"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, January 16, 2010

Akiridhishwa ndani................

Ukiridhishwa nyumba si rahisi kuchepuka mitaani

Njia sahihi ya mwanaume kuthibitiwa kuchepuka kwa Malaya ni kwa yeye kutekwa na penzi la mke wake.
Mwanaume anatakiwa kunywa maji katika kisima chake mwenyewe au anatakiwa kuridhishwa kimapenzi na mke wake nyumbani kwake.

Swali linaloulizwa na Mithali ni:-
Kwa nini kutuliza kitu ya maji ya kisima cha jirani wakati unacho chako nyumbani?
Au nyumbani maji ni machungu?
Au nyumbani maji hayatulizi kiu?
Au nyumbani maji ni machafu?

Jukumu la kuhakikisha maji ya nyumbani ambayo kwa hiari yako mwanaume umechimba kisima chako yanakuwa ni safi, matamu, yanayomaliza kitu na kukupa ridhiko na ni jukumu la mke na mume wote kwa pamoja.

"Ignoring a wife for another woman is like wasting precious water in your home; it makes no sense at all!"

Kumridhisha mke au mume ni jambo la msingi sana.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanandoa wanaotoka nje ni wale ambao wanapata kidogo au kunyimwa kwenye ndoa zao za ndani hivyo hujikuta wapo insecure kwenye suala la marital sex.

Kimsingi kama hakuna maridhiano kimapenzi katika ndoa maana yake mmoja hatapata feelings anazohitaji kwa mwenzako na matokeo yake huanza kuangalia nje ili kuridhisha hisia zake hata kama lengo si kufanya sex moja kwa moja.

Keeping sex in marriage Extra Special Marital Sex can keep it from being Extra Marital Sex

Mithali 5:18
Chemchemi yako na ibarikiwe na ufurahie mke wa ujana wako.


No comments: