"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, January 17, 2010

Je, Inawezekana?

Je, ndoa inaweza kupona baada ya Affair?”

Jibu ni - Ndiyo inawezekana.
Ni kweli baadhi ya tafiti zinaonesha hata ndoa huweza kuimarika zaidi.
Naomba unielewa sijasema kwamba affair ni jambo zuri kwa ndoa yako kwani matokeo ya mapenzi nje ya ndoa (Affair au Extra Marital Sex – EMS) ni jambo linalosumbua, lenye maumivu mno.
Huweza kuchukua miaka na miaka ili kurudisha tena trust na feelings zilizopotea kutoka na EMS.
==================

Kimsingi wanandoa wengi huamini hawawezi kuvumilia au kushinda baada ya mmoja kuleta hekaheka za EMS, na wapo wanandoa ambao kwa maumivu na kazi nzito yenye uvumilivu na kujitoa hutumia affair iliyopo kupata solution hata ya matatizo mengine yaliyokuwepo katika ndoa yao.
Hata hivyo jambo la msingi ni kwamba wanandoa wote wanahitaji kujitoa na kuwa na willingness ya kusaidiana kuponya maumivu na vidonda vilivyosababishwa na EMS.

Mara nyingi sababu ya EMS huwa si sex bali kukosekana kwa mawasiliano (deep) kati ya wanandoa kwani moja ya hamu kubwa ya sisi binadamu hasa kwenye ndoa ni kitendo cha kujiona mwenzako anakuelewa, kuwa na mtu special anayekupenda, anayekuelewa unavyofikiria, unavyojisikia, anakuona wa maana, anayekuamini na yupo committed na hii ndiyo raha kubwa ya mtu duniani ambayo humfanya mtu aridhike katika hitaji ya kwamba kuna mtu anamuhitaji, anamkubali, anamjali na anampenda.
Ni failure ya kuwa na moments kama hizi ndipo tatizo kubwa hujitokeza.

Ukimuuliza mtu yeyote ambaye ameshawahi kuwa kwenye affair yoyote mara nyingi atakwambia “ lengo halikuwa sex ila nilitaka kuwa karibu (closeness) na mtu, kupata mtu anayenikubali, anayenielewa na kunipenda ili nijisikia vizuri na nilikuwa tayari kutoa kitu chochote ili nitimize hizo feelings.
Aina hii ya hitaji si kitu cha ajabu.
Hitaji la mwingine kukuelewa au mtu anayekuelewa (mwanaume au mwanamke) ni kitu ambacho ni very powerful kuliko tunavyoelewa.

Bottom-line ni kwamba sex bila ukaribu (closeness, intimate) na kuelewana (to be understood) ni sex isiyo na ladha yoyote.
Nina amini kwamba wanandoa ambao wapo karibu kimapenzi (intimate) wana mahusiano mazuri kimapenzi ambapo ndani yake kuna kuelewana na kila mmoja kumkubali mwenzake basi itakuwa ngumu sana kuchepuka.

No comments: