"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, January 6, 2010

Kuchepuka!

Hili dude nalo linatumika sana kuchepusha watu! Linapokuja suala la ndoa au mahusiano huu usemi wa kingereza usemao “How Far is too Far’ una maana kwamba je, ni namna gani au utajuaje au ni kufanya kitu gani hueleza kwamba hujawa mwaminifu (Infidelity) kwa mke wako au mume wako.
Kujua hujawa mwaminifu (too far ) ni pale kile unafanya au yale unaongea na mwanaume mwingine au mwanamke mwingine huwezi kumwambia mke wako au mume wako.

MFANO
James ni kijana smart sana kazini na nyumbani na kwa sasa anajiona yupo bored nyumbani hasa kutokana na yale yayoaendelea katika maisha na mke Jane.
Hivyo anaamua kutaniana na kujihusisha zaidi na mwanamke anayeitwa Linda ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisini.
Katika kutaniana (socialize) kwao urafiki unazaliwa na wanajikuta wanakuwa muda mwingi pamojana kuvutiana zaidi; sasa iwe lunch, au kinywaji baada ya muda wa kazi James yupo na Linda.

Baada ya siku na miezi kadhaa wanajiona karibu zaidi (physically involved) na James anajikuta anamwambia Linda siri zake za nyumbani na mkewe na Linda naye anamwambia James siri ambazo hajawahi kumwambia mtu yeyote.
Sasa wakikutana wakiwa wawili ni kupeana kisses na hugs kwa kwenda mbele ingawa bado hawajavuliana nguo.
Yote haya yanapotokea James hajamweleza mke wake.

Je, James amekuwa si mwaminifu (infidelity) kwa mke wake? Au kwa ndoa yake?
Je ungekuwa wewe ni James ungemwambia mke wako huo urafiki na mwanamke Linda?
Au ungekuwa ni mwanamke Linda ambaye umeolewa Ungemwambia mume wako urafiki wako na James?

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA NI NINI?
Kukosa uaminifu katika ndoa (infidelity) ni utendaji unaoanzia ndani ya moyo kuvunja trust na ahadi ya ndoa kimwili, kiakili, kimawazo na kihisia na siri zote za ndoa.
Ni kuvunja agano (covenant) na pia ni kumsaliti mwenzi wako.

Je, unaweza kujihusisha na mtu mwingine nje ya ndoa kihisia (feelings and emotions) na ukabaki mwaminifu kwa ndoa yako?

Jibu ni hapana kwani ulipokubali kuoana naye ulikubali kwamba mtakuwa mwili mmoja (one flesh); kuwa mwili mmoja ni pamoja na emotions, feelings, mawazo na maisha yote ya ndoa kwa ujumla.
Unatakiwa kuwa kwa mwenzi wako kimawazo na kimwili.

Uzinzi wa emotions upo serious sawa na ule wa kimwili
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini'.
Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
(Mathayo 5:27-28)

Uzinzi (adultery) ni sehemu ya infidelity ( kukosa uaminifu katika ndoa) infidelity ni kutimiza hitaji la mwili na hisia nje ya ndoa wakati adultery ni sex nje ya ndoa.

Kama ninyi ni wachumba na mmoja si mwaminifu huo unaitwa ni uasherati na ni vizuri kuachana kwani mchumba asiyemwaminifu huja kuwa mwanandoa asiyemwaminifu.

Washauri wa mambo ya ndoa wanafahamu fika kwamba katika matatizo mengi ya wanandoa suala la kukosa uaminifu (infidelity) kawaida ni nusu ya matatizo yote katika ndoa.

Ujue au usijue kwamba kuna kuchepuka (affair/infidelity) imetokea katika ndoa yako ukweli unabaki kwamba matokeo ya mwanandoa mmoja kuchepuka nje ya ndoa yake ni mabaya sana kwa yeye mwenyewe, ndoa yake na huweza kuleta crisis kubwa ya familia na hata jamii kama si taifa.
Fikiria suala la UKIMWI tu kama unaweza muulize Tiger Woods

VITUKO VYA KUCHEPUKA NJE YA NDOA (infidelity)

Kawaida mwanandoa anayechepuka akikamatwa na kupewa talaka mara nyingi hawezi kuoana na yule aliyekamatwa naye.
Hivyo kama upo kwenye affair na mwanaume wa mtu au mke wa mtu kumbuka kwamba hupati point yoyote au kukuongezea uwezekano wa yeye kuoana na wewe ikitokea amepata talaka.

Affair ni dalili (symptoms) za huzuni iliyopo kwa wanandoa na maana yake mmoja anakosa hisia (feelings) sahihi kwa mwenzake na matokeo yake husukumwa kuchepuka nje na akishachepuka huongeza matatizo mengine zaidi ya ndoa kama vile kuchelewa kurudi nyumbani, matumizi ya pesa na magonjwa.

Si sahihi kwamba kuwa na affair ni kupata great sex, kutoka nje ni vibaya kwa sababu ni kweli kwenye ndoa kuna great sex na "we need to spread the word" kwamba kwenye ndoa sex ni tamu zaidi.

Si kweli kwamba mwanandoa anayechepuka hufuata mwanamke mrembo zaidi kuliko aliyekwenye ndoa yake au mwanaume maridadi zaidi kuliko aliye kwenye ndoa yake, wengi huvutwa na feelings zile wanakosa ndani ya ndoa zao.

Affair nyingi zina base kwenye urafiki na kuungana kihisia na sharing ya siri na feelings mbalimbali na wakati mwingine sex huwa si sababu ya kuwa na affair bali urafiki wa karibu kwa jinsia tofauti.

Tamaduni nyingi humwangalia vibaya mwanamke kuliko mwanaume linapokuja suala la mwanandoa kuchepuka nje.

Kubwa zaidi ni kwamba uwezekano wa kutolewa talaka ni pale mwanamke akionekana ametoka nje ya ndoa (cheating) kuliko mwanaume akitoka nje ya ndoa.
Tutaendelea............................

No comments: