaume aweke commitment ya maisha kwa mwanamke ambaye hawezi kumpa sex?

Kama mke wangu ungeniambia tangu mapema kwamba hamu yako ya kufanya mapenzi itakuwa ni miaka 3 tu nina uhakika nisingepoteza muda wangu kukubaliana kuoana na wewe, nisingekubali kuingia katika shida kubwa namna hii ya kunyimwa sex na mke wako mwenyewe na unajua fika siwezi kupata hii huduma mahali popote isipokuwa kwako na kama nilivyokwambia siwezi kukuacha wala kushawishika kutembea na mwanamke mwingine kwani ninakupenda.

Kinachoniuma zaidi ni kitendo chako cha kuninyima na huku unafurahia na nikitaka tuongee unanijia juu eti mimi ni mpenda sex nisiyejali na ninayejua ndoa ni sex tu.
Nafahamu nimefanya the biggest mistake in my entire life, nimekwama kwa mtu ambaye nampenda na hawezi kutimiza hitaji langu, najiona nimenasa kwenye chambo ya kizamani na Inaumiza sana.
Najuta, najuta najuta mno!

Nimeamini inachukua efforts kidogo sana kumfanya mwanaume afurahi na ni ngumu sana kumfanya mwanamke afurahi.
Nipe sex mara 2 kwa wiki nitakuwa mwanaume mwenye furaha na nitakufanya uwe na furaha ziku zote.
Nini kigumu hapo mke wangu?

Ukinipa sex najisikia nipo connected na wewe kimwili, kinafsi na kiroho!

Najisikia uchungu sana!

James!

17 comments:

Anonymous said...

Kweli hii inashangaza sana, kwa nini ndoa huwa namna hii. Mwenyewe nakumbuka ni juzi tu tukiwa honeymoon mimi na mke wangu masuala la sex yalikuwa super na miaka miwili sasa mke wangu amebadilika ghafla. Na nilikuwa najiambia moyoni kwamba kitu ambacho sitapata shida katika maisha yangu ni suala la sex kwani mke wangu anapenda hata hivyo sasa kibao kimebadilika yaani kutoka 10 tumeingia minus 10 sasa ni mwezi wa tangu ngoma nzito, hakuna kubusu, hakuna kumkumbatia, nimechoka kuomba sex si charity ni haki yangu ama sivyo nitanza mbele bahati nzuri sina watoto!

Anonymous said...

Sasa tupewe majibu ya mke wake atasemaje au ajibu kwa nini anafanya hivyo.

Anonymous said...

Yaani wanawake wanafanana sana na mbwa jike, akizaa tu sex hadi kung’atana meno, kazi kwelikweli!

Anonymous said...

Wanawake wa siku hizi wanataka pesa na kuonekana wameolewa tu hakuna maana ni wachache sana ambao wanafaa.

Anonymous said...

Baada ya miaka 14 ya ndoa na kuendelea kumuangukia mke wangu kumuomba sex na kuambulia mara 2 kwa mwezi sasa nime give up na liwalo na liwe sasa nimeamua kutafuta mwanamke mwingine na nikishikwa basi na nikipewa talaka basi kwani I am tired, ufanye kazi zote hadi kumbeba na bado ukifika chumbani anakupa mgongo!

Anonymous said...

Haaaaaaaaa, imenipasa nijikune kidogo nisije kuwa nimeandika mwenyewe! Afadhari Mwenzangu unapata sex angalau mara moja kwa miezi 3 mwenzio imekuwa miaka 9 mfululizo na anagoma kufanya discussion yoyote na ukianza tu anakwambia “usiniharibie siku yangu au weekend yangu” Ukweli nimekuwa na maisha yangu mwenyewe ndani ya ndoa. Vijana kabla ya kuoa uwe makini kudiscuss issue za sex kwani ukiona hana interest kujadili be extra careful pia fahamu vizuri background yake.

Anonymous said...

