"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, February 24, 2010

Mlalo upi?

Baada ya harusi tu nataka nizae mtoto!

Linapokuja suala la mwanamke kupata mimba (ujauzito/ conception) kuna mijadala mingi ipo kuhusiana na mlalo (sex making position/love making position) upi unafaa kwa ajili ya kutengeneza mtoto.

Hata hivyo hakuna mlalo ambao unajulikana au kushauriwa kwamba ndio unafaa duniani hata hivyo kuna maswali mengi ambayo huhusiana na suala zima la tendo la ndoa na kupata mimba.

Je, Baadhi ya milalo ni bora zaidi ya mingine linapokuja suala la kupata mimba?

ingawa kumekuwa na utafiti mdogo kuhusiana na hili suala bado utafiti umekuwa unaonesha kile hutokea wakati wa tendo la ndoa.

Katika zote missionary position (Mwanaume juu mwanamke chini huku wakiangaliana) inaonekana ndiyo inatoa uwezekano mkubwa zaidi kwa kuwa husaidia kuwa na deep penetration huzihakikishe sperms zaidi ya mlango wa uzazi (womb).

Pia mwanamke kuingiliwa kwa nyuma (rear entry) huwezesha positioning ya sperms vizuri kama missionary position.

Je, kama mwanamke natakiwa kulala na si vinginevyo ili kupata mimba?

Wanasayansi wanasema ili kuondoa uwezekano wa sperms kushindwa kuogelea kutokana na gravity hasa mwanamke anapokuwa amekaa au simama juu ya mwanaume. Kama sperms zina afya hakuna tatizo ingawa kama sperms hazing a afya mwanamke anashauriwa kulala wakati wa tendo la ndoa au hata baada ya tendo la ndoa ili sperms kufikia target.

Je kuna muhimu wowote kufika kileleni (orgasm) ili kupata mimba?

Ni dhahiri kwamba mwanaume ni vizuri afike kileleni (mshindo) katika process ya “baby making” ili kuhakikisha anazipa sperms speed inayotakiwa kufika kwenye target. Utafiti wa karibuni unaonesha pia mwanamke ni vizuri afike kileleni ikiwezekana wakati mmoja na mume wake kwani contractions zinapotokea husaidia sperms kufikia mji wa uzazi.

Je, kama ninataka mtoto wa kike au kiume mlalo gani unafaa?

Suala la milalo halina uhusiano na jinsia ya mtoto bali timing na frequency ndiyo muhimu kwa kusababisha jinsi ya mtoto.

1 comment:

Anonymous said...

Imenibariki sana.