"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, January 28, 2010

Wa aina hii.... Kimbia


Nyumba ikijengwa kwa msingi imara huweza kusisimama kila aina ya dhoruba, hata suala la mahusiano ni kitu kilekile ukijichanganya wakati wa kutafuta mchumba utaishia kwenye ndoa inayochanganya.
Hata hivyo ni muhimu sana kuwa makini na ishara ambazo unaziona kwa yule unaamini anaweza kuwa mke au mume baadae.

Je, yafuatayo ni sehemu ya maisha yake?

Msumbufu:
Anasumbua ingawa ana kazi nzuri.
Jinsi mtu anavyokufanya ujisikie ukiwa naye ni muhimu mara mia kuliko vile asivyokuonyesha ukiwa naye.
Hii ina maana kama ni msumbufu itafika mahali utamchoka hata kama ana kazi nzuri.

Mficha vitu:
Ingawa umekuwa naye kwa muda mrefu lakini unajiona humfahamu yeye halisi (true him/real him).
Anakuficha mambo mengi kuhusu yeye na kila kitu kuhusu yeye.
Anayefaa anakuwa wazi, anakushirikisha mambo mazuri na mambo mabaya yanayotokea katika maisha yake.
Anakwambia vitu vinavyomhusu yeye mwenyewe bila wewe kuchunguza.

Ahadi tupu:
Anaendelea kukuahidi na kukuahidi kwamba atafanya hivi na vile, ila ukimuuliza ni kwanini hatimizi anatoa sababu zaidi ya mia moja na moja.
Anakuahidi kukununulia gari wakati yeye mwenyewe anatunzwa.
Anakuahidi kukutafutia kazi wakati yeye mwenyewe hana kazi.
Ipo siku hasira na kukatishwa tamaa kutakufanya ujute.
Kumbuka anayefaa anatimiza ahadi zake na anayetimiza kile anasema na kuahidi anafaa zaidi kuliko yule wa maneno matupu na asiye timiza ahadi zake.

Mtu wa kupenda sifa:
Kawaida mtu mwenye hekima na busara husifiwa na wenzake na asiye na busara (mjinga) hujisifu mwenyewe.
Matokeo ya kujipa sifa mwenyewe inafika mahali anadharauliwa na kuonekana mtu mdogo sana asiye na maana.

Mtu wa kulaumu:
Kila kitu kibaya kikitokea anakulaumu wewe; mtu wa aina hii hajui responsibility ni kitu gani.
Hata kama ni yeye amefanya makosa atapindisha ili uonekane wewe ndiye uliyekosa.
Hupenda kulaumu kila kitu kama vile chakula, ndugu, marafiki, hali ya hewa, Rais, Boss wake, jua, baridi, mvua nk.

Mwongo:
Kama ameweza kukudanganya jambo kubwa, basi ujue upo na mtu ambaye hushughulikia mambo makubwa kwa kudanganya.

Wednesday, January 27, 2010

Usiache zikajaa!

Kutoweza thibiti hasira husababisha kutokuelewana katika ndoa.
Kila mwanandoa anahitaji kuwa makini na hasira zake ambazo wakati mwingine hupelekea kuwa mtu wa kukefyakefya, mtu wa vijembe na kejeli, pia mtu wa kulaumu kila wakati na vitu kama hivi ni moja ya alama kuonesha kwamba ndoa imeanza kuchimbika.

Tunahitaji constructive ways za ku handle hasira katika ndoa.

Siku zote binadamu hupenda ku-fight back, kitu kidogo huwa issue kubwa kabisa hata hivyo mtu mwenye busara anafahamu fika kwamba kusamehe na kusahau nia kuishi katika mapatano ni sehemu ya gharama ya amani na upendo katika ndoa imara.

Mwanamke mwenye busara husema:-
"Ingawa mume wangu hutupa nguo na soksi huko na huko anapobadilisha namuona ni mume mzuri kwani ananijali, who care! Kama ananitimizia mengine mengi tu hili ni kitu gani linisumbue!"

Mwanaume mwenye busara husema:-
"Hata kama mke wangu hapendi kusafisha nyumba mara kwa mara hivyo jinsi anavyopika chakula kitamu na alivyo mwema kwangu ninampenda na ninaridhika na ndoa yangu".

Ingekuwa wengine kwa matatizo yaliyoelezwa hapo juu basi ingekuwa shughuli nzito kwani wanandoa wengi huangalia negatives badala ya positives na ukweli ni kwamba ukiwa unaangalia negatives maana yake unaweka sumu katika mahusiano yako.

Kumbuka mke na mume wanapoanza kuzozana ni kama kutoboa matundu kwenye bwawa na baada ya muda bwawa zima hupasuka na kutoa maji ya fujo hivyo kuhimilia hasira ni jambo la msingi.

Pia si busara sana kusubiri hasira zijazane (build up) kwani itafika mahali intensity itakuwa kubwa sana na mkaanza kulipuana kama mabomu.

“Health marriage is the one in which couples love each other and are able to resolve difficulties by compromise”.

Kama ikitokea mnabishana kwa ajili ya kitu chochote si vema kumwambia mke wako au mume wako “hoja yako ni rubbish
Uwe makini na kile unaongea ukiwa na hasira

Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.
Mithali 15:1-2

Tuesday, January 26, 2010

Je, ni urefu au Unene?

Hukatwakatwa kama kisu na kurushwa mita kadhaa! Je, urefu wa uume ni suala muhimu kwa mwanamke kuridhika kimapenzi?
Hii ni imani potofu ambayo imewafanya wanaume wengi kujiingiza kufanya surgery za gharama kubwa na wengine kupoteza pesa zao kwa ajili ya kutafuta dawa za kienyeji ili kuongeza maumbile kuwa marefu zaidi.
Huko ni kupoteza muda na pesa.

Ingawa urefu wa uume hauna umuhimu kama imani potofu inavyodai bado suala la msingi ni uimara wa misuli ya uume; kwani misuli ya uume ikiwa imara basi mwanaume huwa na uwezo (strength/flexibility) ambayo itaweza kumpa sifa mume kwa mke wake kuliko kushabikia kuwa na jumbo size.
Hii ina maana bila kujali una urefu kiasi gani au ufupi kiasi gani, kama una misuli imara hilo ndilo jambo la msingi kwa mwanaume.

Tuweke suala la hiyo imani potofu pembeni hivi ni kitu gani mwanamke huhitaji physically ili afurahie tendo la ndoa?
Suala la muhimu ni kuwa na ufahamu wa anatomy kuhusu mwanamke (uke); ukweli ni kwamba nerves nyingi zipo within inches mbili kutoka mlango wa uke (vaginal opening) na asilimia kubwa ya nerves zipo katika mzunguko wa mlango wa uke.
Hii ina maana mwanaume yeyote mwenye uume wa inches mbili kama anajua namna ya kumfikisha mke kuridhika au kufika kileleni kupitia uke (vaginal climax) basi ataweza kumfikisha mke wake kileleni.

Je, ni unene (thickness) wa uume huweza kumridhisha mwanamke kimapenzi?
Ni kweli unene inaweza kuwa ni factor hasa kutokana na uwezo wa mwanamke alionao kukaza misuli ya uke.
Je mwanamke ana umri gani, amekuwa na partners kiasi gani na amezaa watoto wangapi na zaidi amefanya kitu gani kuhakikisha misuli yake (uke) inakuwa imara.

Mfano:
Ingawa suala la thickness si tatizo kwa wanawake wa nchi za Asia kama Japan, Singapore au Philippines kwa kuwa suala la kukaza misuli kwa wanawake ni moja ya sanaa.
Wanawake wa huko hucheza michezo ya kuingiza ping pong-ball (mipira mfano wa tennis) sita kwenye uke na kuzirusha futi 15 ili kuingia kwenye ndoo huku kila kimpira kinapotoka kinaendana na popping sound bila kukosa hata kimoja.
Pia huweza kuingia ndizi iliyomenywa kwenye uke huanza kuzikata ndizo (slice) vipande vipande huku vikidondoka.

Fikiria sasa likija suala la mapenzi hii inaonesha kwamba hao wanawake wanajua jinsi ya kuridhishana na kwao size does not matter.

Bahati mbaya ni kwamba tamaduni nyingi za Africa, ulaya na Amerika hazina mazoea ya kuwa na mazoezi ya kukaza misuli ya uke au uume.

Hivyo thickness ni muhimu kwa mwanamke ambaye uke wake ni loose na weak pia kama misuli yake hoi.
NB:
Hapa sina maana mwanamke ajihusishe na mchezo huu, it is illegal; najaribu kuelezea uwezo wa misuli ya uke ukifanyiwa mazoezi vitu inaweza kufanya.

Je, inakuwaje kama mwanaume ana uume mkubwa (unene na urefu) zaidi ya wastani ambao wanaume wengi huwa?
Tafiti nyingi zinaonesha wanawake wengi hulalamika pale mwanaume anapokuwa na uume mkubwa zaidi ya kawaida na hasa kama hajui namna ya kuutumia.
Wanawake wengi huona ni huge barrier kwa ajili ya ku-enjoy sex kama mke na mume na wakati mwingine mwanamke hujisikia uncomfortable na huishia kukwepa.
Pia wanaume wenyewe ambao wana uume mkubwa tafiti zinaonesha kwamba wengi hujikuta katika huzuni na wanaombolezo kwa sababu partners wao kujisikia maumivu na kuumia na hata imesababisha mahusiano ya kimapenzi kati ya mke na mume kuzolota.

Je, hutokea nini pale mwanaume mwenye jumbo size akakutana na mwanamke mwenye uke uliobana?

Na wanaume ambao ukubwa wa uume (thickness ni zaidi ya kawaida wanapokutana na mwanamke ambaye ana size ndogo ya uke, au hakuwa wet sawasawa au hajazaa mtoto kabisa au bikira suala la sex linakuwa shughuli nzito kuihimili kwani lazima mwanamke akubaliane na pressure na pain za kuta za uke zinapochanwa.

Na pia kama mwanaume ana urefu unaozidi inches 6 ambayo ni average size kwa wanaume basi mwanamke anaweza kujikuta anajuta kwani anaweza kuhisi mwanaume anagonga hadi kwenye kizazi (internal reproductive organs).
Na matokeo yake mwanamke hujikuta anakaribisha magonjwa kama cysts ambayo huhitaji surgery na pia huweza kupata infections ambazo huweza kusababisha kukosa watoto.


Nini kifanyike?
Jambo la msingi ni kwa mwanaume kufahamu namna ya kutumia tool yake vizuri, hii ni pamoja na kuwa caring, kufanya maandalizi ya kutosha.

Je, nini faida ya kuwa na uume mkubwa au uume mdogo?
Kama mwanamke ana uke ambao ni loose na hawezi kuthibiti mwendo (misuli imelegea) basi tool kubwa kama hiyo huweza kumsaidia kupata feelings za kufurahia mapenzi hapa haijalishi mwanaume ana skills zozote au la.
Na mwanaume ambaye ana uume mdogo kuliko kawaida anaweza kuwa na faida kwa mwanamke ambaye ana uke mdogo (tight).

Hii ina maana mwanaume mwenye uume mkubwa ana match na mwanamke mwenye uke loose na hii combination huwezesha hao wawili kuwa na ridhiko kimapenzi.
Na mwanaume mwenye umbile dogo ana match na mwanamke mwenye uke tight.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma hapa na hapa na pale

Sunday, January 24, 2010

Wanamalizana Kabla!

SWALI:
Habari kaka Mbilinyi!
Naomba kuelewa nimesoma blogs mbalimbali kuhusu wedding gown, hivi kuvaa nyeupe ni kweli ina maana bibi harusi ni bikira?
Kama kweli mbona watu wanaolewa na matumbo ambayo hata watoto wanayaona halafu wanavaa gauni jeupe hapo sijaelwa vizuri naomba ufafanuzi wa hili.
Halafu jamani kwa wachungaji wetu wanafungisha ndoa mtu akiwa na tumbo kubwa tuu hapo mtoto asizaliwe nje ya ndoa kwa mimi naona tayari ni nje ya ndoa maana walizini.
Nikutakie siku njema!

Mama P.

JIBU:
Asante sana kwa swali zuri ambalo kwa kweli linaonesha ukweli halisi wa hali ilivyo duniani na namna maadili na hofu ya Mungu ilivyoshuka kwa kiwango cha kutisha.
Kwa ufupi ni kwamba ilikuwa hadi 1840 pale queen Victoria alipoolewa kwa kuvaa vazi jeupe ndipo mabibi harusi wengi walianza kuvaa rangi nyeupe; ila kabla ya hapo hakukuwa na traditions za kuvaa vazi nyeupe kwa bibi harusi.

Hata hivyo vazi la rangi nyeupe kuvaliwa siku ya harusi tangu (zamani) kale ilikuwa ni alama au ishara ya kuonesha usafi, kujitunza au kuwa bikira kwa bibi harusi na huu utamaduni umekuwa msingi mkubwa kwa wakristo wanaofuata mafundisho ya Yesu au Biblia.
Kwa bibi harusi kuvaa vazi jeupe ni kuonesha au dhihirisha au maanisha kwamba amejilinda na dunia (uchafu wote, uzinzi ni uchafu nje ya ndoa) na sasa anajitoa kwa mume wake kama zawadi na kwamba yeye ni bikira kama kanisa (church) ambalo ni mfano wa bibi harusi linavyotakiwa kujilinda na dunia kwa kuwa na vazi safi lisilo na doa kuwa tayari kwa mume wake ambaye ni Kristo siku ya kuja kwake mara ya pili duniani (unyakuo).

Kikristo (hasa wale ambao wameokoka), Bibi harusi huvaa rangi nyeupe kuonesha amejitunza (bikira) na kama amepatikana ni mjamzito basi husubiri hadi azae ndipo afunge harusi yake na mume wake.

Leo hali imekuwa tofauti kwani bibi harusi wote (Christian) huvaa gauni jeupe kwanza kama vazi rasmi la harusi na pili kuonesha furaha, sherehe, hekaheka, shangwe, kutimiza ndoto nk.
Hali imekuwa mbaya zaidi kwani sasa kumetokea wanamitindo mbalimbali (designers) ambao sasa wana design wedding gowns kwa ajili ya bibi harusi mjamzito.

Mwaka 2008 nchini Uingereza kulikuwa na harusi 20,000 za Kikristo ambapo mabibi harusi walikuwa wajawazito siku ya harusi na wote walikuwa chini ya miaka 45 na mara ya kwanza kufunga ndoa.

Kuhusu wachungaji kufungisha ndoa huku wanajua fika bibi harusi ana mimba kubwa ukweli ni kwamba ingekuwa busara kama wangewaacha bibi harusi azae kwanza ndipo wafunge hiyo harusi kwani ni aibu kwa kanisa.

Biblia inakataza mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa na nje ya ndoa; hivyo bibi harusi kuwa na mimba maana yake kuna uzinzi umefanyika na suala hapa si bibi harusi tu bali na bwana harusi ambaye amempa mimba na issue si mimba kwani mimba ni matokeo ya uzinzi.

Ingawa Mungu ni mwaminifu kuweza kusamehe dhambi ya uzinzi hata hivyo ni busara mtoto akazaliwa ndipo wahusika waweze kufunga harusi yao kuliko kufunga harusi huku mwanamke ana tuta kwenye tumbo.
Hii ni kuonesha kwamba kwa sasa duniani uadilifu na hofu ya Mungu imeshuka kwa kiwango cha kutisha.

Je, wale wanaotoa mimba (abort ion) na kuonekana safi machoni pa watu huku bibi harusi akiwa na vazi nyeupe hapo inakuwaje?
Ukweli ni kwamba Wakristo tunahitaji kuwa mfano kwa kuishi kama Biblia inavyosema ndiyo maana ndoa za leo hazidumu kwani wanandoa huingia kwenye ndoa huku wameshadanganya na ndoa yao huwa na msingi wa kudanganya na kutoaminiana maisha yote.

Pia kuna tamaduni ambazo (hata baadhi ya madhehebu ya Kiksristo huruhusu maharusi kupeana mimba ili kuhakikisha kama wana uwezo wa kuzaa ni kama hawataki kusikia eti mke hapati mimba!
Hili ni kinyume na Neno la Mungu.
Na kama tatizo ni mwanaume si atamaliza mabinti wote kanisani na mabinti ndo wataonekana wana matatizo kumbe mzizi wa tatizo ni mwanaume mwenyewe.
Kweli dunia imeisha!
Kwa ujumla this is a rubbish!

Kwa sasa tunahitaji ku-redefine who real Christians are; maana hali ni mbaya na maadili ya kibiblia yanazidi kupotea.
Hata hivyo pamoja na michanganyo yote na takataka zote bado kuna vijana (wa kike na wakiume) ambao huamua kujitunza hadi siku ya kufunga ndoa; naamini kwako ni siku ya furaha na Mungu hujisikia utukufu sana kwao.
Kama ni kijana hujaoa au kuolewa kumbuka kwamba kujitunza hadi siku ya kuolewa ni jambo muhimu sana na lenye utukufu na baraka sana kwa ndoa yako, achana na ushamba wa kujiona eti kuingie kwenye ndoa ukiwa bikira umepitwa na wakati, kumtii Mungu si ushamba wala kupitwa na wakati bali ni kwenda na wakati na kuonesha wewe ni mwenye hekima na busana na kwamba unajali kuhusu future yako.

Friday, January 22, 2010

Wanapenda Ule wa Ndani!

Mapenzi katika ndoa huweza kugawanywa katika sehemu mbili yaani upendo wa ndani (internal) na upendo wa nje (external).

Tunapozungumzia upendo wa ndani tuna maana jinsi tunavyoonesha katika emotions kama vile tendo la ndoa, kuwa pamoja karibu (intimacy), pamoja kimawazo, kujieleza katika feelings, maneno matamu yanayoonesha kujali na kupenda, kupeana busu, kukumbatiana, kupeana zawadi nk.

Tunapozungumzia upendo wa nje huu hujikita zaidi katika huduma (marital duties/responsibilities) kama vile kupika chakula, kuzaa watoto, kujenga au kukarabati nyumba, kufua nguo, kupiga pasi nguo, kuogesha watoto na kazi (ajira) ambazo zinatupa vipato.

Hapo zamani (mababu na mabibi) wao upendo external ulikuwa na maana zaidi kuliko internal na kizazi cha leo ni kinyume chake.

Ndiyo maana ni rahisi sana leo kuishi kama mke na mume zaidi ya miaka miwili na ikafika siku mke au mume akamuuliza mwenzake
“je, unanipenda?”
Hata kama wamefanikiwa kujenga nyumba au kuwa na gari au familia na maisha mazuri kwa ujumla.

Kuuliza je, unanipenda ina maana something is wrong kwenye upendo wa ndani (internal) inawezekana ni tendo la ndoa (love making) au ukaribu kimapenzi (intimacy) au maneno ya kutia moyo na sifa kimoja au vyote havipo sawa.

Leo wanawake wanategemea sana mume alete zawadi (let say flowers) kuliko kuleta mkate.
Mke anataka mwanaume ambaye anaongea maneno matamu na si anayefanya kazi nzuri tu.

Mwanaume kiasili ni bread winner na anapenda mke atambue kwamba kwa kazi anayefanya maana yake anampenda mke na familia sasa baada ya kazi kutwa nzima na kurudi nyumbani na mkate na mke akamuuliza
“Je, Unanipenda?"
Eti kwa sababu asubuhi wakati anaondoka hakuaga kwa busu na hug kwa mwanaume bado ni kitu kinachoshangaza.

Hata hivyo industrial revolution imeleta mabadiliko ambayo wanaume na wanawake wote sasa wanafanya kazi (mchanganyo wa duties na responsibilities za mke na mume) na leo tupo kwenye information society kwa maana kwamba information zina flow ajabu na kila mwanandoa anayaka Mapenzi (romance/intimacy) bila kujali sana kazi anayefanya mwenzake.

