"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, January 14, 2010

Yanatoka yenyewe!

SWALI.
Kwa nini maziwa hunitoka wakati sina mimba na sinyonyeshi?
Jibu
Ukweli ni kwamba ili maziwa yazalishwe (breast milk) tendo zima hutawaliwa na pituitary glands (kiswahili sijui).
Kama unatumia dawa zozote (medications), huweza kuathiri kiwango cha homoni zinazozalishwa mwili mwako.
Kama kuna kuongezeka kwa kiwango cha homoni zinazohusika na kutengeneza maziwa (breast milk) basi unaweza kujikuta maziwa yanatoka wakati huna mimba wala hunyonyeshi.
Pia zipo baadhi ya dawa za uzazi wa mpango huudanganya mwili na kupelekea matiti kutoa maziwa wakati hunyonyeshi na wala huna mimba.
Jichunguze kama huna sababu mojawapo nilizotaja hapo juu.
Kama maziwa yanayotoka yana rangi tofauti au yanaonesha si katika hali ya kawaida basi kumuona daktari ni jambo la msingi zaidi na ni muhimu sana Daktari akwambie ni kweli hakuna tatizo lolote au kuna tatizo.

No comments: