"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, January 24, 2010

Wanamalizana Kabla!

SWALI:
Habari kaka Mbilinyi!
Naomba kuelewa nimesoma blogs mbalimbali kuhusu wedding gown, hivi kuvaa nyeupe ni kweli ina maana bibi harusi ni bikira?
Kama kweli mbona watu wanaolewa na matumbo ambayo hata watoto wanayaona halafu wanavaa gauni jeupe hapo sijaelwa vizuri naomba ufafanuzi wa hili.
Halafu jamani kwa wachungaji wetu wanafungisha ndoa mtu akiwa na tumbo kubwa tuu hapo mtoto asizaliwe nje ya ndoa kwa mimi naona tayari ni nje ya ndoa maana walizini.
Nikutakie siku njema!

Mama P.

JIBU:
Asante sana kwa swali zuri ambalo kwa kweli linaonesha ukweli halisi wa hali ilivyo duniani na namna maadili na hofu ya Mungu ilivyoshuka kwa kiwango cha kutisha.
Kwa ufupi ni kwamba ilikuwa hadi 1840 pale queen Victoria alipoolewa kwa kuvaa vazi jeupe ndipo mabibi harusi wengi walianza kuvaa rangi nyeupe; ila kabla ya hapo hakukuwa na traditions za kuvaa vazi nyeupe kwa bibi harusi.

Hata hivyo vazi la rangi nyeupe kuvaliwa siku ya harusi tangu (zamani) kale ilikuwa ni alama au ishara ya kuonesha usafi, kujitunza au kuwa bikira kwa bibi harusi na huu utamaduni umekuwa msingi mkubwa kwa wakristo wanaofuata mafundisho ya Yesu au Biblia.
Kwa bibi harusi kuvaa vazi jeupe ni kuonesha au dhihirisha au maanisha kwamba amejilinda na dunia (uchafu wote, uzinzi ni uchafu nje ya ndoa) na sasa anajitoa kwa mume wake kama zawadi na kwamba yeye ni bikira kama kanisa (church) ambalo ni mfano wa bibi harusi linavyotakiwa kujilinda na dunia kwa kuwa na vazi safi lisilo na doa kuwa tayari kwa mume wake ambaye ni Kristo siku ya kuja kwake mara ya pili duniani (unyakuo).

Kikristo (hasa wale ambao wameokoka), Bibi harusi huvaa rangi nyeupe kuonesha amejitunza (bikira) na kama amepatikana ni mjamzito basi husubiri hadi azae ndipo afunge harusi yake na mume wake.

Leo hali imekuwa tofauti kwani bibi harusi wote (Christian) huvaa gauni jeupe kwanza kama vazi rasmi la harusi na pili kuonesha furaha, sherehe, hekaheka, shangwe, kutimiza ndoto nk.
Hali imekuwa mbaya zaidi kwani sasa kumetokea wanamitindo mbalimbali (designers) ambao sasa wana design wedding gowns kwa ajili ya bibi harusi mjamzito.

Mwaka 2008 nchini Uingereza kulikuwa na harusi 20,000 za Kikristo ambapo mabibi harusi walikuwa wajawazito siku ya harusi na wote walikuwa chini ya miaka 45 na mara ya kwanza kufunga ndoa.

Kuhusu wachungaji kufungisha ndoa huku wanajua fika bibi harusi ana mimba kubwa ukweli ni kwamba ingekuwa busara kama wangewaacha bibi harusi azae kwanza ndipo wafunge hiyo harusi kwani ni aibu kwa kanisa.

Biblia inakataza mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa na nje ya ndoa; hivyo bibi harusi kuwa na mimba maana yake kuna uzinzi umefanyika na suala hapa si bibi harusi tu bali na bwana harusi ambaye amempa mimba na issue si mimba kwani mimba ni matokeo ya uzinzi.

Ingawa Mungu ni mwaminifu kuweza kusamehe dhambi ya uzinzi hata hivyo ni busara mtoto akazaliwa ndipo wahusika waweze kufunga harusi yao kuliko kufunga harusi huku mwanamke ana tuta kwenye tumbo.
Hii ni kuonesha kwamba kwa sasa duniani uadilifu na hofu ya Mungu imeshuka kwa kiwango cha kutisha.

Je, wale wanaotoa mimba (abort ion) na kuonekana safi machoni pa watu huku bibi harusi akiwa na vazi nyeupe hapo inakuwaje?
Ukweli ni kwamba Wakristo tunahitaji kuwa mfano kwa kuishi kama Biblia inavyosema ndiyo maana ndoa za leo hazidumu kwani wanandoa huingia kwenye ndoa huku wameshadanganya na ndoa yao huwa na msingi wa kudanganya na kutoaminiana maisha yote.

Pia kuna tamaduni ambazo (hata baadhi ya madhehebu ya Kiksristo huruhusu maharusi kupeana mimba ili kuhakikisha kama wana uwezo wa kuzaa ni kama hawataki kusikia eti mke hapati mimba!
Hili ni kinyume na Neno la Mungu.
Na kama tatizo ni mwanaume si atamaliza mabinti wote kanisani na mabinti ndo wataonekana wana matatizo kumbe mzizi wa tatizo ni mwanaume mwenyewe.
Kweli dunia imeisha!
Kwa ujumla this is a rubbish!

Kwa sasa tunahitaji ku-redefine who real Christians are; maana hali ni mbaya na maadili ya kibiblia yanazidi kupotea.
Hata hivyo pamoja na michanganyo yote na takataka zote bado kuna vijana (wa kike na wakiume) ambao huamua kujitunza hadi siku ya kufunga ndoa; naamini kwako ni siku ya furaha na Mungu hujisikia utukufu sana kwao.
Kama ni kijana hujaoa au kuolewa kumbuka kwamba kujitunza hadi siku ya kuolewa ni jambo muhimu sana na lenye utukufu na baraka sana kwa ndoa yako, achana na ushamba wa kujiona eti kuingie kwenye ndoa ukiwa bikira umepitwa na wakati, kumtii Mungu si ushamba wala kupitwa na wakati bali ni kwenda na wakati na kuonesha wewe ni mwenye hekima na busana na kwamba unajali kuhusu future yako.

2 comments:

Anonymous said...

Tumsifu Yesu Kristu!

Asante sana kwa majibu mazuri yaani umejibu kiuzuri mno mpaka raha kuuuuuuuuumbe du jamani!

Mapendo daima!
Mama P!

Lazarus Mbilinyi said...

Mama P,

Asante kama umeridhika na majibu.

Nakutakia siku njema na afya njema.

Upendo daima!

Lazarus