Je, siri ya ndoa imara ni ipi?
Siri ya ndoa iliyobarikiwa na imara ni ile inayohakikisha upendo wa ndani (internal) unaenda sawa na ule wa nje (external), ni ile ndoa ambayo inachanganya tendo la ndoa (intimacy) na majukumu (duties) kuwa kitu kimoja na kukipa nafasi sawa.

Mwanandoa halisi ni yule ambaye leo anaweza kumsaidia mwenzake anayeumwa kwa kufuta matapishi yake na baadae akaendelea kumpa kisses za kutosha.

Mke halisi ni yule anayeweza kuwa mama mchana na kuwa mpenzi usiku chumbani na kumfurahia mume wake kimapenzi kwa kwenda mbele.
Ndoa iliyo imara ni ile ambaye wanandoa ni waaminifu katika kutekeleza uhitaji wa ndani na nje katika ndoa.


Thursday, January 21, 2010

You can give without loving,
but you can never love without giving.

Wednesday, January 20, 2010

Yule Mwanaume!

James alikuwa devastated kusikia kwa rafiki yake kwamba mke wake yupo Beach ya Bagamoyo na mwanaume mwingine wakati aliaga kwamba anaenda Morogoro kumsalimia shangazi yake.
Rafiki yake James ambaye anafanya kazi na James ofisi moja alikuwa Bagamoyo kikazi na wakati wa mapunmziko aliamua kwenda beach kupunga upepo na ghafla akamuona mke wa James akiwa na mwanaume mwingine kwenye beach za Bagamoyo katika mazingira ambayo huhitaji kwenda shule ili ujue kuna something going on.
Ndipo akampigia simu James kumuuliza kulikoni mke kuwa Bagamoyo na mwanaume mwingine katika hekaheka za ajabu ajabu ajabu.

Hata rafiki yake James mwenyewe alikuwa huamini kile anakuona kwani alishangazwa na ujasiri wa mke wa James kuangamiza ndoa ya miaka 10 hivi hivi.

James alikuwa haamini kile anaambiwa na rafiki yake kwani ilichukua muda ili aamini kwa kuthibitishiwa ni kweli alikuwa mke wake na kwamba safari ya Morogoro haikuwepo bali ilikuwa ni Bagamoyo.
Swali lililokuwa linamuumiza james kichwa na kumkata tumbo kama kisu lilikuwa:-
“Je, huyo mwanaume ni nani hadi awe na mke wangu?”

Baada ya kurudi nyumbani ni kweli mke wa James alikiri kwamba ni kweli alikuwa na huyo mwanaume na akamsihi sana James mumewe amsamehe na kwamba atakata mawasiliano na huyo mwanaume milele.
"No more contact rule"

Maumivu na hasira alizokuwa nazo James hakuweza kuvumilia na mke wake alijua kwamba kukiri kosa au dhambi yake kutamfanya James amsamehe kirahisi na kuyamaliza kirahisi hata hivyo James alizidi kuwa na mawazo kuhusu "Yule mwanaume" mwingine na akawa hawezi kula wala kulala usingizi.

Alikuwa na mashaka na hofu kubwa kwani mkewe alikuwa ndiye mwenye kipato kikubwa na ilimuumiza sana kwani alijua inawezekana ipo siku huyo mwanaume anaweza kurudiana naye tena.

Mkewe alimuomba msamaha James tena na tena na akafanya hatua kubwa zaidi kwenda kwa Pastor wake (church) kueleza jinsi aulivyosaliti ndoa yake na kukiri kwamba hatarudia tena hata hivyo kwa James bado mawazo yalizidi kumkandamiza.
+++++++++++++

James na mkewe wanawakilisha mamia ya wanandoa duniani ambao hujikuta issues za affair au (EMS) zinawapa hekaheka na maisha ya ndoa kuonekana ni chungu.
Wengi wakifanya kosa hili huamini wakiomba msamaha basi yule amesalitiwa huweza kusamehe kirahisi na mambo yakawa tambarare.
Cha ajabu ni kwamba unaweza kuwa na wewe umewahi kusaliti hata hivyo likija suala la yeye kusaliti inauma na kuwa uchungu usiovumilika.
"Ukweli hakuna anayependa kusalitiwa na yule anayempenda na kumpa moyo na maisha yake".
Anayeomba msamaha huwa hawatambui maumivu makali ambayo hujitokeza baada ya kukiri kosa lake pia haya maumivu ni sehemu ya healing processing ya issue yenyewe.
Hapa tunaona mke wa James ameshindwa kutambua maumivu aliyosababisha kwa mume wake.
Anaamini kuomba msamaha kunaweza kumaliza makosa yake na maumivu ya mumewe kirahisi na haraka na anashangaa kwa nini hasamehe na kusahau.

Hata hivyo James alikuwa mwoga sana na alijisikia insecure kwamba mkewe anaweza kutoweka moja kwa moja na "Yule mwanaume" badala ya kukubali kwamba ni kweli affair imetokea na ajisikie anavyokisikia na kumuuliza mkewe kupata data zote zinazotakiwa na hatua ambayo inaweza kuchukuliwa ili kuzuia tena kitu kama hicho kusitokee.
Ukweli ni kwamba suala la affair huumiza na ni jukumu la kila mwanandoa kumlinda mwenzake au kujilinda yeye mwenyewe kujiingiza katika issue mbaya na hatari kama hii.


Tuesday, January 19, 2010

Kuimarisha Mpambano!

Dafrao! Baada ya kufunga ndoa au baada ya honeymoon baadhi ya wanandoa hujikuta katika mgogoro inaweza kuwa si kupigiana kelele kama walevi bali ile kujisikia umeumizwa baada ya mambo ambayo ulikuwa unategemea (matarajio) kuwa yangekuwa safi yanakuwa tofauti kabisa na matarajio yako.

Hata hivyo migogoro kama hiyo au mshtuko kama huo husababisha kuleta mabadiliko au kubadilika na kukua (mature) na kujuana zaidi ninyi wawili ambao sasa mnaenda kuishi pamoja na kuwa kitu kimoja kimwili, kiakili, kimawazo, kihisia na kiroho kama inawezekana.

Kuna huu msema ambao kwa asilimia 100 nauamini ni kweli
“Conflicts in a new marriage can be a valuable commodity”

Hata hivyo issue hapo ni maneno “can be” kwani mgogoro wowote ukitokea jambo la msingi ni busara na namna au njia inayotumika kutatua

Mara nyingi wanandoa wanashidnwa handling ya migogoro katika ndoa kwa sababu wengi hukwepa badala ya kukubali na kukaa pamoja na kupambana nayo nah ii inatokana na mitazamo kwamba mgogoro wowote ni kitu kibaya sana katika ndoa hasa kama wewe ni mkristo safi.

Wapo wanandoa wanaumia mioyoni mwao hawataki kusema na kuongea na waume zao au wake zao kwa kuogopa kwamba akiweka jambo lake mezani basi wataanza kupigishana kelele hivyo dawa ni kubaki kimya hata hivyo kubaki kimya ni kujimaliza mwenyewe.

Jane alikuwa anajiuliza:-
“Hivi kwa nini tunakuwa na matatizo kati yangu na mume wangu James?”
Uso wake ulikuwa unaonesha maumivu kuliko matumaini.
Aliendelea kusema kwamba
“Kila wakati tunatofautiana katika maamuzi kwa kitu chochote tunajadili; yeye anataka tuuze Friji nyingine na mimi nataka tubaki nayo kwa kuwa tuliyonayo ikiharibika hatutakuwa na backup plan ya kltunza vitu vyetu.
Mimi nataka tupake rangi nyumba yetu sasa, yeye anasema kwa nini tusisubiri mwisho wa mwaka hata sababu hana”

Ukweli ni kwamba Jane na James wote ni binadamu waliozaliwa familia tofauti, malezi tofauti, wazazi tofauti na inawezekana maeneo tofauti kijiografia na wameathiriwa na jamii na tamaduni walizokulia (lelewa).
Binadamu ni tofauti na ina yoyote ya mashine hivyo kutofautiana katika mawazo ni jambo la kawaida.

Migogoro hujitokeza kwa sababu wanandoa huanza kufanana kwani kazi ya ndoa ni kuwafanya wawili wanaopendana kufanana”

Ni kama kuunganisha mito miwili yenye kelele chini ya mlima; kutakuwa na kelele, hekaheka, kububujika, chemka na kufanya povu na kila aina ya msuguano kwani mito miwili inaunganika kufanya mto mmoja strong.
“Marriage is a merger.”

Kutokukubali mgogoro katika ndoa huweza kusababisha mambo mawili:-
Kwanza mgogoro ukijitokeza tu utaamini kwamba “something is wrong” na utaanza kumlaumu (blaming) mwenzako.

Pili utapata mshtuko wa kukatishwa tama (total disappointment) kwa kuwa ulitegemea kwa njinsi unavyompenda na mnavyopendana basi hamuwezi kutofautiana kama wakati mlipokuwa wachumba.

Unajua mgogoro wa kwanza kwenye ndoa unakuwa na disappointment zaidi ya ile ya kuona mende au nywele kwenye chakula nyumbani kwa mama mkwe.
Vinginevyo wanandoa wanaweza kuanza kutoa reaction bila kutumia busara

Mithali 20:3
Ni kwa heshima ya mtu kuepa ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana

Sunday, January 17, 2010

Hatua za kuchukua .... Affair

Hata kwa uchungu na maumivu lazima ngazi uipande! HATUA ZA KUCHUKUA BAADA YA AFFAIR
Ni ukweli ulio wazi na usiopingika suala la mwanandoa kukosa uaminifu (affair, infidelity, Extra Marital Sex (EMS) ni jambo lenye maumivu makali sana kama vile kukata kisu tumboni, linakasirisha.

Hutoa wazo la kwamba hutamwamini tena na huchukua miezi na miaka mingi sana ili kuanza kurudisha upendo na trust kwake upya hata hivyo siku nyingi hata baada ya miaka 20 ikitokea hujui ameenda wapi unaweza kujikuta unaanza kuwaza labda kaanza tena kwani hiyo hali huendelea kukuwinda maisha mengine yote yaliyobakia katika ndoa yako hapa duniani.

Mwanandoa aliyesalitiwa huanza kuwaza kama kweli hii ndoa itaendelea au ndo imefika mwisho kwani ndoa hujengwa kwa trust na EMS hubomoa trust ya ndoa seriously.

Unapoambiwa kwa mara ya kwanza kwamba mume wako au mke wako ana affair basi unajikuta unasongwa na mawazo negative ambayo hupelekea shock kihisia, uchungu, huzuni ya uhakika, ukali, kutoamini kilichotokea na wakati mwingine unaweza kujikuta upo mad (mwehu); hata hivyo hizo feelings ni kitu cha kawaida na una haki ya kujisikia hivyo.

Hii ina maana kama nikulia lia sana, pia utakosa usingizi na hamu ya chakula pia utasongwa na mawazo kuhusu affair hadi kushindwa kufanya concentration ya kuwaza vitu vingine muhimu kama kazi nk (usipokuwa makini na unavyovuka barabara unaweza kugongwa na magari.

Maisha huanza kuongozwa na emotions badala ya wewe kuongoza maisha na unakuwa na hofu kwamba unaweza usiwe mtu mwenye furaha tena maishani.
Inakuwa ngumu sana kuamini kwamba ipo siku utarudi kwenye hali yako ya kawaida.
+++++++++++++++++++++++++
+++++++++++++++++++

Je ni hatua gani zichukuliwe ili kurudi kwenye hali ya kawaida?
Kwanza ni muhimu sana yule ambaye amesalitiwa kuhakikisha anamweleza mhusika vile anajisikia kama ni hasira au maumivu.
Pia anaweza kuuuliza maswali yoyote ili kupata ukweli kuhusu affair ilikuwaje ingawa kuuliza maswali sana huwa na faida na hasara faida ni kwamba utaambiwa ukweli (facts) kuliko kuwa na wasiwasi kutojua affair ilikuwaje.

Hasara ni kwamba unaweza kupewa details ambazo zinaweza kukupa uchungu na hasira zaidi kwani unaweza kuambiwa mambo ambayo yatakufanya utamani kutapika.
Hivyo kabla ya kuuliza jipime kwamba kama una uwezo wa kuvumilia details utakazosikia.

Pili yule ambaye amemsaliti mwenzake anatakiwa kuachana na mwanamke au mwanamke amefanya naye dhambi (affair)
“No more contact rule”
Hakuna mawasiliano kwa kuonana, email, simu, twitter, face book, barua au njia yoyote ya mawasiliano duniani.
Kama anayehusika amegoma hii kanuni basi ni dhahiri hajaacha na ataendelea kumuumiza mwanandoa mwenzake.

Kama mtu wa tatu (affairee) au yule mwanamke au mwanaume ametembea na mwanandoa ataendelea kusumbua kuwasiliana na mwanandoa aliyemsaliti mwenzake inabidi msaliti awasiliane na mwanandoa mwenzake kwamba
“Yule mwanaume au yule mwanamke bado ananisumbua kutaka tuwasiliane
ili kila mmoja ajue namna ya kusaidiana kukata mawasiliano kwani kuendelea kuwasiliana hudhoofisha process za healing.

Tatu, kwa aliyesalitiwa kubali kwamba feelings ulizonazo katika janga hili ni kitu halisi na zinaumiza na ni kitu kigumu.
Huna haja ya Kujikataa na kuamua kupunguza. mawazo, maombolezo, kushuka chini ni vitu vya kawaida.

Nne, uliesalitiwa unaweza kumtafuta mtu unayemwamini ambaye unaamini anaweza kukusaidia ushauri na kukuombea na unatakiwa kuelezea the whole story hata kama inauma.
Lazima uwe makini na mtu unayemuomba ushauri kwani kuna mwingine badala ya kujenga; atakubomoa vipande vipande na kuharibu maisha yako miaka 50 ijayo.

Tano wote wawili (mkosaji na aliyekosewa) kukaa pamoja na kujadili ili kujua sababu ya affair ilikuwa nini, affair ilikuwa na maana gani

Jenga mahusiano upya

Tutaendelea -------------------

Je, Inawezekana?

Je, ndoa inaweza kupona baada ya Affair?”

Jibu ni - Ndiyo inawezekana.
Ni kweli baadhi ya tafiti zinaonesha hata ndoa huweza kuimarika zaidi.
Naomba unielewa sijasema kwamba affair ni jambo zuri kwa ndoa yako kwani matokeo ya mapenzi nje ya ndoa (Affair au Extra Marital Sex – EMS) ni jambo linalosumbua, lenye maumivu mno.
Huweza kuchukua miaka na miaka ili kurudisha tena trust na feelings zilizopotea kutoka na EMS.
==================

Kimsingi wanandoa wengi huamini hawawezi kuvumilia au kushinda baada ya mmoja kuleta hekaheka za EMS, na wapo wanandoa ambao kwa maumivu na kazi nzito yenye uvumilivu na kujitoa hutumia affair iliyopo kupata solution hata ya matatizo mengine yaliyokuwepo katika ndoa yao.
Hata hivyo jambo la msingi ni kwamba wanandoa wote wanahitaji kujitoa na kuwa na willingness ya kusaidiana kuponya maumivu na vidonda vilivyosababishwa na EMS.

Mara nyingi sababu ya EMS huwa si sex bali kukosekana kwa mawasiliano (deep) kati ya wanandoa kwani moja ya hamu kubwa ya sisi binadamu hasa kwenye ndoa ni kitendo cha kujiona mwenzako anakuelewa, kuwa na mtu special anayekupenda, anayekuelewa unavyofikiria, unavyojisikia, anakuona wa maana, anayekuamini na yupo committed na hii ndiyo raha kubwa ya mtu duniani ambayo humfanya mtu aridhike katika hitaji ya kwamba kuna mtu anamuhitaji, anamkubali, anamjali na anampenda.
Ni failure ya kuwa na moments kama hizi ndipo tatizo kubwa hujitokeza.

Ukimuuliza mtu yeyote ambaye ameshawahi kuwa kwenye affair yoyote mara nyingi atakwambia “ lengo halikuwa sex ila nilitaka kuwa karibu (closeness) na mtu, kupata mtu anayenikubali, anayenielewa na kunipenda ili nijisikia vizuri na nilikuwa tayari kutoa kitu chochote ili nitimize hizo feelings.
Aina hii ya hitaji si kitu cha ajabu.
Hitaji la mwingine kukuelewa au mtu anayekuelewa (mwanaume au mwanamke) ni kitu ambacho ni very powerful kuliko tunavyoelewa.

Bottom-line ni kwamba sex bila ukaribu (closeness, intimate) na kuelewana (to be understood) ni sex isiyo na ladha yoyote.
Nina amini kwamba wanandoa ambao wapo karibu kimapenzi (intimate) wana mahusiano mazuri kimapenzi ambapo ndani yake kuna kuelewana na kila mmoja kumkubali mwenzake basi itakuwa ngumu sana kuchepuka.

Saturday, January 16, 2010

Akiridhishwa ndani................

Ukiridhishwa nyumba si rahisi kuchepuka mitaani

Njia sahihi ya mwanaume kuthibitiwa kuchepuka kwa Malaya ni kwa yeye kutekwa na penzi la mke wake.
Mwanaume anatakiwa kunywa maji katika kisima chake mwenyewe au anatakiwa kuridhishwa kimapenzi na mke wake nyumbani kwake.

Swali linaloulizwa na Mithali ni:-
Kwa nini kutuliza kitu ya maji ya kisima cha jirani wakati unacho chako nyumbani?
Au nyumbani maji ni machungu?
Au nyumbani maji hayatulizi kiu?
Au nyumbani maji ni machafu?

Jukumu la kuhakikisha maji ya nyumbani ambayo kwa hiari yako mwanaume umechimba kisima chako yanakuwa ni safi, matamu, yanayomaliza kitu na kukupa ridhiko na ni jukumu la mke na mume wote kwa pamoja.

"Ignoring a wife for another woman is like wasting precious water in your home; it makes no sense at all!"

Kumridhisha mke au mume ni jambo la msingi sana.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanandoa wanaotoka nje ni wale ambao wanapata kidogo au kunyimwa kwenye ndoa zao za ndani hivyo hujikuta wapo insecure kwenye suala la marital sex.

Kimsingi kama hakuna maridhiano kimapenzi katika ndoa maana yake mmoja hatapata feelings anazohitaji kwa mwenzako na matokeo yake huanza kuangalia nje ili kuridhisha hisia zake hata kama lengo si kufanya sex moja kwa moja.

Keeping sex in marriage Extra Special Marital Sex can keep it from being Extra Marital Sex

Mithali 5:18
Chemchemi yako na ibarikiwe na ufurahie mke wa ujana wako.


Friday, January 15, 2010

"The most important thing in life is to learn how to give out love, and to let it come in.”

Ndoto zingine mmmm!

Kama unaamini kuna Mungu basi ni dhahiri unaamini kwamba kuna shetani na malaika zake kama vile mapepo, majini, vinyamkela (hata wazungu wana majini na mapepo yao kama vile pornography)

MAJINI MAHABA NA NDOA
Watu wanaosumbuliwa na majini ya Mahaba huota ndoto wanafanya sex na mtu wasiyemjua kama anayeota ni mwanamke basi mumewe akishtuka atakuta mke wake ana mbegu za kiume sehemu za siri za mke wake ingawa hakufanya naye tendo la ndoa.

Pia mtu mwenye majini mahaba anaweza kuwa na mambo mengine yafuatayo:-
Kwanza uhusiano wa ndoa yaani mke na mume huwa na matatizo na mwanandoa mwenye hayo majini basi hukosa hamu ya tendo la ndoa kwa mkewe au mumewe.

