"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, December 6, 2009

Wanampinga!

Kuna mwanaume ambaye kanisa limempendekeza awe moja ya viongizi wa kanisa, mke wake pamoja na wale waliompendekeza kuwa kiongozi wamekasirika sana kwani wengi (washirika wa kanisa) wanapingana na huyo mwanaume kuwa kiongozi wa kanisa kwa kuwa huyu mwanaume alishatoa talaka kwa mke wake wa kwanza na kanisa limeweka sheria kwamba kila anayekuwa kiongozi wa kanisa anatakiwa asiwe ni Yule amewahi kutoa talaka au kupewa talaka (divorced).
Kwa ufahamu wangu naamini Mungu anachukia talaka lakini anawapenda waliotalikiana na amewasaheme kwani divorce ni dhambi inayosameheka.
Je, maandiko yanasemaje kuhusu hili?

Kwanza swali lako siyo jipya sana hasa kwa makanisa ya magharibu (ulaya na Amerika) ambako hata viongozi wa kanisa au ministries walishakumbana na talaka iwe kwa washirika wao au wao wenyewe.
Mojawapo ni John Hagee, Juanita Bynum, Paula White, Joyce Meyer nk.
Na hili suala la divorce limewagawa watu katika makundi mawili wale wanaokubali (liberal) na wale wanaokataa (conservative).
Pia suala la divorce na remarriage lilikuwa gumu sana wakati wa Musa na likawa gumu sana kwa mafarisayo hadi wakati wa yesu ilibidi wamtege (test) kwa swali la talaka (soma Mathayo 19:1-10) pia limekuwa suala gumu sana kwa kanisa leo na bado ni gumu hata hivyo Biblia ipo wazi kuelezea kila ugumu uliopo.

Kwa kifupi ili kujibu swali lako hapa kuna mambo mawili muhimu
Kwanza ni kweli Mungu anasamehe dhambi zote katika Kristo.
Na upo sahihi kwamba Mungu anasamehe dhambi zote.

Kuna dhambi moja tu ambayo huwezi kusamehewa nayo ni kumkufuru Roho mtakatifu
Biblia inaelezea kwamba ni kweli binadamu huweza kusamehewa dhambi za uzinzi
(1 Wakoritho 6:9-11)

Jambo la pili ni kwamba kusamehewa dhambi hakuwezi kuondoa matokeo (consequences) ya dhambi umefanya.
Kusamehewa maana yake Mungu hakuhesabii dhambi tena na anayesamehewa hahukumiwi tena hata hivyo matokeo ya zile dhambi katika jamii bado zitakukuta na utapambana nazo mbele ya safari.
Kama kabla ya kuokoka au kuamini ulifumaniwa na wakakukata mkono kwenye hekaheka za kufumaniwa, siku unatubu dhambi ya uzinzi na kuokoka haina maana mkono wako uliokatwa utarudi au kuota, kilema cha kukatwa mkono utapambana nacho kama matokeo ya dhambi ya uzinzi (kufumaniwa) katika maisha yako hata kama umeokoka.

Kama kabla ya kuokoka ulikuwa na wake wengi, ukiokoka ndiyo unasamehewa lakini Biblia ipo wazi kwamba huwezi kuwa kiongozi wa kanisa na si kwa sababu hujasamehewa na Mungu bali kwa sababu kanisa halitakiwa kuongozwa na watu wasio na sifa njema, kanisa linahitaji kuongozwa na watu wenye ushuhuda mwema mbele ya watu na wasio na lawama
(1 Timotheo 3:2, Tito 1:6)

Unapotoa talaka au kupewa talaka maana yake miaka ijayo mbele huwezi kupewa uongozi katika kanisa kwa kuwa una sifa mbaya ambayo ni lawama kwa wengine wanaoliangalia kanisa la Mungu kuwa mfano kwao.
Hivyo wanaompinga wapo sahihi kama kweli sheria ya kanisa imesema ukiwa divorced huweza kushika uongozi wa kanisa.

Kumbuka Unapoachana na mke au mume na kupewa talaka ni label ya maisha ambayo utatembea nayo na inasema wewe ni failure.

No comments: