"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, January 9, 2010

Usiingie kizembe!

Mmoja wa wasomaji ya hii blog amelalamika kwamba mwaka 2009 nilikuwa naandika mambo mengi kuhusu ndoa na si masuala ya uchumba; nakubali ni kweli hata hivyo jambo la msingi ni kwamba kuna ushauri mmoja tu muhimu sana kwa yule anatafuta mchumba ili awe mke au mume nao ni kwamba usikimbilie au kuingia haraka bila kuchunguza kwamba huyo unataka kuingia naye kwani ukiingia hakuna haraka ya kutoka kwani ni shimo ambalo kutoka ni hadi kifo.
Kama wewe ni binti au msichana au mwanamke ambaye unatamani kuolewa jambo la msingi ni kuhakikisha umejua tabia (character) kabla ya kuamua kuoana naye.
Na kama wewe ni mvulana au mwanaume ambaye unatamani kuoa jambo la msingi ni kuhakikisha unajua fika tabia ya huyo binti au mwanamke unataka kumuoa.
Kuna mambo mawili muhimu sana ambayo binadamu hufanya uamuzi na uamuzi wake huweza kuathiri maisha yake hapa duniani na maisha yake baada ya kufa, mambo mawili ni wokovu na ndoa.
Ndoa si safari ya majaribio kwamba nikiingia haraka haraka basi hata kutoka nitatoka haraka haraka, usijidanganye!
Adhabu ya kuingia kizembezembe kwenye ndoa ni kuvumilia maisha ya huzuni (sorrow) na maumivu maisha yako yote yaliyobaki duniani na huyo utakaye oana naye.
Kabla ya kuoa au kuolewa tumia muda wa kutosha kutafakari majaribu, matatizo, shida na magumu yote ambayo hutokea kwa wanandoa na kwamba una uhakika mwanaume au mwanamke unayetaka kuingia naye kwenye ndoa ana hizo sifa ya kusaidiana na wewe kuhakikisha ndoa inakuwa kitu cha Baraka kwako.
Jiulize mwenyewe kama mwanamke au binti je, nina uwezo wa kimwanamke (womanhood), stamina na tabia ya kuweza kubeba majukumu ya ndoa kwa uangalifu maisha yako yote ya ndoa?
Na kama ni mvulana au mwanaume jiuliza je, ninao uwezo na tabia ya kuweza kuwa baba wa watoto na kichwa cha nyumba au familia na kuwa mwanaume bora kwa mke wangu maisha yangu yote yaliyobaki duniani na mwanamke naenda kumuoa?
Unaweza kuingia harakaharaka kwenye ndoa kwa kuwa unatamani kuolewa; kumbuka ukiingia kwenye ndoa hakuna kutoa wala hakuna haraka ya kutoka ni hadi kifo kitakapowatenganisha.
Biblia haifundishi kuhusu talaka mahali popote na hakuna mahali Biblia inatoa ruhusa kutoa talaka hata kama ndoa itafika mahali ikaonekana kwamba ni busara wanandoa watenganishwe, hakuna talaka! Ukioa umeoa na ukiolewa umeolewa for life.

2 comments:

Anonymous said...

Bwana asifiwe kaka nashukuru kwakuwa umenijibu maombi yangu kuhusu somo la uchumba.Na pia nashukuru kwa ushauri wako kuhusu ombi langu.Katka ushauri wako umeniuliza kwamba je tukikutana huwa tunazungumzia nini na je tumewahi kuzungumzia habari hizi.Ukweli ni huu mimi na huyu kaka tumekuwa marafiki wa karibu sana kwa mda mrefu na kila mmoja anamjua mwenzake kitabia.Hata wakati mwingine tukiwa katka mazungumzo yanayohusu ndoa au uchumba yeye huwa anajaribu kama kusema jambo lakini anaishia kucheka na kusema tutasemaga na kujaribu kuniuliza nini malengo yangu ya maisha na kujaribu kunipa kama ushauri nk.Kwa ujumla tunapatana sana zaidi wote tunampenda sana yesu.Ushauri wako ni mzuri tena ni wabusara kwa mtu anayependa kwenda mbinguni.Nitaufanyia kazi hata baada yamafanikio nitakutaarifu.ubarikiwe.Ek

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Hongera sana kwa ujumbe wako.

Ni jambo la msingi kwamba wewe na mpendwa wako mnampenda Yesu kwani hilo ndilo jambo la msingi sana duniani.

Je, anakuweka kwenye maongezi yake kuhusu future kama elimu, kazi, wazazi wako na wazazi wake, ndugu zake na ndugu zako (Je, anapoongelea future wewe upo included?)
Kama anakuweka kwenye future yake basi amevutiwa na wewe kuwa mke wake hapo baadae, vinginevyo inabidi uwe makini na Kumuomba Mungu ili akupe kibali kwani Mungu ni mwaminifu na hutimiza ahadi zake kwetu.
Umesema mnajuana tabia kiasi cha kutosha naamini hilo ni jambo la msingi sana jambo la msingi ni wewe kuendelea kumuomba Mungu kama kweli huyu kijana ni kwa ajili yako basi na iwe hivyo kwani Mungu akisema NDIYO inakuwa NDIYO na akisema HAPANA inakuwa HAPANA.
Jambo la msingi wasiliana naye vizuri kwa hekima na busara baada ya kuwa umeomba na kupata kibali mbele za Bwana na muulize kama kweli urafiki wenu una maana yoyote linapokuja suala la uchumba au kuoana kwani unaweza kuwa wewe upo serious kumbe mwenzako yupo kawaida tu na ameshawekeza sehemu nyingine kwako ni kuongea tu, kumbuka mwanaume na mwanamke huwasiliana tofauti na huongea tofauti hivyo usizunguke sana badala yake uwe logical na ongea naye bayana kama ana mchumba au la maaana umempenda.

Mwisho, jiamini na shukuru Mungu kwa kila jambo kwani yote yanayotokea katika maisha yetu ni Mungu anayepanga na usilazimishe. Mungu anampango na makusudi (plan and purpose) na maisha yako hivyo uwe na furaha siku zote.

Ubarfikiwe na Bwana