Pili kama ni mwanaume basi anakosa nguvu za kiume na pia sperms zake hushindwa kusafiri hadi kufikia fertilization.
Tatu anakuwa na roho ya kukataliwa kwa maana kwamba mambo yote yanakuwa yayaendi iwe kazini, biashara nk
Nne kama ni mwanamke atakosa siku zake (menstrual cycle) na pia hukosa kushika mimba na huweza kupata fibroids (uvimbe kwenye kizazi).
Kuwa na hizo dalili haina maana ya moja kwa moja kwamba una majini issue je unaota ndoto unafanya mapenzi na mwanaume au mwanamke usiyemjua?

JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO HILI
Kama unasumbuliwa kuota ndoto unafanya mapenzi na mtu usiyemjua pamoja na dalili zingine kama zilivyoorodheshwa hapo juu maana yake unahitaji msaada, kwani majini huwa hayatibiwa kwa medication yoyote, wala X ray yoyote wala operation yoyote wala vipimo vyovyote vya hospitalini bali MAOMBI TU KWA JINA LA YESU.

Kwa msaada zaidi piga simu hii +255 755 850 924 uliza Dada GB

Thursday, January 14, 2010

Yanatoka yenyewe!

SWALI.
Kwa nini maziwa hunitoka wakati sina mimba na sinyonyeshi?
Jibu
Ukweli ni kwamba ili maziwa yazalishwe (breast milk) tendo zima hutawaliwa na pituitary glands (kiswahili sijui).
Kama unatumia dawa zozote (medications), huweza kuathiri kiwango cha homoni zinazozalishwa mwili mwako.
Kama kuna kuongezeka kwa kiwango cha homoni zinazohusika na kutengeneza maziwa (breast milk) basi unaweza kujikuta maziwa yanatoka wakati huna mimba wala hunyonyeshi.
Pia zipo baadhi ya dawa za uzazi wa mpango huudanganya mwili na kupelekea matiti kutoa maziwa wakati hunyonyeshi na wala huna mimba.
Jichunguze kama huna sababu mojawapo nilizotaja hapo juu.
Kama maziwa yanayotoka yana rangi tofauti au yanaonesha si katika hali ya kawaida basi kumuona daktari ni jambo la msingi zaidi na ni muhimu sana Daktari akwambie ni kweli hakuna tatizo lolote au kuna tatizo.

Yule mwanamke!

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA HUUMIZA SANA
Mume wa Jane alipokiri kwamba ni kweli “Nilikuwa na uhusiano na yule mwanamke”.
Jane alipata mshituko ambao hauelezeki ni zaidi ya shock ya umeme.

Kwanza alijiuliza
“Imekuwaje sikuweza kujua dalili kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea na nilikuwa mjinga kiasi gani nisijue;
je, nilikuwa sioni matatizo ya ndoa yangu hadi mume wangu anafikia hatua hiyo, nilikuwa kipofu kiasi gani?
Na huyo mwanamke ametumia mbinu gani hadi kumpata mume wangu nami nisijue?”
Alijiuliza hayo maswali huku machozi yakibubukika kutelemka kwenye mashavu kama mvua za Alnino.

Jane alijikuta yupo katika wimbi kubwa la msongo wa mawazo mazito, hasira na kutojiamini kukaongezeka.
Wakati mwingine alikuwa anafua nguo na ghafla anajikuta anaishiwa pumzi na mapigo ya moyo kubadilika na viganja kuanza kutoa jasho nyembamba kama vile amakutana na simba ghafla.

Wakati mwingine hata kama anatazama TV ili kupoteza mawazo, ikitokea kukawa na program inaonesha affair yoyote ya ndoa basi hujikuta hasira zinampanda na kuzima Tv na kuanza kulia kwa machozi.

Zaidi ya miezi miwili usingizi umeota mabawa na hakuwa na hamu ya chakula na matokeo yake afya yake ikaanza kuzorota na kila mtu akajua Jane anaumwa kwani ule uchangamfu wake na afya yake vinaleta maswali zaidi ya majibu.

Ingawa mume wake alikiri kwamba hawasiliani tena na yule mwanamke, bado Jane alijikuta bado anawaza na kupata picha ya mume wake akiwa anafanya mapenzi ya yule mwanamke na akajikuta anamthibiti mume wake kila movement anayofanya maana haaminiki tena na kitu kidogo tu kilimchukiza mno Jane.
Jane alijitahidi sana asiwaze kuhusu huyo mwanamke hata hivyo alivyokuwa anajitahidi kusahahu ndivyo alivyozidi kukumbuka na kuwaza zaidi na alijikuta mawazo kuhusu huyo mwanamke yanazidi kujirudia na kulata hasira zaidi.

Tukumbuke kwamba ni kweli affair huumiza sana na maumivu yake ni makali kimwili, kiroho na kihisia.
Kukiwa na affair huwezi kukwepa kuwa na msongo mawazo kama ya Jane.
Jambo la msingi ni kwamba Jane si mtu wa hasira za kupigana na kelele kama sisi wengine kwani angekuwa mwingine hapa pasingekalika kabisa.

Msongo wa mawazo huja na mawazo huja kutokana na issue kwamba yule unayemwamini kuliko mtu yeyote duniani anakuwa amekusaliti kirahisi hivyo tena bila wewe kujua.

Wanandoa ambao wanapambana na issue ya affair huwa na kiwango kikubwa cha depression kuliko matatizo mengine ya ndoa.

Ni kweli affair ni dhambi na chukuzo kwa Mungu na ni kitendo kinacholaaniwa kwa nguvu zote hata hivyo hata kama umeumizwa sana jambo la msingi ni kukumbuka kwamba huwezi kujisia hivyo (msongo na mawazo na hasira) milele.
Ukweli ni kwamba kujisikia hivyo upo sahihi na unatakiwa kuweka malengo mapya ya kurudi katika hali yako ya kawaida kitu ambacho naamini ni kigumu sana.
Unatakiwa kuhimili hali uliyonayo ili hayo maumivu na feelings ulizonazo zisikufanye kilema hata ukajiumiza zaidi kama vile kujinyonga au kunywa sumu kwani hapa ndipo utasikia mapenzi yanaua.

Ni muhimu kuchukua hatua Zifuatazo ili kurudi kwenye hali yako ya kawaida;
Jiruhusu mwenyewe kujisikia vile unajisikia, kama ni kulia, lia tena kwa machozi mazito, kama kukasirika basi kasirika na muuliza maswali anayehusika kadri ya unavyotaka ili kujua ukweli. Zaidi jikubali na ukubali kwamba ni kweli yametokea.

Tafuta mtu unayemwamini (mshauri, mchungaji nk) akusaidia kuhimili maumivu na uchungu ulionao kwani kwa kuongea na mtu unayemwamini maumivu huondoka.

Jitoe, jikabidhi (moyo) kwa Mungu.
Yeye peke yake ndiye anajua maumivu.
Mungu ametuahidi kutupa faraja wakati wa dhiki na maumivu hata kama shetani ana mpango wa kuharibu ndoa zetu bado tukiishi katika blueprint ya ndoa kama Mungu anavyotaka tutaishi maisha ya furaha amani na ushindi.
Tutaendelea.....

Wednesday, January 13, 2010

Huona aibu.....

Kwanza lazima nikiri kwamba wanaume wengi hujikuta wanasisimka pale mke wake akiwa hali ya nakedness.
Mungu alituumba sisi wanaume kuitikia kwa kusisimka kwa mwili wa mwanamke akiwa hivyo, na wakati mwingine tunasisimka hata kama sex halikuwa wazo kichwani mwetu yaani mwili huamua kufanya kile ambacho hatujautuma.
Hivyo wanawake wote mlio kwenye ndoa ni vizuri kufahamu kwamba ukiona dalili za kusisimka usifanya conclunsion kwamba lengo la mume wako kuwa hivyo ilikuwa ni kutaka sex.

Pia ni vizuri kama mume kufahamu kwamba wenzetu wanawake hawawezi kusisimka kwa kuona mwanaume upo naked kama sisi wanaume tunavyosisimka kuona wake zetu wapo naked.
Bottom line ni kwamba ni muhimu sana na vizuri sana kwa wanandoa kujifunza kufurahishana (mume na mke) kwa njia ya kuwa uchi (naked/nudity) kwani ni raha kwa mwili na afya ya ubongo.

Kwa nini mke na mume kuwa naked ni suala muhimu?
Kwanza kuwa uchi ni mke na mume tu, hivyo kuwa uchi hujenga aina ya bonding kwani hakuna mtu unaweza kuwa uchi isipokuwa mke na mume, otherwise utakuwa kichaa!
Pia kama lengo ni skin contact huleta raha; basi jinsi ngozi inavyozidi kuwa kubwa kugusana na raha huongezeka maradufu kama mke na mume watakuwa uchi.

Je ni nyakati zipi wanandoa huweza kuwa uchi na kila mmoja kumfurahia mwenzake?
Wakati wa kulala
Wakati wa kuoga
Wakati ambao si kuoga wala kulala bali wawili chumbani (kucheza, kupeana joto nk)

KULALA PAMOJA
Kulala pamoja kama mume na mke ni jambo ambalo lipo kwenye mind zetu na ni jambo muhimu sana.
Suala si kulala kitanda kimoja na kuamka pamoja tu bali kulala pamoja uchi na kuwa na maongezi, kukumbatiana na kujenga ukaribu zaidi.
Utafiti wa karibuni unaonesha kwamba kulala pamoja (uchi) husaidia wanandoa kupeana homoni za pheromones (ambazo hufanya kazi ya kuimarisha bond kati ya mke na mume) hivyo kuwa uchi ni kujipa exposure kubwa ya kupeana pheromones na matokeo yake ni kujisikia mpo closer na more secure kama mume na mke na pia hizi homoni husaidia kujisikia una afya njema kimwili na kiakili.
Kama unajisikia aibu au mwoga kuwa uchi kwa mke wako au mume wako basi kuna tatizo kubwa.

KUOGA PAMOJA
Je, Unakumbuka ni lini ulioga na mume wako au mke wako pamoja?
Je, umeshakumbatiwa wakati wa kuoga?
Umeshawahi kumuogesha mwenzako au wewe kuogeshwa?
Wakati mwingine ukiona mke wako au mume wako anaenda kuoga mpe surprise kwa wewe kuomba muwe wote kwani kuna raha yake.

WAKATI AMBAO SI KUOGA WALA SI KULALA
Hii inaweza kuwa ni wakati kabla ya kulala usiku au asubuhi wakati unataka kuamka au kuondoka kitandani, unaweza kumkumbatia mume au mke kwa dakika kadhaa bila kuongea maneno yoyote, muhimu ni mwili kuwa na total contact na kuwa one flesh.

Wanawake wengi huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba hii inaweza kuwa janja ya mwanaume kutaka sex usiku kabla ya kulala au asubuhi kabla ya kuamka (one for the road) na wanaume huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba mwanamke anaweza akagoma sex baada ya mwanaume kujikuta amesisimka na anahitaji sex.

Suala ambalo husumbua kwa mwanamke na mwanaume ni kwamba mke na mume wakiwa uchi akili ya mwanaume hufikiria sex na akili ya mwanamke hufikiria romance/intimacy na kila mmoja akiona haja yake haijatimizwa hujiona hajaridhika.

Jambo la msingi kwa mwanaume ni kukumbuka kwamba mke wako huhitaji kuguswa mwili wake mara kwa mara na si lazima iwe sex (non-sexual touch) na hii hupelekea yeye kuwa na afya njema katika mwili na emotions zake na kukosa kupokea mguso wa kimwili husababisha asiwe na hamu ya sex.
Mwanamke kukosa ukaribu wa kimapenzi (intimacy/touch) huathiri utendaji wa ubongo wake.

Pia jambo la msingi kwa mwanamke ni kukumbuka kwamba mume wako ana hamu kubwa sana ya sex na ingawa anaweza kuzuia kile angefanya hiyo haiwezi kumsaidia kuzuia anavyojisikia. Anapokuwa amepitiliza muda mrefu bila kutoa nguvu zake kupitia sex, ubongo wake huathirika pia kama wewe mwanamke unapokosa physical touch na ukaribu kutoka kwa mume wako. Hisia zake za kutaka sex si ubinafsi bali ni response ya ubongo wake kutokana na kitendo cha kukosa sex.

Jambo la kukumbuka kwa wote ni kwamba ni muhimu sana kila mmoja kujitoa kwa mwenzake na kumfahamu vizuri mwenzi wako na weka lengo kuhakikisha unatimiza mahitaji yake hata wewe usipotimiziwa mahitaji yako.
Wewe kutokuwa selffish ni baraka kwa mumeo au mkeo na wewe kutimiza mahitaji yake kutafanya na yeye atimize mahitaji yako.

Tukumbuke kwamba kuwa comfortable kuwa uchi kwa mume wako au mke wako ni faida kwako ndani na nje ya kuta za chumba chenu cha kulala.


Saturday, January 9, 2010

Usiingie kizembe!

Mmoja wa wasomaji ya hii blog amelalamika kwamba mwaka 2009 nilikuwa naandika mambo mengi kuhusu ndoa na si masuala ya uchumba; nakubali ni kweli hata hivyo jambo la msingi ni kwamba kuna ushauri mmoja tu muhimu sana kwa yule anatafuta mchumba ili awe mke au mume nao ni kwamba usikimbilie au kuingia haraka bila kuchunguza kwamba huyo unataka kuingia naye kwani ukiingia hakuna haraka ya kutoka kwani ni shimo ambalo kutoka ni hadi kifo.
Kama wewe ni binti au msichana au mwanamke ambaye unatamani kuolewa jambo la msingi ni kuhakikisha umejua tabia (character) kabla ya kuamua kuoana naye.
Na kama wewe ni mvulana au mwanaume ambaye unatamani kuoa jambo la msingi ni kuhakikisha unajua fika tabia ya huyo binti au mwanamke unataka kumuoa.
Kuna mambo mawili muhimu sana ambayo binadamu hufanya uamuzi na uamuzi wake huweza kuathiri maisha yake hapa duniani na maisha yake baada ya kufa, mambo mawili ni wokovu na ndoa.
Ndoa si safari ya majaribio kwamba nikiingia haraka haraka basi hata kutoka nitatoka haraka haraka, usijidanganye!
Adhabu ya kuingia kizembezembe kwenye ndoa ni kuvumilia maisha ya huzuni (sorrow) na maumivu maisha yako yote yaliyobaki duniani na huyo utakaye oana naye.
Kabla ya kuoa au kuolewa tumia muda wa kutosha kutafakari majaribu, matatizo, shida na magumu yote ambayo hutokea kwa wanandoa na kwamba una uhakika mwanaume au mwanamke unayetaka kuingia naye kwenye ndoa ana hizo sifa ya kusaidiana na wewe kuhakikisha ndoa inakuwa kitu cha Baraka kwako.
Jiulize mwenyewe kama mwanamke au binti je, nina uwezo wa kimwanamke (womanhood), stamina na tabia ya kuweza kubeba majukumu ya ndoa kwa uangalifu maisha yako yote ya ndoa?
Na kama ni mvulana au mwanaume jiuliza je, ninao uwezo na tabia ya kuweza kuwa baba wa watoto na kichwa cha nyumba au familia na kuwa mwanaume bora kwa mke wangu maisha yangu yote yaliyobaki duniani na mwanamke naenda kumuoa?
Unaweza kuingia harakaharaka kwenye ndoa kwa kuwa unatamani kuolewa; kumbuka ukiingia kwenye ndoa hakuna kutoa wala hakuna haraka ya kutoka ni hadi kifo kitakapowatenganisha.
Biblia haifundishi kuhusu talaka mahali popote na hakuna mahali Biblia inatoa ruhusa kutoa talaka hata kama ndoa itafika mahali ikaonekana kwamba ni busara wanandoa watenganishwe, hakuna talaka! Ukioa umeoa na ukiolewa umeolewa for life.

Thursday, January 7, 2010

Kuchepuka (2)

Moral standard za ndoa sasa zimeshuka kiasi kwamba
si ajabu tena kuona bibi harusi na vazi la harusi huku ana mimba kubwa! Karibu watu wote wanaokamatwa na suala la kutokuwa waaminifu katika ndoa zao (infidelity/Affair/cheating) hukubali kwamba ni kweli wamekosea na wengine husema ni shetani tu aliwaingia.
Tafiti zinaonesha kwamba katika jamii yoyote duniani asilimia 25 ya wanaume huchepuka nje ya ndoa zao na asilimia 10 ya wanawake hukiri kuchepuka kwenye ndoa zao hii haina maana wanandoa wenzao hujua suala ni kwamba huwa wanakiri kwamba wamewahi kutoka nje ya ndoa zao.

NINI HUSABABISHA WENGI KUCHEPUKA
Kutoridhika na ndoa zao idara zote na kuanza kutafuta mtu wa nje ili kuridhishwa.
Matatizo ya familia.
Wengine hujikuta amempenda mtu mwingine (fall in love).
Kutengana kwa muda mrefu mume na mke inaweza kuwa masomo au kazi nk.
Kushuka kwa kiwango cha kiroho cha wanandoa.
Kuhitaji kuridhishwa zaidi kimapenzi; kuna watu wana libido la ajabu!
Kutafuta Kujiamini na kutambuliwa kwamba yeye ni nani katika jamii ( kama ujinga fulani hivi)
Kuikata kweli ya Neno la Mungu.
Ukaidi na uhuni.
Hitaji la kupendwa baada ya kutelekezwa.
Kuzaliwa mtoto wa kwanza katika ndoa; Feelings za kumpa mume huhamia kwa mtoto na wanandoa hujikuta wapo emotionally distant.
NINI HUSABABISHA WENGI KUGOMA KUCHEPUKA.
Kujitoa (commitment) kwa ndoa na kulinda ahadi na agano (covenant)
Kuaminiana kwa wanandoa (strong trust)
Sababu dini yaani wokovu (uhusiano binafsi wa mwanandoa na Mungu)
Kuogopa matokeo ya kuchepuka kama vile magonjwa (UKIMWI) na crisis zingine.
Kujifahamu na kukomaa kiakili na Kujiamini.
Kupenda mke na watoto na kuwapa heshima iliyotukuka na kuishi kwa mfano kimatendo na kimaneno.
Uadilifu (moral standard)

Wednesday, January 6, 2010

Kuchepuka!

Hili dude nalo linatumika sana kuchepusha watu! Linapokuja suala la ndoa au mahusiano huu usemi wa kingereza usemao “How Far is too Far’ una maana kwamba je, ni namna gani au utajuaje au ni kufanya kitu gani hueleza kwamba hujawa mwaminifu (Infidelity) kwa mke wako au mume wako.
Kujua hujawa mwaminifu (too far ) ni pale kile unafanya au yale unaongea na mwanaume mwingine au mwanamke mwingine huwezi kumwambia mke wako au mume wako.

MFANO
James ni kijana smart sana kazini na nyumbani na kwa sasa anajiona yupo bored nyumbani hasa kutokana na yale yayoaendelea katika maisha na mke Jane.
Hivyo anaamua kutaniana na kujihusisha zaidi na mwanamke anayeitwa Linda ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisini.
Katika kutaniana (socialize) kwao urafiki unazaliwa na wanajikuta wanakuwa muda mwingi pamojana kuvutiana zaidi; sasa iwe lunch, au kinywaji baada ya muda wa kazi James yupo na Linda.

Baada ya siku na miezi kadhaa wanajiona karibu zaidi (physically involved) na James anajikuta anamwambia Linda siri zake za nyumbani na mkewe na Linda naye anamwambia James siri ambazo hajawahi kumwambia mtu yeyote.
Sasa wakikutana wakiwa wawili ni kupeana kisses na hugs kwa kwenda mbele ingawa bado hawajavuliana nguo.
Yote haya yanapotokea James hajamweleza mke wake.

Je, James amekuwa si mwaminifu (infidelity) kwa mke wake? Au kwa ndoa yake?
Je ungekuwa wewe ni James ungemwambia mke wako huo urafiki na mwanamke Linda?
Au ungekuwa ni mwanamke Linda ambaye umeolewa Ungemwambia mume wako urafiki wako na James?

