"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, January 14, 2010

Yule mwanamke!

KUKOSA UAMINIFU KATIKA NDOA HUUMIZA SANA
Mume wa Jane alipokiri kwamba ni kweli “Nilikuwa na uhusiano na yule mwanamke”.
Jane alipata mshituko ambao hauelezeki ni zaidi ya shock ya umeme.

Kwanza alijiuliza
“Imekuwaje sikuweza kujua dalili kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea na nilikuwa mjinga kiasi gani nisijue;
je, nilikuwa sioni matatizo ya ndoa yangu hadi mume wangu anafikia hatua hiyo, nilikuwa kipofu kiasi gani?
Na huyo mwanamke ametumia mbinu gani hadi kumpata mume wangu nami nisijue?”
Alijiuliza hayo maswali huku machozi yakibubukika kutelemka kwenye mashavu kama mvua za Alnino.

Jane alijikuta yupo katika wimbi kubwa la msongo wa mawazo mazito, hasira na kutojiamini kukaongezeka.
Wakati mwingine alikuwa anafua nguo na ghafla anajikuta anaishiwa pumzi na mapigo ya moyo kubadilika na viganja kuanza kutoa jasho nyembamba kama vile amakutana na simba ghafla.

Wakati mwingine hata kama anatazama TV ili kupoteza mawazo, ikitokea kukawa na program inaonesha affair yoyote ya ndoa basi hujikuta hasira zinampanda na kuzima Tv na kuanza kulia kwa machozi.

Zaidi ya miezi miwili usingizi umeota mabawa na hakuwa na hamu ya chakula na matokeo yake afya yake ikaanza kuzorota na kila mtu akajua Jane anaumwa kwani ule uchangamfu wake na afya yake vinaleta maswali zaidi ya majibu.

Ingawa mume wake alikiri kwamba hawasiliani tena na yule mwanamke, bado Jane alijikuta bado anawaza na kupata picha ya mume wake akiwa anafanya mapenzi ya yule mwanamke na akajikuta anamthibiti mume wake kila movement anayofanya maana haaminiki tena na kitu kidogo tu kilimchukiza mno Jane.
Jane alijitahidi sana asiwaze kuhusu huyo mwanamke hata hivyo alivyokuwa anajitahidi kusahahu ndivyo alivyozidi kukumbuka na kuwaza zaidi na alijikuta mawazo kuhusu huyo mwanamke yanazidi kujirudia na kulata hasira zaidi.

Tukumbuke kwamba ni kweli affair huumiza sana na maumivu yake ni makali kimwili, kiroho na kihisia.
Kukiwa na affair huwezi kukwepa kuwa na msongo mawazo kama ya Jane.
Jambo la msingi ni kwamba Jane si mtu wa hasira za kupigana na kelele kama sisi wengine kwani angekuwa mwingine hapa pasingekalika kabisa.

Msongo wa mawazo huja na mawazo huja kutokana na issue kwamba yule unayemwamini kuliko mtu yeyote duniani anakuwa amekusaliti kirahisi hivyo tena bila wewe kujua.

Wanandoa ambao wanapambana na issue ya affair huwa na kiwango kikubwa cha depression kuliko matatizo mengine ya ndoa.

Ni kweli affair ni dhambi na chukuzo kwa Mungu na ni kitendo kinacholaaniwa kwa nguvu zote hata hivyo hata kama umeumizwa sana jambo la msingi ni kukumbuka kwamba huwezi kujisia hivyo (msongo na mawazo na hasira) milele.
Ukweli ni kwamba kujisikia hivyo upo sahihi na unatakiwa kuweka malengo mapya ya kurudi katika hali yako ya kawaida kitu ambacho naamini ni kigumu sana.
Unatakiwa kuhimili hali uliyonayo ili hayo maumivu na feelings ulizonazo zisikufanye kilema hata ukajiumiza zaidi kama vile kujinyonga au kunywa sumu kwani hapa ndipo utasikia mapenzi yanaua.

Ni muhimu kuchukua hatua Zifuatazo ili kurudi kwenye hali yako ya kawaida;
Jiruhusu mwenyewe kujisikia vile unajisikia, kama ni kulia, lia tena kwa machozi mazito, kama kukasirika basi kasirika na muuliza maswali anayehusika kadri ya unavyotaka ili kujua ukweli. Zaidi jikubali na ukubali kwamba ni kweli yametokea.

Tafuta mtu unayemwamini (mshauri, mchungaji nk) akusaidia kuhimili maumivu na uchungu ulionao kwani kwa kuongea na mtu unayemwamini maumivu huondoka.

Jitoe, jikabidhi (moyo) kwa Mungu.
Yeye peke yake ndiye anajua maumivu.
Mungu ametuahidi kutupa faraja wakati wa dhiki na maumivu hata kama shetani ana mpango wa kuharibu ndoa zetu bado tukiishi katika blueprint ya ndoa kama Mungu anavyotaka tutaishi maisha ya furaha amani na ushindi.
Tutaendelea.....

4 comments:

Anonymous said...

What about him kaka Mbilinyi. Is that fair kwamba mimi tu ndio nichukue hizo efforts ili kurudisha mahusiano yetu katika mstari mnyofu na kuweza kumuamini tena na kurudisha mapenzi yangu kwake kwa yeye tu kuniambia kwamba haendelei na mahusiano na huyo mwanamke. Kaka Mbilinyi hii mada imenigusa na u a just like an angel sent from above. Yani kwa kifupi ndio situation niliyon nayo hivi sasa. My hubby alikuwa na affair before we got marriage. Worse enough imedevelop into a kid!!! U can imagine the man of my dream apart from all the pain kujua tu kwamba alikuwa ana cheat wakati tuko wachumba still amezaa na mwanammke mwengine. Smthing I was always dreaming to bring him his 1st kid. It hurts so much kaka Mbilinyi I do not know when am gonna heal. He cried a lot alivyoniambia alicheat na ana mtoto na m/mke mwengine na amesema anaregret every part of it na kwamba walikata mawasiliano wakati hy m/mke ana mimba. Bt since mtoto ameshazaliwa na inabidi amtunze hapo sasa ndio ngoma kaka angu. M/mke kila mwezi anawekewa hela ya matunzo kwenye account lakini kila siku ni simu kwa mume wangu. Na mume jinsi alivyo hawezi hata kugomba anachofanya ni kuikata. Jamani, how can I trust kama huwa hawaongei nikiwa sipo pamoja na mume wangu? Nimeshamwambia kuhusu hy hali sasa kinachofanyika ni kuwa na simu muda wote na simu iko in silent mode. Hope u understand kaka angu.Hata mtu uwe na moyo wa chuma utasense maumivu ya kuwa unakuwa deceived. He always tells me kwamba it was a mistake na kwamba am the one he wants to spend the life with lakini kaka Mbilinyi, I dont see kama anafanya effort yoyote kuwa mbali na huyo m/mke. Dont know labda nina wivu sana........ But it hurts me so very bad!!!! Sijawahi kumwambia mtu yoyote as am not a person to talk on my private life na sina rafiki close tunayeshare private life zetu. To talk to mu mum naona kama nitamchanganya as am just eight months in marriage. Dont know what to do

Sister H.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada H,
Kwanza pole sana kwa shida iliyokupata, naamini hakuna binadamu anayefahamu maumivu uliyonayo ila wewe na zaidi unaumiza sana kufanyiwa kitendo kama hicho na mwanaume ambaye ulimpenda na kumpa trust hata kuamua kuishi pamoja maisha yote yaliyobakia hapa duniani.

Inaumiza sana na upo sahihi kujisikia hivyo unavyojisikia ingawa inaonesha wewe ni mwanamke mvumilivu sana.

Kutokana na maelezo yako inaonesha mume wako sasa ana wake wawili huyo mwenye mtoto na wewe kitu kinachofanya uumie zaidi kwani zaidi ya yeye kukiri kosa bado anapoendelea kuwasiliana naye automatically kwako ni maumivu kwani huwezi jua wanapowasiliana wanaongea kitu gani.

Siyo kwamba una wivu bali ni feelings kwani huyo ni mume wako na unavyojisikia upo sahihi jambo la msingi mnatakiwa kuja na permanent solution ingawa bado na ndoa nayo ni changa mno.

Kinachotakiwa sasa ni Mume wako kukuhakikishia kwamba hana mawasiliano na huyo mwanamke na anashindwa kukata mawasiliano kwa sababu ana mtoto huko kitu ambacho kinaumiza zaidi.

Hakuna jambo lisilo na mwisho na hivyo unajisikia hutajisikia milele.

Kabla sijatoa mapendekezo jinsi ya kukabiliana na hii hali kuna maswali ya kukuuliza kwanza kama unaweza nitumie email kupitia lazarusmbilinyi@gmail.com

Pole sana!

mende adui said...

Kaka Mbilinyi,

Shida yangu ni kubwa sana ninavyo iona,,kwani nimeolewa miaka hata miwili hajapita kisha mumeo wangu ameenda nje ya ndoa na mwanamke mwingine na hapa ninapongea amepata mtoto wa miazi kama mitatu sasa...mie nilirukwa na kichwa nilipojua tena yeye mwenyewe ndio aliyeniambia kwa sababu waligombana huko mwadada huyo akasema anamletea mwanae kwangu, ndiyo kisa cha mumeo wangu kuja nyumbani kama farasi na kuniita chumbani kunieleza yote...sasa funny enough mie ni mtu nasoma nje ya nchi..kinacho niuma ni kwamba mumeo wangu alikuwa anajifanya wakati mie niko nyumbani lakini nikipanda ndege tu basi anarudi anaserebuka na huyo mwanamke...la kushangaza huyo mwanadada ni mtoto mdogo sana ukilenganisha na mume wangu..lakini sasa mume anasema ati ni shetani na kwa vile am not home ati niko masomoni...ndiyo maana kikatokea kitu hicho...kilicho niudhi zaidi ni kwamba sisi ni waiislamu basi mumeo wangu kabla mtoto kuzaliwa alienda akafanya ndoa ya siri na mwanadada na akamlipia nyumba mwaka moja..ndoa hiyo ilikuwa ya sire sana hata mtu hakujua alafu alitoka dar kaenda kuifanyia Arusha..pia kaniomba ruhusa ati anakwenda kikazi kumbe mwenzangu mie anaenda kufunga ndoa....sasa mambo yalipo haribika nilimwambie anipe talaka yangu nirudi kwetu na kienda huko ninakosoma basi sirudi tena bongo...mume wangu kaja juu kweli na akasema hawezi kunicha hata kwa dawa tena kasema anamuandikia huyo mwanadada talaka yake ,,,yaani ndoa ya less than 5 moths sasa...jamani mie am confused karibu nijuuwe ...sasa masomo yananishoda,,moyo ulishtuka mpaka madaktari wanasema nichunge sana...yaani sijui ni kwambiaje...hakuna hata mtu mmoja katika familiar yangu anajua na hata kaka yake mmoja amejaribu sana kujua kunaendelea nini lakini mimi nimeficha lakini mume wangu kamwabia ukweli...sasa huyo kaka yake animbembela sana kwa kweli kupita maelezo...sasa siwezi tena kumuani mume wangu...kinacho niuma sana ni kwamba mie ni mtu na status yangu lakini nijirudi sana kuolewa nae cause of natural love nilikuwa nao kwake...kisha basi nilimkuta na watoto wake lakini wote niliwachukuwa na walea mie...imagine hata watoto hajui anything. halafu mie sina mtoto wa kumzaa kwani nilipata mimba ikatoka...am going cray

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana. Naomba email yako, yangu ni lazarusmbilinyi@gmail.com