"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, February 24, 2010

Huwa Bado Nimekasirika!

Swali:

Kaka Mbilinyi,

Asante sana kwa blog hii kwani tunajifunza mambo mengi sana katika ndoa zetu.

Swali langu ni kwamba kila tukiwa na msuguano (fight) mume wangu huniomba tufanye sex ili tusawazishe mambo hata hivyo binafsi hujikuta nimekasirika bado na sina mood na yeye analalamika kwamba bado nina donge moyoni na kwamba hatujayamaliza?

Ni mimi Mama Anon.

Mama Anon.

Kwanza asante sana kwa kuwa msomaji wa hii blog na pia kwa swali zuri ambalo inaonesha mume wako anakuweka kwenye njia panda.

Kila wanandoa wana aina yao ya kumaliza mambo baada ya valangati wengine hata wakimaliza bado hukaa kila mmoja na hasira hadi saa kadhaa au siku kadhaa au wiki, mwezi.

Kawaida wanandoa wakiwa na argument (kitu ambacho hakiwezi kuepukika kwani hata ndoa imara huwa na arguments na tofauti kubwa ndoa nzuri kukiwa na argument wanamaliza na kuendelea na kupendana) kunakuwa na mtazamo negative kila mmoja kwa mwenzake, hata hivyo jambo la msingi ni ninyi wote kujadiliana vile kila mmoja anajisikia na zaidi kila mmoja vile anapenda kuondoa zile negatives zilizo kwenye brain.

Tofauti kubwa kati ya mwanamke na mwanaume ni kuhusiana na namna ya emotions zinavyofanya kazi kwani mwanaume ni rahisi kumaliza mgogoro na kuweza kujihusisha na sex muda huohuo na mwanamke ni ngumu kidogo kwani bado unakuwa hujafunguka bado kihisia ndiyo maana huwa unajisikia bado umekasirika na huwezi kujiingiza kwenye suala la sex.

Baada ya mzozo kwisha ni vizuri kujikumbusha wewe mwenyewe ni vitu gani unavipenda kutoka kwa mume wako ili kubadilisha ubongo wako uondoe negatives kuhusu mume wako.

Kawaida unahitaji mambo mazuri matano ili kusawazisha negative moja kuhusu ubaya wa mume wako (argument).

Ni vizuri kujihusisha katika sex pale ukiona kila kitu kipo shwari na feelings zako zimerudi kwenye mstari kwani sex bila ukaribu ni kuumizana.

Ni muhimu kujadiliana na mume wako namna ambavyo huwa unajisikia baada ya mzozo ili afahamu na zaidi wote kwa pamoja mfurahie ndoa yenu badala ya wewe kujihusisha huku una hasira.

1 comment:

Anonymous said...

Ni kweli namunga mkono mama anon kwan hata kwangu mara nyingi hutokea hivyo sasa nitakuwa nimepata ufumbuzi baada ya kusoma hii post.