"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, January 2, 2010

Ni zawadi si Haki yako!

Tendo la ndoa ni Zawadi siyo Haki
Mungu alitoa sex kama zawadi kwa waliooana.
Ametoa zawadi ya sex ili kutufundisha kuhusu yeye na uhusiano wake na sisi.
Utendaji wa sex ni picha ya muunganiko (sharing) kwa kutoa vyote (vile tulivyo) kwa mwenzako (mke au mume) na pia ni picha ya kumkubali kumpokea mwenzako (wote) kama alivyo kwako.

Kuna faida wazi kabisa kwa uhusiano wa tendo la ndoa kwa mke na mume kama vile afya ya mishipa, kupunguza maumivu, kufanya MP kuwa stable, kupunguza depression (unyonge wa kihisia), kupunguza (stress) msongo wa mawazo na kuongeza kuridhika kwa mahusiano ya ndoa.

Mungu anawapa uhuru wanandoa kunywa na kufurahi raha ya mapenzi kila mmoja kwa mwenzake kama wanandoa, hata hivyo sababu za kiroho na kisayansi haziwezi kutumika kama silaha ya mwanandoa mwingine kumthibiti mwenzake.
Uwezo wa kimapenzi kati ya mke na mume bado ni zawadi ambayo tunatakiwa kupeana bure na kwa kupenda na kwa moyo wa furaha (kutoa na kupokea kila mmoja kwa mwenzake katika ndoa).
Pale mwanandoa mmoja anapokuwa na mtazamo kwamba tendo la ndoa ni haki basi kunakusinyaa kwa aina fulani katika mahusiano huanza kujitokeza.
Mke hawezi kuwa na raha ya mapenzi katika ndoa kama mume atakuwa ni mtu wa kulazimisha na kutaka kwa nguvu kama haki yake (demanding) na pia si raha sana pale mke anapotoa tendo la ndoa kwa sababu anawajibika kutoa hata kama hakuwa tayari.

Tendo la ndoa linaloridhisha (great sex and satisfying sex) ni pale kila mwandoa anakuwa amejiadabisha kutoa kwa uhuru mwili wake kwa mwenzake.
Unapotoa kwa uhuru mwili wako kwa mume au mke wako na kupokea mwili wake kwa uhuru unaipa ndoa kitu sahihi cha asili yake na Mungu hufurahia na kutoa kibali.

Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu, nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu, nimekula sega langu la asali na asali yangu, nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.
(Song of Songs 5:1).

2 comments:

Anonymous said...

kaka kwakweli unanibari sana maana ningeyajua wapi haya maana hata viongozi wetu wa imani hawafundishi haya kwa wanandoa ndio maana utakuta kuna migogoro mingi kwenye ndoa.namshukuru Mungu kwa kuwa nimeyajua haya kabla ya kuingia kwenye ndoa naamini ndoa yetu itakuwa ya baraka sana.Ndi yune mnyalamasani kwa vabena ek ubarikiwe

Lazarus Mbilinyi said...

Be Mnyalamasani!
Kamwene be!

Asante sana kwa maoni yako mazuri. Ni kweli kuna mambo mengi sana ya msingi huwa hatufundishwi kabla ya kuoana na tungekuwa tunajua basi wengi wasingekuwa wanajiingiza kwenye matatizo makubwa katika ndoa zao, hata hivyo naamini tukishirikiana tunaweza kujifunza mengi zaidi na mahusiano yetu yakawa mazuri zaidi na hata migogoro ikijitokeza itakuwa commodity nzuri sana kwa ndoa zetu kwani kupitia tofauti katika mahusiano ndipo wanandoa hufahamiana zaidi na kupendana zaidi.

Nitajitahidi kutoa articles nyingi sana zinazohusu uchumba kwani ukiwa na ujuzi wa ndoa wakati bado upo kwenye uchumba utakuwa mwanandoa imara na mwenye busara.

Tuzidi kuombeana kwani nina mambo mengi ya kuandika kuliko muda ninaokuwa nao online kwani majukumu yanazidi kuwa mengi ila kwa neema itokayo juu yote yanawezekana.

Upendo daima