"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, February 15, 2010

Maneno Matupu

Kuwa na jibu la kitu fulani haina maana una majibu ya kila kitu.

Kufahamu au kujua jinsi au namna ya kulea mtoto wako kuwa na tabia njema haina maana kwamba mtoto wako atakuwa na tabia njema kwani kufahamu tu haitoshi bali kutendea kazi.

"Knowing does not always lead to doing"
Mtu hawezi kuitwa ni mwenye hekima na busara kwa kuwa anajua kweli na haki bali ni pale anapokuwa mkweli na mtu wa haki.

Kuijua Biblia au maandiko peke yake hakuwezi kukufanya maisha yako kuwa na mabadiliko hati pale utakapoitendea kazi ndipo itabadilisha maisha yako.

Kujua ua kufahamu mambo yanayoweza kuifanya ndoa yako kuwa imara haisaidii chochote kama hutendei kazi hata kile kidogo unachokijua.

Utasoma magazeti yote, vitabu vyote, blogs zote na kuhudhuria semina zote, mikutano yote kama hutendei kazi kile unajifunza bado ni bure.

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ujumbe mzito sana huu...Mwenye sikio na asikie