Natamani ningesoma hii miaka 3 iliyopita kwani mimi nilikuwa kama huyo mwanamke na mume wangu aliniacha na kwenda kwa mwanamke mwingine. Hata hivyo nami nikapata mwanaume mwingine ambaye sasa yeye ndo hana hamu ya kufanya mapenzi. Kumbe mwanaume anapokutaka tendo la ndoa unajisikia anakuhitaji na asiposema inauma sana. Mungu anasamehe kwani navuna nilichopanda. Ushauri kwa wanawake wengine Jitahidi kumtimizia mume hitaji la sex kwani sex ndiyo hufanya mwanaume kukuona special na pia kuwa connected na wewe. Hasira zingine za wanaume hutulizwa kwa kumpeleka kitandani mara kwa mara

Anonymous said...

Asante kwa kuiweka hii, nami ni mmoja ya wanaume wambao wanakumbana na janga linalofanana. Mara 4 kwa mwaka kwake hakuna shida. Najuta sana kuoa mwanamke huyu wa kizungu. Nami nimekwamba isingekuwa watoto basi!

Anonymous said...

Asante sana kwa barua hii. Pia unaonekana ni mwanaume caring sana na unselfish, si ustaarabu kabisa kukataliwa hitaji lako namna hii.
Mwenyewe napenda sana kuwa na mume wangu sexually huku tunapendana. Sex ni moja ya njia ya kuwa karibu wanandoa. Sex hufanya ndoa kwua wonderful.
Life is too short!

Anonymous said...

Wow! Nilifikiri nipo mwenyewe tu. Mke wangu yeye ni the best kwenye hili kwani mimi ndiye nafanya kazi, fua ngu, take care watoto na linapokuja suala la sex ukipata mara moja kwa wiki 2 basi una bahati! Na pia hapendi asikie unaongea na mwanamke yeyote, ninachoshukuru ni kwamba nina watoto wawili wazuri sana, that is what I care about!

Anonymous said...

Ni kama nasoma feelings zangu mwenyewe. Ningeweza kuandika neno kwa neno ninayokutana nayo. Ni kweli ni ngumu sana kufanya mwanamke afurahi.

Anonymous said...

Hata mimi ningeandika barua kama hii, kweli Inaumiza sana kuishi na mtu ambaye anaishi kama anakupenda hata hivyo mkiingia kitandani anakupa mgongo. Unaharibu sana kujiamini kwa mtu ambaye anakutana na kukataliwa kimapenzi namna hii.

Anonymous said...

Mchumba wangu ana miaka 23 na mimi miaka 25 na si muda mrefu tutaoana, napenda sana na yeye angesoma hii article ili aweze kufahamu nasi safari yetu itakuwaje.
Adam.

Anonymous said...

Nasikia maumivu ambayo huyu mwanaume anayapata kama vile ni mimi mwenyewe. Inaonekana anaongea kwa niaba ya maelfu ya wanaume ambao wanakutana na issue hii.

Anonymous said...

Mimi naishi na mwanamke ambaye hana hamu ya tendo la ndoa, nami ningependa niandike kila najisikia, article nzuri sana.

Anonymous said...

jamani hii kitu wanawake wangejua wangesaidia sana kizazi hiki kupona na ukimwi. Tuko wengi sana kumbe.

Anonymous said...

Mhhh, jamani kama ingekuwa si wanaume wengi wamechangia hapo nisingeamini sana kama kweli wanawake wengi hawapendi sex na wana hiyo tabia.

Sijaolewa bado na kwa neema ya Mungu nimechagua kuabstain mpaka nitakapoolewa. Lkn kwa vita ninayopambana nayo kushinda majaribu sidhani kama nikiolewa nitachezea hiyo fursa ya kururahia tendo la ndoa.

Labda wanawake wengi hawaenjoy tendo hilo kutokana na waume zao kutolifanya kwa namna ya kuleta burudani au kukosekana kwa uhuru wa mawasiliano na urafiki wa karibu. Mhh, infact inaogopesha km kweli mtu anaweza kuamua tu kuchukia tendo hilo bila sababu.

Ndo maana namuomba sana Mungu anisaidie nipate mume ambaye atakuwa rafiki yangu sana, nitakuwa huru kwake kujieleza (bila kuogopa au kuhofia kuonekana mjinga) naye pia asinionee aibu wala kuogopa kujieleza na kunikosoa pia itakapobidi.

Nafikiri utayari wa kujifunza na kufundishwa unahitajika sana ktk mapenzi. Watu wasijione kuwa wao ndo wanajua sana hata inakuwa ngumu kushauriwa au kujieleza kwake.