"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, January 7, 2010

Kuchepuka (2)

Moral standard za ndoa sasa zimeshuka kiasi kwamba
si ajabu tena kuona bibi harusi na vazi la harusi huku ana mimba kubwa! Karibu watu wote wanaokamatwa na suala la kutokuwa waaminifu katika ndoa zao (infidelity/Affair/cheating) hukubali kwamba ni kweli wamekosea na wengine husema ni shetani tu aliwaingia.
Tafiti zinaonesha kwamba katika jamii yoyote duniani asilimia 25 ya wanaume huchepuka nje ya ndoa zao na asilimia 10 ya wanawake hukiri kuchepuka kwenye ndoa zao hii haina maana wanandoa wenzao hujua suala ni kwamba huwa wanakiri kwamba wamewahi kutoka nje ya ndoa zao.

NINI HUSABABISHA WENGI KUCHEPUKA
Kutoridhika na ndoa zao idara zote na kuanza kutafuta mtu wa nje ili kuridhishwa.
Matatizo ya familia.
Wengine hujikuta amempenda mtu mwingine (fall in love).
Kutengana kwa muda mrefu mume na mke inaweza kuwa masomo au kazi nk.
Kushuka kwa kiwango cha kiroho cha wanandoa.
Kuhitaji kuridhishwa zaidi kimapenzi; kuna watu wana libido la ajabu!
Kutafuta Kujiamini na kutambuliwa kwamba yeye ni nani katika jamii ( kama ujinga fulani hivi)
Kuikata kweli ya Neno la Mungu.
Ukaidi na uhuni.
Hitaji la kupendwa baada ya kutelekezwa.
Kuzaliwa mtoto wa kwanza katika ndoa; Feelings za kumpa mume huhamia kwa mtoto na wanandoa hujikuta wapo emotionally distant.
NINI HUSABABISHA WENGI KUGOMA KUCHEPUKA.
Kujitoa (commitment) kwa ndoa na kulinda ahadi na agano (covenant)
Kuaminiana kwa wanandoa (strong trust)
Sababu dini yaani wokovu (uhusiano binafsi wa mwanandoa na Mungu)
Kuogopa matokeo ya kuchepuka kama vile magonjwa (UKIMWI) na crisis zingine.
Kujifahamu na kukomaa kiakili na Kujiamini.
Kupenda mke na watoto na kuwapa heshima iliyotukuka na kuishi kwa mfano kimatendo na kimaneno.
Uadilifu (moral standard)

2 comments:

Anonymous said...

Habari!

Pole na masomo!
Bado kaka Mbilinyi nakudai kuvaa gaun jeupe la harusi maana yake ni nini hasa maana kama huyo na hilo tumbo halafu kaavaa white nielewavyo mimi ni kuwa wewe ni bikira ndio maana unavaa white sasa mbona wanavaa wajawazito?

mamaP!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Heri ya mwaka mpya!

Nakutakia mwaka mpya wenye afya, furaha na amani.
Nilijua tu nimekuchokoza kwani nilipokuwa naitafakari hiyo picha nikawa natafakari lileee swali lako, hata hivyo swali lako nimeshaliandalia majibu yake si muda mrefu nitatoa majibu yake kwani swali si vazi jeupe tu au kuwa bikira tu bali historia nzima ya kuvaa vazi jeupe wakati wa harusi na maana yake kwa ujumla na nini kitu cha msingi kuzingatia kuvaa kwa maharusi.

Upendo daima!