"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, January 13, 2010

Huona aibu.....

Kwanza lazima nikiri kwamba wanaume wengi hujikuta wanasisimka pale mke wake akiwa hali ya nakedness.
Mungu alituumba sisi wanaume kuitikia kwa kusisimka kwa mwili wa mwanamke akiwa hivyo, na wakati mwingine tunasisimka hata kama sex halikuwa wazo kichwani mwetu yaani mwili huamua kufanya kile ambacho hatujautuma.
Hivyo wanawake wote mlio kwenye ndoa ni vizuri kufahamu kwamba ukiona dalili za kusisimka usifanya conclunsion kwamba lengo la mume wako kuwa hivyo ilikuwa ni kutaka sex.

Pia ni vizuri kama mume kufahamu kwamba wenzetu wanawake hawawezi kusisimka kwa kuona mwanaume upo naked kama sisi wanaume tunavyosisimka kuona wake zetu wapo naked.
Bottom line ni kwamba ni muhimu sana na vizuri sana kwa wanandoa kujifunza kufurahishana (mume na mke) kwa njia ya kuwa uchi (naked/nudity) kwani ni raha kwa mwili na afya ya ubongo.

Kwa nini mke na mume kuwa naked ni suala muhimu?
Kwanza kuwa uchi ni mke na mume tu, hivyo kuwa uchi hujenga aina ya bonding kwani hakuna mtu unaweza kuwa uchi isipokuwa mke na mume, otherwise utakuwa kichaa!
Pia kama lengo ni skin contact huleta raha; basi jinsi ngozi inavyozidi kuwa kubwa kugusana na raha huongezeka maradufu kama mke na mume watakuwa uchi.

Je ni nyakati zipi wanandoa huweza kuwa uchi na kila mmoja kumfurahia mwenzake?
Wakati wa kulala
Wakati wa kuoga
Wakati ambao si kuoga wala kulala bali wawili chumbani (kucheza, kupeana joto nk)

KULALA PAMOJA
Kulala pamoja kama mume na mke ni jambo ambalo lipo kwenye mind zetu na ni jambo muhimu sana.
Suala si kulala kitanda kimoja na kuamka pamoja tu bali kulala pamoja uchi na kuwa na maongezi, kukumbatiana na kujenga ukaribu zaidi.
Utafiti wa karibuni unaonesha kwamba kulala pamoja (uchi) husaidia wanandoa kupeana homoni za pheromones (ambazo hufanya kazi ya kuimarisha bond kati ya mke na mume) hivyo kuwa uchi ni kujipa exposure kubwa ya kupeana pheromones na matokeo yake ni kujisikia mpo closer na more secure kama mume na mke na pia hizi homoni husaidia kujisikia una afya njema kimwili na kiakili.
Kama unajisikia aibu au mwoga kuwa uchi kwa mke wako au mume wako basi kuna tatizo kubwa.

KUOGA PAMOJA
Je, Unakumbuka ni lini ulioga na mume wako au mke wako pamoja?
Je, umeshakumbatiwa wakati wa kuoga?
Umeshawahi kumuogesha mwenzako au wewe kuogeshwa?
Wakati mwingine ukiona mke wako au mume wako anaenda kuoga mpe surprise kwa wewe kuomba muwe wote kwani kuna raha yake.

WAKATI AMBAO SI KUOGA WALA SI KULALA
Hii inaweza kuwa ni wakati kabla ya kulala usiku au asubuhi wakati unataka kuamka au kuondoka kitandani, unaweza kumkumbatia mume au mke kwa dakika kadhaa bila kuongea maneno yoyote, muhimu ni mwili kuwa na total contact na kuwa one flesh.

Wanawake wengi huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba hii inaweza kuwa janja ya mwanaume kutaka sex usiku kabla ya kulala au asubuhi kabla ya kuamka (one for the road) na wanaume huogopa sana hii kwa kuhofia kwamba mwanamke anaweza akagoma sex baada ya mwanaume kujikuta amesisimka na anahitaji sex.

