"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, February 19, 2010

Ananitaka!

Kaka Mbilinyi,

Mimi ni binti wa miaka 28 nimepata mchumba ambaye sasa ni miezi 4 tangu tumefahamiana na tatizo kubwa ambalo naomba msaada ni kwamba huyu mchumba wangu sasa ameanza kunitaka mapenzi (sex) kabla ya kuoana na mimi ninampenda Mungu na pia nampenda mchumba wangu anioe sasa nifanyeje?

Dada Herieth,

Dada Herieth,

Asante sana kwa swali zuri ambalo naamini akina dada wengi hujikuta wapo njia panda katika kutoa uamuzi kuhusiana na wanaume wa aina hiyo ya kwako.

Suala la sex kabla ya ndoa na Yule unategemea atakuoa au kuolewa naye mara nyingi ni kutembea na mume ambaye atakuwa mume wa mwenzako kwani akishatembea na wewe uwezekano wa kukuacha unakuwa mkubwa zaidi.

Mwanaume makini na mwenye upendo wa kweli hata kama utasafiri kwenda sayari ya Mars au North pole bado atakuwa tayari kusubiri na kuvumilia kufanya mapenzi na wewe hadi ndoa kwanza.

Kufanya sex ni kujuana, na ukishamjua mtu basi amekwisha, zawadi kubwa ambayo mwanaume huweza kumpa mwanamke anayempenda ni kuvumilia hadi siku wakioana au kufunga naye ndoa kwanza ndipo sex.

Pia wanaume wanajua mwanamke wa kuchezea na mwanamke wa kuoa, mwanamke wa kuoa huwa hakubali kuchezewa mwili hadi siku aolewe (precious woman) na mwanamke wa kuchezea ni Yule mwanaume akimtishia kidogo kwamba sikuoi kama hunipi nionje (mwanamke rahisi au cheap) atakubali yaishe, anajifariji eti wanaume siku hizi hawapatikani!

Ni mwanaume gani duniani na akili zake au busara zake atakubali kuoa mwanamke rahisi, cheap?

HAKUNA

Ni saikolojia ya mwanaume akishamjua mwanamke hasa kabla ya ndoa kuachana naye na kutafuta Yule ambaye atafaa kumjua (SEX) baada ya ndoa.

Thamani ya mwanamke hupungua sana baada ya kufanya mapenzi (sex) na mwanaume kabla ya ndoa na ni sababu tosha kwa mwanaume kutafuta mwanamke ambaye ataoana naye kwanza then sex.

Hata kama mwanaume atamshauri mwanamke waishi pamoja kwanza ndipo wafunge ndoa kwa maana ya kujuana kwanza ndipo wafunge ndoa, bado si ticket ya kwamba atakuoa bali ni kukuchezeana tu kwani hana ahadi wala kifungo kinachomfunga au kinachokulinda wewe, hapo mnafanya uasherati tu!.

KUMBUKA!

Kabla ya kuolewa huna commitment or covenant yoyote na mwanaume anayekwambia anakupenda na baada ya ndoa kunakuwa na commitment na covenant au agano/ahadi nzito ambayo mwanaume huitoa mbele za Mungu, watumishi wa Mungu, ndugu zake na ndugu zako, marafiki na jamaana kukubali kuishi na wewe katika maisha yake yote hadi kifo.

Kabla ya ndoa chochote kinaweza kubadilishwa na baada ya ndoa hakuna kinachoweza kubadilishwa.

Baada ya ndoa huwezi kubadilisha mawazo au maamuzi au hisia kuhusu kuoana.

Unafanya sex ukijua kwamba hajakuoa, ndio ukweli, kujisikia atakuoa hakuwezi kukufanya uwe umeolewa; na kufanya sex hakukufanyi uwe umeolewa, kinachofanya uwe umeolewa ni ahadi zenu wawili mbele za watu, kanisa na Mungu kwamba mnataka kuishi pamoja kama mke na mume hadi kifo kitakapowatengenisha.

Wakati wa ndoa wawili mnatoa ahadi kwa Mungu na baina yenu na mbele ya kanisa ambao ni mashahidi.

Kabla ya ndoa hakuna ahadi mbele za Mungu wala mbele za mashahidi hata kama amekuvalisha pete ya uchumba (engagement) inayong’aa kama dhahabu zilizotumika kujenga hekalu la mfalme Suleman au hata kama anakwambia anakupenda from earth to the moon, unadhani kumpa mwili wako kabla ya ndoa ndo kuolewa au hawezi kukuacha, utajuta bure!

Akishafanya sex na wewe anakuwa tayari ameshajua wewe ni wa ladha gani na jinsi unavyozidi kumpa ndivyo anazidi kukinai na kuhitaji mwingine ambaye ni mke wa kuoa.

Anajua kabisa kwa kuwa mmevunja amri kubwa ya Mungu ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa hutamwamini kabisa baada ya kuoana kwani anajua utakuwa unawaza na kujiuliza swali kwamba; kama aliweza kuvunja sheria za Mungu kabla ya ndoa, je si anaweza kutembea na mwanamke mwingine hata katika ndoa?.

Biblia inakataa sex kabla ya ndoa hata kama ulimwengu unaona sahihi ila ndani ya nafsi yako wewe mwenyewe ni shahidi kwamba ni makosa.

Kufanya mapenzi na mwanaume ambaye amekuahidi kukuoa hakufanyi uwe hujavunja sheria hata kama mnasali sala tano kwa siku, ukweli unabaki palepale kwamba hata mkiingia kwenye ndoa hamtaaminiana tena.

Kumbuka msingi wa nyuma au ndoa hujengwa kwenye uchumba na kama kwenye uchumba mmeanza kwa kuvunja sheria basi hata kwenye ndoa itakuwa kila mmoja kuvunja sheria kwa kwenda mbele.

Afadhari uachwe hujafanya naye sex kuliko kuachwa huku umefanya naye sex ni aibu, ni maumivu, ni uchungu na kuchezewa mwili na utu wako kusiko tamkika.

Wakati mwingine unaachwa na magonjwa au mimba na kupoteza utu wako na heshima yako na pia ni kama label ambayo utatembea nayo katika maisha yako kwamba wewe ni failure!

Hata hivyo habari njema ni kwamba bila dhambi hakuna msamaha na tunaye mwokozi ambaye tukimuomba msamaha yeye hutusaheme na kutuondolea dhambi zetu zote.

(1Yoh: 2:1-2)

4 comments:

Anonymous said...

Yaani,umenikosha kaka!
Hii site i hope wanaisoma vijana wote pamoja na watarajiwa wote wa ndoa!Ina mafundisho mengi sana hasa ya kimaadili na hii ni hoja moja ambayo ninakubaliana nayo sana.
Mimi niliwahi kuwa na uhusiano kwa takriban miaka 14 na huyo rafiki yangu aliwahi nitamkia tujiingize ktk tendo la ndoa lakini kwa kuwa nililelewa ktk maadili kama hayo,nilikataa.Sikatai,ni rahisi kufikiria,"akinitamkia tufanye ngono,si "ninamkatalia tu"!
Hapana,si rahisi na hasa kama mnapendana sana na kuaminiana still the outcome ni kama ulivyoeleza.Heshima ya mwanamke yote ni ktk kujitunza kwake na kamwe usijidanganye kwamba,"mimi ni mzuri,nitapata mume"..si kweli kwani ktk tamaduni zetu za KiAfrika,ni mwanaume atamkaye/tangaza ndoa,si mwanamke kwa hiyo ni kama kujigonga kwako tu,"Waswahili",husema,"kumbeleza ndoa"!
Ninachotaka kusema ni kwamba,kumkatalia ni kumemfanya aniheshimu mpaka leo!
So vijana,msife moyo,"subira yavuta heri"....iwapo mtakuja achana,"Mungu hamtupi mja wake" hata siku moja,atakupatia tu mwenzi anayekufaa...
From the bottom of my heart,thank you so much bro,keep it up,
NN

Lazarus Mbilinyi said...

Dada NN,

Hongera sana kwa ujumbe wako na pongezi nyingi ni kile kitendo cha kukataa sex kabla ya ndoa.

Ni kweli kwa kuongea unaweza sema ni rahisi kukataa ila kama unajua kupenda na kumpenda mtu basi kukataa sex ni ujasiri wa hali ya juu sana na Mungu akubariki sana.

Hata hivyo kwa kukataa ulijenga msingi mzuri wa kuaminiana ndani ya ndoa ndiyo maana anakuheshimu hata leo pia nimpongeze mume wako kwa kuvumilia pia kwani naamini sasa anafahamu wewe ni mwanamke wa thamani kiasi gani.

Naamini wapo vijana wengi ambao wanajikuta kwenye njia panda hata hivyo uamuzi wako ndiyo utakufanya ujute au ubarikiwe.

Mungu ni mwaminifu na ahadi zake ni kamilifu kwako wanaotii sheria zake.

Upendo daima

Anonymous said...

Hello kaka yangu,
Thank you for your encouraging words but i need to clarify:the gentleman and i have not married.We actually broke up due to to religion differences.Thank you again,
N.N

Lazarus Mbilinyi said...

NN,

Thanks for the information.
You are strong woman!

Keep it up

Love always