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA NI NINI?
Kukosa uaminifu katika ndoa (infidelity) ni utendaji unaoanzia ndani ya moyo kuvunja trust na ahadi ya ndoa kimwili, kiakili, kimawazo na kihisia na siri zote za ndoa.
Ni kuvunja agano (covenant) na pia ni kumsaliti mwenzi wako.

Je, unaweza kujihusisha na mtu mwingine nje ya ndoa kihisia (feelings and emotions) na ukabaki mwaminifu kwa ndoa yako?

Jibu ni hapana kwani ulipokubali kuoana naye ulikubali kwamba mtakuwa mwili mmoja (one flesh); kuwa mwili mmoja ni pamoja na emotions, feelings, mawazo na maisha yote ya ndoa kwa ujumla.
Unatakiwa kuwa kwa mwenzi wako kimawazo na kimwili.

Uzinzi wa emotions upo serious sawa na ule wa kimwili
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini'.
Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
(Mathayo 5:27-28)

Uzinzi (adultery) ni sehemu ya infidelity ( kukosa uaminifu katika ndoa) infidelity ni kutimiza hitaji la mwili na hisia nje ya ndoa wakati adultery ni sex nje ya ndoa.

Kama ninyi ni wachumba na mmoja si mwaminifu huo unaitwa ni uasherati na ni vizuri kuachana kwani mchumba asiyemwaminifu huja kuwa mwanandoa asiyemwaminifu.

Washauri wa mambo ya ndoa wanafahamu fika kwamba katika matatizo mengi ya wanandoa suala la kukosa uaminifu (infidelity) kawaida ni nusu ya matatizo yote katika ndoa.

Ujue au usijue kwamba kuna kuchepuka (affair/infidelity) imetokea katika ndoa yako ukweli unabaki kwamba matokeo ya mwanandoa mmoja kuchepuka nje ya ndoa yake ni mabaya sana kwa yeye mwenyewe, ndoa yake na huweza kuleta crisis kubwa ya familia na hata jamii kama si taifa.
Fikiria suala la UKIMWI tu kama unaweza muulize Tiger Woods

VITUKO VYA KUCHEPUKA NJE YA NDOA (infidelity)

Kawaida mwanandoa anayechepuka akikamatwa na kupewa talaka mara nyingi hawezi kuoana na yule aliyekamatwa naye.
Hivyo kama upo kwenye affair na mwanaume wa mtu au mke wa mtu kumbuka kwamba hupati point yoyote au kukuongezea uwezekano wa yeye kuoana na wewe ikitokea amepata talaka.

Affair ni dalili (symptoms) za huzuni iliyopo kwa wanandoa na maana yake mmoja anakosa hisia (feelings) sahihi kwa mwenzake na matokeo yake husukumwa kuchepuka nje na akishachepuka huongeza matatizo mengine zaidi ya ndoa kama vile kuchelewa kurudi nyumbani, matumizi ya pesa na magonjwa.

Si sahihi kwamba kuwa na affair ni kupata great sex, kutoka nje ni vibaya kwa sababu ni kweli kwenye ndoa kuna great sex na "we need to spread the word" kwamba kwenye ndoa sex ni tamu zaidi.

Si kweli kwamba mwanandoa anayechepuka hufuata mwanamke mrembo zaidi kuliko aliyekwenye ndoa yake au mwanaume maridadi zaidi kuliko aliye kwenye ndoa yake, wengi huvutwa na feelings zile wanakosa ndani ya ndoa zao.

Affair nyingi zina base kwenye urafiki na kuungana kihisia na sharing ya siri na feelings mbalimbali na wakati mwingine sex huwa si sababu ya kuwa na affair bali urafiki wa karibu kwa jinsia tofauti.

Tamaduni nyingi humwangalia vibaya mwanamke kuliko mwanaume linapokuja suala la mwanandoa kuchepuka nje.

Kubwa zaidi ni kwamba uwezekano wa kutolewa talaka ni pale mwanamke akionekana ametoka nje ya ndoa (cheating) kuliko mwanaume akitoka nje ya ndoa.
Tutaendelea............................

Tuesday, January 5, 2010

Kufuli lake......

Akijua ufunguo wako halisi, kwake ni rahisi mno! Mke mtiriri (sensuous) anafahamu namna ya kumfanya mume wake kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa (seduce) pia ni kweli kwamba mume mtiriri (sensuous) anafahamu namna ya kumfanya mke wake kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa (turned on).

Kitu kinachoshangaza (au bahati mbaya) ni kwamba Malaya (wanaume na wanawake) ndio wanaojua kushawishi (seduce) vizuri linapokuja suala la sex kuliko wanandoa.
(Can we pick a leaf from them?)

Kitu maalumu ni kwamba wanawake wana faida (advantage) kubwa zaidi ya wanaume linapokuja suala kuanzisha romantic encounter yoyote,Kwani ni rahisi mno kutabiri au kukisia, kujua au kufahamu kile kinaweza kumsisimua kimapenzi mwanaume ndani ya hata dakika 5.
Wakati si rahisi wakati mwingine kutabiri ni namna gani unaweza kumfanya mwanamke awe turned on chini ya dakika 5.

Kinachomsisimua mwanamke mwezi huu kimapenzi kinaweza kuwa hakina maana yoyote mwezi unaofuata, ndiyo maana mwanaume mwenye busara ni mbunifu kufahamu nini mke wake anahitaji kimapenzi ili aweze kumridhisha.
Kwa kuwa anasisimka sana akishikwa matiti au kisimi au G-spot, au yeye kuwa juu, au ukimfanyia massage au busu mwili mzima mwezi huu basi na mwezi ujao atasisimka au mwaka mzima ukifanya the same atasisimka; utachanganya mambo!

Wakati mwanaume kusisimka kimapenzi ni sawa na uhusiano wa kufuli na ufunguo wake (padlock and key), kwani ili kufungua kufuli lake lililofungwa (locked) ni rahisi mno kwani anachohitaji mwanamke ni kuwa na ufunguo halisi wa kufuli la mumewe.
Mara nyingi ukitumia kufuli la kuwa naked au half naked mwanaume anakuwa turned on.

Hata hivyo linapokuja suala la mwanamke ukweli ni kwamba kufuli lake ni complex hata kama unao ufunguo halisi wa kufungua hilo kufuli lake, hii haina maana utafungua kirahisi kwani lazima uwe na funguo aina tofauti tofauti kutokana na mood, mazingira nk ili kufungua kufuli hilohilo moja (Too complex)

Hivyo mwanaume mwenye busara hubeba funguo zote ambazo zinahitaji kwa ajili ya kufungua kufuli moja la mwanamke kutokana na siku au mwezi au mazingira au mood (kinyongo).

Hii ina maana mwanaume ili mambo yawe sawa (mwanamke asisimke na kuwa tayari kwa mapenzi) unahitaji kuwa na lundo la funguo (keys) tofauti kufungua kufuli lake moja la mwili wake vinginevyo utakuwa unavunja mlango na kuingia ndani ya nyumba yake na matokeo yake ni yeye kujisikia maumivu au kuwa bored.

Nisikuchoshe; kafanye kazi!

Sunday, January 3, 2010

Kumbuka!

Usione vinaelea, vimeundwa! Je, umawahi kujiuliza ni nini siri ya mahusiano yanayodumu kwa muda mrefu let say miaka nenda rudi na wahsika wakawa na furaha na kicheko bila unafiki?
Tumeanza mwaka 2010 na tunahitaji kuwa na resolutions kwa kila idara ya maisha yetu na mahusiano iwe uchumba au ndoa ni muhimu sana kwani huwezi kukwepa mahusiano labda uwe.......

Mwaka 2010 jitahidi kufanya yafuatayo naamini mahusiano yako yatakuwa imara na yenye afya

Hakikisha unasifia zaidi kuliko kulaumu
Ukiwa na rafiki zako hakikisha unaongea mambo 2 au 3 mazuri kuhusu mpenzi wako au mke wako au mume wako.
Kumbuka kwamba kufanya vitu kila mtu kwa tofauti ni kitu cha kawaida kwani kuna njia nyingi sana za kumenya kiazi au kukunja nguo.

Hakikisha mnakuwa na muda wa pamoja na mpenzi wako.
Kama hujaoa au kuolewa hakikisha unaoana na mwanaume au mwanamke ambaye unapenda kumsikiliza na anavyoongea.
Kumbuka ndoa wakati mwingine ni kitanda cha maua ya waridi na wakati mwingine ni ndoa ni kitanda cha miiba.

Kumbuka zawadi nzuri sana kwa watoto wako ni kumpenda mama yao.
Pia kumbuka kuhakikisha unajihusisha vizuri na kazi ndogondogo za nyumba kama ni mwanaume kama vile kufungua nguo, kusafisha nyumba nk.

Ukiona kuna uwezekana wa kuzipiga kikwelikweli basi hakikisha mnapigana mkiwa uchi! Serious!
Kubali, kutokukubaliana.
Usitamke kabisa neon talaka
Usiende kulala huku umekasirika labda iwe ni saa tisa usiku na umechoka huwezi kufanya chochote.


Mawasiliano mazuri ni ufunguo wa ndoa na mahusiano yako.
Usisahau kusema “Nakupenda”
Uwe na kimbelembele cha kusema “Nimekosa nisamehe’
Hakikisha ndugu (inlaws) wanakaa mbali na ndoa yako

Usilinganisha ndoa yako au mahusiano yako na wengine kwani unachokiona nje haina maana kinaweza kupatikana ndani.

Hakikisha si kitanda kilekile, milalo ileile, chumba kilekile, nyumba ileile, wakati uleule wa kufanya mapenzi na mke wako au mume wako kwani tofauti huleta maana.
Mwisho!
Uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana katika mahusiano, Mungu ndiye mwenye upendo hivyo unavyozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo unavyozidi kuwa na upendo na mtu unayejua kupenda.
Mafanikio ya ndoa yoyote yanauhusiano mkubwa sana na uelewa kuhusu Yesu Kristo ni nani katika maisha yako.
Usipuuze bila Yesu ni zerooo............................

Saturday, January 2, 2010

Ni zawadi si Haki yako!

Tendo la ndoa ni Zawadi siyo Haki
Mungu alitoa sex kama zawadi kwa waliooana.
Ametoa zawadi ya sex ili kutufundisha kuhusu yeye na uhusiano wake na sisi.
Utendaji wa sex ni picha ya muunganiko (sharing) kwa kutoa vyote (vile tulivyo) kwa mwenzako (mke au mume) na pia ni picha ya kumkubali kumpokea mwenzako (wote) kama alivyo kwako.

Kuna faida wazi kabisa kwa uhusiano wa tendo la ndoa kwa mke na mume kama vile afya ya mishipa, kupunguza maumivu, kufanya MP kuwa stable, kupunguza depression (unyonge wa kihisia), kupunguza (stress) msongo wa mawazo na kuongeza kuridhika kwa mahusiano ya ndoa.

Mungu anawapa uhuru wanandoa kunywa na kufurahi raha ya mapenzi kila mmoja kwa mwenzake kama wanandoa, hata hivyo sababu za kiroho na kisayansi haziwezi kutumika kama silaha ya mwanandoa mwingine kumthibiti mwenzake.
Uwezo wa kimapenzi kati ya mke na mume bado ni zawadi ambayo tunatakiwa kupeana bure na kwa kupenda na kwa moyo wa furaha (kutoa na kupokea kila mmoja kwa mwenzake katika ndoa).
Pale mwanandoa mmoja anapokuwa na mtazamo kwamba tendo la ndoa ni haki basi kunakusinyaa kwa aina fulani katika mahusiano huanza kujitokeza.
Mke hawezi kuwa na raha ya mapenzi katika ndoa kama mume atakuwa ni mtu wa kulazimisha na kutaka kwa nguvu kama haki yake (demanding) na pia si raha sana pale mke anapotoa tendo la ndoa kwa sababu anawajibika kutoa hata kama hakuwa tayari.

Tendo la ndoa linaloridhisha (great sex and satisfying sex) ni pale kila mwandoa anakuwa amejiadabisha kutoa kwa uhuru mwili wake kwa mwenzake.
Unapotoa kwa uhuru mwili wako kwa mume au mke wako na kupokea mwili wake kwa uhuru unaipa ndoa kitu sahihi cha asili yake na Mungu hufurahia na kutoa kibali.

Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu, nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu, nimekula sega langu la asali na asali yangu, nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.
(Song of Songs 5:1).

Husisimuliwa zaidi ........

Wanawake wengi huhitaji kusisimuliwa kisimi ili kufika kileleni.
Zaidi ya asilimia 60 ya wanawake lazima wasisimuliwe kisimi ili kuweza kufika kileleni.
Ukweli ni kwamba kuamini kwamba mwanamke anaweza kufika kileleni kwa uume kuwa kwenye uke (intercourse) ni sawa na kuamini kwamba mwanaume anaweza kufika kileleni kwa kuchezea testicles (tafsiri mwenyewe kwa Kiswahili)
Haina haja kuachana na uwezo wa anatomy ya mwili.

Ukweli ni kwamba kisimi (clitoris) ni sensitive sawa na kichwa cha uume (penis) na mara kwa mara kisimi hakiwezi kusisimuliwa tu wakati uume upo kwenye uke.

Hata hivyo jambo la msingi ni kwamba si sahihi kwamba mwanaume anayewahi moja kwa moja kwenda kwenye kisimi na kuanza kazi ataweza kumfikisha mke wake haraka kileleni kwani wanawake huja kwa kila aina ya shapes na sizes kimwili, kihisia hivyo njia sahihi ya kumpatia ni kumuuliza nini anapenda afanyiwe na kisimi chake.

Ni wanawake wachache sana watakubali na kujisikia raha kuchezewa kisimi kabla hawajasisimka sehemu zingine za mwili na anaweza kukwazwa au kuwa turned off.
Kama uume, kisimi hujawa na damu na kudinda baada ya kusisimka hivyo kumgusa kisimi kabla hajasisimka huwa haifurahishi na wakati mwingine huumiza.

Wanawake hupishana sana namna kisimi kinatakiwa kichezewa (stimulated) na pia kitu kikubwa ni kwamba hata aina ya stimulation inayotakiwa hutofautiana kwa namna tofauti kwa tendo moja la ndoa.

Itakuwa msaada mkubwa na furaha au raha kama mke atakuwa anawasiliana na mume wake nini anahitaji huku kufanyiwa kwenye kisimi chake huku wakiendelea na furaha yao ya tendo la ndoa.

Je ni pressure kiasi gani, haraka au polepole kiasi gani anahitaji movement kuwa kwa alama au maneno kila wanandoa wana codes zao za chumbani au kitandani.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Waume zetu nao.......

Alywas; handle with care!Makosa wanaume hufanya wakiwa na wake zao kitandani
HAKUNA KUBUSU
Kuepuka kubusu lips zake na kwenda moja kwa moja kwenye erogenous zones zake unafanya ajisikie ni kama malaya anayelipwa kwa saa kile mnafanya.
Kumpa passionate kiss ya uhakika ni moja ya essentials za great sex kwa mume na mke.

KUVUTA MATITI
Wanaume wengi wanapokuwa kitandani na wake zao ile kukabidhiwa mwili tu hurukia kwenye matiti na kuanza kuyabonyeza kama vile anapima watermelons kama zimeiva.
Matiti huchezewa kwa ulaini, so caress and smooth them.
KUUMA CHUCHU
Si ustaarabu kuuma chuchu kama vile unataka kung’oa matiti yote na kuondoka nayo badala ya raha inakuwa karaha.
Chuchu zipo sensitive mno na haziwezi kuhimili kitendo cha kung’atwa.
Kwa nini usizimung’unye na kuzilamba kwa upole na kuzungusha ulimi wako kwa ustadi huku ukimpa raha yake?
KUKOMALIA UKE NA MATITI TU.
Mke ana mwili ambao ni kiwanja kikubwa sana ambacho unahitaji kucheza.
Kwa nini ukimbilie moja kwa moja kwa matiti na chini wakati kuna uwanja mkubwa wa kumchezea.
Kumbuka mwili wa mwanamke kama ulivyo ni one single sex organ.
UZAZI WA MPANGO NI JUKUMU LA WOTE
Tabia ya kumwachia mke mess ya Life style utilities (condom) uliyovaa wewe na kuitumia wewe si sahihi kama unaivaa, store it, use it and dispose it, wewe na si yeye, kwa nini umwachie kama zawadi wakati si zawadi.
Si hutaki kuzaa watoto 35 basi na wewe wajibika!
KUVAMIA KISIMI
Kuvamia na kugandamiza kwa nguvu au kubonyeza kwa nguvu (direct presure) huumiza ama sivyo muulize mke wako anajisikiaje kwani wanawake nao huja kwa size tofauti, namna tofauti, maumbo tofauti, kelele tofauti, wembamba tofauti, ufupi na urefu tofauti, rangi tofauti na mahitaji ya kitandani tofauti
KUJIPA MAPUMZIKA GHAFLA
Wanawake tofauti na wanaume hawawezi kurudi kwenye hali ya kwanza wakiachwa solemba, kama ukisimama wao hurudi square one ghafla.
Hivyo ukianza mziki lazima uhakikisha unaendelea kwa gharama zote.
KUMVUA NGUO KAMA VITA
Hakuna mwanamke anapenda kuonekana stupid, unamvua nguo kwa vita hadi inakwamba shingoni kwa dakika 10 ni kumfanya aonekane stupid, mvue nguo sawa na unavyofungua zawadi special siyo kama unavyofungua toy la mtoto wako.
KUCHANGANYIKIWA NA UKE.
Ingawa wanaume wengi wanaweza kufahamu kisimi kipo wapi kwenye uke wa mwanamke bila ramani, bado mtazamo wao kuhusu uke unashangaza, haichukui sekunde baada ya kupewa mwili kupeleka mkono pale chini na kuanza kuchachafya mkono kama anaiba noti mpya za bank kupitia chimney ya nyumba.
Ni kweli lazima uhangaike kuhakikisha mke wako yupo aroused hata hivyo kuwa mwangalifu bila kumuumiza ni jambo la busara zaidi.
Pia ni vizuri kujihusisha zaidi na kisimi chake na maeneo ya nje kidogo kabla ya kuingia ndani zaidi na pia kuwa na mawasiliano naye kuuliza anajisikiaje.
MASSAGE JEURI
Eti unataka kumpa sensual and relaxing massage ili kumuweka kwenye mood kwa kutumia magoti na kiwiko! Kwa kutumia viganja vya mikono na vidole it is okey na si vinginevyo.

KUMVUA NGUO MAPEMA
Yaani hata hajaonesha move yoyote tayari unaanza kumvua nguo zote, huo ni uhuni
Au hata hamjafika popote mwanaume umeshatoa nguo zote na kujiweka tayari tayari, wewe unataka uogopwe kama njaa.
KWENDA HARAKA
Ukishaambiwa yupo tayari sasa unaweza kuingia kwako ni vita una pump kama industral power tool, si muda mrefu atajisikia yupo kwenye assembly line inayotumie technologia ya mwaka 47. nenda polepole, safi na kwa utaratibu.
Haraka zako zinakufanya mara umgonge na kiwiko au magoti kwenye tumbo lake lain na maumivi ni zaidi ya teke la punda.

KUMALIZA HARAKA AU KUCHELEWA SANA
Hapa ndipo kwenye hofu kubwa ya wanaume wengi, kama ukishuti kabla ya kuona macho yake kugeuka na kuwa blue umechemka!
Otherwise uwe na backup plan B kuhakikisha anaendelea kupata raha hadi awe na macho ya blue.
Kama unadhani kumpigisha gwaride zaidi ya saa moja bila kufika kileleni wewe ni shujaa, kwake pia ni stress kwani ni aina gani ya uke zaidi ya saa hakuna kitu.
Lazima ujue kusoma ramani, majira na nyakati kwani too much is harmful.

Zipo adha nyingi wanawake hukutana na hekaheka za wanaume kitandani naamini kwa leo inatosha!