Suala ambalo husumbua kwa mwanamke na mwanaume ni kwamba mke na mume wakiwa uchi akili ya mwanaume hufikiria sex na akili ya mwanamke hufikiria romance/intimacy na kila mmoja akiona haja yake haijatimizwa hujiona hajaridhika.

Jambo la msingi kwa mwanaume ni kukumbuka kwamba mke wako huhitaji kuguswa mwili wake mara kwa mara na si lazima iwe sex (non-sexual touch) na hii hupelekea yeye kuwa na afya njema katika mwili na emotions zake na kukosa kupokea mguso wa kimwili husababisha asiwe na hamu ya sex.
Mwanamke kukosa ukaribu wa kimapenzi (intimacy/touch) huathiri utendaji wa ubongo wake.

Pia jambo la msingi kwa mwanamke ni kukumbuka kwamba mume wako ana hamu kubwa sana ya sex na ingawa anaweza kuzuia kile angefanya hiyo haiwezi kumsaidia kuzuia anavyojisikia. Anapokuwa amepitiliza muda mrefu bila kutoa nguvu zake kupitia sex, ubongo wake huathirika pia kama wewe mwanamke unapokosa physical touch na ukaribu kutoka kwa mume wako. Hisia zake za kutaka sex si ubinafsi bali ni response ya ubongo wake kutokana na kitendo cha kukosa sex.

Jambo la kukumbuka kwa wote ni kwamba ni muhimu sana kila mmoja kujitoa kwa mwenzake na kumfahamu vizuri mwenzi wako na weka lengo kuhakikisha unatimiza mahitaji yake hata wewe usipotimiziwa mahitaji yako.
Wewe kutokuwa selffish ni baraka kwa mumeo au mkeo na wewe kutimiza mahitaji yake kutafanya na yeye atimize mahitaji yako.

Tukumbuke kwamba kuwa comfortable kuwa uchi kwa mume wako au mke wako ni faida kwako ndani na nje ya kuta za chumba chenu cha kulala.


4 comments:

Anonymous said...

Wooooooow!
Una uwezo mkubwa sana wa kufikiri kuhusu ndoa zetu hicho nikpaji ambacho Mungu amekupatia leo umenena vema yaani Baba Karen haya unayoongea watu wangekuwa wanatekeleza sidhani kama hata mahakamani watu wangefika au ndoa kuvunjika eti nimenyimwa tendo la ndoa.Kikubwa kuliko yote ambayo unaongeaga (Kibenam hiyo ga) ni kukaa chini wana ndoa na kujadiliana kuhusu mambo yenu yahusuyo ndoa yenu yaani hili ulinena jamani hapo nyuma ni muhimu sana nimegundua kama unapenda mumeo au mkeo akufanyie hv ongea mwambie express u'r self woow!
Kitu kingine watu tungekuwa tunaona aibu kiasi hicho maambukizo ya ukimwi yangepungua kwa kiasi kikubwa sana, maana utakuta mtu anamuonea aibu mumewe ndani lakini utasikia ana mahawala si chini ya wawili kweli huyo ni aibu au?

Mapendo daima!

Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P.

Mungu akubariki sana kwa ujumbe wako pia kwa mawazo mazuri naamini Mungu amekubariki sana na amebarikiwa mwanaume ambaye wewe ni mke wake.

Upendo daima!

Anonymous said...

mh haya mambo kaka yanakuna kweli,haka ka hofu ka sisi wanawake asubuhi ni kweli huwa tunako hasa ukizingatia wanawake hawapendi tendo la ndoa asubuhi,basi huwa mnatulazimisha,hivyo linapokuja suala la kukumbatiwa unajua tu bwana mkubwa anataka game,hivyo unajiwahisha kuamka mapema.

Anonymous said...

Good